Wapendwa ndugu,jamaa na marafiki
popote pale mlipo,yamebaki masaa kadhaa kuuaga mwaka 2012,ambao kwa
hakika ulikuwa na changamoto nyingi za kimaisha,dhoruba za hapa na pale
wengi zilitukumba,lakini kwa kudra za Mwenyezi Mungu akatushika mkono
akatuinua na maisha yakaendelea.
Binafsi
mpaka dakika hii namshukuru Mungu nikiwa mwenye afya njema
kabisa.Maisha ya sasa Wanadamu wengi wamekuwa dhaifu kwa mambo
mengi,lakini Mungu ndiyo njia sahihi wa kumtumia katika sala zako
kuyashinda majaribu na madhaifu ya Dunia.Yako mengi ambayo naweza
nikayaandika hapa lakini bado yasitoshe pia.Nasema asanteni kwa
ushirikiano wenu mkubwa kwa namna moja ama nyingine,kama kuna mahali
nilikosea,tukakwaruzana kidogo basi “NAFSI NI NYONGE” Tusameheane na
maisha yaendelee.
Tunahamia
mwaka mwingine mpya kabisa 2013,basi na tuendelee na ushirikiano huu
tuliokuwa nao kwa mambo mbalimbali yenye kujenga na kuleta tija katika
maisha yetu,Mwaka 2013 uwe wa kuhakikisha kweli sote pia tumehamia
kwenye mfumo wa kidijitali,tushauriane,tuelemishane tunyooshane njia
iliyo sahihi ili kila mmoja kila wakati abaki nafsini mwake mwenye
furaha daima,Pia tumtangulize Mungu kila wakati kwa kila jambo ili pia
azidi kuzibariki kazi za mikono yetu daima.
Kwa
Blogaz wenzangu,changamoto nyingi tumekumbana nazo 2012,ikiwemo tatizo
kuu la KUKOPY NA KUPASTE.! Na nyinginezo nyingi tuzijuazo zinatusumbua
kwa namna moja ama nyingine,basi ni nyema 2013 iwe ya kuzitafutia
ufumbuzi,kama si kuzimaliza kabisa basi angalau tuendelee kuzipunguza
ili kuzimaliza kabisa,huku suala la kujituma na ubunifu vikiwa ndio ngao
kuu ya mabadiliko miongoni mwetu.Ushirikiano tuliokuwa nao umeonesha
tuna uwezo mkubwa wa kuisadia jamii inayotuzunguka na hata serikali pia
kwa namna moja ama nyingi,basi tusimame kidete kuhakikisha ushirikiano
huu hauteteleki ama haupotei kirahisi,badala yake tuiimarishe zaidi kila
kona .
Natoa
shukurani za dhati kabisa kwa makampuni na wadau mbalimbali
ambayo/ambao kiukweli yametoa mchango mkubwa kuhakikisha tunasonga mbele
na libeneke hili ,si vibaya nikiyataja makampuni hayo kuwa ni Serengeti
Breweries Ltd,Airtel,Bayport,Msama Promotions Ltd,kampuni ya
R&R,Dada Teddy Mapunda,Hoyce Temu,Blogaz wote (bila kinyongo) na
wengine waliotupa hatua ya kusogea kwa namna moja ama nyingine,Mungu
awabariki sana.
Asanteni
Nawatakia heri ya sikukuu ya Mwaka mpya.
No comments:
Post a Comment