Katibu
Mkuu Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Meja Jenerali Projest Rwegasira
akila kiapo cha kuwa Katibu wa Tume ya Utumishi ya Jeshi la Polisi na
Magereza mbele ya Jaji Kiongozi wa Mahakama Kuu, Shabani Lila (kushoto)
jijini Dar es Salaam leo. Tume hiyo inashughulikia masuala ya kiutumishi
kwa askari Polisi na Magereza. Katikati ni Msajili wa Mahakama Kuu,
Ilvin Mugeta.
Jaji
Kiongozi wa Mahakama Kuu, Shabani Lila (kushoto) akimpongeza Naibu
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Injinia Hamad Masauni mara baada ya
kumuapisha kuwa Makamu Mwenyekiti wa Tume ya Utumishi ya Jeshi la Polisi
na Magereza, katika tukio lililofanyika katika Mahakama hiyo, jijini
Dar es Salaam leo. Tume hiyo inashughulikia masuala ya kiutumishi kwa
askari Polisi na Magereza.
Jaji
Kiongozi wa Mahakama Kuu, Shabani Lila (kushoto) akimkaribisha ofisini
kwake Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Injinia Hamad Masauni
kabla ya kumuapisha kuwa Makamu Mwenyekiti wa Tume ya Utumishi ya Jeshi
la Polisi na Magereza, katika tukio lililofanyika katika Mahakama hiyo,
jijini Dar es Salaam leo. Tume hiyo inashughulikia masuala ya kiutumishi
kwa askari Polisi na Magereza.
Naibu
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Injinia Hamad Masauni akila kiapo cha
kuwa Makamu Mwenyekiti wa Tume ya Utumishi ya Jeshi la Polisi na
Magereza mbele ya Jaji Kiongozi wa Mahakama Kuu, Shabani Lila (kushoto)
jijini Dar es Salaam leo. Tume hiyo inashughulikia masuala ya kiutumishi
kwa askari Polisi na Magereza. Katikati ni Msajili wa Mahakama Kuu,
Ilvin Mugeta.
Naibu
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Injinia Hamad Masauni (kushoto),
Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Meja Jenerali Projest Rwegasira (kulia)
wakiwa katika picha ya pamoja na Jaji Kiongozi wa Mahakama Kuu, mara
baada ya Jaji huyo kuwaapisha kuwa viongozi wa Tume ya Utumishi ya Jeshi
la Polisi na Magereza katika tukio lililofanyika Mahakamani hapo,
jijini Dar es Salaam leo. Injinia Masauni katika Tume hiyo amekuwa
Makamu Mwenyekiti, na Meja Jenerali Rwegasira amekuwa Katibu. Picha zote
na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
No comments:
Post a Comment