TAN

TAN

Bayport

Bayport

Kikoa

Kikoa

Myway entertainment

Myway entertainment

FORE PLAN CLINIC

FORE PLAN CLINIC

MPINGA CUP 2016

MPINGA CUP 2016

Mashujaa Fm 89.3, Lindi

Wednesday, November 11, 2015

MAONYESHO YA KIMATAIFA YA UTALII JIJINI MONTREAL, CANADA YAFANA

Maonyesho hayo ambayo yamefanyika katika mahali maarufu panapofahamika kwa jina la “la Place Bonaventure” katika jiji la Montreal, ambalo liko upande wa Mashariki mwa Canada, eneo ambalo wanaozungumza Kifaransa, yamekuwa na hamasa na mashiko makubwa mwaka huu kwa kupata wahudhuriaji zaidi ya elfu thelathini na tatu (33,000).
Kutokana na wingi wa watu, wakiwemo watalii wanaopenda kuzuru nchi mbalimbali, waliohamasika kuhudhuria maonesho hayo, Balozi wa Tanzania Mhe. Jack Mugendi Zoka aliamua kuwa kati ya waonyeshaji na watoa taarifa za vivutio vya utalii katika banda lake kama ionekanavyo katika picha hapo chini. 
Aidha, mabalozi wa nchi mbalimbali walifika katika banda la utalii la Tanzania kujionea ni jinsi gani limeweza kuwa kivutio cha watalii wengi. Balozi wa nchi jirani ya Kenya alikuwa miongoni mwa watembeleaji katika banda hilo
Kati ya mambo yaliyoonyesha kuwavutia watalii hao na hatimaye kutoa ahadi ya kutembelea Tanzania ni: Mlima mrefu kuliko yote Afrika, Kilimanjaro, ambao sasa wamefahamu uko Tanzania, mbuga za wanyama na kisiwa kinachonukia marashi ya karafuu cha Zanzibari.
Kutoka Tanzania Wizara ya Maliasili na Utalii iliwakilishwa na Mamlaka ya Hifadhi ya Taifa ya Ngorongoro ambao walikuwa sambamba za Kampuni Binafsi ya Wasafirishaji Watalii ya ZARA (Zara Tours). Banda la Utalii la Tanzania ambalo lilisimamiwa na Ofisi ya Ubalozi wa Tanzania, Ottawa liligawa zaidi ya vipeperushi elfu kumi (10,000) kwa watu waliolitembelea. 

www.shaabanmpalule.blogspot.com

No comments:

Post a Comment