TAN

TAN

Bayport

Bayport

Kikoa

Kikoa

Myway entertainment

Myway entertainment

FORE PLAN CLINIC

FORE PLAN CLINIC

MPINGA CUP 2016

MPINGA CUP 2016

Mashujaa Fm 89.3, Lindi

Wednesday, March 11, 2015

43 WAAPISHWA KUWA MANAIBU WASAJILI WA MAHAKAMA YA TANZANIA LEO JIJINI DAR ES SALAAM.

 Jaji Kiongozi wa Mahakama Kuu ya Tanzania Mhe. Shaaban Ali Lila akimwapisha Mhe. Lenatus Ishengoma (kulia) kuwa Naibu Msajili wa Mahakama ya Tanzania leo jijini Dar es salaam. Wanaoshuhudia kiapo hicho ni Jaji Mkuu wa Tanzania Mhe. Mohamed Othman Chande (kushoto) na Mhe. John Kahyoza, Msajili Mahakama Kuu ya Tanzania.
 Jaji Kiongozi wa Mahakama Kuu ya Tanzania Mhe. Shaaban Ali Lila akimkabidhi Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Mwongozo wa utendaji kazi wa Mahakama Mhe. Zahara Abdallah Mlacha mara baada ya kumwapisha kuwa Naibu Msajili wa Mahakama ya Tanzania leo jijini Dar es salaam.
Mhe. Elizabeth Mkwizu  akisaini hati ya kiapo cha kuwa Naibu Msajili wa Mahakama mbele ya Jaji Kiongozi Mhe. Shaaban Ali Lila baada ya kuapishwa leo leo jijini Dar es salaam.
 Naibu Msajili wa Mahakama ya Tanzania Mhe. Hussein Shaaban Mushi akipokea Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Mwongozo wa utendaji kazi wa Mahakama  kutoka kwa Jaji Kiongozi  Mhe. Shaaban Ali Lila mara baada ya kuapishwa kuwa Naibu Msajili wa Mahakama ya Tanzania leo jijini Dar es salaam.
 Mhe. Isaya Khalfan (kulia) akila kiapo cha kuwa Naibu Msajili wa Mahakama ya Tanzania mbele ya Jaji Kiongozi wa Mahakama Kuu ya Tanzania Mhe. Shaaban Ali Lila (kulia) leo jijini Dar es salaam.
Jaji Kiongozi wa Mahakama Kuu ya Tanzania Mhe. Shaaban Ali Lila (aliyekaa) akisaini kiapo cha Mhe. Angela Maria Thei (kulia) aliyeapishwa kuwa  Msajili wa Mahakama ya Tanzania katika hafla fupi iliyofanyika viwanja vya Mahakama ya Rufani leo jijini Dar es salaam. Anayetazama kiapo hicho ni Msajili wa Mahakama kuu ya Tanzania Mh. John Kahyoza (katikati).Picha na Aron Msigwa –MAELEZO.

No comments:

Post a Comment