![]() |
| Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Habari,Vijana,Utamaduni na Michezo Prof.Elisante Ole Gabriel akiwa katika picha ya pamoja na wanakikundi cha MWAMKO FARM GROUP na baadhi ya Maafisa toka Wilaya ya Mkuraga. |
TAN
Bayport
Kikoa
Myway entertainment
FORE PLAN CLINIC
MPINGA CUP 2016
Mashujaa Fm 89.3, Lindi
Sunday, January 12, 2014
Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Habari,Vijana,Utamaduni na Michezo amaliza ziara yake katika Mkoa wa Pwani.
RAIS KIKWETE AWAANDALIA MABALOZI SHEREHE YA KUUKARIBISHA MWAKA IKULU
Rais
Jakaya Mrisho Kikwete na viongozi wengine akisikiliza hotuba toka kwa
Balozi wa DRC nchini Mhe Asumani Mpango ambaye pia ndiye Kiongozi wa
Mabalozi nchini akihutubia wakati wa Sherehe ya Kuukaribisha Mwaka
Mpya(Sherry Party) Ikulu jijini Dar es salaam leo January 10, 2014
| Rais Jakaya Mrisho Kikwete akizungumza na mabalozi na wawakilishi wa taasisi za kimataifa wanawake wakati wa Sherehe ya Kuukaribisha Mwaka Mpya(Sherry Party) aliyowaandalia Ikulu jijini Dar es salaam leo January 10, 2014 |
PINDA AKUTANA NA UONGOZI WA KAMPUNI YA CMHI YA CHINA INAYOJENGA BANDARI YA BAGAMOYO
Waziri
Mkuu, Mizengo Pinda akizungumza na viongozi wa Kampuni ya Kichina ya
China Merchant Holdings International (CMHI) Ofisini kwake jijini Dar
es salaam Januari 10, 2013. Kushoto kwake ni Kiongozi wa Ujumbe huo
, Hu Jianhua na kulia ni Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Dr.
Mary Nagu. Kampuni hiyo inatarajiwa kujenga bandari mpya ya Bagamoyo.
(Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri
Mkuu, Mizengo Pinda akisalimiana na Kiongozi wa Ujumbe kutoka Kampuni
ya kichina ya China Merchant Holdings International (CMHI), Bw. Hu
Jianhua kabla ya mazungumzo yao, Ofisini kwa Waziri Mkuu, jijini Dar es
salaam Januari 10, 2014. Kampuni hiyo inatarajiwa kujenga kampuni mpya
ya Bagamoyo. (picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
DAWATI LA JINSIA NA WATOTO LAJENGEWA UWEZO.
Pichani
washiriki wa mafunzo ya namna ya kutambua makosa ya ukatili wa kijinsia
na unyanyasaji wa watoto wakimsikiliza mgeni rasmi, Naibu Kamishna wa
Polisi (DCP) Adolfina Chialo, wakati wa kufuata mafunzo ya kutambua
makosa ya ukatili wa kijinsia na watoto, yaliyofanyika mkoani Morogoro,
mafunzo hayo yaliwakutanisha washiriki kutoka katika kanda tatu za mikoa
ya Dodoma, Pwani pamoja na wenyeji mkoa wa Morogoro.( Picha na
Demetrius Njimbwi, Jeshi la Polisi )
…………………………………………………………………………
Na Demetrius Njimbwi, Jeshi la Polisi
Mkuu wa Dawati la Jinsia na
Watoto Nchini, Naibu Kamishna wa Polisi (DCP) Adolfina Chialo, amewataka
wananchi kote nchini, kutofumbia macho vitendo vya ukatili na
unyanyasaji ambavyo vimekuwa vikitokea katika jamii yetu huku vikiathiri
idadi kubwa ya wanawake na watoto.
Kauli hiyo ameitoa jana wakati
akifunga semina ya mafunzo kwa askari Polisi ya namana ya kutambua
viashiria vya makosa ya ukatili wa kijinsia na unyanyasaji wa watoto,
mafunzo yaliyofanyika kwa muda wa siku tano katika mkoa wa Morogoro,
huku yakiwakutanisha washiriki kutoka katika kanda tatu za mikoa ya
Dodoma, Pwani pamoja na wenyeji wa mafunzo hayo mkoa wa Morogoro.
Hata hivyo, Kamishna Chialo,
alisema kuwa, lengo la mafunzo haya kwa askari na maofisa wa Jeshi la
Polisi, ni kuwajengea uwezo katika kutoa huduma bora katika kazi za
dawati la jinsia na watoto, ikiwa pamoja na kufahamu mbinu mbalimbali za
kutambua makosa ya ukatili wa kijinsia huku wakitambua kuwa suala la
utoaji wa huduma bora kwa mteja si hiari bali ni lazima.
Naye kwa upande wake mwakilishi
wa Kituo cha Sheria ( legal Sector) waliofadhili mafunzo hayo, Bi.
Wanyenda, alisema kuwa, Jeshi la Polisi linamchango mkubwa katika
kuwahudumia waathirika wa ukatili wa kijinsia na hivyo kutokana na
mafunzo haya yatawasaidia askari katika kupambana na matukio ya ukatili
wa kijinsia ambayo kwa kiasi kikubwa yamekuwa yakitendeka katika jamii.
Bi. Wanyenda, aliongeza kuwa, ni
vyema askari waliopatiwa mafunzo haya wakaitumia fursa hii waliyoipata
kuweza kutoa elimu kwa askari ambao hawakuweza kushiriki katika mafunzo
haya kwa lengo la kuwajengea uwezo na namna ya kutambua viashiria vya
makosa ya ukatili wa kijinsia na unyanyasaji.
Akisoma risala mbele ya mgeni
rasmi kwa niaba ya washiriki wenzake, Mkaguzi msaidizi wa Polisi, Letea
Mofuga, alisema kuwa, mafunzo waliyopatiwa yamewasaidia kutambua na
kubaini viashiria pamoja na dalili za mtu aliyefanyiwa ukatili na hivyo
kuahidi kufanya kazi kwa kuzingatia miongozo waliojifunza.
MAKAMU WA RAIS DKT. BILAL AFUNGUA SHULE YA SEKONDARI YA KIEMBE SAMAKI ZANZIBAR
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib
Bilal, akizungumza jambo na Mwalimu Mkuu wa Shule ya Sekondari ya
Kiembe Samaki, Amina Salum Khalfan, wakati alipokuwa akitembelea chumba
cha Maabara baada ya kuzindua rasmi Shule hiyo wakati wa hafla fupi
iliyofanyika shuleni hapo mjini Zanzibar leo Jan 10, 2014. Picha na OMR
Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal,
akizungumza na mmoja wa wanafunzi wa shule ya Sekondari ya Kiembe
Samaki, baada ya uzinduzi rasmi wa shule hiyo uliofanyika leo Jan 10, 2014, mjini Zanzibar. Picha na OMR
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib
Bilal, akisikiliza maelezo kutoka kwa Mwalimu Mkuu wa Shule ya
Sekondari ya Kiembe Samaki, Amina Salum Khalfan, wakati alipotembelea
katika chumba cha Mawasiliano na mafunzo ya Kompyuta cha shule hiyo,
baada ya uzinduzi rasmi wa shule hiyo uliofanyika leo Jan 10, 2014,
mjini Zanzibar. Picha na OMR 
Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal,
akikagua moja ya vitabu vya kumbukumbu za Maktaba ya Shule mpya ya
Sekondari ya Kiembe Samaki wakati alipotembelea chumba hicho cha Maktaba
baada ya kuzindua rasmi Shule hiyo wakati wa hafla fupi iliyofanyika
shuleni hapo mjini Zanzibar leo Jan 10, 2014. Kulia ni Mwalimu Mkuu wa
shule hiyo, Amina Salum Khalfan. Picha na OMR 
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib
Bilal, akitembelea chumba cha Maabala kati ya vyumba vinne vilivyopo
shuleni hapo. Picha na OMR 
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib
Bilal, akitembelea chumba cha Maabala kati ya vyumba vinne vilivyopo
shuleni hapo. Picha na OMR
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib
Bilal, akikata utepe kuzindua shule ya Sekondari ya Kiembe Samaki,
wakati wa hafla fupi iliyofanyika shuleni hapo mjini Zanzibar leo Jan
10, 2014. Kulia ni Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali, Ali Juma
Shamhuna. Picha na OMR
Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal,
akifunua kitambaa kuashiria kuweka jiwe la Msingi la shule ya Sekondari
ya Kiembe Samaki, wakati wa hafla fupi ya uzinduzi wa shule hiyo
iliyofanyika shuleni hapo mjini Zanzibar leo Jan 10, 2014. Picha na OMR
Wanafunzi wa shule ya Msingi Kiembe Samaki, wakitoa burudani wakati wa hafla hiyo ya uzinduzi.
MATOKEO YA SENSA YA IDADI YA TEMBO KATIKA MFUMO WA IKOLOJIA WA SELOUS-MIKUMI NA RUAHA-RUNGWA
Wizara
ya Maliasili na Utalii inapenda kuujulisha umma matokeo ya sensa ya
tembo iliyofanyika mwezi Oktoba na Novemba mwaka huu ili kuiwezesha
Serikali kutambua hali ya rasilimali ya wanyamapori ndani na nje ya
maeneo yaliyohifadhiwa.
Wizara
kwa kushirikiana na wataalamu wa ndani na nje ya nchi imefanya sensa
katika Maeneo ya Mfumo ikolojia wa Selous – Mikumi na Ruaha – Rungwa
pekee kwa kuwa ni maeneo yenye tembo wengi nchini.
Matokeo
ya sensa hii yanaonyesha kwamba Mfumo wa ikolojia wa Selous-Mikumi kwa
sasa una tembo wapatao 13,084 na Ruaha–Rungwa una tembo wapatao 20,090.
Takwimu hizi zinaonesha kupungua kwa idadi ya tembo na hasa katika mfumo ikolojia wa Selous-Mikumi ikilinganishwa na Sensa za awali.
Takwimu
za muda mrefu zinaonesha kwamba mwaka 1976 katika mfumo ikolojia wa
Selous–Mikumi kulikuwa na tembo 109,419. Idadi hii ilipungua kufikia
22,208 mwaka 1991 kutokana na wimbi la ujangili uliokuwepo katika
kipindi cha mwaka 1984 -1989. Hata hivyo, idadi hiyo iliongezeka na
kufikia 70,406 mwaka 2006 baada ya Operesheni Uhai iliyofanyika mwaka
1989 na 1990 na juhudi za kimataifa za uhifadhi ikiwemo kusitisha
biashara ya meno ya tembo.
Aidha,
idadi ya tembo nchini ilipungua hadi kufikia jumla ya tembo 38,975
mwaka 2009 na kuendelea kupungua hadi kufikia tembo 13,084 hivi sasa.
Hali
kama hiyo inaonekana pia katika mfumo wa ikolojia wa Ruaha-Rungwa
ambapo sensa ya mwaka 1990 ilionesha kuwa na tembo 11,712 kutokana na
wimbi la
ujangili. Idadi hii iliongezeka na kufikia 35,461 mwaka 2006. Hata
hivyo, idadi hiyo imepungua na kubakia tembo 20,090 hivi sasa.
Kwa
matokeo haya inaonesha kuwa katika mfumo ikolojia wa Selous-Mikumi
idadi ya tembo imepungua kwa asilimia 66 ikilinganishwa na idadi ya
mwaka 2009 ambapo kulikuwa na jumla ya tembo 38,975. na katika Mfumo
ikolojia wa Ruaha–Rungwa Tembo wamepungua kwa asilimia 36.5
ikilinganishwa na idadi ya mwaka 2009 ambapo kulikuwa na jumla ya tembo wapatao 31,625.
Kupungua
huku kunathibitishwa na idadi ya mizoga ya tembo iliyohesabiwa wakati
wa zoezi la sensa. Jumla ya mizoga 6,516 na 3,496 ilihesabiwa katika
mifumo ikolojia ya Selous-Mikumi na Ruaha–Rungwa. Katika zoezi hili
Wizara ilitumia vigezo vya uwiano wa mizoga na tembo hai waliohesabiwa
(carcass ratio) kubaini vyanzo vya vifo hivyo. Katika hali ya kawaida,
uwiano wa asilimia 7 – 8 unaashiria vifo vya asili kama vile ugonjwa na
uzee. Zaidi ya asilimia hiyo inaashiria vifo visivyo vya asili.
Sensa
iliyofanyika mwaka huu imeonesha uwiano wa asilimia 30 kwa mfumo
ikolojia wa Selous-Mikumi na asilimia 14.6 kwa Ruaha–Rungwa. Kwa mujibu
wa matokeo hayo, idadi kubwa ya vifo vya tembo vimetokana na vifo
visivyo vya asili.
Uchambuzi
wa kina umebainisha kuwa asilimia 95 na 85 ya mizoga iliyoonekana
katika mifumo ikolojia ya Selous-Mikumi na Ruaha–Rungwa ni ya zaidi ya
miezi 18 iliyopita.
Hii
inaonesha kuwa juhudi za makusudi zilizofanywa na serikali ikiwa ni
pamoja na kuimarisha doria na operesheni maalum mbalimbali za hivi
karibuni zimesaidia kupunguza wimbi la ujangili kwa kiasi kikubwa.
Aidha,
kukamatwa kwa meno ya tembo yenye uzito wa kilogramu 32,987 ndani na
nje ya nchi katika kipindi cha 2008 hadi Septemba 2013 ni ishara tosha
kuwa ujangili ni mojawapo ya sababu kubwa za kupungua kwa idadi ya tembo
nchini.
Sababu
nyingine ni kuongezeka kwa mifugo katika maeneo yaliyohifadhiwa na
shoroba za wanyamapori. Mathalan, katika Pori Tengefu la Kilombero
ambalo ni sehemu ya ikolojia ya Selous – Mikumi, mwaka 2002 lilikuwa na
tembo 2,080, katika sensa ya mwaka huu, hukukuwa na tembo hata mmoja.
Ongezeko
la bei katika masoko ya biashara haramu ya meno ya tembo hususan katika
nchi za Mashariki ya mbali ni kichocheo na kisababishi kikubwa.
Kufuatia
hali hii, Wizara inaimarisha ulinzi wa wanyamapori kwa kushirikiana na
vyombo vya ulinzi na usalama na taasisi nyingine za kanda na kimataifa
pamoja na kuelimisha na kushirikisha wananchi katika masuala mbalimbali
ya uhifadhi.
Ili
kuimarisha na kuboresha shughuli za uhifadhi, Wizara iko katika hatua
za mwisho za kuanzisha mamlaka mpya ya wanyamapori. Vilevile sheria za
uhifadhi zinapitiwa ili kuruhusu kuanzishwa kwa mfumo wa kijeshi kwa
watumishi wa sekta ya wanyamapori.
Wizara
inapenda kuwatambua na kuwashukuru wafadhili wote waliofanikisha sensa
hii iliyogharimu kiasi cha dola za kimarekani 160,000ikiwa ni fedha za
serikali na wafadhili. Wafadhili hao ni Shirika la Misaada ya Kiufundi
la Ujerumani (GIZ) kupitia Frankfurt Zoological Society (FZS) na Shirika
la Umoja wa Mataifa la Maendeleo (UNDP) kupitia Mradi wa TANAPA wa
SPANEST.
Imetolewa na
Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii
Mhe. Lazaro Nyalandu (MB)
Mh. Lowassa akagua miradi ya maji jimboni kwake Monduli
Waziri
Mkuu Mstaafu na Mbunge wa Jimbo la Monduli,Mh. Edward Lowassa
(katikati) akiongozana na wadau mbali mbali wa maendeleo wakati ziara
yake ya kukagua maendeleo ya Mradi wa ujenzi wa bwawa la maji katika
kata ya Meserani kijiji cha Nalarami,jimbo la Monduli.Wa tatu kushoto ni
Diwani wa kata hiyo,Edward Lenanuu.
Waziri
Mkuu Mstaafu na Mbunge wa Jimbo la Monduli,Mh. Edward Lowassa
akisikiliza maelezo kutoka kwa kaimu mhandisi wa maji wa wilaya ya
Monduli,Bw. Wasiwasi Mgala (kushoto) wakati alipotembelea Mradi wa
ujenzi wa bwawa la maji katika kata ya Meserani kijiji cha
Nalarami,jimbo la Monduli.Katikati mwenye shati jekundu ni mwenyekiti wa
CCM Monduli,Ruben Kunayi.
DK.Shein Mgeni Rasmi katika Fensi Kibandamaiti
Rais
wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk Ali Mohamed Shein
akiwapungia mkono wasanii wa asili na vikundi vya ngoma wakati Fensi
katika barabara ya Kibandamaiti Wilaya ya Mjini jana,katika shamra
shamra za miaka 50 ya Mapinduzi ya Zanzibar,wengine waliokaa Makamo wa
Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi,Mkuu wa Mkoa wa Mjini
Magharibi Abdalla Mwinyi Khamis na Mke wa Rais wa Zanzibar Mama
Mwanamwema Shein,[Picha na Ramadhan Othman,Ikulu.]
Wasanii
wa fensi ambao hujipaka mafuta machafu (mobile) wakiwa na mishale
wakipita mbele ya mgeni rasmi Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza
la Mapinduzi Dk Ali Mohamed Shein pamoja na Viongozi mbali mbnali na
wananchi waliohudhuria kuangalia fensi hiyo iliyoshirikisha kazi za
taasisi za Serikali na Binafsi,katika Barabara ya Kibandamaiti Mjini
Unguja jana,ikiwa ni shamra shamra za miaka 50 ya Mapinduzi Matukufu ya
Zanzibar.[Picha na Ramadhan Othman,Ikulu.]

Wasanii
wakionesha namna ya tiba za asili kwa njia ya kupandisha mizuka ikiwemo
ngoma za pungwa, wakati wa Fensi iliyopita katika barabara ya
Kibandamaiti,Wilaya ya Mjini jana,katika shamra shamra za miaka 50 ya
Mapinduzi ya Zanzibar,[Picha na Ramadhan Othman,Ikulu.] 
Baadhi
ya Wananchi wa Mji wa Unguja na Vitongoji vyake wakiangalia Fensi
iliyopita katika Barabara ya Kibandamaiti Mjini Unguja jana,ikiwa ni
shamra shamra za miaka 50 ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar.[Picha na
Ramadhan Othman,Ikulu.]
Ngoma ya Beni (Mbwa kachoka) ikipita mbele ya mgeni rasmi Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk Ali Mohamed Shein, katika barabara ya Kibandamaiti Mjini Unguja jana,ikiwa ni shamra shamra za miaka 50 ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar.[Picha na Ramadhan Othman,Ikulu.
TAARIFA YA JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA KWA VYOMBO VYA HABARI
WILAYA YA RUNGWE – MAUAJI.
MNAMO
TAREHE 09.01.2014 MAJIRA YA SAA 06:00HRS HUKO KATIKA KIJIJI CHA ILENGE,
KATA YA KYIMO, TARAFA YA UKUKWE WILAYA YA RUNGWE MKOA WA MBEYA.
MAGRETH D/O IJUMBA, MIAKA 55, KYUSA, MKULIMA, MKAZI WA KIJIJI CHA ILENGE
ALIUAWA AKIWA NYUMBANI KWAKE KWA KUPIGWA JIWE KICHWANI NA MTU/WATU
WASIOFAHAMIKA KISHA KUTUPWA KATIKA SHAMBA LAKE LA MIGOMBA UMBALI WA MITA
69 KUTOKA NYUMBANI KWAKE. MBINU NI KUVUNJA MLANGO WA NYUMBA YA MHANGA
AMBAYE ANAISHI PEKE YAKE KUINGIA NDANI NA KUMUUA KWA KUTUMIA JIWE. AIDHA
WATU HAO PIA WALIKWENDA MTAA WA PILI NA WALIMSHAMBULIA KISA W/O
EPHRAIM, MIAKA 50, KYUSA, MKULIMA, MKAZI WA KIJIJI CHA ILENGE KWA
KUTUMIA JIWE KICHWANI NA AMELAZWA HOSPITALI YA MISHENI IGOGWE. CHANZO
NI IMANI ZA KISHIRIKINA. KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHNA
MSAIDIZI MWANDAMIZI WA POLISI AHMED. Z. MSANGI ANATOA WITO JAMII KUACHA
KUAMINI IMANI POTOFU ZA KISHIRIKINA KWANI ZINA MADHARA MAKUBWA KATIKA
JAMII. AIDHA ANATOA WITO KWA YEYOTE MWENYE TAARIFA ZA MTU/WATU
WALIOHUSIKA NA TUKIO HILI AZITOE KATIKA MAMLAKA HUSIKA ILI WAKAMATWE NA
SHERIA ICHUKUE MKONDO WAKE.
WILAYA YA MBEYA VIJIJINI – MAUAJI.
MNAMO
TAREHE 09.01.2014 MAJIRA YA SAA 16:00HRS HUKO MLIMA NYOKA, KATA YA
IGAWILO, TARAFA YA IYUNGA, WILAYA YA MBEYA VIJIJINI, MKOA WA MBEYA, WATU
WAWILI 1. CHARLES S/O LIVINGSTONE, MIAKA 32, MSAFWA, MKULIMA, MKAZI WA
ITEZI NA 2. TATIZO S/O MBWIGA, MIAKA 27, MSAFWA, MKULIMA, MKAZI WA
NSALAGA WALISHAMBULIWA KWA KUPIGWA NA KUNDI LA WANANCHI WALIOAMUA
KUJICHUKULIA SHERIA MKONONI WAKITUMIA SILAHA ZA JADI FIMBO NA MAWE HADI
KUFA. CHANZO NI TUHUMA ZA WIZI WA PIKIPIKI T.693 CBD AINA YA SHANLEY
MALI YA KEVEN S/O MSEMWA, MIAKA 24, MUWANJI, MKULIMA, MKAZI WA UYOLE.
MAREHEMU CHARLES S/O LIVINGSTONE ALIKUWA ANATOKA MAHAKAMA YA MWANZO
UYOLE AKIWA MLALAMIKAJI KATIKA KESI CC 568/2013 KOSA SHAMBULIO AKIWA NI
MLALAMIKAJI NA MAREHEMU TATIZO S/O MBWAGA ALIKUWA ANAMSINDIKIZA NA
WALIPOFIKA ENEO LA UYOLE KATI WALIIBA PIKIPIKI HIYO. KAMANDA WA POLISI
MKOA WA MBEYA KAMISHNA MSAIDIZI MWANDAMIZI WA POLISI AHMED. Z. MSANGI
ANATOA WITO JAMII KUACHA TABIA YA KUJICHUKULIA SHERIA MKONONI KWANI NI
KINYUME CHA SHERIA. AIDHA ANATOA WITO KWA YEYOTE MWENYE TAARIFA ZA
MTU/WATU WALIOHUSIKA NA TUKIO HILI AZITOE KATIKA MAMLAKA HUSIKA ILI
WAKAMATWE NA SHERIA ICHUKUE MKONDO WAKE.
WILAYA YA MBEYA VIJIJINI – KUPATIKANA NA BHANGI.
MNAMO
TAREHE 09.01.2014 MAJIRA YA SAA 09:00HRS HUKO MBALIZI KATA YA BONDE LA
SONGWE, TARAFA YA USONGWE, WILAYA YA MBEYA VIJIJINI, MKOA WA MBEYA.
ASKARI POLISI WAKIWA DORIA/MSAKO WALIMKAMATA GEOFREY S/O SACKSON, MIAKA
23, MNYIHA, MKULIMA, MKAZI WA MBALIZI AKIWA NA BHANGI KETE 27 SAWA NA
UZITO WA GRAM 135. MTUHUMIWA NI MUUZAJI /MTUMIAJI WA BHANGI. TARATIBU
ZINAFANYWA ILI AFIKISHWE MAHAKAMANI. KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA
KAMISHNA MSAIDIZI MWANDAMIZI WA POLISI AHMED. Z. MSANGI ANATOA WITO
JAMII KUACHA KUTUMIA DAWA ZA KULEVYA KWANI NI KINYUME CHA SHERIA NA NI
HATARI KWA AFYA YA MTUMIAJI. AIDHA ANATOA WITO KWA YEYOTE MWENYE TAARIFA
AU MWENYE KUONA VIASHIRIA VYOVYOTE VYA MTU/WATU WANAOJIHUSISHA NA
UUZAJI NA USAMBAZAJI WA DAWA ZA KULEVYA AZITOE ILI WAKAMATWE NA SHERIA
ICHUKUE MKONDO WAKE.
WILAYA YA MBARALI – KUPATIKANA NA NYARA ZA SERIKALI.
MNAMO
TAREHE 09.01.2014 MAJIRA YA SAA 09:00HRS HUKO KATIKA KIJIJI CHA
KWATWANGWA NDANI YA HIFADHI YA TAIFA YA RUAHA, TARAFA YA RUJEWA, WILAYA
YA MBARALI, MKOA WA MBEYA. ASKARI WANYAMAPORI [TANAPA] WAKIMKAMATA
JUMA S/O KALINDI, MIAKA 72, MSUKUMA AKIWA NA NYARA ZA SERIKALI PEMBE
MBILI ZA DIGIDIGI NA NYAMA YA TEMBO. THAMANI BADO KUFAHAMIKA. MTUHUMIWA
NI MUWINDAJI HARAMU. KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHNA MSAIDIZI
MWANDAMIZI WA POLISI AHMED. Z. MSANGI ANATOA WITO JAMII KUACHANA NA
TAMAA ZA MALI KWA KUTUMIA NJIA ZISIZO HALALI NA BADALA YAKE WAFANYE KAZI
HALALI ILI WAJIPATIE KIPATO. AIDHA ANATOA WITO KWA JAMII KUENDELEA
KUTOA TAARIFA KATIKA MAMLAKA HUSIKA JUU WA MTU/WATU WANAOJIHUSISHA NA
UWINDAJI HARAMU ILI WAKAMATWE NA SHERIA ICHUKUE MKONDO WAKE.
[AHMED Z. MSANGI – SACP]
KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA.
NHIF & KfW yakabidhi vifaa tiba Mbeya na Tanga
Naibu
Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii, Dk. Seif Rashid akizungumza katika
hafla ya kukabidhi vifaa tiba vitakavyotumika katika vituo vya kutolea
huduma vinavyohudumia wanufaika wa mradi wa akina mama wajawazito
unaofadhiliwa na Benki ya Maendeleo ya Watu wa Ujerumani (KfW) kwa
kushirikiana na Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF).
Naibu
Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii, Dk. Seif Rashid akikabidhi moja ya
vifaa tiba kwa Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Dk.Noman Sigalla.
Naibu waziri wa Afya Dk Seif Rashid akimkabidhi moja ya mashine ya
kusaidia watoto wachanga matroni Mary Mlay aliyemwakilisha mkuu wa
mkoa wa Tanga katika hafla hiyo.
kusaidia watoto wachanga matroni Mary Mlay aliyemwakilisha mkuu wa
mkoa wa Tanga katika hafla hiyo.
Kaimu
Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya, Hamis Mdee akitoa
maelezo ya Mradi wa KfW unaoendeshwa kwa ushirikiano wa Benki wa Watu wa
Ujerumani na NHIF.
Kaimu Mkuu wa Mbeya Dk. Noman Sigalla akitoa salaam za Mkoa kwa wadau wa mradi huo mbele ya Naibu Waziri wa Afya.
Maofisa wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (mbele) wakifuatilia hotuba ya Naibu Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii.
Sehemu ya wadau wa sekta ya afya kutoka Mbeya na Tanga waliohudhuria hafla hiyo.
………………………………………………………………………………….
Na Mwandishi Wetu, Mbeya
MFUKO
wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) kwa kushirikiana na Benki ya Maendeleo
ya watu wa Ujerumani (KfW) imeunga mkono mkakati wa Kitaifa wa kupunguza
vifo vya akina mama wajawazito na watoto chini ya umri wa miaka mitano
kwa kutoa vifaa tiba katika vituo vya matibabu vinavyohudumia kundi
hilo.
Msaada
huo unaohusisha mikoa ya Mbeya na Tanga wenye thamani ya shilingi
milioni 989.1 umekabidhiwa leo na Naibu Waziri wa Afya na Ustawi wa
Jamii Dk. Seif Rashid kwa niaba ya Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii Dk.
Hussein Mwinyi kwa Waganga Wakuu wa mikoa hiyo.
Akikabidhi
msaada huo, Dk. Rashid alisema kuwa msaada huo utaboresha huduma za
akina mama wajawazito na kupunguza vifo vitokanavyo na uzazi lakini pia
ni fursa ya vyanzo vya mapato kwa Halmashauri na watoa huduma.
“Sote
tunafahamu kuwa matibabu sahihi yanatokana na vipimo sahihi hivyo
uwekezaji unaofanywa kwa pamoja na NHIF & KfW kupitia mradi huu kwa
lengo la kuviwezesha vituo vya matibabu kupata vifaa tiba utasaidia sana
kupunguza tatizo la upatikanaji wa huduma ya vipimo kwa akina mama
wajawazito na watoto,” alisema Dk. Rashid.
Kutokana
na hali hiyo, Dk. Rashid aliwaagiza Waganga Wakuu ambao wamekabidhiwa
vifaa hivyo kuhakikisha vinatumika ipasavyo na kutunzwa kwa faida ya
Taifa ili vipumguze vifo vya akina mama hao na watoto.
“Ni
vyema walengwa wa mradi huu wakapata huduma bora na si bora huduma,
msaada huu uwe na matokeo mazuri kwa walengwa ili mradi uwe na manufaa
kwa nchi yetu,” alisema.
Naye
Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya, Hamisi Mdee
alisema Mfuko unatarajia mafanikio ya utekelezaji wa mradi huo
yatashawishi akina mama wengi zaidi kutumia huduma za uzazi salama
katika vituo vya matibabu lakini pia wafadhili kupanua maeneo ya mradi
katika mikoa wanayofadhili.
Aidha
alizitaka Halmashauri kuwasilisha kwa wakati madai yao baada ya kutoa
huduma kwa wanachama pamoja na maombi ya fedha za tele kwa tele ili
kuboresha huduma za matibabu katika vituo vyao.
Akizungumzia
mafanikio ya mradi, alisema kuwa hadi sasa umefikia walengwa 74,099
ambao ni sawa na asilimia 105 na jumla ya shilingi 644,1118,912
zimelipwa kwa vituo vya matibabu vya mikoa ya Mbeya na Tanga vilivyotoa
huduma kwa akina mama hao lakini pia shilingi milioni 400.4 zimetumika
kulipia familia za akina hao kujiunga na Mfuko wa Afya ya Jamii (CHF).
Dr. Shein weka Jiwe la Msingi Mnara wa Kumbu kumbu ya Miaka 50 ya Mapinduzi
Rais
wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein
akitambulishwa kwa mshauri wa Ujenzi wa kampuni ya Hab Consult Bw.Habib
Nuru,Katibu Mkuu Ofisi ya Makamo wa Pili wa Rais wa Zanzibar Dkt.Khalid
Salum,alipofika viwanja vya Kisonge,Michenzani Mjini Unguja, kuweka
Jiwe la Msingi Mnara wa Kumbu kumbu ya Miaka 50 ya Mapinduzi Zanzibar
leo asubuhi.[Picha na Ramadhan Othman,Ikulu.]
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed
Shein akifungua pazia kuweka jiwe la msingi Ujenzi wa Mnara wa Kumbu
kumbu ya Miaka 50 ya Mapinduzi Zanzibar, katika viwanja vya
Kisonge,Michenzani Mjini Unguja leo asubuhi.[Picha na Ramadhan
Othman,Ikulu.]
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed
Shein akiwapungia mkono wananchi waliohudhuria katika sherehe za uwekaji
wa jiwe la msingi Mnara wa Kumbu kumbu ya Miaka 50 ya Mapinduzi ya
Zanzibar katika viwanja vya Kisonge,Michenzani Mjini Unguja leo
asubuhi.[Picha na Ramadhan Othman,Ikulu.]
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed
Shein akiwapungia mkono wananchi waliohudhuria katika sherehe za uwekaji
wa jiwe la msingi Mnara wa Kumbu kumbu ya Miaka 50 ya Mapinduzi ya
Zanzibar katika viwanja vya Kisonge,Michenzani Mjini Unguja leo
asubuhi.[Picha na Ramadhan Othman,Ikulu.]
Wananchi
na wanachama wa CCM Jimbo la Mpendae wakimsikiliza Rais wa Zanzibar na
Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein,akitoa hutuba
yake wakati wa sherehe za uwekaji wa jiwe la msingi Mnara wa Kumbukumbu
ya miaka 50 ya Mapinduzi ya Zanzibar katika viwanja vya
Kisongo,Michenzani Mjini Unguja leo asubuhi.[Picha na Ramadhan
Othman,Ikulu.]
Wananchi
naa wanachama wa CCM Jimbo la Mpendae wakimsikiliza Rais wa Zanzibar na
Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein,akitoa hutuba
yake wakati wa sherehe za uwekaji wa jiwe la msingi Mnara wa Kumbukumbu
ya miaka 50 ya Mapinduzi ya Zanzibar katika viwanja vya
Kisongo,Michenzani Mjini Unguja leo asubuhi.[Picha na Ramadhan
Othman,Ikulu.]
Wafanyakazi
wa ZSSF,wakimsikiliza Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la
Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein,akitoa hutuba yake wakati wa sherehe za
uwekaji wa jiwe la msingi Mnara wa Kumbukumbu ya miaka 50 ya Mapinduzi
ya Zanzibar katika viwanja vya Kisongo,Michenzani Mjini Unguja leo
asubuhi.[Picha na Ramadhan Othman,Ikulu.]
Rais
wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein
akitoa hutuba yake kwa wananchi wakati wa sherehe za uwekaji wa jiwe la
msingi Mnara wa Kumbukumbu ya miaka 50 ya Mapinduzi ya Zanzibar, katika
viwanja vya Kisongo,Michenzani Mjini Unguja leo asubuhi,(kulia) Waziri
wa Ofisi ya Makamo wa Pili wa Rais Mohamed Aboud Mohamed.[Picha na
Ramadhan Othman,Ikulu.]
IAA and TPDF signs MoU to equip military personnel with Strategic Studies
A group photo of members of military and IAA staff members after the signing ceremony early today.
The Command and Staff College (CSC) Commandant Maj General Kyunga signs a document of Memorandum of Understanding (MoU) in Arusha today to allow military personnel with the necessary skills and knowledge in Strategic Studies at IAA
The Institute of Accountancy Arusha (IAA) Rector Prof. Prof. Johannes Monyo (2nd from R) exchange a Memorandum of Understanding (MoU) with The Command and Staff College (CSC) Commandant Maj General Ezekiel-Elias Kyunga (1st
from L). The MoU signed today in Arusha will equip military personnel
with the necessary skills and knowledge in Strategic Studies at IAA.
IAA Rector Prof. Johannes Monyo signs a document of Memorandum of Understanding (MoU) in Arusha today to allow military personnel with the necessary skills and knowledge in Strategic Studies at IAA.
………………………………………………………………………………..
By Our Reporter
The
Institute of Accountancy Arusha (IAA) Rector Prof. Johannes Monyo said
ion speech: “Today I have great pleasure to officiate a special ceremony
on signing the Memorandum of Understanding between the Institute of
Accountancy Arusha (IAA) and Tanzania People’s Defense Forces (TPDF).
This is a great event and privilege for both IAA and TPDF. CSC deserves a
special mention as the institution that initiated the event”
He
added: “It is our understanding that many institutions in Tanzania are
not used to working closely with Military personnel. TPDF and Command
and Staff College realized that members of military forces are good
partners in development. It is true that once good partnership is
established the country tends to prosper faster” He also said that the Command and Staff College (CSC) has good working relationship with the Institute of Accountancy Arusha
(IAA) that has lasted for 8 years. In
2006 a special CSC tailored programme was developed and this was the
beginning of a close working relationship between the two institutions.
In this relationship the academic staff from IAA were invited to
facilitate in a number of other related programmes conducted by CSC. But the target of CSC was to have long term programmes and academic partner with a capacity to run the new targeted programmes.
CSC
initially, consulted several institutions and universities in the
country to establish long term courses in strategic studies but this
effort was unsuccessful. It is the flexibility of IAA management and the
IAA Governing Council that authorized the commitment of resources in
the year 2011 and allowed the development of Strategic Studies
programmes at CSC- Monduli.
“Two
curricula were developed in the area of Strategic Studies and these
included the Ordinary Diploma and Postgraduate Diploma in Strategic
Studies. These curricula were developed following NACTE standards. The
Ordinary Diploma curricula comprising of NTA levels 5 and 6 were
submitted to NACTE for validation and were approved. Furthermore, IAA
developed Postgraduate Diploma in Strategic Studies Programme. These
programmes are
currently in progress and have a total of 52 participants from EAC and SADC countries” he said
He
revealed that both programmes are aimed at equipping Military personnel
with the necessary skills and knowledge in Strategic Studies that are
needed at their workplace and elsewhere in the world. These programmes
which commenced in May 2013 are expected to produce the first graduands by March this year (2014).
Although
this is the first collaborative arrangement with a partner from within
the country IAA has two other collaborations with partners from foreign
countries. IAA signed a MoU with Coventry University of UK way back in
2009 to run four masters degree programmes (MBA – ITM, MBA – LM, MBA –
PSM and MSc. FI). These programmes have been running for last four
years. In 2013 IAA signed another MoU with Galgotias University of India
to run three masters degree programmes namely; Master in Information
Security, Master in Software Engineering and Master in Computer
Application. These programmes started in November 2013.
In the same vein we are working with TMA to establish a Bachelor Degree in Military Science. This degree is expected to be run
effective 2015 if the accreditation processes will be completed in time.
Today
we are here to officially sign the MoU between IAA and TPDF and inform
Tanzanians in particular and the world at large that Military staff are
good partners in development.
I
would also like to take a moment of personal privilege to acknowledge
some of those who helped to make this day and the event surrounding
possible. I wish to thank members of IAA Academic staff, members of CSC
staff, TPDF headquarters, members of the Governing Council, NACTE, TMA
and all others not mentioned above but helped in one way or the other to
make this day possible.
Subscribe to:
Posts (Atom)









