Na Maelezo Zanzibar
Sherehe za miaka 49 ya Mapinduzi
ya Zanzibar zinaanza rasmi kesho kwa kazi za kufanya usafi wa mazingira
katika Wilaya zote za Unguja na Pemba.
Kwa mujibu wa Ratiba iliyotolewa na Kamati ya Sherehe na maadhimisho ya kitaifa imeonesha kuwa Miradi ipatayo 62 inatarajiwa kuzinduliwa katika Visiwa vya Unguja na Pemba.
Kwa mujibu wa Ratiba iliyotolewa na Kamati ya Sherehe na maadhimisho ya kitaifa imeonesha kuwa Miradi ipatayo 62 inatarajiwa kuzinduliwa katika Visiwa vya Unguja na Pemba.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania Dkt. Jakaya Kikwete atafungua Skuli mpya ya Sekondari ya
Mlimani, iliyopo Matemwe Mkoa wa Kaskazini Unguja ikiwa ni Shamra shamra
za Sherehe hizo.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa
Baraza la Mapinduzi Dkt.Ali Mohamed Shein naye atazindua miradi
mbalimbali ikiwemo Ufunguzi wa Jengo la Chuo cha Utawala wa Umma huko
Tunguu Wilaya ya Kati Unguja.
Pia atafungua mradi wa
E-Government katika Wilaya ya Magharibi Unguja na kufungua Skuli mpya ya
Sekondari ya Umoja, iliyopo Uzini Wilaya ya Kati Unguja pamoja na
kuzindua Barabara kutoka Mfenesini hadi Bumbwini Wilaya ya Kaskazini B
Unguja.
Hali kadhalika Dkt.Shein
atafungua Mradi wa kuhama kutoka Teknolojia ya Analojia kwenda Dijitali
na Ufunguzi wa Studio ya kurikodia Sanaa na Muziki ambapo kwa upande wa
Pemba atafungua Skuli mpya ya Sekondari ya Shamiani iliyopo Chake Chake Mkoa wa Kusini Pemba.
Mbali na Shughuli hizo siku ya
kilele hapo January 12 kwenye Uwanja wa Amani Rais Shein atakagua
Gwaride lililoandaliwa na Vikosi vya ulinzi na usalama na Vikosi vya SMZ
pamoja na kulihutubia Taifa na Usiku kuhudhuria Taarab rasmi huko
katika Ukumbi wa Salama Hoteli ya Bwawani
Naye Makamo wa Kwanza wa Rais
Maalim Seif Shariff Hamad atafanya uzinduzi mbali mbali kwa ufunguzi wa
Skuli na Maabara wakati Makamo wa Pili wa Rais Balozi Seif Idd atafanya
Shughuli kama hizo kwa ufunguzi wa Skuli na Majengo mapya ya nyumba za
Wazee zilizopo Sebleni Wilaya ya Mjini Unguja.
Mbali na shughuli hizo baadhi ya
Marais wastaafu,Mawaziri mbali mbali wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar
na Muungano watafanya shughuli za ufunguzi wa Miradi mingine ikiwemo ya
Maji, Skuli na Mradi wa Mnara wa Radio wa Masafa ya Kati uliopo Bungi
Wilaya ya Kati Unguja.
No comments:
Post a Comment