TAN

TAN

Bayport

Bayport

Kikoa

Kikoa

Myway entertainment

Myway entertainment

FORE PLAN CLINIC

FORE PLAN CLINIC

MPINGA CUP 2016

MPINGA CUP 2016

Mashujaa Fm 89.3, Lindi

Thursday, March 12, 2015

Mgodi wa Dhahabu Chunya wahesabiwa siku

images
Baraza la Taifa la Hifadhi naUsimamizi wa Mazingira na Wataalam wa Mazingira wameagizwa kutoa elimu ya mazingira kwa wawekezaji wa Mgodi wa Dhahabu wa Sunshine uliyopo Wilaya ya Chunya mkoani Mbeya . Agizo hilo limetolewa na Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Mazingira, Injinia Binilith Mahenge jana alipotembelea machimbo ya Mgodi huo nakubaini kuwa unaendeshwa bila kuzingatia Kanuni za Mazingira. Katika ziara hiyo Mh. Mahenge alibaini kuwa mgodi huo hauna mtambo wa kutibu maji-taka yake kabla ya kuyatiririsha katika mazingira pia bwawa linalotumika kuhifadhi maji-taka hayo halikidhi viwango vya Kanuni za Mazingira pamoja na kuzibwa kwa mfereji wa asili hivyo kuzuia mkondo wa mvua. Kutokana na hali hiyo, Waziri Mahenge alitoa siku 30 kwa wataalam wake kuwapatia elimu ya Kanuni za Mazingira wawekezaji wa Mgodi wa Sunshine ikiwa ni pamoja na kuwataka wawekezaji hao kutekeleza kanuni hizo ndani ya siku 30 kuanzia jana. Wakati huo huo Mh. Mahenge alitembelea Machimbo ya Dhaabu ya Mek na Mgodi wa Shanta Wilayani Chunya ambapo Wataalam wake Mazingira walibainisha kuwa wawekezaji wa migodi hiyo wametiza kanuni za mazingira. Sanjari na hayo Injiania Mahenge alikutana na Watendaji wa Halmashauri ya Chunya na kukabidhiwa Mapendekezo ya Mradi Maalumu wa kulinusuru Ziwa Rukwa ili lisitoweke kutokana na kilimo holela, uchimbaji wa madini na utirirshwaji wa maji-taka kwenye vyanzo vya Ziwa hilo. Katika makabidhiano ya Mapendekezo hayo Mh. Mahenge aliwaahidi Watendaji wa Halmashauri ya Chunya kuwa atayafanyia kazi Mapendekezo yao lakini pia aliwaomba na wao kuishauri Wilaya waingize Mazingira katika bajeti zao .

No comments:

Post a Comment