Pambano
la kirafiki la kimataifa kati ya Tanzania (Taifa Stars) na Jamhuri ya
Kidemokrasi ya Congo-DRC (Leopards) lililofanyika jana (Februari 23
mwaka huu) Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam limeingiza sh. 32,229,000.
Fedha
hizo zimepatikana kutokana na watazamaji 11,420 waliokata tiketi
kushuhudia mechi kwa kiingilio cha sh. 2,000, sh. 5,000, sh. 7,000, sh.
10,000 na sh. 15,000.
Mgawanyo
wa mapato hayo ulikuwa kama ifuatavyo; asilimia 18 ya Kodi ya Ongezeko
la Thamani (VAT) ni sh. 5,916,288, gharama ya kuchapa tiketi sh.
2,250,000, malipo kwa kamishna wa mchezo sh. 150,000, malipo kwa waamuzi
wanne sh. 480,000, ulinzi na usafi kwa Uwanja wa Taifa sh. 2,350,000,
Wachina sh. 2,000,000, umeme sh. 300,000 na maandalizi ya uwanja (pitch
marking) sh. 400,000.
Nyingine
ni asilimia 20 ya gharama za mchezo sh. 3,676,542, asilimia 10 ya
uwanja sh. 1,838,271, asilimia 5 ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Afrika
(CAF) sh. 919,136 na asilimia 65 ya Shirikisho la Mpira wa Miguu
Tanzania (TFF) sh. 11,948,763.
No comments:
Post a Comment