TAN

TAN

Bayport

Bayport

Kikoa

Kikoa

Myway entertainment

Myway entertainment

FORE PLAN CLINIC

FORE PLAN CLINIC

MPINGA CUP 2016

MPINGA CUP 2016

Mashujaa Fm 89.3, Lindi

Saturday, July 26, 2014

MKURANGA KUTEKELEZA MIRADI YAKE, MWENGE WAZINDUA MIRADI YA BILIONI MOJA

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu mchimati@gmail.com au piga namba +255767869133. 
Mkimbiza mwenge kitaifa, Rachael Kassanda
Mkimbiza mwenge kitaifa, Rachael Kassanda, amezindua miradi 13 ya maendeleo, katika wilaya ya Mkuranga, mkoa wa Pwani, yenye thamani ya zaidi ya shilingi bilioni moja .
Alizindua miradi hiyo katika kijiji cha Mkiu ikiwamo mnada na matenki ya maji katika kijiji cha Kiramba, katika shule ya msingi Kimanzichana na maabara katika shule ya sekondari Tambani.
Alisema lengo la kuizundua miradi hiyo ni kuwasaidia wananchi kupata maendeleo na kuwaongezea kipato.
Akiwahutubia wakazi hao aliwataka wajitokeze katika kuchangia maoni ya upatikanaji wa katiba mpya  ambayo itawasaidia kupata haki katika mambo mbalimbali yanyoizunguka jamii.
Alisema bila ya kujitokeza katika masuala ya katiba na kutoa maoni wanaweza kupata katiba ambayo italalamikiwa kutokana na kutokuwa na mahitaji yao.
Aliwataka vijana kujituma kwa kufanya kazi ambazo zitawaingizia vipato badala ya kujiingiza katika utumiaji wa madawa ya kulevya.
Akizungumzia ugonjwa wa Ukimwi, Kassanda alisema kuwa hauna kinga na umeteketeza idadi kubwa ya vijana ambao ndiyo taifa la kesho na kuwataka vijana kutoshiriki ngono zembe na kujenga utamaduni wa kuangalia afya zao mara kwa mara.
Mkuu wa wilaya hiyo, Mercy Sila, ambaye aliupokea mwenge huo katika kijiji cha Njopeka ukitokea Rufiji, alisema lengo la kuzindua miradi hiyo ni njia mojawapo ya kutumiwa na wakazi wa wilaya hiyo kwa ajili ya kuwaletea maendeleo, sambamba na kuwaongezea kipato.
Mwenge huo baada ya kuzindua miradi katika Wilaya hiyo, umekabidhiwa na Sila katika Wilaya ya Kisarawe.
CHANZO: NIPASHE

No comments:

Post a Comment