|
Wakala
wa Vipimo (WMA), Mkoa wa Arusha unatarajia kuanza kufanya msako wa
mizani zisizokuwa na ubora katika maduka ya mkoani Arusha zinazodaiwa
kutumika kuwapunja wananchi.
Meneja wa WMA wa mkoa huo, Dunford Manzi amesema leo kuwa mizani hizo zinadaiwa kutengenezwa nchini India na China.
Amesema kabla ya kuanza msako huo, watatoa elimu kwa wananchi na wafanyabiashara kuhusu umuhimu wa kutumia mizani zenye ubora.
Pia, amewataka wafanyabiashara wabadilishe mizani hizo na kuweka halisi kabla ya kuchukuliwa hatua za kisheria.
“Sheria
ya Vipimo Sura 340 (19) inatutaka tufanye ukaguzi wa mara moja kwa
mwaka, katika kipindi cha mwezi mmoja tulikagua mizani na mashine kwenye
vituo vya mafuta tumebaini mizani zilizopo sokoni hazina ubora
zinapaswa kuondolewa.
Amewataka
wafanyabiashara kuitumia ofisi ya WMA kupata ushauri wa vipimo sahihi
ili kuepuka kuwapa hasara wateja wao.Pia, amewataka wateja kukagua
mizani kabla ya kununua bidhaa ili kujiridhisha na kuepuka kuibiwa.
Mkazi
wa Kwamrombo, Zaidi Jonathani amesema wafanyabiashara wengi wanatumia
mizani iliyorekebishwa kwa lengo la kujipatia faida kubwa isivyo halali
kwani unaweza kupima bidhaa moja kwenye mizani mbili na ikakupa vipimo
tofauti. “Wafanyabiashara wanakuwa na mizani halisi na iliyofanyiwa
ujanja, lengo lao wakija watu wa vipimo wanaonyesha iliyokaguliwa,”
amesema.
Muuza
nyama katika Soko la Kilombero, Loishiye Mollel amesema mizani yake
hukaguliwa mara mara huku akiwaondoa hofu watu wanaodhani wanapunjwa.
MWANANCHI
|
Waziri
wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Prof. Makame Mbarawa ametoa mwezi
mmoja kwa makandarasi wote nchini kuhakikisha wanasaini mikataba ya
ajira na wafanyakazi katika miradi ya ujenzi wa barabara inayoendelea
nchini kote.
Akizungumza
jijini Arusha mara baada ya kufanya ukaguzi wa mradi wa ujenzi wa
barabara ya Sakina-Tengeru yenye urefu wa Km 14.1 na barabara ya mchepuo
ya kusini (Arusha bypass) yenye urefu wa Km 42.4, Prof. Mbarawa amesema
mkandarasi atakayeshindwa kutoa mikataba kwa mujibu wa sheria za
Tanzania, atanyang’anywa kazi ya ujenzi kwa kuvunja sheria.
“Barabara
zinajengwa kwa kodi za wananchi hivyo wajenzi wa barabara nao ni lazima
wafuate sheria za nchi ili kuhakikisha Serikali inapata kodi stahili na
wafanyakazi wazawa nao wanapata haki stahili kwa mujibu wa ajira zao",
amesema Waziri Prof. Mbarawa.
Amezitaka
taasisi za TRA, NSSF na nyingine zinazosimamia ajira za wafanyakazi
kufuatilia miradi ya ujenzi ili kuona fursa za mapato ambazo serikali
inaweza kupata na kusajili wafanyakazi katika hifadhi ya mifuko ya
jamii.
Waziri
Prof. Mbarawa amewataka mameneja wa tanroads na maafisa kazi kukagua
mikataba ya ajira za ujenzi katika maeneo yao ili kuona haki inatendeka
kwa makandarasi na kwa wafanyakazi ili ujenzi wa barabara ukamilika kwa
wakati na kwa ubora unaotakiwa.
Katika
hatua nyingine Prof. Mbarawa amefungua mkutano wa Sita wa Baraza la
Wafanyakazi la Wakala wa Barabara nchini (TANROADS) na kuwataka kuweka
mikakati itakayowezesha kulinda hifadhi ya barabara, kudhibiti magari
yanayozidisha uzito na kusimamia kasi katika miradi ya ujenzi wa
barabara.
“Mmekua
mkifanya kazi nzuri, endeleeni kufanya kazi kwa uadilifu, uwazi, weledi
na kujiwekea malengo ya kujipima mwaka hadi mwaka ili muendelee kuwa
tassisi ambayo watu watakuja kujifunza kwenu”, amesisitiza Waziri Prof.
Mbarawa.
Naye
Mtendaji Mkuu wa TANROADS Eng. Patrick Mfugale amemhakikishia Waziri
Mbarawa kuwa TANROADS imejipanga kuhakikisha miradi ipatayo 90 ya ujenzi
wa barabara inayoendelea nchini kote inakamilika katika ubora
unaotakiwa na unao uwiana na thamani ya fedha.
Aidha,
Waziri Prof. Mbarawa amemuagiza Meneja wa Wakala wa Majengo nchini
(TBA), mkoa wa Arusha, Bw. Victor Baltazar kukusanya madeni yote kwa
haraka ili kukamilisha miradi ya ujenzi wa nyumba za wafanyakazi na za
biashara inayosimamiwa na Wakala huo mjini Arusha kukamilika kwa wakati.
Prof.
Mbarawa ambaye yuko katika ziara ya mikoa ya kanda ya kaskazini
amezitaka taasisi zilizo chini wa wizara hiyo kuhakikisha zinafanya kazi
kibiashara ili kuboresha mapato ya Serikali na hivyo kuiwezesha
Serikali kutoa huduma bora kwa wananchi.
|
Wiki
iliopita, mnamo tarehe 16 Februari, 2016, aliyekuwa mjumbe wa Timu ya
Kampeni ya Chama Cha Wananchi (CUF), Ndugu Mohamed Ahmed Sultan
Al-Mugheiry (maarufu kwa jina la Eddy Riyami), alipokea barua ya wito
kutoka kwa Jeshi la Polisi Zanzibar ikimtaka kufika Makao Makuu ya
Polisi, Ziwani, Zanzibar siku inayofuata, yaani tarehe 17 Februari,
2016, saa 2 asubuhi kwa kile kilichoelezwa kwamba “kuna mambo muhimu
yanayomhusu” ambayo walitaka kuzungumza naye.
Bila
ya kukosa, Eddy Riyami aliitikia wito huo na kufika Makao Makuu ya
Polisi, Zanzibar na kuonana na SSP Simon S. Pasua wa Idara ya Upelelezi
wa Makosa ya Jinai (CID). Hata hivyo, hakuhojiwa na badala yake alipewa
simu na kutakiwa azungumze na Naibu Mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya
Jinai, Bw. Salum Msangi ambaye alimwambia arudi tena Jumatatu, tarehe
22 Februari, 2016.
Eddy
Riyami, akiwa raia mwema, alirudi tena jana kama alivyoagizwa.
Alipofika hapo alihojiwa na Polisi na baadaye mwanasheria aliyefuatana
naye akatakiwa kutafuta wadhamini wawili watakaomdhamini hadi
atakapoitwa tena. Wakati mwanasheria wake aliporudi na wadhamini,
akaelezwa kwamba Polisi imebadili uamuzi wake na imeamua kumuweka ndani
hadi leo, tarehe 23 Februari, 2016. Mwanasheria na familia yake
wakatakiwa kwenda tena Makao Makuu ya Polisi hiyo leo, saa 3 asubuhi.
Walipofika leo asubuhi, wakaambiwa kwamba DCI kaacha maagizo kuwa suala
la Eddy Riyami liachwe kwanza na wao warudi tena saa 6 mchana.
Hadi
tunapotoa taarifa hii, hakujapatikana maelezo yoyote ya msingi juu ya
kinachoendelea na wala Eddy Riyami hajafikishwa Mahkamani kusomewa
mashtaka yoyote.
La
ajabu zaidi, ni kwamba hata mke wake alipofika kituo cha polisi cha
Madema anakoshikiliwa kwa ajili ya kwenda kumuona, hakuruhusiwa kumuona.
Kutokana
na mwenendo huu, Chama Cha Wananchi (CUF) kinalichukulia suala hili
kwamba ni mwendelezo wa vitendo vya unyanyasaji wa kisiasa dhidi ya
wapinzani wa CCM, vitendo ambavyo tunaamini vinafanywa kwa shinikizo la
wanasiasa.
Itakumbukwa
kwamba kwa muda mrefu tokea wakati wa kampeni za uchaguzi mkuu wa
Oktoba 25, 2015 tumekuwa tukitoa tahadhari za kuwepo mipango ya
kuwakamata viongozi wa CUF na wanaharakati wengine ili kufanikisha
malengo ya kisiasa ya Chama Cha Mapinduzi (CCM). Tuna kila sababu ya
kuamini kwamba hatua ya kumkamata Eddy Riyami na kumuweka ndani bila ya
kumfikisha Mahkamani ni utekelezaji wa mipango hiyo. La si hivyo, ikiwa
Eddy Riyami ametenda kosa basi angelishafikishwa Mahkamani ndani ya muda
wa saa 24 tokea kukamatwa kama sheria inavyotaka.
Chama
Cha Wananchi (CUF) kinalitaka Jeshi la Polisi kuacha kutumiwa na
kutumika kisiasa kufanikisha malengo ya kisiasa ya CCM. Tunashangazwa
kwamba siku zote wanaoitwa kuhojiwa, kukamatwa na kuwekwa ndani ni
wanasiasa wa vyama vya upinzani na wanaharakati wengine lakini
hatujawahi kushuhudia viongozi wa CCM kuitwa kuhojiwa, kukamatwa na
kuwekwa ndani. CUF imetoa taarifa kadhaa kwa Jeshi la Polisi zinazohusu
matamshi na vitendo vya viongozi wa CCM vyenye mwelekeo wa uhalifu
lakini hakuna hatua zozote zilizochukuliwa. Hizo ni dalili za waziwazi
za Polisi kutumiwa na kukubali kutumika kisiasa.
Tunalitaka
Jeshi la Polisi iwapo kweli lina kesi dhidi ya Eddy Riyami basi
limfikishe Mahkamani haraka ili hatua za kisheria zifuate mkondo wake.
Na iwapo hawana kesi, basi wamwachie huru mara moja.
Umefika
wakati wa Jeshi la Polisi kufanya kazi zake kitaalamu kama sheria na
kanuni zao zinavyoagiza badala ya kuwatumikia wanasiasa wa CCM.
HAKI SAWA KWA WOTE
HAMAD MASOUD HAMAD
KAIMU MKURUGENZI WA HABARI NA MAWASILIANO NA UMMA - CUF
|
Wanahabari
na Watafiti kutoka Tume ya Taifa ya Sayansi na Teknolojia (Costech),
waliokuwa katika ziara ya kuzungumza na wakulima wa mkoa wa Mwanza
kuhusu changamoto za kulimo zinazo wakabili pamoja na matumizi ya
bioteknolojia katika kilimo wakiwa mbele ya kaburi la Baba wa Taifa
Mwalimu Julius Kambarage Nyerere walipozuru kaburi hilo hivi karibuni
Kijiji cha Mwitongo Butiama mkoani Mara.
Mtafiti
Kiongozi wa Tume ya Taifa ya Sayansi na Teknnolojia (Costech),
Dk.Nicholaus Nyange (kushoto), na Mtafiti Mkuu wa Jukwaa la
Bioteknolojia Tanzania (OFAB), Dk.Emmarold Mneney wakiwa wamesimama
ilipo sanamu ya Hayati Baba wa Taifa Mwalimu Julius Nyerere.
Hapa ni picha ya pamoja katika sanamu ya Baba wa Taifa.
Mwendeshaji wa mtandao wa www. habari za jamii.com Dotto Mwaibale akivinjari katika moja ya jengo katika makazi ya Baba wa Taifa.
Matembezi yakiendelea katika makazi ya Baba wa Taifa.
Mratibu Mkuu wa Jukwaa la Bioteknolojia Afrika, Daniel Otunge (kushoto) Mtafiti
Kiongozi wa Tume ya Taifa ya Sayansi na Teknnolojia (Costech),
Dk.Nicholaus Nyange (katikati), na Mtafiti Mkuu wa Jukwaa la
Bioteknolojia Tanzania (OFAB), Dk.Emmarold Mneney wakiwa wamekaa katika kibanda alichokuwa akipenda kupumzika Hayati Nyerere wakati wa
uhai wake.
Jamii
inayofanya shughuli mbalimbali nyumbani kwa Baba wa Taifa Hayati
Mwalimu Julius Nyerere wakionesha upendo kwa kunywa chai pamoja katika
makazi ya Mwalimu Nyerere yaliyopo Kijiji cha Mwitongo, wilayani
Butiama mkoani Mara kama walivyonaswa na kamera yetu katika ziara hiyo.
Picha ya pamoja katika nyumba maalumu lilipo kaburi na Mwalimu Nyerere.
Dereva
wa Msafara huo, Mr Stanley akiwa mbele ya gari na mtafiti Kutoka Kituo
cha Utafiti cha Ukiriguru cha jijini Mwanza, Isabela Msuya.
Mwendeshaji wa mtandao wa www. habari za jamii.com Dotto Mwaibale akiweka maua kwenye kaburi la Baba wa Taifa.
|
Na Chalila Kibuda,Globu ya Jamii.
MKAZI
wa Mafinga, David Isack ( 32) alivamiwa na majambazi na kuporwa
sh.milioni 12 ambazo alikuwa akipeleka katika Benki ya DTB, ambapo
alivamiwa na watu watano wanatuhumiwa kuwa ni majambazi wakiwa na
usafiri wa pikipiki mbili aina ya boxer.
Akizungumza
na waandishi wa habari ijini Dar es Salaam leo, Kamanda wa Polisi Kanda
Maalum ya Dar es Salaam, Kamishina Simon Sirro amesema kuwa tukio hilo
lilitokea Februari 12 mwaka huu katika eneo la Uwanja Ndege , katika
kurupushani za kutaka kuchukua fedha hizo walitokea askari na
kuwazingira na kisha kuanza kukimbia na kuweza kudondosha bunduki aina
ya SMG pamoja na risasi 24 ambazo zilitakiwa kutumika katika tukio hilo.
Amesema
askari walipowakamata wananchi walikusanyika katika tukio hilo na
kuanza kuwapiga watu wanaodaiwa kuwa majambazi mpaka kupoteza maisha
kutokana kushambuliwa huko na wengine watatu waliweza kukimbia na kiasi
hicho cha fedha.
Kamishna
Sirro amesema Isac alikuwa akitokea benki ya NMB na kwenda kupeleka
fedha hizo katika benki ya DTB iliyopo Quality Plaza.
Katika
operesheni nyingine imefanikiwa kukamata bastola moja ambayo
ilipatikana Februari 19 mwaka huu maeneo ya Kiwalani Kwa Gude kutokana
na polisi kupata taarifa juu ya watu kujificha katika kichaka kwa ajili
ya kufanya uhalifu na baada ya kugundua polisi wapo eneo hilo
walikimbia na kuacha silaha hiyo na jeshi la polisi linafanyia kazi
mmiliki wa silaha.
Hata
hivyo Jedhi la Polisi Kanda Maalumu linawashikilia watu wane wanaodaiwa
kuwa ni majambazi sugu waliowakamata eneo la Buguruni kwa Mnyamani
ambao ni Mohamed Hassan maarufu kwa jina Kidali (21)Mkazi wa Vingunguti
Speco,Hamis Alli (20) Mkazi wa Buguruni kwa Mnyamani, Adam Salum (23)
Mkazi wa Buguruni kwa Madenge, Bakari Hamis (19) Mkazi wa Buguruni.
Aidha
amesema katika taarifa usalama Barabarani wameweza kukusanya zaidi ya
Sh. Bilioni moja ya ni fedha iliyotokana na makosa ya magari kuanzia
Januari 02 hadi Februari 22 mwaka huu.
CHANZO: MICHUZI BLOG |
Waziri
wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Charles Kitwanga (kushoto meza kuu), Naibu
Waziri wa Wizara hiyo, Injinia Hamad Masauni (kulia meza kuu) wakifurahi
jambo pamoja na Watendaji Wakuu wa Idara ya Uhamiaji (kushoto) na Wakuu
wa Idara wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi (kulia), wakati wa kikao
cha kujadili masuala mbalimbali ya utendaji kazi ndani ya Idara hiyo na
Wizara kiujumla. Kikao hicho kilifanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa
Wizara hiyo, jijini Dar es Salaam leo. Wakwanza upande wa kulia ni Naibu
Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Balozi Simba Yahya, na wakwanza upande wa
kushoto ni Kaimu Kamishna wa Uhamiaji, Victoria Lembeli. Picha zote na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
Waziri
wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhe. Charles Kitwanga ameagiza yafanywe
mabadiliko makubwa katika Vitengo mbalimbali vya Idara ya Uhamiaji ili
kuboresha huduma na kuimarisha uadilifu katika Vitengo hivyo.
Mheshimiwa
Kitwanga ametoa maagizo hayo leo wakati alipofanya kikao na Viongozi wa
Idara ya Uhamiaji ambapo pia kilihudhuriwa na Viongozi wa Wizara ya
Mambo ya Ndani ya Nchi, wakiwemo Wakuu wa Idara na Vitengo vya Wizara.
Kikao hicho kilifanyika katika Makao Makuu ya Wizara ya Mambo ya Ndani
ya Nchi.
Katika
kikao hicho, Mheshimiwa Kitwanga ameagiza watumishi wote wa Idara ya
Uhamiaji walioko Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere, Dar es
Salaam na Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Kilimanjaro, wahamishwe na
kupelekwa maeneo mengine nchini, wakiwemo wale wa Teknolojia ya Habari
na Mawasiliano.
Wengine
watakaohamishwa ni kutoka Kitengo cha Pasipoti, Uhasibu, Hati za Ukaazi
na Kitengo cha Upelelezi, vyote vya Makao Makuu ya Uhamiaji jijini Dar
es Salaam.
Aidha
ameagiza pia kuwa Wakuu wote wa Vitengo vya Upelelezi vya wilaya
zilizopo jijini Dar es Salaam, na pia wale wa Vituo vya Tunduma,
Mtukula, Holili na Kasumulo, wahamishiwe maeneo mengine, na pia
watumishi wote waliokaa kwa zaidi ya miaka mitatu katika Vituo hivyo.
Amesema
hatua hii inayochukuliwa sasa ni mwanzo tu wa mabadiliko makubwa
yatakayofanywa katika Idara ya Uhamiaji ili kuboresha huduma
zinazotolewa na Idara hii ambayo ni moja ya Idara muhimu za Serikali.
Amesema
katika kuisafisha Idara hii, uangalifu mkubwa utachukuliwa ili
kuhakikisha kuwa hakuna mtumishi anayeonewa wala kupendelewa, lakini
lengo kubwa ni kuvunja mtandao wa wapokea rushwa na wale wasiowajibika.
Amesema
kufuatana na utafiti uliofanywa hivi karibuni umeonyesha kuwa matatizo
ya rushwa katika Idara ya Uhamiaji yanashika nafasi ya kwanza kwa kuwa
na asilimia 30, asilimia 20 ni uongozi mbovu na asilimia 20 ni matumizi
mabaya ya madaraka. Asilimia 15 inahusisha vitendea kazi wa mifumo
hafifu ya kufanya kazi, asilimia 10 huduma mbovu na asilimia 5 ukabila
na upendeleo.
Amewataka
Viongozi na watumishi wote wa Idara ya Uhamiaji kufanya kazi zao kwa
kuzingatia sheria, kanuni na maadili ya kazi na waepuke vitendo vya
kupokea rushwa na kusaidia wahamiaji haramu na wauza madawa ya kulevya.
Imetolewa na Kitengo cha Mawasiliano ya Serikali
Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi
23 Februari, 2016
|
Mtafiti
Kiongozi Tume ya Taifa ya Sayansi na Teknolojia (Costech), Dk.Nicholaus
Nyange (katikati), akizungumza na wakulima wa Wilaya ya Rorya Mkoani
Mara katika mafunzo ya siku moja kwa wakulima hao ya kutumia simu
kupashana habari za kilimo na kujua changamoto zinazo wakabili. Kulia ni
Mratibu wa Jukwaa la Bioteknolojia za Kilimo Afrika (OFAB), Daniel
Otunge na kushoto ni Mtafiti Mkuu wa Jukwaa la Bioteknolojia Tanzania
(OFAB), Dk.Emmarold Mneney.
Ofisa Kilimo wa Wilaya ya Rorya, Dominick Ndentabura akizungumza na wakulima hao kabla ya kuanza kwa semina hiyo.
Wakulima wa Rorya wakiwa kwenye mafunzo hayo.
Mkulima Saye Okelo akizungumzia changamoto ya ukosefu wa mbegu katika mafunzo hayo.
Mkulima Sinde Mjinja akielezea changamoto ya bei kubwa ya pembejeo za kilimo.
Mkulima akizungumizia magonjwa ya mbegu za mhogo na pembejeo kuchelewa kuwafikia wakulima.
Mkulima Emmanuel Lugombo akizungumzia kuoza kwa mbegu ya mkombozi.
Mkulima
Sophia Charles kutoka Kijiji cha Roche akizungumzia changamoto ya
ukosefu wa soko la zao la mhogo ambapo wanategemea zaidi soko nchini
Kenya.
Mkulima Charles Ruola akizungumzia changamoto ya kilimo cha mahindi.
Mkulima
wa Kijiji cha Kowaki kilichopo Wilaya ya Rorya mkoani Mara, Elias
Kaseno akizungumzia changamoto ya kilimo cha muhogo na mahindi mbele ya
watafiti kutoka Jukwaa la Bioteknolojia (OFAB) na Watafiti kutoka Tume
ya Taifa ya Sayansi na Teknolojia (Costech), waliopo wilayani humo jana
kujua changamoto mbalimbali za wakulima na kutoa mafunzo ya matumizi ya
Bioteknolojia katika kilimo.
Wakulima wakiwa kwenye mafunzo.
Wakulima wakiwa mafunzo hayo.
Wakulima wakiwa kwenye mafunzo hayo.
Wakulima hao wakibadilishana mawazo baada ya kupiga picha.
Jengo la Halmshauri ya Wilaya ya Rorya.
Shamba
la muhogo lililoshambuliwa na ugonjwa wa batobato lililopo jirani na
jengo la Halmshauri ya Rorya ambapo wapo wataalamu wa kilimo.
Na Dotto Mwaibale
KATIKA
hali isiyotegemewa shamba lenye ukubwa wa ekari moja la zao la muhogo
lililopo nyuma ya Ofisi ya Halmashauri ya Wilaya ya Rorya mkoani Mara
ambapo ofisi ya wilaya ya kilimo ipo halipo katika matunzo ya kilaalamu
ambapo mwandishi wa habari hii ambaye yupo katika ziara ya kilimo na
watafiti kutoka Tume ya Taifa ya Sayansi na Teknolojia (Costech)
alitembelea.
Mwandishi wa habari hii alidhani kuwa shamba hilo la muhogo ni maalumu kwa ajili ya kufundishia wakulima kuhusu ugonjwa unaoshambulia zao hilo ujulikanao kama batobato na athari zake kumbe ni shamba la mkulima ambalo limekosa huduma za ugani licha ya maofisa ugani kuwepo mita chache ya eneo hilo. Kutokana na hali hiyo inapaswa wakulima wa namna hiyo kupata huduma za kilimo kutoka maeneo mengine kutokana na maofisa ugani hao kushindwa kutoa elimu ambapo shamba hilo limekuwa ni chanzo cha kueneza ugonjwa huo katika maeneo mengine. Akizungumza katika mafunzo ya matumizi ya simu katika kilimo kwa wakulima wa wilaya ya Rorya Mratibu wa Jukwaa la Bioteknolojia Tanzania (OFAB), Philbert Nyinondi alisema mafunzo hayo ya siku moja yatawasaidia wakulima kupashana habari za kilimo na changamoto zao. "OFAB imeleta mafunzo haya kwa wakulima ambao ni wadau wetu ili waweze kupashana habari za kilimo, changamoto zinazo wakabili na kutafuta masoko ya mazao yao kwa njia ya simu badala ya kutumia simu hizo kupigiana kwa mambo ya kawaida" alisema Nyinondi. Alisema kupitia mafunzo hayo wakulima hao wataweza kushirikiana na mitandao mingine ya kijamii ili kutatua changamoto zao za kilimo zikiwemo za wadudu waharibifu wa mazao, ukame na nyinginezo. Alisema washiriki wa mafunzo hayo walikuwa ni 20 kutoka katika wilaya hiyo na kuwa shirikisha wataalamu wa kilimo. |
ENDELEA KUTUFUATILIA KWA TAARIFA ZAIDI
CHANZO: ITV TANZANIA |
Katika
makala yake itakayochapishwa kwa ukamilifu katika gazeti hili kesho,
Profesa Lipumba alisema Rais Magufuli amejipambanua kuwa kiongozi
anayeguswa na matatizo ya wanyonge, hapendi makuu, anahimiza ukusanyaji
wa mapato ya Serikali na matumizi mazuri ya fedha za umma.
“...Hata hivyo, Watanzania hawajui mshahara wake ni kiasi gani?” alihoji Profesa Lipumba.
Profesa
huyo aliyejikita katika masuala ya uchumi, alirejea mijadala mbalimbali
iliyowahi kuibuliwa kuhusu mshahara wa Rais, ikiwamo ule uliyowahi
kuibuliwa mwaka 2013 na Zitto Kabwe, wakati huo akiwa Naibu Katibu Mkuu
wa Chadema kuwa Rais analipwa Sh32 milioni kwa mwezi.
Pia
alirejea taarifa iliyochapishwa na Mwananchi, Julai 27, 2015,
iliyoandikwa kutoka katika mtandao wa African Review kuwa Rais mstaafu
Jakaya Kikwete ni wa nne miongoni mwa marais wa Afrika kwa kupata
mshahara mkubwa wa dola za Marekani 192,000 kwa mwaka sawa na dola
16,000 kwa mwezi, ambayo ni sawa na Sh32 milioni kwa mwezi. Hadi jana
jioni, dola moja ya Marekani ilikuwa sawa na Sh2,187.
“Taarifa
ya Ikulu ilikanusha vikali habari zilizochapishwa na Mwananchi. Ikulu
ilieleza kuwa habari hizo siyo za kweli. Hata hivyo, haikueleza mshahara
wa Rais na marupurupu yake ni kiasi gani?
Pia,
katika mjadala wa mshahara wa Rais, Naibu Spika wa Bunge lililopita
ambaye ndiye Spika wa sasa, Job Ndugai alinukuliwa akieleza kuwa
mshahara wa mtu ni siri yake. Waziri wa Nchi Katika Ofisi ya Rais,
Menejimenti ya utumishi wa Umma wa wakati huo, Celina Kombani (kwa sasa
ni marehemu) alisema kuwa ni kosa kutangaza mshahara wa Rais.
“…Kwa
hivi sasa Rais Magufuli atangaze mshahara na marupurupu yake na kama
mapato yake ni Sh32 milioni kwa mwezi, basi ajitolee alau nusu ya mapato
hayo kuchangia elimu na afya ya wanyonge. Hatua hii itaimarisha taswira
inayojengeka barani Afrika kuwa yeye ni Rais wa wanyonge,” ameandika
Lipumba.
Wakati
akizungumza na wazee wa Dar es Salaam wiki iliyopita, Rais Magufuli
aliwataka mawaziri, naibu mawaziri na makatibu wakuu wachangie Sh1
milioni katika mishahara yao kuchangia elimu.
Pia
Rais alieleza kuwa yeye mwenyewe, makamu wake na waziri mkuu
watachangia Sh6 milioni kila mmoja, ili zifike Sh100 milioni kusaidia
changamoto za elimu bure Mkoa wa Dar es Salaam.
Kutokana
na tangazo hilo, Profesa Lipumba alisema, “Ikiwa Sh6 milioni zitakatwa
katika mshahara wake wa mwezi mmoja ni wazi mshahara wake na ule wa
makamu wake na waziri mkuu ni zaidi ya Sh6 milioni kwa mwezi.
“Mishahara
na marupurupu ya viongozi wa Tanzania hayako wazi. Watanzania hawajui
kila mwezi Rais, Makamu wa Rais na viongozi wakuu wa Serikali wanalipwa
kiasi gani? Malipo ya wabunge pia hayako wazi?” alihoji.
Profesa
Lipumba ambaye amewahi kuwa msaidizi wa Rais katika masuala ya uchumi
kati ya mwaka 1991 na 1993, alisema kwa kuwa Rais Magufuli amejivisha
joho la kuwa Rais wa wanyonge, anawajibika kuwaeleza Watanzania
mshahara na marupurupu yake.
“Ikiwa mshahara ni mkubwa sana achukue hatua za kuupunguza kama alivyofanya Mwalimu Nyerere mwaka 1965.”
Hata
hivyo, alisema kifungu cha Katiba cha 43 (2) kinaeleza kuwa mshahara na
malipo mengineyo yote ya Rais havitapunguzwa wakati Rais atakapokuwa
bado ameshika madaraka yake kwa mujibu wa masharti ya Katiba.
Profesa Lipumba alisema Rais Magufuli akitaka kupunguza mshahara wake itabidi kwanza abadilishe kifungu hicho cha Katiba.
“Anaweza kujitolea mchango wa kudumu utakaokatwa kutoka kwenye mshahara wake kusaidia sekta ya afya au elimu,”alisema.
Profesa
Lipumba ambaye ni mshauri wa Benki ya Dunia (WB) na Benki Kuu ya
Tanzania (BoT) katika masuala ya uchumi, alisema ili kuimarisha utawala
bora ni muhimu uongozi ulio madarakani utumie mamlaka waliopewa kwa
manufaa ya Taifa.
“Mishahara
na marupurupu ya viongozi yawe wazi na yaamuliwe na kupangwa na taasisi
iliyo huru. Kuweka utaratibu ulio wazi wa kuamua mishahara na
marupurupu ya viongozi wa umma wakiwamo Rais na makamu wake, mawaziri,
wabunge, majaji, makatibu wakuu na viongozi wengine,”alisema.
Alisema ni muhimu katika ujenzi wa utawala bora, uwajibikaji na uwazi wa viongozi wa umma kwa wananchi wanao waongoza.
“
Inasemekana mshahara wa mbunge katika Bunge lililopita ulikuwa Sh3.4
milioni kila mwezi. Pia mbunge alilipwa Sh8.2 milioni, nyingine kama
posho ya jimbo, gharama za ofisi, mafuta, malipo ya wasaidizi wake na
dereva.
“Vile
Vile, mbunge anapohudhuria kikao cha Bunge alilipwa posho ya Sh80,000
za kujikimu, Sh50,000 za mafuta ya gari na Sh200,00 za kuhudhuria kikao
cha Bunge, jumla ni Sh330,000 kwa siku.
“Posho
ya siku moja ya mbunge ni zaidi ya mara mbili ya kima cha chini cha
mshahara wa Serikali kwa mwezi mzima ambacho ni Sh150,000. Mishahara
inakatwa kodi, marupurupu hayakatwi kodi,”alisema.
MWANANCHI
|
Dk
Kalemani alitoa rai hiyo juzi katika mkutano mkuu wa kwanza wa Numet,
akisema njia pekee ya kumaliza matatizo ya wafanyakazi ni kufichua
unyanyasaji unaofanywa na waajiri wageni.
“Shirikianeni
na vyombo vingine vya uchunguzi kufuatilia maovu yanayofanywa migodini
na wawekezaji, wajibu wenu ni kuishauri Serikali na kutupatia takwimu
sahihi. Tutahakikisha tunazifanyia kazi taarifa mtakazotupatia.
“Undeni
bodi itakayokisimamia chama, tasnia hii ina uwezo wa kuinua uchumi wa
mwananchi mmoja mmoja na |Taifa. Mkipata matatizo tushirikisheni
tutakuwa bega kwa bega kuyapatia ufumbuzi,” alisema Dk Kalemani katika
mkutano huo.
Mwenyekiti
wa chama hicho, Albert Machumu alisema walisajili wanachama 3,413 kwa
miaka mitatu, lakini kwa sasa wapo 1,857 baada ya wengine kuachishwa
kazi kutokana na sababu mbalimbali.
Katika
mkutano huo, chama hicho kilitoa tamko la kujiunga na kushirikiana na
vyama vingine kuunda muungano wa vyama vya wafanyakazi mbali na
Shirikisho la Vyama vya Wafanyakazi (Tucta) .
|
Fisi
hao wawili walimshambulia kwa kumng’ata Gamalaya maeneo mbalimbali ya
mwili na kusababisha kifo chake, huku wakimjeruhi Ngeleja mikono na
miguu.
Kamanda
wa Kikosi cha Kuzuia Ujangili Kanda ya Magharibi, Charles Msilanga
alisema jana (juzi) kuwa baada ya polisi kumpiga risasi fisi mmoja na
kumuua, mwingine alikimbia.
Alisema wanaendelea kumsaka fisi huyo ili kuzuia madhara zaidi kwa wakazi wa kitongoji hicho.
“Fisi aliyekimbia anaweza kuleta madhara kwa watu na ndiyo maana tunamsaka kwa udi na uvumba,” alisema Msilanga.
Mwenyekiti
wa kitongoji hicho, Iddi Cheyo alisema Gamalaya alifariki dunia baada
ya kukaa muda mrefu bila matibabu tangu aliposhambuliwa na fisi hao.
Baadhi
ya wakazi wa kitongoji hicho, Sophia William na Juma Kapambala walisema
tukio hilo limewastaajabisha kwani kwa miaka mingi wanafanya shughuli
zao ndani ya msitu huo bila kushambuliwa na wanyama.
“Tunafanya
shughuli zetu katika msitu huu kwa miaka mingi bila kuvamiwa, lakini
hatujaona mnyama kuingia eneo hilo,” alisema Sophia.
MWANANCHI
|
Mkurugenzi
mkuu wa shirikisho la riadha la Kenya bwana Isaac Mwangi amepigwa
marufuku na shirikisho la riadha duniani IAAF, kwa siku 180.
Bwana
Mwangi anatuhumiwa kwa kuwaitisha hongo wanariadha wawili waliopatikana
na hatia ya kutumia madawa ya kuongeza nguvu mwilini ilikupunguza
kipindi cha marufuku yao.
Mwangi amekanusha madai dhidi yake.
Mkurugenzi huyo mkuu tayari amejiondoa kwa siku 21 ilikufanikisha uchunguzi dhidi yake.
Kufuatia
marufuku hii yakamati ya maadili basi bwana Mwangi hatakuwa na mchango
wowote katika mashindano ya olimpiki yatakayofanyika mjini Rio Brazil
mwaka huu.
Kupitia
kwa taarifa maalum mkuu wa kamati ya maadili bwana Michael Beloff QC
amepigwa marufuku kwa kujaribu kuhujumu kampeini dhidi ya madawa ya
kuongeza nguvu mwilini.
Marufuku yake inaanza mara moja yaani kuanzia tarehe 22 mwezi Februari 2016.
Mkurugenzi
huyo alijipata matatani baada ya wanariadha wawili Joy Sakari na
Francisca Koki Manunga kudai kuwa Mwangi alikuwa amewaitisha hongo ya
takriban dola elfu hamsini ilikupunguza kipindi cha marufuku.
Joy
Sakari na Francisca Koki Manunga walipatikana na hatia ya kutumia
madawa ya kuongeza nguvu mwilini katika mashindano ya riadha duniani
yaliyofanyika huko Beijing Uchina.
Source: BBC
|
Balozi Pierre Mutemba (katikati) akiimba wimbo wa Taifa.Na Maria Inviolata
Balozi
mpya wa Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo nchini Tanzania (DRC) Pierre
Mutamba amewataka Wakongomani waishio nchini Tanzania kuwa na umoja na
kufanyakazi kwa bidii ili waweze kujenga nchi yao, amesema hayo
wakati Balozi huyo akianza kazi rasmi, leo katika ofisi za Ubalozi huo
zilizopo Upanga jijini Dar es salaam.
Balozi
Mutamba amewaambia wanajumuia hao kuwa falsafa yake ni “Ni hapa kazi
tu” inayofuata nyayo za Kauli Mbiu ya Rais John Pombe Magufuri wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Balozi
Mutamba alitoa Bendera za Taifa lake kwa kila Kiongozi wa jumuia ya
Wakongomani waishio hapa nchini ikiwa ni ishara ya Uzalendo wa Taifa
lao, Balozi huyo alisema kuwa Bendera ni Nembo ya Nchi, kwa hiyo ni
jukumu la kila Mkongomani kuijenga nchi yake.
|
TAN
Bayport
Kikoa
Myway entertainment
FORE PLAN CLINIC
MPINGA CUP 2016
Mashujaa Fm 89.3, Lindi
Wednesday, February 24, 2016
African Diaspora Leaders Policy Briefing. TAXES, ACCOUNTING AND LIFE INSURANCE SERVICES WAKALA WA VIPIMO (WMA) KUFANYA MSAKO WA MIZANI FEKI YA MADUKANI MKOANI ARUSHA PROF. MBARAWA ATOA MWEZI MMOJA KWA MAKANDARASI WOTE NCHINI KUTOA MIKATABA YA AJIRA KWA WAFANYAKAZI TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI KUTOKA CHAMA CHA WANANCHI (CUF) WANAHABARI, WATAFITI KUTOKA COSTECH WAZURU KABURI LA BABA WA TAIFA BUTIAMA MKOANI MARA WATU WANAOSADIKIKA KUWA MAJAMBAZI WAPORA MILIONI 12 JIJINI DAR PANGAPANGUA YATINGA IDARA YA UHAMIAJI, WAZIRI KITWAGA AAGIZA KUFANYIKA MABADILIKO MAKUBWA WAKULIMA WILAYANI RORYA MKOANI MARA WAPATIWA MAFUNZO YA KUPATA HUDUMA ZA UGANI KWA NJIA YA SIMU Kichupa cha leo Kamikaze Shori Official Music Video BASI LA NATA RAHA LAPATA AJALI BUNDA LEO ASUBUHI LIPUMBA AMTAKA RAIS MAGUFULI ATANGAZE MSHAHARA WAKE DK KALEMANI: CHUNGUZENI MAOVU YA WAWEKEZAJI WAGENI FISI WALA WATU WAUA, KUJERUHI MKOANI TABORA MKUU WA RIADHA KENYA ASIMAMISHWA KWA MIEZI 6 BALOZI PIERRE MUTAMBA AWATAKA WAKONGO KUFANYAKAZI KWA BIDII, AKUNWA NA UTENDAJI KAZI WA RAIS MAGUFULI MAGAZETI YA LEO FEB 23, 2016 VODACOM TANZANIA KUPITIA PROGRAMU YA PAMOJA NA VODACOM WATOA MSAADA WA MASHINE YA KUDURUSU KARATASI SHULE YA SEKONDARI SHIMBWE. Zaidi ya trilioni 1 zilivyokusanywa na kugawanywa ndani ya mwezi mmoja Jerry Muro kawajibu wanaosema Yanga alipendelewa dhidi ya Simba Feb 20 2016 Mwanamuziki Linah Sanga Akiri 'Kubanjuka' na Wizkid Hotelini... MTANDAO WA MODEWJIBLOG WAPATA KWIKWI YA KIUFUNDI KURUDI HEWANI HIVI PUNDE IDRIS Sultan Amjibu Mange Kimambi Baada ya Mange Kumshauri Wema Atafute Manager wa Bank Mwenye Pesa Kuliko Vijana wa Laki Laki
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment