TAN

TAN

Bayport

Bayport

Kikoa

Kikoa

Myway entertainment

Myway entertainment

FORE PLAN CLINIC

FORE PLAN CLINIC

MPINGA CUP 2016

MPINGA CUP 2016

Mashujaa Fm 89.3, Lindi

Wednesday, March 11, 2015

Mrembo Miss Tanzania aongoza wakazi wa dar katika zoezi la uchangiaji damu

Mshindi
wa tatu wa Miss Tanzania 2014,Doris Mollel akishiriki zoezi la
uchangiaji damu katika ikiwa ni sehemu ya kusherehekea Siku ya wanawake
Duniani,iliyofanyika Buguruni Chama jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki. Kushoto
Ofisa Muuguzi kutoka Benki ya Damu Salama,Selina Joseph. Zoezi hilo la
uchangiaji damu liliandaliwa na Mrembo huyo. Katika kuadhimisha siku ya wanawake duniani,mrembo Doris Mollel
ambaye ni Miss Tanzania namba tatu kwa mwaka 2014 ameongoza mamia ya
watanzania katika zoezi la kizalendo la kuhamasisha kuchangia damu kwa
watanzania kwa ajili ya wagonjwa mbalimbali,zoezi ambalo limefanyika
jijini Dar es salaam mwishoni mwa wiki. 
Zoezi hilo ambalo lilikuwa
linaongozwa na mpango wa taifa wa damu salama kwa udhamini wa kampuni ya
METL lilikuwa na lengo la kupata damu kwa ajili ya kuokoa maisha ya Mama na Mtoto kwani matatizo ya damu katika hospitali za Tanzania
yamekuwa yakiongezeka siku hadi siku,jambo lililompelekea mrembo huyo
kuamua kujitoa kuhamasisha watanzania kujitokeza kwa wingi katika zoezi
hilo. 


Zoezi hilo lilifanyika Machi 8 mwaka huu katika maeneo ya Buguruni
Chama kwa muda wa siku nzima,ambapo jumla ya uniti 65 za damu
zimepatikana kiwango ambacho kimetajwa kuwa kinatia matumaini kwa mrembo
huyo kufanikiwa katika kuwahamasisha watanzania kujitokeza kwa wingi. 


Akizungumza na wanahabari kuhusu kitu kilichomsukuma
kuendesha zoezi hilo,Doris alisema kuwa ameamua kufanya hivyo baada ya
kugundua kuwa wakina mama wengi pamoja na watoto hufariki dunia wakati wa
kujifungua kutokana na kukosa damu ya kuongezewa,jambo ambalo amesema ni
lazima watanzania kuungana kwa pamoja kutafuta damu ya kutosha katika
kila hospitali ili kuiondoa hali hiyo ambayo inaweka hatarini maisha ya
mama na mtoto wa kitanzania. 
Amesema kuwa swala la
kujitolea damu ni swala la kizalendo zaidi na moyo wa kujitoa kwa kuwa
kila mtanzania anaweza kuwa na uhitaji wa damu muda wowote hivyo ni
lazima watanzania wawe na utamaduni wa kuchangia damu mara kwa mara
kwani itasaidia endepo kutatokea uhitaji wa damu katika mahospitali
yetu. Aidha amewataka watanzania wengine ambao wanauwezo
wa kuhamasisha watu wengine kuchangia damu wafanye hivyo kwani kuna
uhitaji mkubwa sana wa damu katika mahospitali ya kitanzania na kufanya
hivyo ni kuokoa maisha ya watanzania wengi wenye uhitaji wa damu hiyo. 

Doris
Mollel alijizolea umaarufu mwaka 2014 baada ya kufanikiwa kushika
nafasi ya tatu katika shindano la Miss Tanzania mwaka huo ambapo
aliwashinda warembo wengine waliokuwa wanawania taji hilo.

 Mtoto wa Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam,Mh. Said Meck Sadick,Bi Mariam Meck Sadick akiungana na wananzania wengine kwenye zoezi la kuchangia damu ikiwa ni sehemu ya kumuunga mkono Mrembo Doris Mollel.
Baadhi
ya wakazi wa jiji la Dar es Salaam wakishiliki zoezi la uchangiaji damu
katika kusherehekea Siku ya wanawake Duniani,iliyofanyika Buguruni
Chama jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki.
Mpiga
Picha wa Kampuni ya New Habari (2006) Ltd,John Dande akipima uzito
tayari kwa kushiriki zoezi la uchangiaji damu,ikiwa ni sehemu kuunga
mkono sherehe za Siku ya wanawake Duniani.zoezi hilo lilifanyika
Buguruni Chama jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki.Picha na John Dande.

No comments:

Post a Comment