Mkurugenzi
wa Huduma Shirikishi za Tiba katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili
(MNH), Dk Praxeda Ogweyo akifungua zoezi la utoaji damu linaloendelea
leo katika viwanja vya Karume mkabala na ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es
Salaam. Zoezi hilo linaendea hadi kesho.
Mkurugenzi
wa Huduma Shirikishi za Tiba katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili
(MNH), Dk Praxeda Ogweyo akiongoza zoezi la utoaji damu leo katika
viwanja vya Karume mkabala na Ofisi za Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam.
Muuguzi
wa Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH), Nemganga Kizega akipima afya
ya Mkazi wa Vingunguti jijini Dar es Salaam, Merry Kapande aliyefika leo
kuchangia damu katika viwanja vya karume mkabala na ofisi za Mkuu wa
Mkoa wa Dar es Salaam.
Wanafunzi wa Tambaza wakichangia damu leo katika zoezi linaloendelea leo jijini Dar es Salaam.
Dk Patrick
Shao ni mmoja wa wafanyakazi wa Muhimbili ambaye alifika katika viwanja
hivyo kwa ajili ya kuchangia damu ili kuokoa maisha ya wagonjwa wenye
uhitaji wa damu.
Wanafunzi
wa Shule ya Sekondari ya Tambaza na Jangwani wakisubiri kutoa damu leo
katika viwanja wa Karume mkabala na ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es
Salaam.
……………………………………………………………
Hospitali
ya Taifa Muhimbili (MNH) leo emeendesha zoeti la kuchangia damu katika
viwanja vya Karume jijini Dar es Salaam ambako watu wamejitokeza kwa
wingi kutoa damu ili kuokoa maisha ya wagonjwa wenye uhitaji wa damu.
Zoezi
hilo limeanza leo asubuhi na litaendelea hadi kesho. Wanafunzi wa
Jangwani Sekondari na Tambaza ni kati ya makundi yaliojitokeza kutoa
damu.
Pia
watu mbalimbali wamejitokeza kwa wingi kutoa damu akiwamu Mkurugenzi wa
Huduma Shirikishi za Tiba katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili, Dk
Praxeda Ugweyo, madaktairi wa muhimbili na kijana Joseph Starford Mgoha
aliyetembea kwa mguu kutoka Mwanza hadi Dar es Salaam kwa ajili ya
kumuunga mkono Rais John Pombe Magufuli kutokana na utendaji wake
uliotukuka.
Katika
zoezi hilo Dk Ogweyo amewaomba Watanzania kujitokeza kwa wingi kuchagia
damu ili kuokoa maisha ya wagonjwa wanaohitaji damu.
Pia,
amesema zoezi hilo litakuwa endelevu na amewaondoa shaka Watanzania
kwamba utoaji wa damu hauna madhara yoyote kwa kuwa kabla ya mtu kutoa
damu anaandaliwa kitaalamu ili kufanikisha kazi hiyo.
No comments:
Post a Comment