TAN

TAN

Bayport

Bayport

Kikoa

Kikoa

Myway entertainment

Myway entertainment

FORE PLAN CLINIC

FORE PLAN CLINIC

MPINGA CUP 2016

MPINGA CUP 2016

Mashujaa Fm 89.3, Lindi

Wednesday, November 11, 2015

JESHI LA POLISI LAANZA KUTOA ELIMU KWA ABIRIA NA MADEREVA ILI KUKABILIANA NA AJALI KATIKA KIPINDI CHA MWISHO WA MWAKA

Mkuu wa Kitengo cha Elimu kwa Umma, Makao Makuu ya Trafiki, Dar es Salaam, ASP Abel Swai akitoa elimu ya usalama barabarani kwa abiria, muda mfupi kabla ya kuanza safari za mikoani katika kituo Kikuu cha mabasi Ubungo, jijini Dar es Salaam, elimu ambayo inalenga kudhibiti ajali za barabarani kuelekea kipindi cha mwisho wa mwaka, (Picha zote na Abubakari Akida, Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi)
Askari wa Kikosi cha Usalama Barabarani, PC Asha Adam, akiwasisitiza abiria kufunga mikanda iliyopo kwenye viti walivyoketi muda wote wa safari muda mfupi kabla ya magari kuondoka katika kituo Kikuu cha mabasi ya abiria Ubungo, jijini Dar es Salaam, kama hatua ya kudhibiti majeraha na vifo vitokanavyo na ajali za barabarani, kuelekea kipindi cha mwisho wa mwaka
Askari wa Kikosi cha Usalama Barabarani,Inspekta Ibrahim Omary Samwi(kushoto), na PC Elisante Bura(kulia), wakikagua moja ya magari yanayofanya safari zake mikoani, kutekeleza mkakati wa Jeshi la Polisi kupitia Kitengo cha Usalama Barabarani kudhibiti ajali kuelekea kipindi cha mwisho wa mwaka.Zoezi hili limefanyika muda mfupi kabla ya magari kuondoka katika kituo Kikuu cha mabasi Ubungo,jijini Dar es Salaam kuelekea mikoa mbalimbali ya Tanzania .
Askari wa Kikosi cha Usalama Barabarani,Inspekta Ibrahim Omary Swami(aliyeko chini ya uvungu wa gari), akikagua moja ya magari yanayojiandaa kuelekea mikoani, zoezi ambalo limefanyika muda mfupi kabla ya magari kuanza kuondoka katika kituo Kikuu cha Mabasi, Ubungo jijini Dar es Salaam.aliyenyoosha kidole juu ni PC Elisante Bura. Hatua hii ya Jeshi la Polisi nchini linalenga kudhibiti ajali kuelekea kipindi cha mwisho wa mwaka,.
Askari wa Kikosi cha Usalama Barabarani,Sajenti Jackson Mafuru (kulia), na PC Elisante Bura(kushoto), wakikagua moja ya magari yanayofanya safari zake mikoani. zoezi hili ambalo limefanyika muda mfupi kabla ya magari kuondoka katika kituo Kikuu cha mabasi Ubungo,jijini Dar es Salaam, ni moja ya hatua ya Jeshi la Polisi kupitia Kitengo cha Usalama Barabarani kudhibiti ajali kuelekea kipindi cha mwisho wa mwaka,.
Askari wa Kikosi cha Usalama Barabarani,Koplo Abdallah Bwasi akikagua moja ya magari yanayofanya safari zake nje ya mkoa wa Dar es Salaam, muda mfupi kabla ya magari kuondoka katika kituo Kikuu cha mabasi Ubungo,jijini Dar es Salaam.Hatua hii ya Jeshi la Polisi kupitia Kitengo cha Usalama Barabarani imekuja kwa lengo la kudhibiti ajali kuelekea kipindi cha mwisho wa mwaka.

Imeandaliwa na Kitengo Cha Mawasiliano ya Serikali- Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi

No comments:

Post a Comment