Mamlaka
ya Chakula na Dawa (TFDA) ni wakala wa Serikali iliyo chini ya Wizara
ya Afya na Ustawi wa Jamii yenye jukumu la kudhibiti ubora, ufanisi na
usalama wa vyakula, dawa, vipodozi na vifaa tiba ili kulinda afya ya
jamii.
TFDA
inapenda kuutaarifu umma kuwa imebaini kuwepo kwa dawa bandia ya
kutibu ugonjwa wa Malaria katika soko. Dawa hiyo inaitwa Eloquine (Quinine Sulphate 300mg U.S.P) na ipo
katika makopo ya vidonge 1000 (elfu moja) kila moja. Maelezo yaliyopo
katika lebo yanaonesha kuwa dawa hiyo imetengenezwa na kiwanda cha
Elys Chemical Industries Ltd cha nchini Kenya.
Hata
hivyo, TFDA imebaini kuwa kiwanda cha Elys Chemical Industries Ltd
hakitengenezi dawa yenye jina la biashara la ‘ELOQUINE’. Kiwanda hicho
kimesajili Tanzania Quinine Sulphate 300mg B.P isiyo na jina la
kibiashara. Aidha, kiwanda cha Elys Chemical Industries Ltd
kimebainisha tofauti mbalimbali zilizopo katika lebo ya dawa bandia
ikilinganishwa na dawa halisi inayotengenezwa na kiwanda hicho
iliyosajiliwa na TFDA na hivyo kuthibitisha kuwa kiwanda hicho
hakitengenezi dawa hiyo.
Katika
kudhibiti usambazaji wa dawa hiyo hapa nchini, hadi sasa TFDA
imekamata jumla ya makopo 155 ya dawa hiyo bandia ya Eloquine jijini
Dar Es Salaam yaliyokuwa yakisubiri kusambazwa. Aidha, kopo moja lenye
vidonge 115 limekamatwa Moshi, Kilimanjaro. Tayari mtuhumiwa mmoja
amekwishafikishwa mahakamani na upelelezi wa chanzo na wasambazaji wa
dawa hii unaendelea kwa kushirikiana na Jeshi la Polisi.
Uchunguzi wa dawa bandia katika maabara umebaini kuwa vidonge hivyo havina kiambato hai (active ingredient) cha Quinine Sulphate kwa ajili ya kutibu ugonjwa wa Malaria na hivyo matumizi yake ni hatari kwa afya ya binadamu.
Maelezo ya kina yanayotofautisha dawa halisi iliyosajiliwa na dawa bandia ni kama yalivyoainishwa katika jedwali hapa chini.
Dawa halisi iliyosajiliwa | Maelezo ya dawa bandia |
|
|
Wafanyabiashara
wote wa dawa na wananchi wanatahadharishwa kutozitumia dawa hizi na
wale wote waliouziwa dawa hizi wanaelekezwa kuzirudisha dawa hizo
katika ofisi za TFDA, vituo vya afya vya Serikali au vituo vya polisi
vilivyo jirani nao.
TFDA
inapenda pia kuwakumbusha wafanyabiashara wa dawa, wasafirishaji wa
vifurushi na wananchi kutoa taarifa haraka iwezekanavyo pale
wanapohisi kuuziwa dawa duni, bandia au zilizoisha muda wa matumizi.
Taarifa zitolewe ofisi za TFDA makao makuu zilizopo Barabara ya
Mandela, EPI Mabibo External, Dar es Salaam na Ofisi za Kanda zilizopo
mtaa wa Nkurumah, Mwanza, Mtaa wa Sakina – Arusha, Hosptali ya mkoa ya
Dodoma na Jengo la Ofisi ya Mifugo Mkoa wa Mbeya.
Kwa maelezo zaidi tafadhali wasiliana na:-
MKURUGENZI MKUU
MAMLAKA YA CHAKULA NA DAWA
EPI MABIBO EXTERNAL,
DAR ES SALAAM
No comments:
Post a Comment