Kiingilio
cha chini katika mechi ya mchujo ya Kombe la Mataifa ya Afrika kati ya
Tanzania (Taifa Stars) na Msumbiji (Mambas) itakayochezwa Februari 29
mwaka huu Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam ni sh. 3,000.
Jumla
viti 36,693 (rangi ya bluu na kijani) ndivyo vitakavyotumika kwa
kiingilio hicho katika uwanja huo wenye uwezo wa kuchukua watazamaji
60,000 wakiwa wameketi.
Viingilio
vingine ni sh. 5,000 kwa viti vya rangi ya chungwa, sh. 10,000 kwa VIP
C, sh. 15,000 kwa VIP B wakati kwa watakaokuwa miongoni mwa watakaokaa
katika viti VIP A ambavyo viko 748 tu watalazimika kulipa sh. 20,000
kwa kila mmoja.
Tiketi
zitaanza kuuzwa siku moja kabla ya mchezo katika vituo vya Shule ya
Sekondari Benjamin Mkapa, Kituo cha mafuta cha Bigbon kilichopo Msimbazi
(Kariakoo), mgahawa wa Steers ulioko Barabara ya Samora/Ohio, Kituo
cha mafuta cha Oilcom Ubungo na Uwanja wa Taifa.
No comments:
Post a Comment