Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha Ramadhan Khijjah akifungua mkutano wa siku tatu wa wakaguzi wa ndani wa
Sekretarieti za mikoa na Mamlaka za Serikali za Mitaa leo jijini Dar
es salaam wenye lengo kuwaelimisha juu ya marekebisho ya Sheria ya Fedha
Sura 348 ya juni 2010 yaliyopelekea Wizara ya Fedha kuanzisha Idara ya
Mkaguzi wa Ndani wa Serikali(Internal Auditor General Division) ambayo
pia inajukumu kusimamia na kuboresha ukaguzi wa ndani kwenye Mamlaka
za Serikali za Mitaa na Sekrietarieti za Mikoa.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha Ramadhan Khijjah na baadhi ya wakaguzi wa ndani wa
Sekretarieti za mikoa na Mamlaka za Serikali za Mitaa baada ya
ufunguaji wa mkutano wa siku tatu wenye lengo kuwaelimisha juu ya
marekebisho ya Sheria ya Fedha Sura 348 ya juni 2010 yaliyopelekea
Wizara ya Fedha kuanzisha Idara ya Mkaguzi wa Ndani wa Serikali(Internal
Auditor General Division) ambayo pia inajukumu kusimamia na kuboresha
ukaguzi wa ndani kwenye Mamlaka za Serikali za Mitaa na Sekrietarieti
za Mikoa ulianza jana jijini Dar es salaam.
Na Tiganya Vincent-MAELEZO-Dar es salaam
Serikali imewaagiza wakaguzi wa ndani wa Sekretarieti za mikoa na Mamlaka za Serikali za Mitaa kuhakikisha kuwa hesabu za miradi
yote ya maendeleo katika maeneo yao ya kazi inakaguliwa ili
kuhakikisha kuwa inatoa matokeo mazuri yanayolingana na thamani ya
fedha kwa matumizi yanaliyofanywa.
Kauli
hiyo ilitolewa jana jijini Dar es salaam na Katibu Mkuu wa Wizara ya
Fedha Ramadhan Khijjah wakati akifungua mkutano wa siku tatu wa wakaguzi
wa ndani wa Sekretarieti za mikoa na Mamlaka za Serikali za Mitaa.
Mkutano wa siku tatu wa wakaguzi wa ndani wa
Sekretarieti za mikoa na Mamlaka za Serikali za Mitaa unalenga
kuwaelimisha juu ya marekebisho ya Sheria ya Fedha Sura 348 ya juni 2010
yaliyopelekea Wizara ya Fedha kuanzisha Idara ya Mkaguzi wa Ndani wa
Serikali(Internal Auditor General Division) ambayo pia inajukumu
kusimamia na kuboresha ukaguzi wa ndani kwenye Mamlaka za Serikali za
Mitaa na Sekrietarieti za Mikoa.
Alisema
kuwa ni wajibu wa wakaguzi kuanzia serikali kuu hadi Serikali za mitaa
kuhakikisha kuwa miradi zaidi ya maendeleo inakaguliwa na taarifa
kuifikia Wizara ya Fedha mapema ili hatua muafaka ziweze kuchukuliwa kwa
lengo la kuboresha dosari zinazojitokeza ili miradi inayopelekwa
katika jamii inasaidia e kuleta maendeleo yaliyokusudiwa na wananchi.
“Ni
wajibu wenu katika kuongeza uwajibikaji na uwazi katika usimamizi wa
matumizi ya rasilimali za umma , ili Serikali iweze kupata thamani ya
fedha zinazotumika na kuboresha huduma kwa jamii “ alisema Khijjah.
Aidha Katibu Mkuu huyo aliwaagiza kuwa wakaguzi hao wa ndani kujielimisha zaidi kwa kusoma miongozo mbalimbali ya ukaguzi wa ndani na namna ya kuweka kumbukumbu vizuri ili kufanya kazi ya ukaguzi katika viwango vinavyokubalika kitaifa na kimataifa.
Alisema
kuwa hatua hiyo itawasaidia kuwa watendaji wazuri na wanaotoa taarifa
zinazoonyesha ukweli halisi wa matumuzi ya fedha na rasilimali za
wananchi kwa ajili ya maendeleo yao na Taifa kwa ujumla.
Khijjah
alisema kuwa Serikali ilianzisha Idara ya Mkaguzi Mkuu wa Ndani wa
Serikali kupitia marekebisho ya Sheria ya Fedha Sura 348 yaliyopitishwa
na Bunge Juni ,2010 kwa lengo ya kuimarisha utendaji na uwajibikaji
katika udhibiti na usimamizi wa matumizi ya rasilimali za umma na
utawala bora.
Mkutano
Waziri
wa wizara ya Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia Prof. Makame Mbarawa
akiongea na waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam kuhusu
usitishwaji wa matangazo ya Televisheni kwa kutumia Technolojia ya
analogia na kuhamia teknolojia ya utangazaji ya dijitali ambao
utasitishwa rasmi tarehe 31 Disemba mwaka 2012 saa sita kamili usiku.
Kulia ni Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Dk. Frorens Turuka.
(Picha na Anna Itenda - Maelezo)
World
class football stars made the dreams of four lucky football fanatics
from across East Africa come true in the GUINNESS® FOOTBALL CHALLENGE™
Celebrity Finale last night and football icon Jay Jay Okocha showed why
he is ‘so good they named him twice’ as he helped his partner hit the
jackpot and win USD50K!
The
episode kicked off with the four footballing heroes, Jay Jay Okocha,
Marcel Desailly, Rigobert Song and Kalusha Bwalya, stepping out onto
the pitch to pick their team mate. The Tanzania nation waited with
baited breath to see which excited top scorer from the GUINNESS®
FOOTBALL CHALLENGE™ mobile phone game got partnered with each celebrity
footballer as they together took on the challenge to a life changing
some of money.
It
was Kenyan businessman James Nderitu from Nairobird who bagged
Nigerian football icon Jay Jay and together went on to win USD50K.
James has succeeded in business, succeeded in being partnering with a
world class hero and succeeded in winning the Celebrity Finale!
Speaking of his epic win, James said, “Winning makes me feel on top of
the world – the whole experience, starring in the show and meeting Jay
Jay – has been is a real dream come true.”
In
classic hero style, Jay Jay gallantly donated his share of the
winnings to the other three contestants in recognition of their
incredible efforts on the show, so they took each took home just over
USD8K .
Commenting
on his experience of taking part in the show, Jay Jay said: “It was an
incredible experience to be a part of, meeting the contestants, the
audience and the hosts. This episode was filled with everything -
drama, tears and laughter. Taking part you feel an amazing pressure,
something that I did not expect to feel out on the GUINNESS® FOOTBALL
CHALLENGE™ pitch. I am delighted that I came through for my team mate,
he put in a great performance too and hitting the final target on the
Guinness® Money Wall meant we secured a truly life changing amount of
money for him.”
Together
the duo saw off tough competition, so who are the other knowledgeable
football fans that are now the envy of football lovers across East
Africa?
- The top scorer from the East Africa region was ICT officer, George Otieno from Mombasa who was paired up with his dream football partner, former French international, Marcel Desailly
- Stepping up to represent Tanzania was bachelor of commerce and Liverpool FC fan, Hance Kimola from Kinondoni, Dar Es Salaam who was teamed up with his ultimate football hero, former Cameroonian international, Rigobert Song
- Back for a second time and ready to show off his knowledge on behalf of Uganda was radio journalist, Patrick Ogua from Arua, who was standing alongside Zambia’s great ever footballer, Kalusha Bwalya
All
four contestants battled the mobile phone game leader board and
demonstrated that they knew the offside rule from the free kick rule
and their Pele from their Ronaldo, but in this Celebrity Finale it was
the chance for their football heroes to take centre stage as they went
head-to-head on the physical challenges to see if they could get their
partners to the final round.
The
footballers were on fire throughout the episode with some incredible
displays of skill, some closely fought rounds and some extravagant
celebrations from former Cameroonian international Rigobert Song. But
it was James and Jay Jay who worked together to see off the other teams
and secure themselves the chance to take on the Guinness® Money Wall.
The
Guinness® Money Wall had defeated many teams throughout the series,
but the question on everyone’s lips was, would a member of Nigeria’s
‘Dream Team’ have the skill to beat the wall?
It
was a fantastic team effort for the duo with James correctly answering
all the questions and Jay Jay demonstrating some phenomenal skill as
he worked his way up the targets. The tension in the studio was
immense when they had one target left and just one final ball. And as
you would expect, Jay Jay delivered and hit the target when it counted,
securing the pair the jackpot and earning himself the honour of being
the first ever player on the show to hit target six!
Please remember to drink responsibly – 18+.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete na Waziri masuala ya Jumuiya ya Madola, Umoja wa Mataifa na Afrika na Mazingira ( Parliamentary Under Secretary responsible for Africa, United Nations, economic issues, conflict resolution, and climate change)
wa Uingereza Bw Hendry Bellingham wakishuhudia Waziri wa Mambo ya
nje na Ushirikiano wa Kimataifa Mh Bernad Membe akiweka saini sambamba
na Waziri wa Mambo ya Nje wa Uingereza William Hegue
kuhusu makubaliano kati ya nchi hizo mbili juu ya taratibu za
kukabadhiana watuhumiwa wa uharamia na mali zilizokamatwa katika
matukio ya uharamia katika bahari kuu leo February 23, 2012 Lancaster
House, London.
(PICHA NA IKULU)
Mchezaji
Ilunga (kushoto)wa Jamhuri ya Kiodemokrasia ya Congo akichuana vikali
na mchezaji Hussein Javu wa timu ya taifa ya Tanzania Taifa Stars wakati
wa mchezo wao wa kirafiki unaofanyika uwanja wa taifa jijini Dar es
salaam jioni hii.
Mchezo huo ulikuwa ni kwa ajili ya kujipima nguvu kabla ya mapambano ya
timu hizo kuwania kufuzu fainali za kombe la mataifa ya Afrika nchini
Afrika Kusini, ambapo Taifa Stars itakutana na Msumbiji na RDC Congo
itakutana na Sychelies, mpaka mpira unamalizika hakuna timu iliyopata
goli hivyo matokeo ya timu hizo mpaka mwisho yamekuwa 0-0 kwa timu zote.
Kocha
wa timu ya Taifa Stars Jan Paulsen akimuelekeza jambo Aggrey Morris
mchezaji wa timu hiyo kabla ya mchezo huo kuanza kwenye uwanja wa taifa.
Wachezaji wa Timu ya RDC Congo na Taifa Stars wakisalimiana kabla ya mchezo huo kuanza kwenye uwanja wa taifa.
Rais
Jakaya Mrisho Kikwete akiwasili Lancaster House jijini London jana
February 23, 2012 kijiunga na viongozi wa nchi mbalimbali katika mkutano
wa kujadili mstakabali wa nchi ya Somalia ambayo imekuwa katika
misukosuko kwa zaidi ya miaka 20 ambapo jumuiya ya kimatifa ikiongozwa
na Uingereza imepania kumaliza matatizo mbalimbali katika nchi hiyo
ikiwemo kutokuwa na serikali inayoeleweka, uharamia, ugaidi pamoja na
kujaribu kurudisha amani.
PICHA NA IKULU
MUIGIZAJI filamu
nyota nchini, Charles Magali maarufu kwa jina la Mzee Magali,
atachezesha mechi ya soka ya kuamua mbabe kati ya wasanii wa vichekesho
wa Dar es Salaam na Mwanza katika Uwanja wa CCM Kirumba.
Kwa mujibu wa mratibu wa mechi hiyo iliyoandaliwa na Kampuni ya Brayance
Promortes, Pearson Samwel, Mzee Magali amechaguliwa kuwa mwamuzi baada
ya kupendekezwa na wasanii wa pande zote.
“Mzee Magali amekuwa kivutio kikubwa kwa wasanii wa Mwanza na hata
nilipowaambia wachekeshaji wa luninga wa Dar es Salaam kwamba refarii
atakuwa msanii huyo, wamefurahi sana,” alisema Samwel.
Alisema kuwa nyota huyo wa filamu nchini amekubali kupuliza filimbi
katika mechi ya kumaliza ubishi juu ya wasanii gani wanaweza kusakata
soka kati ya wa Dar es Salaam na Mwanza ‘rock city’.
Samwel alisema kuwa viingilio katika mechi hiyo itakayochezwa Machi 3,
mwaka huu, vitakuwa sh. 5,000 katika jukwaa kuu na sh 2,000 mzunguko.
Mratibu huyo ameongeza kwamba, kampuni inayoratibu mechi hiyo ipo katika
mchakato wa kutafuta mgeni rasmi.
Wasanii kutoka Dar es Salaam watakaoshuka uwanjani ni Kingwendu, Sharo
Milionea, Mboto, Senga, Pembe, Bambo, Mtanga, Mau, Ringo na Chilly.
Wengine Defender, Zimwi, Muhogo Mchungu, Masele, Erick, Kiuno na Hawa,
ambao watawasili Mwanza mwishoni mwa mwezi huu kujiandaa kucheza na
wapinzani wao.
Timu ya wachekeshaji wa Mwanza inaundwa na Babu Mkombe,Sharobaro wa
Kihaya, Mchele, Chugu, Ngosha, Brother K, Mama Brandina, Msimbe wa
ukweli,Okech Okech, Kafuku Kaukananga, Mzee Dude, Itagata, Malapulapu,
Choko na Tengambili.
Wasanii wengine watakuwepo siku hiyo ni Tatu Mkate wa Arusha, Avodia
Tolu, Mrefu kwenda chini na Jully Tax, ambao wamepania kuwafunga
wachekeshaji wenzao wa Dar es Salaam.
Waziri
wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano Samia Suluhu Hassan akipata
Maelezo Kuhusu Upakuwaji wa Makontena katika Bandari ya Zanzibar kwa
Mkuu wa Mipango{ZPC]Ali Haji Haji wakati wa Ziara yake yakutembelea
Miradi ya Maendeleo, Kulia Kaimu Mkurugenzi wa Bandari Bw Msanifu Haji
Mussa na Maofisa wa Bandari ya Zanzibar[Picha na Ali Meja]
Waziri
wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Dkt. Emmanueli Nchimbi (kulia)
akizungumza na Rais wa Kituo cha Utamaduni na Uhusiano wa Kiislam
kutoka nchini Iran Dkt. Mohammed Basheir Khurrqmshad (kushoto) mara
baada ya kuwasili katika Ofisi za Wizara hiyo leo jijini Dar es
salaam. Pamoja na mambo mengine Rais huyo ameahidi kuendeleza
ushirikiano kati ya Tanzania na Iran katika sekta ya utamaduni na
michezo ikiwemo kusaidia kuleta makocha wa mchezo wa riadha.
(PICHA NA ARON MSIGWA WA MAELEZO)
Benjamin Sawe na Ismail Ngayonga
Kitengo cha Habari
WHVUM.
Waziri wa Habari,Vijana,Utamaduni na Michezo Dk. Emmanuel John Nchimbi ameishukuru Jamhuri
ya Kiislamu ya Iran kwa kuanza utekelezaji wa kupatiwa kocha wa mchezo
wa riadha ikiwa ni mkataba wa ushirikiano baina ya nchi hizo mbili.
Dk. Nchimbi aliyasema hayo (leo) alipokutana na Waziri wa Utamaduni na Muongozo wa Kiislamu wa Iran Dk.Mohammad Bagher Khurramshad jijini
Dar es Salaam ambapo alisema hatua hiyo ni moja ya utekelezaji wa
mkataba wa ushirikiano kati ya Serikali ya Tanzania na Iran.
Alisema
nchi ya Iran imekuwa ni moja kati ya nchi yenye makocha bora na wenye
uzoefu katika mchezo wa riadha kwa miaka mingi na kusema ni wakati
muafaka kuichangamkia ofa hiyo.
“Nchi
ya Iran ina makocha bora wa mchezo wa mbio za riadha sasa ni wakati
muafaka kwa Chama cha Mchezo wa Riadha kuichangamkia ofa hii ili mchezo
huu uweze kuiweka nchi katika ramani ya michezo duniani’’.Alisema Dr.
Nchimbi.
Kwa Upande wake Waziri wa Utamaduni na Muongozo wa Kiislamu wa Iran Dk. Khurramshad
alisema Iran itaendelea kuisaidia Tanzania katika sekta ya
Michezo,Utamaduni na Sanaa ikiwa ni kuboresha uhusiano baina ya nchi
hizo mbili.
“Huu
ni mwanzo tu wa makubaliano ya mkataba lakini tutaendelea kuisaidia
Tanzania katika sekta za utamaduni na sanaa kama tulivyokubaliana katika
mkataba baina yetu”.Alisema Dr.Khurramshad
Serikali
ya Tanzania na Jamhuri ya Kiislam ya Iran mwezi uliopita zilitiliana
saini mkataba wa ushirikiano katika sekta za Utamaduni na Sanaa ambapo
kwa upande wa Serikali ya Tanzania iliwakilishwa na Waziri wa
Habari,Vijana,Utamaduni na Michezo Dr. Emmanuel Nchimbi na upande wa
Jamhuri ya Kiislam ya Iran iliwakilishwa na Waziri wa Utamaduni na Muongozo wa Kiislamu Dk.Khurramshad.
Katika
mkataba huo uliosainiwa Jijini Tehran moja kati ya makubaliano ni
pamoja na ushirikiano katika sekta ya Utamaduni na Sanaa ambapo Serikali
ya Tanzania iliombwa na ilikubali kuandaa Wiki ya Utamaduni wa Tanzania
nchini Iran.
Wizara ya Maliasili na Utalii inatoa taarifa kuwa Tanzania itakuwa mwenyeji wa Kongamano la Kwanza la Africa kuhusu Uendeshaji, Changamoto na Fursa katika Uhifadhi wa Mbuga za Wanyamapori na Maeneo yaliyohifadhiwa (The 1st Pan-African Conference on Sustainable Tourism Management In National Parks and Protected Areas: Challenges and Opportunities).
Kongamano
hilo la siku Tano limepangwa kufanyika katika Kituo ya cha Kimataifa
cha Mikutano cha Arusha (AICC) tarehe 15 hadi 19 Oktoba 2012. Washiriki
wapatao 300 kutoka nchi mbalimbali wanatarajia kuhudhuria.
Tanzania
imeteuliwa kuwa mwenyeji wa Kongamano hilo na Shirika la Umoja wa
Mataifa la Utalii Duniani (UNWTO) kufuatia mkutano wake (UNWTO General Assembly) ambao ulifanyika nchini Korea 2011. Katika Mkutano huo Tanzania pia ilichaguliwa kuwa mjumbe katika Baraza la Utendaji (Executive Council) la Shirika hilo, nafasi ambayo itakuwa nayo hadi mwaka 2015.
Kongamano hilo la Oktoba 2012 ni la kwanza na la aina yake litawakuwakutanisha wahifadhi na wadau wa sekta ya Utalii ili wajadili namna ya kufanikisha uhifadhi na utalii duniani.
Tanzania imepata fursa ya kuwa mwenyeji wa Kongamano hilo kutokanana
na sifa nzuri na uzoefu ilio nao katika kuanzisha na kuendeleza hifadhi
za Taifa.
Tanzania inategemea kupata manufaa
kutokana na Kongamano hilo kwani washiriki watapata fursa ya
kutembelea vivutio vya utalii vilivyoko nchini na hivyo kuvitangaza
warudipo makwao. Pia watanzania watapata fursa ya kuuza huduma
mbalimbali kwa wageni watakaohudhuria Kongamano hilo, kama vile malazi,
chakula, burudani na usafiri.
Faida nyingine ni kuwa, washiriki kutoka Tanzania watapata fursa ya kubadilishana ujuzi na ueledi na wenzao watakaotoka nchi mbalimbali duniani.
Wizara
inatoa wito kwa wanachi, wafanyabiashara na wadau wote kujiandaa
ipasavyo ili kunufaika na ujio huo wa Kongamano hilo la kimataifa
nchini.
Taarifa mbalimbali zitaendelea kutolewa kuhusu maendeleo ya maandalizi ya Kongamano hilo.
George Matiko
MSEMAJI
WIZARA YA MALIASILI NA UTALII
Uzinduzi
wa kumbu kumbu ya mwanzilishi wa skauti Ulimwenguni bw Robert Baden
PowelL na mkewe Bi. Oliva Powell(lady baden powell)kimkoa umefanyika leo
na kilele ni siku ya tar.25 ya mwenzi huu kwenye viwanja vya sheikh
Amri Abeid jijini hapa kwa maonyesho na matamasha kote nchini.
Hayo
yamesemwa nakamishina mkufunzi mkuu wa taifa bi Margareth Olumbe
wakati akisoma risala ya maskauti wa kike hapa Arusha na kusema kuwa
girl guide hapa nchini ilanzishwa mnamo mwaka 1928 na girl guide 9 na
walijiita 1st Kilimanjaro na walikuwa na uhusiano na mke wa
gavana wa wakati huo ukaingia ukimya wa muda mrefu na guiding
haikusikika hadi 1934 mke wa gavana Lady Mack alianzisha kampuni
nyingine Dar es-salaam na ikaitwa 1st Dar –es-salaam kampuni na ilikuwa na wazungu tu baadae alianzisha first dar-es-salaam Brownes na ilkuwa mchanganyiko.
Kuna
changamoto nyIngi kubwa zinazowakabili girl guide hapa mkoani na taifa
kwa ujumla zikiwemo kuwatoa watoto katika tabia hatarishi kuwa raia
wema,wazazi ambao wangesaidiana nasi wamekuwa na shughuli nyingi na
wengine hawafikiki hata na watoto wao,mwitiko wa wananchi
Akatoa
ombi kwa mgeni rasmi ambaye alimwakilisha mlezi wa skauti wa kike hapa
nchini mama Salma Kikwete bi Pendo Laizer kutoka(CASEC) kuwa awe mlezi
wa girl guide wa arusha na mgeni huyo kukubali kuwa mlezi na
kuwatafutia wafadhli wakukisaidia girl guide mgeni huyo aliambatana na
mgeni kutoka nchini uingereza bi jill Nicholson na Yona .M.Mziba kutoka
kitengo cha polisi jamii mkoani hapa
Na Gladness Mushi - Arusha
Tanzania
inajipanga vizuri kutekeleza sera ya makuzi na malezi ya awali ya
mtoto wa kitanzania katika kutoa elimu ya awali hapa nchini na kuwa
kila shule itatakiwa kuwa na shule ya awali kwani maandalizi tayari
yalikwishaanza kwa walimu wa cheti kuwa ndio wafundishaji wa elimu
hiyo.
Kauli hiyo imetolewa na waziri wa elimu na mafunzo ya ufundi stadi Dr.Shukuru Kawambwa wakati akiongea na vyombo vya habari katika
jukwaa la kwanza la kitaifa linalo jadili utungwaji sera ya makuzi na
malezi ya awali ya mtoto jukwaa hilo lililo andaliwa na banki ya dunia
kupitia shirika la bennian la marekani inayofanyika jijini hapa.
Dr.kawambwa
alisema kuwa kuangalia sera za maendeleo ya awali ya mtoto ni jambo
ambalo serekali inajipanga nalo na kuwa inalipa umuhimu mkubwa ndiyo
maana umeona mawaziri mbali mbali kutoka wizara za Elimu,Fedha,ofisi
yawazirimkuu(Tamisemi),Afya na Maendeleo ya jamii jinsia na watoto na
kuwa sera ya makuzi na malezi ni tofauti na sera nanipana zaidi kuliko
sera ya elimu ilyopo hapa nchini kwa sasa.
'Unapoanza kuwekeza katika
kuandaa sera na mafunzo ya awali kwa mtoto inamaana kuwa unamjali na
kumthamini na kugundua vipaji vya watoto na huko ndiyo kujenga msingi wa
awali wa mtoto ili anapoanza elimu ya msngi teyari anakuwa na msingi
imara'.alisema Kawambwa
Alisema
kuwa serekali njia iliyosawa hawajapotea kwani elimu ya kiwango cha
chini inatolewa japo haikuwa inapewa kipaumbele lakini sasa tunaangalia
uwezekano wakuanza kutoa chakula kwa shule zetu zote japo si kwa mwaka
huu na hii inatokana na ukosefu wa fedha na akalishukuru shirika la
chakula ulimwenguni (WFP)kwa kutoa chukula kwa baadhi ya shule za jamii
za kifugaji hapa nchini na mafaniko meyaona kwani shule hizo viwango
vimepanda.
No comments:
Post a Comment