Waandishi wa habari wakiwa wanamuangalia mnyama aina ya kobe aliopo ndani ya hifadhi ya mkomazi
Na Woinde Shizza,Same
Vita dhidi ya magonjwa ya mifugo ,majanga ya moto ,ongezeko
la watu pamoja na ukame ni changamoto
kubwa inayoikabili hifadhi ya taifa ya Mkomazi ilipo wilayani same Mkoani
Kilimanjaro ambapo imesababisha baadhi ya wanyama ambao ni vivutio vikubwa
katika hifadhi hiyo kutoweka .
Hayo yamebainishwa na afisa utalii mwandamizi wa hifadhi ya mkomazi Pellagy
Marandu wakati akiongea na waandishi wa habari waliotembelea hifadhi hiyo
kujionea vivutio ambavyo vinapatikana ndani ya hifadhi hiyo.
Alisema changamoto hizo zimekuwa zinaletwa na wafugaji
,wakulima ambao wamekuwa wanaleta wanyama ndani ya hifadhi ambapo alibainisha
kuwa wanyama wengine wanaweza wakawa na magonjwa ya kuambukiza hivyo
wanapoingia ndani ya hifadhi wanaweza kuambukiza wanyama walioko hifadhini hali
ambayo inaweza kusababisha janga kubwa kwa hifadhi.
“kwa upande wakulima wamekuwa wakileta madhara wakati wa
kuandaa mashamba yao kwa ajili ya kilimo ambapo wamekuwa wakiaribu mazingira
kwa kuchoma moto mabaki ya mazao ambayo walipanda msimu uliopita “alisema
Marandu
Aidha ilikukabiliana na changamoto hizo wamekuwa wakifanya
doria kwa kushirikiana na wananchi wanaozunguka hifadhi ambao ni ujirani mwema
ambapo wamekuwa wakiweza kufichua wale wote ambao wanaingiza mifugo ndani ya
hifadhi kinyume cha sheria ambao wamekuwa wakipigwa faini huku wengine
wakifikishwa mahakamani .
Kwa upande wake mkuu
wa hifadhi ya Mkomazi Donat Simon Mnyagatwa Alisema kuwa mbali na kuwepo
na changamoto hiyo ya kuingiza mifugo ndani ya hifadhi pia wanakabiliwa na
changamoto ya ukosefu wa maji ambapo alibainisha kuwa hili ni tatizo kubwa linaloikabili hifadhi hiyo kwani maji ni uhai
,kuanzia kwa binadamu na hata kwa wanyama .
“Ni kweli ili nitatizo kubwa lakini pia tumeanza kuandaa
mipango mathubuti kwa ajili ya kutatua
tatizo hili ambapo kwa upande wa binadamu tupo kwenye mkakati wa kuanza
kuchimba visima virefu ili kuweza kupa maji mengi ambayo pia maji hayo yataweza
kukusanywa kwa pamoja kwa ajili pia ya wanyama wetu,pia tunampango wa kuongeza
mabwawa yaliyopo ndani ya hifadhi ili kuakikisha pia tunaondokana na changamoto
hiyo”alisema Mnyagatwa
Aidha alibainisha kuwa mbali na changamoto hiyo pia
wanakabiliwa na tatizo la ukosefu wa miundo mbinu ya barabara pamoja na nyumba
za kuishi watumishi ambapo alisema kuwa mpaka sasa zaidi ya familia tisa
zinaishi ndani ya hifadhi huku familia
zingine zikiishi nje ya hifadhi ,pamoja changamoto hizo ameiomba Halmashauri ya
same kupitia Tanroad kurekebisha barabara ya kuelekea hifadhini ili iweze kupitika
kwa urahisi kwa kipindi chote.
Mnyagatwa alibainisha kuwa kwa lengo la ujirani mwema
wananchi ambao wamekuwa wakizunguka hifadhi wamekuwa wakipatiwa mafunzo maalumu
ya kutambua umuimu wa utunzaji wa hifadhi pamoja na kutambua mipaka ya hifadhi
na athari za kuingiza wanyama hifadhini ,mathara ya uaribifu wa mazingira
ambapo alisema wamefanikiwa kwa kiasi kikubwa kuwaelimisha na elimu hii
imesaidia kupunguza kwa kiasi kikubwa uhalifu ndani ya hifadhi.
No comments:
Post a Comment