TAN

TAN

Bayport

Bayport

Kikoa

Kikoa

Myway entertainment

Myway entertainment

FORE PLAN CLINIC

FORE PLAN CLINIC

MPINGA CUP 2016

MPINGA CUP 2016

Mashujaa Fm 89.3, Lindi

Wednesday, July 23, 2014

Miss Kanda Mashariki Vipaji kufanyika Idd Pili

Warembo 14 wanaowania taji la Kanda ya Mashariki ( Redds Miss Eastern Zone 2014) watashindania taji la vipaji (talent award) lililopangwa kufanyika siku ya Idd Pili kwenye ukumbi wa Maisha Plus, Kibaha, Mkoa wa Pwani.
 
Akizungumza jijini leo, mratibu wa mashindano hayo, Alex Nikitas alisema kuwa kutokana na mashindano hayo ya vipaji, kambi ya warembo iliyopangwa kuanza Julai 29 kwenye hotel ya Usambara Safari Lodge, sasa itaanza Julai 28 kwenye hotel ya Precision mkoani Pwani.
 
Nikitas alisema kuwa maandalizi ya mashindano hayo yamekwisha kamilika na warembo hao mbali ya kushindana katika vipaji, pia watatoa msaada kwa kituo cha watoto yatima cha mkoa wa Pwani na baadaye kurejea mkoani Morogoro tayari kwa mashindano yaliyopangwa kufanyika  Nashera Hotel Agosti 8.
 
Alisema kuwa mashindano hayo yatashirikisha jumla ya warembo  14 kutoka mikoa minne ambayo ni Pwani, Lindi, Mtwara na mwenyeji, Mkoa wa Morogoro chini ya udhamini wa Redds Original, Zanzi Cream Liquer, Pepsi, Usambara Safari Lodge, Kitwe General Traders, Starwing Lodge, Nashera Hotel, CXC Africa, Sykes Travel, Sasa Saloon, Grand Villa Hotel, Shabibi Line na Clouds FM.
 
Warembo  hao ni Lucy Julius Diu, Prisca  Mengi, Tarchisia Noback Mtui na Angel  Shio ambao wanatoka Morogoro.  Warembo wengine ni Elizabeth Tarimo, Lilian  Andrew na Leila  Abdul  Ally ambao wanatoka mkoa wa Lindi ambapo kutoka Mtwara ni  Nidah Fred Katunzi, Lightness  Mziray na Nelabo  Emmanuel.
 
Pia warembo kutoka Pwani ni Khadija Ramadhan Sihaba, Irene Rajabu Soka, Mary  Mpelo na Arafa Shaban. Nikitas alisema kuwa warembo hao watakuwa kambini kuanzia Julai 29 kwenye hotel ya Usambara Safari Lodge chini ya Miss Kanda ya mashariki mwaka jana,  Diana Laizer.

No comments:

Post a Comment