TAN

TAN

Bayport

Bayport

Kikoa

Kikoa

Myway entertainment

Myway entertainment

FORE PLAN CLINIC

FORE PLAN CLINIC

MPINGA CUP 2016

MPINGA CUP 2016

Mashujaa Fm 89.3, Lindi

Thursday, July 24, 2014

TAMASHA LA NACTE INTER COLLEGE TANZANIA 2014/15,

 Mratibu wa Tamasha la Nacte Inter College Tanzania 2014/15- (BONANZA). Bi. Magreth Kilawe(kulia), akifafanua jambo kuhusiana na Michezo ya Vyuo Vya Elimu ya Kati, katika ngazi ya Cheti na Stashahada, ambayo inaanza kufanyika katika Vyuo Mbalimbali hapa Nchini, katika hafla iliyofanyika kwenye Ukumbi wa Idara Habari Maelezo, Dar es Salaam,Leo, kushoto ni Mkurugenzi wa Kampuni na Mwenyekiti wa Kamati ya NACTE INTER COLLEGE TANZANIA, Mh, Mpalule Shaaban,
 (Picha Zote Kwa Hissani ya Miss Demokrasia Tanzania).
 Waandaaji wa Tamasha la NACTE INTER COLLEGE TANZANIA 2014/2015, kutoka Kulia ni Mwakilishi wa Wakuu wa Vyuo vya NACTE TANZANIA, Mwl. Kasilima, Mwenyekiti wa Kamati Mh.Mpalule Shaaban, Mratibu wa Tamasha, Bi, Magreth Kilawe, Afisa Mahusiano wa Miss Demokrasia Tanzania, Bi, Rosina Mchomvu na Bi, Jane Charles kutoka Ikondolelo Hoteli Lodge, wadhamini wa Vikao vya Maandalizi.
 Mwenyekiti wa Kamati Mh.Mpalule Shaaban, Mratibu wa Tamasha, Bi, Magreth Kilawe, Afisa Mahusiano wa Miss Demokrasia Tanzania, Bi, Rosina Mchomvu
 Mwenyekiti wa Kamati Mh.Mpalule Shaaban, Mratibu wa Tamasha, Bi, Magreth Kilawe, Afisa Mahusiano wa Miss Demokrasia Tanzania.
 Mwenyekiti wa Kamati Mh.Mpalule Shaaban, Mratibu wa Tamasha, Bi, Magreth Kilawe, Afisa Mahusiano wa Miss Demokrasia Tanzania,
 Mwenyekiti wa Kamati Mh.Mpalule Shaaban, Mratibu wa Tamasha, Bi, Magreth Kilawe, Afisa Mahusiano wa Miss Demokrasia Tanzania.
 Baadhi ya Waandishi wa Habari wa vyombo mbali wakifuatilia kwa makini Mazungumzo wakati wa kuelezea Tamasha la NACTE INTER COLLEGE TANZANIA.
 Mwakilishi wa wakuu wa vyuo, Mwl Kasilima kutoka kushoto, Mwenyekiti wa Kamati Mh.Mpalule Shaaban,Mwakilishi wa Serikali za Wanafunzi na Mshauri wa Chuo cha C.B.E-Dar es salaam, Mr. Stephano, Mratibu wa Tamasha, Bi, Magreth Kilawe.
 kutoka kushoto ni Mwakilishi wa wakuu wa vyuo, Mwl Kasilima, Mwenyekiti wa Kamati Mh.Mpalule Shaaban,Mwakilishi wa Serikali za Wanafunzi na Mshauri wa Chuo cha C.B.E-Dar es salaam, Mr. Stephano, Mratibu wa Tamasha, Bi, Magreth Kilawe.
 Mratibu wa Tamasha, Bi, Magreth Kilawe,(kati)akifafanua jambo, wengine Mdhamini mdogo wa Tamasha kutoka Mlonge Moringa, wanaojiusisha na masuala ya Dawa na Vipodozi kuoka mlonge, Mwakilishi wa Serikali za Wanafunzi na Mshauri wa Chuo cha C.B.E-Dar es salaam, Mr. Stephano,wa pili kulia ni Afisa Uhusiano wa Miss Demokrasia Tanzania, Bi. Rosina Mchomvu, na Mwakilishi wa IKONDOLELO LODGE, Mdhamini wa Vikao vya Maandalizi, Bi. Janet Charles
 Mratibu wa Tamasha, Bi, Magreth Kilawe,(kulia)wengine ni Mdhamini mdogo wa Tamasha kutoka Mlonge Moringa(kushoto), wanaojiusisha na masuala ya Dawa na Vipodozi kuoka mlonge, Mwakilishi wa Serikali za Wanafunzi na Mshauri wa Chuo cha C.B.E-Dar es salaam, Mr. Stephano
 Mwenyekiti wa Kamati ya NACTE INTER COLLEGE TANZANIA 2014/2015, Mh. Mpalule Shaaban, akifafanua jambo mbele ya waandishi wa habari, Idara Habari Maelezo, kuhusiana na Tamasha la Vyuo vya Elimu ya Kati na Vilivyopata Usajili wa NACTE, wengine ni (wa pili kulia)Mratibu wa Tamasha, Bi, Magreth Kilawe,(kati,Mdhamini mdogo wa Tamasha kutoka Mlonge Moringa, (wa tatu kushoto), wanaojiusisha na masuala ya Dawa na Vipodozi kuoka mlonge, (kati ni Mwakilishi wa Serikali za Wanafunzi na Mshauri wa Chuo cha C.B.E-Dar es salaam, Mr. Stephano na Afisa Uhusiano wa Miss Demokrasia Tanzania, Bi, Rosina Mchomvu.
Wandishi wakifuatilia.
 Bidhaa mbalimbalia zitokano za zao la MLONGE, wakati wa Hafla ya Waandishi wa Habari, Waandaaji na Wadhamini.
 Viongozi wa Tamasha la NACTE TANZANIA.
 Viongozi


Mratibu wa Tamasha, Bi, Magreth Kilawe,(kati)akiwa na baadhi ya Wanakati na wawakilishi wa Vyuo, na Mdhanini Mdogo.
--------------------------------------------------





TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
PRESS RELEASE
                                                                       
NACTE INTER - COLLEGE TANZANIA BONANZA 2014/15.
(BALOZI WA DEMOKRASIA TANZANIA).
                                                                                                                                24/7/2014
HABARI za wakati huu,
Waandishi wa habari wote, wakuu wa vyuo na viongozi wa Serikali 
za wanafunzi wa vyuo shiriki, wadhamini, Karibuni sana.
Leo ni siku rasmi, ya kutangaza kuanza kwa mchakato mzima 
wa maandalizi ya mashindano ya NACTE Inter-College Tanzania Bonanza 2014/15, ambayo kwa mara ya kwanza yataanza kuonesha sura na muonekano mpya katika Sekta ya Elimu kwa ngazi ya Vyuo vya Kati.
Bonanza hili limepangwa kufanyika 21-23/11/2014 katika viwanja
 vilivyopendekezwa ikiwa ni pamoja na The Mwalimu Nyerere Memoria Academy,(Kigamboni) Chuo Kikuu Dar es Salaam, Leaders Club, TCC Sigara (Chang’ombe, na viwanja vya Shule ya Sekondari Kibaha Katika michezo mbali mbali .
Ndugu wandishi, tamasha hili lipewa kibali na baraza la elimu ya ufundi yaani NACTE katika barua yao ya tarehe 21/6/2014 yenye kumb No. NACTE/EB/64/650/Vol.1/2 ambayo inairuhusu kampuni ya Miss Demokrasia Tanzania, kuandaa na kuwa mwenyeji wa Tamasha la NACTE Inter College Tanzania.
Nichukue fursa hii kuishukuru Serikali kwa kukubali kuipa heshima kubwa kampuni ya Miss Demokrasia Tanzania, ubavu wa kuandaa tamasha hili, lakini pia tunaiomba Serikali kuhamasisha wadau kujitokeza kusaidia vifaa vya michezo hii.
kwa kushirikiana na  vyombo vya habari hapa nchini na vyuo husika, Wadhamini ambao hao ni wadau namba moja, wawezeshaji   tutaifanaya kwa ustadi na kwa makini mkubwa ili mwaka ujao kuwe na msisimko zaidi,
 ikumbukwe kuwa michezo  hii inafanyika kwa mara ya kwanza hapa Tanzania. Itakuwa ni fursa kwa wanafunzi wa vyuo vya kati, kwa nafasi zao kuendeleza vipaji walivyonavyo,  kwa kuwa,  kwa muda mrefu hawajapata nafasi kama hii,  ya kushiriki katika michezo pindi wanapoingia kwenye vyuo,  baada ya masomo ya Elimu za Sekondari.
Ndugu waandishi, Michezo, kama tunavyofahamu ndiyo pekee inayoweza kutoa fursa kwa vijana,  kupata afya nzuri, ajira katika michezo, pamoja na nafasi ya kuitangaza Tanzania,
 kupitia Michezo vijana upata fursa ya kusikilizwa na kufikisha mawazo yao, na mambo mbalimbali yanayohusu afya na maendeleo yao ikiwemo Ujasiriamali, Elimu ya UKIMWI na mengine mengi yakiwemo kutambua nafasi ya kijana katika kutunza na kulinda amani ya Nchi yetu.
Pamoja na kuwa na nchi yenye amani; michezo pia utoa fursa ya vijana kujiendeleza kiujasiriamali,  lakini pia kwa kupitia tamasha hili inaweza kuwa fursa ya makampuni, wahisani, wadau, kukamilisha ndoto zao, katika kuongeza wigo wa ajira kwa vijana wanaohitimu vyuo vya kati.
tumieni  kalamu zenu, Mic, Kamera, kuhamasisha Michezo hii na Wadau kujitokeza kusaidia michezo hii ya vyuo vilivyo pata usajili wa NACTE.
wito unatolewa kwa vyuo, kuthibitisha ushiriki wao mapema, kabla ya tarehe 15/8/2014, Michezo hii ni kwa vyuo vyote vya NACTE Tanzania, baada ya Dar es salaam, itafuata Mikoa ya Mwanza, Arusha, Mbeya, Dodoma na Zanzibar Fomu zinapatikana kwenye Tovuti,
Kampuni ya Miss Demokrasia Tanzania, ilianzishwa Mwaka 2009, na kupata Usajili wa kudumu wa Makampuni unaotambuliwa Kisheria wa Act, 2002 No. 74413 mwaka 2010, na TIN No: 109-267-554. Kampuni hii ambayo kwa ujumla kama lilivyo jina lake, (Miss Demokrasia Tanzania) ina malengo mengi, ikiwa na pamoja na kusaidia jamii hususani vijana wa kike, ambao muda mwingi wamekuwa wakishindwa kufikia malengo kutokana na ukosefu wa miundo mbinu ya kujikomboa kielimu, Utamaduni na Michezo, Ajira,  kwani wengi wao wameoonewa na kunyimwa haki zao.
kampuni hii inalinda na kutetea haki za watu wote ikiwa ni pamoja na kuwapa changamoto Viongozi mbali mbali wa serekali na Taasisi binafsi dhidi ya utendaji wao wa kazi na majukumu ili kuongeza na kuboresha ufanisi wao wa kazi kwa wananchi, imejikita sana kwenye masuala ya Intertainment Michezo, Maonesho, Burudani, Mikutano, Mijadala (Debate), Elimu kwa Jamii, na Urembo (Modal) kwa namna ya kipekee.
Mwisho: kabisa nirudie tena kuishukuru Serikali na Uongozi wa NACTE kwa kuweka na kukubali mpango huu wa Michezo kwenye vyuo vya kati. Tutumie nafasi hii, kuwakaribisha wahisani na Wadhamini wote, kushiriki kikamili na kwa namna yoyote ile ili kufanikisha Tamasha hili la NACTE – INTER – COLLEGE - TANZANIA – 2014 / 2015.
Niwashukuru wadhamini walioanza kujitokeza, IKONDOLELO HOTELI Lodge wanaopatikana Kibamba CCM, MLONGE MORINGA, na Tone on line Radio T-z.  Baada ya kusema hayo. Asanteni Wote kwa kunisikiliza.  niwape nafasi wawakilishi wa Vyuo, na wadhamini waseme japo waliyo nayo…
Magreth Kilawe                                                                                             Rosina Mchomvu                      
Afisa Masoko                                                                                                   Afisa Habari

Kwa Mawasiliano Zaidi:
Miss Demokrasia Tanzania and Entertainment C.o LTD.
Plot No.
S.L.P 8017, Dar Es Salaam,
Simu: +255-767-869-133
+255-765-056-399

No comments:

Post a Comment