TAN

TAN

Bayport

Bayport

Kikoa

Kikoa

Myway entertainment

Myway entertainment

FORE PLAN CLINIC

FORE PLAN CLINIC

MPINGA CUP 2016

MPINGA CUP 2016

Mashujaa Fm 89.3, Lindi

Wednesday, March 12, 2014

Wakufunzi vya vyuo mbalimbali wapigwa msasa

_DSC0076Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais, Eng. Angelina Madete (Katikati) na Mkurugenzi wa mazingira Dkt. Julius Ningu (Kulia) wakimsilikiza Bw. Julio Esterban Mshauri Mwelekezi kutoka UNIDO akitoa ufananuzi kwa wakufunzi kutoka Vyuo vya ufundi nchini._DSC0100Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais, Eng. Angelina Madete akitoa hotuba ya ufunguzi wa warsha ya Mafunzo ya wakufunzi kutoka Vyuo vya Ufundi Nchini, mafunzo hayo yanafanyika katika Hotel ya Blue Pearl jijini Dar es Salaam
_DSC0111Washiriki wa Mafunzo wakiwa katika picha ya Pamoja na Mgeni rasmi Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais Eng. Angelina Madete watatu kutoka kulia mara baada ya ufunguzi wa warsha.
_DSC0119Sehemu ya washiriki wa warsha wakifatilia hotuba ya ufunguzi kutoka kwa mgeni rasmi.
Na Lulu Mussa na Rashda Swedi,
 Ofisi ya Makamu wa Rais, Dar es Salaam
Serikali inaendelea na jitihada za kutoa elimu kwa umma juu ya njia bora za kuhudumia majokofu na viyoyozi ili kulinda tabaka la Ozoni.
Hayo yamesemwa jijini Dar es Salaam jana na Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais, Eng. Angelina Madete wakati wa ufunguzi wa Warsha ya Mafunzo kwa Wakufunzi kutoka Vyuo mbalimbali vya Ufundi Nchi.
Katika Hotuba yake Bi Madete amesema kuwa kemikali haribifu zinauwezo mkubwa kuharibu tabaka la Ozoni na kuongeza joto angani. Kutokana na sababu hizo, Serikali ya Tanzania kwa kushirikiana na jamii za kimataifa zimekubaliana kufanya jitihada za kuondoa kemikali  hizo hatarishi.
Bi Madete ameainisha baadhi ya kemikali hizo kuwa ni methyl bromide, halons na chloroflorocarborns ambazo hutumika kama vipozi katika majokofu, viyoyozi, vifaa vya  kuzima moto, usafishaji chuma, ufukizaji wa mazao katika maghala na utengenezaji wa magodoro ambazo huleta madhara kwa tabaka la ozoni na adhari zake hutokea kwa binadamu, mimea na viumbe hai.
Katika awamu ya kwanza, Tanzania imefanikiwa kuondoka tani  296 za kemikali hizo haribifu ikiwa ni utekelezaji wa Mkataba wa Montreal na Vienna ambayo Tanzania iliridhia mwaka 1993.
Aidha, Bi Madete ameyataja madhara yatokanayo na uharibifu wa Tabaka la Ozoni kuwa ni kuongezeka kwa magonjwa ya saratani ya ngozi,uharibifu wa macho maarufu mtoto wa jicho, na upungufu wa uwezo wa mwili kujikinga na maradhi.  Athari hizi kwa kiasi kikubwa zinatokana na shughuli za kibinadamu kama vile matumizi ya kemikali haribifu na zisizo rafiki kwa mazingira. 
Warsha hii ya siku mbili imeratibiwa na Ofisi ya Makamu wa Rais na inajumuisha wakufunzi kutoka Vyuo vya Ufundi vya Zanzibar na Mikoa ya Kilimanjaro, Arusha, Kigoma, Mbeya na Mwanza.

No comments:

Post a Comment