TAN

TAN

Bayport

Bayport

Kikoa

Kikoa

Myway entertainment

Myway entertainment

FORE PLAN CLINIC

FORE PLAN CLINIC

MPINGA CUP 2016

MPINGA CUP 2016

Mashujaa Fm 89.3, Lindi

Wednesday, March 11, 2015

MSHINDI PROMOSHENI YA ‘WEKA NA USHINDE’ AONDOKA NA GARI

Mkurugenzi Mtendaji wa BOA bank Tanzania, Bw. Ammish Owusu-Amoah, akiangalia funguo za gari hilo kabla ya kumkabidhi, Bw. Said Mohamed Bakari, mshindi wa gari aina ya Toyota Berevis, baada ya kushinda promosheni ya ‘Weka na Ushinde’ iliyoendeshwa na benki hiyo, Dar es Salaam leo. Kulia ni Afisa wa Benki hiyo, Bw. Solomon Haule.
Mshindi wa Gari Bw. Bw. Said Mohamed Bakari akingia ndani ya gari hilo leo baada ya kukabidhiwa
Mkurugenzi Mtendaji wa BOA bank Tanzania, Bw. Ammish Owusu-Amoah akizungumza na waandishi wa habari baada ya kukabidhi zawadi ya gari kwa mshindi.
Waandishi wa habari wakizungumza na mshindi wa promosheni ya gari, Bw. Said Mohamed Bakari

Mwakilishi wa mshindi wa pili wa Promosheni ya ‘Weka na Ushinde’, Bi. Rhoda Manase (aliyemwakilisha Bi. Thureiya Zabron) akipoke pikipiki hiyo kutoka kwa Mkurugenzi Mtendaji wa BOA bank Tanzania, Bw. Ammish Owusu-Amoah Dar es Salaam leo.
“Tumemaliza salama”, ndivyo wanavyosema Mkurugenzi Mtendaji wa BOA benk Tanzania, Bw. Ammish Owusu-Amoah na Afisa wa Benki hiyo, Bw. Solomon Haule, baada ya kukabidhi zawadi kwa washindi leo



Mshindi wa Gari, Bw. Bw. Said Mohamed Bakari akiwapungia waandishi wa habari mkono wakati akiondoka na gari hilo leo.


MSHINDI PROMOSHENI YA ‘WEKA NA USHINDE’ AONDOKA NA GARI

Mshindi wa Promosheni ya ‘Weka na Ushinde’ iliyoendeshwa na Benki ya Afrika Tanzania (BOA Bank), Bw. Said Mohamed Bakari ambaye ni mteja wa benki hiyo mkoani Mtwara, ameondoka Dar es Salaam leo na gari mpya aina ya  Toyota Brevis.

Bw. Bakari ameondoka kwenye viwanja vya benki hiyo, Kijitonyama baada ya kukabidhiwa gari hilo na Mkurugenzi Mtendaji wa BOA bank Tanzania, Bw. Ammish Owusu-Amoah watika wa hafla fupi iliyofanyika.

Akizungumza kwa furaha baada ya kupokea funguo za hari hilo, Bw. (34) ambaye ni mfanyibiashara wa vifaa vya umeme mjini Mtwara, amesema pamoja na kupigiwa simu akifahamishwa kuwa mshindi wa promosheni ya ‘Weka na Ushinde, hakuamini kuwa amejishindia gari.

“Niliona kama ndoto za mchana, sikutegemea kama nitamiliki gari kama hii, bado naona kama ndoto, nimefurahi sana kushinda na kupewa gari
leo hii” alisema Bw. Bakari alipoongeza na waandishi wa habari Dar es Salaam leo huku akisisitiza kuwa amefurahi sana na kuishukuru benki hiyo kwa kuanzisha promosheni hiyo.

Bw. Bakari amesema anaona fahari kubwa kuwa mteja wa BOA bank Tanzania na kwamba kitendo cha yeye kushiriki kwenye promosheni hiyo hakijamsaidia tu kwa kushinda gari, bali pia kimemsaidia kujenga utamaduni wa kujiwekea akiba. “Pamoja na kushinda zawadi hii kubwa, pia promosheni hii pia imenisaidia sana kuongeza bidii ya kujiwekea akiba katika benki, kitendo ambacho kimesaidia sana katika shughuli zangu za kijamii na kiuchumi” alisema

Amewaasa wananchi hususan wafanyabiashara wa aina zote kujijengea utamaduni wa kujiwekea akiba katia benki hiyo mara kwa mara ili waweze kushinda zawadi.

 Akizungumza baada ya kukabidhi gari hilo kwa mshindi, Mkurugenzi Mtendaji wa BOA bank Tanzania, Bw. Ammish Owusu-Amoah amesema benki yake imefurahishwa sana na imani kubwa waliyonayo watanzania kwa benki hiyo  na kwamba hiyo imewafanya wahakikishe waongeze jitihada za kutoa huduma bora za kibenki zinazoendana na mazingira halisi ya soko la Tanzania.

Bw.  Ammish Owusu-Amoah amesema promosheni ya ‘Weka na Ushinde’ ni moja ya hatua ya benki hiyo kujwashawishi watanzania kujenga utamaduni wa kujiwekea akiba, kwani hilo ni suala la msingi sana kwa mtu kupata maendeleo kwa kujiwekea akiba.

“Tumekuwa hapa Tanzania kwa Zaidi ya miaka 10 Sasa na tunafurahi kuona kuwa tumechangia kwa kiasi kikubwa katika ukuaji wa huduma za kibenki hapa nchini. Pia tumeanzisha huduma na bidhaa mbalimbali ambazo zinawalenga wateja wetu wa kada mbalimbali za kimaisha na kiuchumi”, anasema Bw. Ammish na kuongeza kuwa ndani ya kipindi hicho, benki hiyo imefanikiwa kukua kwa kila Nyanja ikiwemo mtaji, idadi ya wateja pamoja na mtandao wa matawi yake.

Amesema kwa sasa BOA bank Tanzania ina mtandao wa matawi 21 ambapo 11 yapo jijini Dar es Salaam kikiwemo kituo cha kibiashara na mengine 9 yapo  Arusha, Mwanza, Kilimanjaro (Moshi), Morogoro (Morogoro Mjini na Mtibwa), Mbeya, Mtwara, Tunduma na Kahama.

Mkurugenzi huyo amesema benki yake ipo kwenye mchakato wa kufungua matawi mengine maeneo mbalimbali ya nchi ndani ya miezi sita.

Promosheni ya ‘Weka na Ushinde’ ilianza Octoba mwaka jana na takriban wateja 2,000 walishiriki huku wakijishindia zawadi mbalimbali ikiwemo T- shirts, kofia, simu za mkononi, Tablets, Shopping Vouchers, na zawadi za juu ambazo ni Pikipiki na Gari aina ya Toyota Brevis.



No comments:

Post a Comment