TAN

TAN

Bayport

Bayport

Kikoa

Kikoa

Myway entertainment

Myway entertainment

FORE PLAN CLINIC

FORE PLAN CLINIC

MPINGA CUP 2016

MPINGA CUP 2016

Mashujaa Fm 89.3, Lindi

Wednesday, November 11, 2015

‘Marufuku kutumia ramani ya Tanzania isiyo sahihi’


SERIKALI imesema itavichukulia hatua vyombo vya habari pamoja na watu watakaobainika kutumia ramani ya Tanzania ambayo sio sahihi.

Akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam, Mkurugenzi wa Idara ya Habari (MAELEZO), Assah Mwambene, alisema kumekuwa na matumizi ya ramani ya Tanzania ambayo inaonesha Ziwa Nyasa lipo katika nchi ya Malawi pekee huku Tanzania ikionekana kutohusika kabisa katika ziwa hilo.

Mwambene alisema ramani sahihi ya Tanzania inaonesha Ziwa Nyasa lina mpaka katikati ambao unaonesha umiliki wa ziwa hilo upo upande waTanzania na Malawi. Aliongeza kuwa hivi karibuni kumekuwa na vyombo vya habari ambayo vimekuwa vikitumia ramani hiyo ambayo sio ramani sahihi.

“Ni vibaya sana vyombo vya habari kutumia ramani ambayo sio sahihi kwani kufanya hivi ni kuharibu utaifa na utambulisho wetu,” alisema Mwambene.

No comments:

Post a Comment