Wakfu wa Tasnia ya habari Tanzania(Tanzania Media Foundation-TMF), imerithi kazi za mradi wa mfuko wa vyombo vya habari tanzania, (Tanzania Media Fund Project), uliofanya kazi kutoka juni 2008 hadi septemba 2015, TMF mpya ambayo ilianza shughuli zake octoba 2015, ina maono ya kuimarisha tasnia ya habari na kuifanya kuwa huru ili kukuza uwajibikaji.
TMF imedhamilia kubadili sekta ya habari kwa kutoa Ruzuku na mafunzo ya kivitendo ili sekta hii iwe huru na endelevu na inayowajibika kikamilifu kuibua masuala yenye maslai mapana kwa umma, TMF inafanya kazi zake kwa misingi ya uwazi bila upendeleo, kwa fikra tofauti na mpya, kwa ubora kwa kujifunza na kufikirisha, kwa ari ya kupata matokeo na utendaji kazi wa pamoja.
TMF kwa sasa inatekeleza mpango mkakati wa mwaka 2015-2018, Kuimarisha Tasnia ya Habari ili kuleta Uwajibikaji. kwa kutekeleza mkakati huo, TMF inatarajia kupata matokeo matatu ikiwa ni pamoja na kuongezeka kwa kiwango cha kuridhika kwa watumiaji habari wa vyombo vya habari vilivyojengewa uwezo na TMF kufuatia upatikanaji zaidi wa habari za uchunguzi na zenye maslahi mapana kwa umma.
2. kuongezeka kwa uimara na uendelevu wa taasisi za habari zinazojengewa uwezo na TMF, lakini pia kuwepo kwa TMF imara na Endelevu.
Wakati sehemu moja ya matokeo inahusu uimara na uendelevu wa TMF kama taasisi, matokeo mawili ya mwanzo yanahusu kuongeza uwezo wa weledi kwa vyombo vya habari na wadau wa habari sambamba na kuongeza ubora, wingi na habari tofautitofauti za uandishi wa kiuchunguzi na wenye maslahi ya umma katika sekta ya habari.
Matokeo haya mawili yanahusu moja kwa moja aina ya ruzuku tano ambazo TMF itatoa kuanzia 2016. Ruzuku zinazowalenga waandishi binafsi ni Ruzuku ya habari za vijijini, Ruzuku ya Ushirika wa Kubobea na Ruzuku ya masuala ya Kimkakati, Ruzuku zinazolenga taasisi ni Ruzuku ya Maudhui Maalum na Ruzuku ya Mabadiliko kwa Maudhui Endelevu.
Sharti la Msingi kwa kila aina ya ruzuku inayotolewa ni kwa kumshirikisha kila mnufaika katika mpamgo wa jifunze wa TMF inayofuata misingi ya kujifunza kwa vitendo kwa maelekezo na ushauri kutoka kwa gwiji wa habari.
KWA NINI RUZUKU KWA WAANDISHI WA HABARI?
Wahitimu wa uandishi wa habari nchini, mara nyingi wanaanza kazi wakiwa na ujuzi mdogo wa vitendo. Tafiti za TMF za miaka ya 2013,2014 na 2015 ziliangalia kwa kina ubora wa mahudhui ya habari. Tafiti hizi zinaweza kupatikana kwa maombi au katika tovuti ya TMF. hali inayoonekana katika vyombo vya habari vya Tanzania ni uandishi uliojikita katika habari za mjini na masuala ya kisiasa ambapo raia wanapewa fursa ndogo ya kutoa maoni yao ikilinganishwa na wataalamu na maafisa wa Serikali. Matumizi ya vyanzo vya habari na anuani zake yako chini, jambo hili linaweka ukomo wa uwezo wa vyombo vya habari kufanya wajibu wake kama mdhibiti.
kuanzia 2016 TMF inatumia mbinu ya kile inachiita mnyororo wa ruzuku, kama ilivyoonyeshwa kwenye jedwali kwa mbinu hii, TMF itawekeza zaidi katika kuthamini namna ambavyo uwezo wa mwandishi aliyenufaika na ruzuku za TMF amekua katika taaluma na weledi.
inaendelea............
No comments:
Post a Comment