MANISPAA ya Kinondoni
imeahidi kuongeza nguvu katika kushughulikia masula ya migogoro ya
ardhi , huku pia ikiwataka wananchi kutoa ushirikiano wao katika
mapambano dhidi ya watu wote wanaokwenda kinyume na utaratibu uliopo.Akizungumza
na jiji Dar es Salaam jana, Mkurugenzi wa Manispaa hiyo, Fortunatus
Fwema alisisitiza kuwa katika kukabiliana na migogoro hiyo, uongozi wa
manispaa umekuwa ukichukua hatua za haraka kuhakikisha viongozi na
watendaji wanaojihusisha na migogoro na kashfa za ardhi wanachukuliwa
hatua mara moja.
Alisema katika kuishughulikia
migogoro hiyo, manispaa imekuwa ikiendelea kuyafanyia kazi mapendekezo
ya Kamati ya migogoro ya ardhi iliyoundwa kwa maelekezo ya Rais, hatua
aliyosema kuwa kwa kiasi kikubwa imeweza kuleta mafanikio.
“Hadi sasa migogoro iliyokuwepo
imeshughulikiwa kwa asimilia 95 na kupatiwa ufumbuzi, kwa sasa migogoro
iliyopo ni ile inayotokana na uvamizi wa ardhi unaofanywa na makundi ya
watu kinyjme na sheria ambayo manispaa kwa kushirikiana na Serikali kuu
imeendelea kuipatia ufumbuzi” alisema Fwema.
Aidha alisema kumekuwa na mawazo
potofu ya baadhi ya watu kwamba manispaa hiyo imekuwa ikifanya
upendeleo kwa wakubwa wakati wa uuzaji wa viwanja vyake, madai aliyosema
kuwa si ya kweli na zaidi yamelenga kuichafua manispaa hiyo.
“Madai haya si ya kweli
ikizingatiwa kuwa katika kipindi kinachokaribia miaka 10 manispaa ya
Kinondoni haijawahi kupima viwanja na kuviuza kwa wananchi kutokana na
changamoto mbalimbali hasa zinazohusiana na utwaaji wa ardhi na ukosefu
wa fedha kwa ajili ya kugharamia fidia na upimaji” alisema Fwema.
Alisema manispaa kwa muda mrefu
imekuwa ikihangaika kutafuta fedha za kupimia viwanja kutoka sehemu
mbalimbali zikiwemo taasisi za fedha na madhumuni ni kuvipima viwanja
hivyo ili kukabiliana na ongezeko la ujenzi holela katika maeneo
yasiyopangwa.
Kuhusu utoaji wa vibali vya ujenzi
na kushughulikia maombi ya kubadili matumizi ya ardhi, Fwema alisema
manispaa hiyo kwa kutumia wataalam wake, kabla ya kutoa vibali hivyo
wameweka utaratibu wa kuhakikisha maombi yaliyotolewa, hayakinzani na
matumizi yaliyopo na yaliyoidhinishwa katika mpango wa matumizi ya
ardhi.
No comments:
Post a Comment