TAN

TAN

Bayport

Bayport

Kikoa

Kikoa

Myway entertainment

Myway entertainment

FORE PLAN CLINIC

FORE PLAN CLINIC

MPINGA CUP 2016

MPINGA CUP 2016

Mashujaa Fm 89.3, Lindi

Tuesday, March 11, 2014

Mkutano wa Kimataifa wa Biashara Haramu ya Wanyamapori kuanza Uingereza jana

IMG_6222Rais Jakaya Kikwete akiongoza Kikao cha Ujumbe wa Mawaziri na Wakuu wa Taasisi za Uhifadhi nchini kabla ya kuanza rasmi kwa Mkutano wa Kimataifa wa Kuzuia Biashara Haramu ya Wanyamapori jijini London, Uingereza. (Picha na Pascal Shelutete, TANAPA) 
Na Pascal Shelutete, TANAPA
Mkutano wa Kimataifa kuhusu Biashara Haramu ya Wanyamapori (Conference on Illegal Wildlife Trade) unaanza rasmi leo katika ukumbi wa Lancaster House.
Mkutano huu utakaohudhuriwa na jumla ya mataifa 47 na Mashirika 13 ya Kimataifa umeitishwa na Serikali ya Uingereza kwa lengo la  kujadiliwa na masuala maalum matatu kuhusiana na biashara haramu ya wanyamapori. Masuala maalum uyanayotarajiwa kujadiliwa ni Jinsi ya Kuimarisha Usimamizi wa Sheria (Law Enforcement) na mchango wa mfumo mzima wa sheria za jinai  (criminal justice system) katika kukabiliana na biashara hiyo.
Aidha, utajadili Jinsi ya kupunguza hitaji la bidhaa zinazotokana na wanyamapori (demand for wildlife products) na Jinsi ya kusaidia Maendeleo Endelevu kwa Jamii zilizoathiriwa na biashara hiyo haramu.
Mkutano huu utazungumzia wanyama aina ya tembo, faru na tiger. Wanyama hawa wamechaguliwa kwa kuzingatia jinsi wanavyoshambuliwa zaidi na makundi ya wawindaji haramu kwa lengo la kuu pembe na ngozi zao.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete tayari ameshawasili Uingereza akiongoza ujumbe wa maafisa kutoka Serikali ya Tanzania kwa ajili ya kushiriki Mkutano huu

No comments:

Post a Comment