TAN

TAN

Bayport

Bayport

Kikoa

Kikoa

Myway entertainment

Myway entertainment

FORE PLAN CLINIC

FORE PLAN CLINIC

MPINGA CUP 2016

MPINGA CUP 2016

Mashujaa Fm 89.3, Lindi

Tuesday, March 11, 2014

MSD YAZINDUA KITUO CHA USAMBAZAJI DAWA MULEBA MKOANI KAGERA

Naibu Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii, Dk. Kebwe Kebwe akihutubia kwa niaba ya 
Makamu wa Rais Dk. Mohamed Garib Bilal aliyekuwa mgeni rasmi wa ufunguzi wa kituo hicho.
Ofisa Rasilimali Watu na Utawala wa Bohari ya Dawa (MSD), Shangwe Stephen akiwa kwenye hafla hiyo.
Mbunge wa Muleba Kaskazini, Profesa Anna Tibaijuka. (kulia), akiteta jambo na Meneja wa MSD, Kanda ya Mwanza ambaye pia anahudumia kituo hicho cha Muleba, Dyekwifo Sabura.
Wananchi mbalimbali wa wilayani Mulena na mkoa wa Kagera wakiwa katika hafla hiyo.
Na Mwandishi Wetu, Muleba
SERIKALI imeipongeza Bohari ya Dawa (MSD) kwa kuanzisha utaratibu wa kuweka alama ya GOT katika dawa inazosambaza jambo litakalo saidia dawa za serikali kutambulika kirahisi kwa wananchi hivyo kupunguza vitendo vya wizi.
Pongezi hizo zilitolewa na Naibu Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii, Dk. Kebwe Kebwe kwa niaba ya Makamu wa Rais Dk.Mohamed Gharib Bilali ambaye alikuwa mgeni rasmi katika uzinduzi wa Kituo cha Usambazaji dawa cha MSD wilayani Muleba mkoani Kagera kilicho zinduliwa mwishoni mwa wiki.
“Naamini utaratibu huu wa kuweka alama hiyo umeanza kufanyika hivyo naagiza utekelezwe haraka na dawa zote ziwekewe alama hiyo ili kuepusha upotevu wa dawa za Serikali” alisema Kebwe.
Kebwe alisema Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii kwa kushirikiana na Bohari ya Dawa imekuwa na ushirikiano mzuri  na  wadau mbalimbali wa maendeleo kama vile; Mfuko wa Kimataifa wa Kupambana na UKIMWI, Malaria na Kifua Kikuu (Global Fund) na Shirika la Misaada la Maendeleo la Marekani (USAID) ambao tayari wamekwishatoa msaada mkubwa wa ujenzi wa maghala ya kisasa ya kuhifadhia dawa katika mikoa mbalimbali nchini.
Waziri Kebwe alitoa ushauri ushirikiano huo uendelezwe ili wadau hao waweze pia kutoa msaada wa ujenzi wa ghala la kisasa katika Halmashauri ya Muleba la kuhifadhia dawa na vifaa tiba.
Alisema ufunguzi wa kituo hicho cha kusambazia dawa mkoani Kagera, ni mchango tosha katika kutekeleza Malengo ya Milenia hususan, kupunguza vifo vya akina mama na watoto, na kupambana na UKIMWI na Malaria.
” Kituo hiki kitatumika kuongeza ufanisi wa mfumo kufikisha dawa karibu na wananchi na kwa wakati ili kufanikisha lengo hilo mahsusi” alisema Dk. Kebwe.
Alisema Serikali ilianzisha Bohari ya Dawa ili kufanikisha majukumu ya kununua, kuhifadhi na kusambaza dawa na vifaa tiba katika vituo vya umma vya kutolea huduma ya afya hapa nchini.
Aliongeza kuwa pamoja na juhudi kubwa ambazo Serikali inafanya kupitia MSD ili kufanikisha upatikanaji endelevu wa dawa na vifaa tiba, bado vituo vingi vya kutolea huduma ya afya hasa vijijini vimekuwa na tatizo sugu la uhaba wa dawa muhimu hivyo Serikali itaendeleza juhudi hizo ili tatizo hilo liweze kupungua au kudhibitiwa kabisa.
Alisema kwa sasa Bohari ya Dawa inawajibika kufikisha dawa na vifaa tiba moja kwa moja hadi kituo husika cha huduma ya afya badala ya kuishia kwa Mganga Mkuu wa Wilaya kama ilivyokuwa hapo awali.
Kebwe alisema mfumo huu wa ufikishaji dawa moja kwa moja hadi katika vituo vya huduma na hospitali kwa kiasi kikubwa umesaidia sana upatikanaji wa dawa katika vituo vya umma vya kutolea huduma ya afya hasa vijijini.
“Naagiza kuwepo ushirikiano wa karibu kati ya Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii (kupitia Bohari ya Dawa) na Wizara ya Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (kupitia Ofisi ya Waziri Mkuu) ili kuhakikisha ufanisi katika jambo hili” alisema Kebwe.
Katika hatua nyingine Dk. Kebwe amesema anatambua tatizo la dawa na vifaa tiba vya Serikali kupatikana katika maduka ya dawa ya watu binafsi jambo linaloikera sana Serikali hivyo ameiagiza Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii kwa kushirikiana na Jeshi la Polisi kufanya msako endelevu ili kuwafichua na kuwachukulia hatua za kisheria wale wote watakaopatikana na dawa za Serikali kinyume cha Sheria.
Mwenyekiti wa Bodi ya Udhamini (MSD), Profesa Idris Mtulia alisema mkakati wa kushirikisha sekta binafsi ili kufanikisha upatikanaji wa dawa pindi Bohari ya Dawa inapokuwa na upungufu, unaendelea kutekelezwa sanjari na halmashauri zote nchini kuhimizwa kununua dawa kutoka MSD kwa kutumia vyanzo vingine vya fedha (kama vile Basket Fund, NHIF, Tele kwa Tele)
Alisema pamoja na changamoto mbalimbali inazokabiliana nazo, Bohari ya Dawa kwa kushirikiana na Serikali na wadau wengine, itaendelea kutoa huduma bora na kuhakikisha kuwa dawa zenye ubora na bei nafuu zinakuwepo wakati wote kwa manufaa ya Watanzania.

No comments:

Post a Comment