TAN

TAN

Bayport

Bayport

Kikoa

Kikoa

Myway entertainment

Myway entertainment

FORE PLAN CLINIC

FORE PLAN CLINIC

MPINGA CUP 2016

MPINGA CUP 2016

Mashujaa Fm 89.3, Lindi

Tuesday, March 10, 2015

KATIBU MKUU WA CCM NDUGU ABDULRAHMAN KINANA AMALIZA ZIARA YAKE CHILONWA, KESHO KUENDELEA JIMBO LA MTERA

2 Katibu Mkuu Ndugu Abdulrahman Kinana akipuliza dawa ya kuua wadudu wanaoshambulia zabibu kwenye shamba la mradi wa kilimo cha zabibu katika kijiji cha Chinangali II wilayani Chamwino Kinana yuko katika ziara ya mikoa mitatu ya Dodoma, Arusha na Kilimanjaro akihimiza na kukagua utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya CCM ya mwaka 2010 akiongozana na Nape Nnauye Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi ambapo kesho atakuwa katika jimbo la Mtera linalowakilishwa na mbunge kijana machachali Mh. Livingstone Lusinde.(PICHA NA KIKOSIKAZI CHA FULLSHANGWE- CHAMWINO -DODOMA) 3Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Dodoma Mh. Adam Kimbisa naye akishiriki katika kazi ya kupuliza dawa ya kuuwa wadudu katika shamba la Zabibu katika kijiji cha Chinangali II.
4 Katibu Mkuu Ndugu Abdulrahman Kinana akisalimiana na Mbunge wa jimbo la Mtera Mh. Livingstone Lusinde wakati alipofanya ziara katika jimbo la Chamwino mkoani Dodoma. 5Nape Nnauye Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi akisalimiana na Mbunge wa jimbo la Mtera Mh. Livingstone Lusinde wakati wa ziara ya Kinana katika jimbo la Chamwino mkoani Dodoma. 7 Katibu Mkuu Ndugu Abdulrahman Kinana aki akizungumza na wajumbe wa mkutano mkuu wa jimbo la Chilonwa  wakati alipofanya ziara katika wilaya hiyo leo. 8 Katibu Mkuu Ndugu Abdulrahman Kinana akiongozana na mkuu wa wilaya ya Chamwino Bi. Farida Mgomi wakati alipokagua ujenzi wa shule ya Jakaya Kikwete iliyopo Chamwino na kushiriki shughuli za ujenzi katika shule hiyo 9 Katibu Mkuu Ndugu Abdulrahman Kinana akishiriki kuchimba shimo la vyoo vya shule hiyo pamoja na mafundi. 10 11Mkuu wa mkoa wa Dodoma Luteni Mstaafu Chiku Galawa na Mjube wa NEC wilaya ya Chamwino Bw. Samwel Malecela wakishiriki kuchanganya udongo kwa ajili ya kufyatulia matofali yanayotumika katika ujenzi wa shule hiyo.. 12Nape Nnauye Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi akimtunza mmoja wa watoto waliokuwa wakipiga ngoma wakati wa mapokezi ya Ndugu Abdulrahman Kinana wakati alipofika katika kijiji cha Msanga. 14 Katibu Mkuu Ndugu Abdulrahman Kinana akishiriki ujenzi wa madarasa katika shule ya msingi Msanga. 15 Katibu Mkuu Ndugu Abdulrahman Kinana akishiriki ujenzi wa zahanati ya kijiji cha Mahampha. 16 Katibu Mkuu Ndugu Abdulrahman Kinana akishiriki kupiga ngoma za utamaduni na wanavikundi mbalimbali wakati alipowasili katika kijiji cha Majereko. 17Mkuu wa mkoa wa Dodoma Mh. Chiku Galawa kushoto na Mkuu wa wilaya ya Chamwino Bi. Farida Mgomi nao wakipiga ngoma wakati Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana alipowasili katika kijiji cha Majereko. 18Nape Nnauye akipokea ngoma kutoka kwa Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana mara baada ya kushirikiana vyema na vikundi vya utamaduni vilivyofika kumpokea katika kijiji cha Majereko. 19Wananchi na wageni mbalimbali walifika  katika mkutano wa kijiji cha Majereko. 20Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Kinana akisoma  taarifa ya kijiji hicho huku Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Dodoma Mh. Adam Kimbisa akiwa amevaa kofia katika staili ya Kimbisa. 21Bw. Samwel Malecela akisalimiana na wananchi katika mkutano huo. 22Mnec Deo Ndejembi kushoto na Bw. Samwel Malecela kulia wakiwa katika mkutano huo. 23Nape Nnauye akihutubia wananchi hawapo pichani katika kijiji cha Majereko. 24Baadhi ya wananchi wakisikiliza hotuba mbalimbali za viongozi. 25Kinana akizungumza na wananchi katika mkutano huo. 26Kinana akijadiliana jambo na Deo Ndejembi na Samwel Malecela kulia mara baada ya kumalizika kwa mkutano huo.

No comments:

Post a Comment