TAN

TAN

Bayport

Bayport

Kikoa

Kikoa

Myway entertainment

Myway entertainment

FORE PLAN CLINIC

FORE PLAN CLINIC

MPINGA CUP 2016

MPINGA CUP 2016

Mashujaa Fm 89.3, Lindi

Sunday, December 7, 2014

MAHAFALI YA 49 YA CHUO CHA ELIMU YA BIASHARA(CBE) KAMPASI YA MBEYA YAFANA.

Katibu Mkuu Wizara ya Viwanda na Biashara, Musa Uledi akitoa tamko la kuwatunuku vyeti vya Astashahada katika fani za ununuzi na ugavi, uhasibu na uendeshaji wa biashara Wahitimu 37 katika mahafali ya 49 ya Chuo cha Elimu ya biashara (CBE) Kampasi ya Mbeya yaliyofanyika katika viwanya vya Mbeya Hotel. 
 
Mkuu wa Chuo cha elimu ya Biashara Kampasi ya Mbeya, Dionise Lwanga akitoa neno la Shukrani kwa mgeni rasmi baada ya kumaliza kuwatunuku wahitimu katika mahafali ya 49 ya Chuo hicho.
Makamu mkuu wa Chuo cha Elimu ya Biashara(CBE), Taaluma, utafiti na Ushauri Dk.Mbise akizungumza jambo katika Mahafali ya 49 ya Chuo hicho Kampasi ya Mbeya.
Afisa Taaluma wa Chuo cha Elimu ya Biashara Kampasi ya Mbeya, Thotnant Kayombo akisoma majina ya Wahitimu wa fani mbali mbali katika Mahafali ya 49 ya Chuo hicho yaliyofanyika katika viwanja vya Hotel ya Mbeya.
Afisa Uhusiano wa Chuo cha Elimu ya Biashara (CBE) Leonidas Tibanga ambaye alikuwa mshehereshaji katika mahafali ya 49 ya Chuo hicho Kampasi ya Mbeya  akiendelea na shughuli zake.
Wahitimu wakivaa kofia zao baada ya kutunukiwa vyeti na mgeni rasmi katika Mahafali ya 49 ya CBE
Baadhi ya Wahitimu wakionesha nyuso za furaha baada ya kutunukiwa vyeti
Mwanafunzi aliyefanya vizuri katika masomo yake, Eliesia Mwalwibaakipokea zawadi kutoka kwa mgeni rasmi.
Baadhi ya Wahadhiri wakifuatilia kwa makini shughuli za mahafali
Kikundi cha burudani cha Kihumbe kikionesha makeke yake kwa wahitimu wazazi na wageni waalikwa katika mahafali
Picha ya Pamoja kati ya Wahadhiri na mgeni rasmi
Picha ya pamoja kati ya Wanafunzi waliofanya vizuri na meza kuu
Picha ya pamoja kati ya wahitimu na meza kuu.

Vijana wa Jumuiya ya Afrika Mashariki wakutana Arusha kujadili Sera ya Vijana wa EAC

unnamed 
Naibu Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) Mhe. Jesca Eriyo (kushoto) akitoa mada wakati wa mkutano wa kwanza wa Vijana wa EAC kuhusu Sera ya Vijana wa EAC unaoendelea makao makuu ya Jumuiya ya Afrika Mashariki Jijini Arusha Tanzania. Kulia ni mwenyekiti wa Mkutano huo ambaye ni Mwanasheria wa Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Bibi. Ester Riwa.
Mbunge kutoka Kenya Mhe. David Ocheng akitoa hotuba wakati wa mkutano wa kwanza wa Vijana wa EAC kuhusu Sera ya Vijana wa EAC unaoendelea makao makuu ya Jumuiya ya Afrika Mashariki Jijini Arusha Tanzania. unnamed2 
Mmoja wa vijana kutoka Uganda Bi. Helena Okiring akichangia wakati wa mkutano wa kwanza wa Vijana wa EAC kuhusu Sera ya Vijana wa EAC unaoendelea makao makuu ya Jumuiya ya Afrika Mashariki Jijini Arusha Tanzania unnamed3 
Bi. Stella Massekwe kutoka Uganda akitoa mchango wake kuhusu masuala mbalimbali yaliyozungumzwa wakati wa mkutano wa kwanza wa Vijana wa EAC kuhusu Sera ya Vijana wa EAC unaoendelea makao makuu ya Jumuiya ya Afrika Mashariki Jijini Arusha Tanzania, Kushoto ni kijana Baraka Chelego kutoka Tanzania. unnamed4 
Baadhi ya Vijana kutoka nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) ambazo ni Tanzania bara na visiwani, Kenya, Uganda, Rwanda na Burundi wakifuatilia matukio yaliyokua yanaendelea wakati wa mkutano wa kwanza wa Vijana wa EAC kuhusu Sera ya Vijana wa EAC unaoendelea makao makuu ya Jumuiya ya Afrika Mashariki Jijini Arusha Tanzania.
Picha na: Genofeva Matemu – Maelezo

Usalama ni muhimu zaidi kwa Fastjet!

index
Ndege ya Fastjet FJA FN141 inayofanya safari kati ya Dar es Salaam na Mwanza, ikiwa imebeba abiria 142 iliruka kutoka airport ya kimataifa ya Julius Nyerere mida ya takribani saa 12:49 asubuhi siku ya Alhamisi ya tarehe 4 Disemba 2014.Muda mfupi baada ya ndege kuruka chombo hicho kilikumbana na ndege aliyekuwa akiruka. Kama sehemu ya maangalizi rubani wa ndege hiyo aliamua kugeuza safari na kurudi katika uwanja wa Julius Nyerere,  Dar es Salaam.
 Ndege ilitua salama bila kashikashi zozote zile. Abiria wote na wahudumu wa ndege walikuwa salama bila majeruhi ya aina yeyote ile.Abiria waliwekwa kwenye ndege za baadae na mida ya safari za Fastjet za siku hiyo zilibadilika kimasaa kutokana na msukosuko huo. Injini ya ndege husika ilirekebishwa ndani ya siku moja na kuendelea na shughuli zake kesho yake siku ya tarehe 5 Ijumaa Disemba 2014.
Uongozi wa Fastjet unasisitiza kuwa usalama ni kitu muhimu zaidi kwa kampuni ya Fastjet na inashukuru kwa uelewa wa wateja wote na kuomba radhi kwa usumbufu wowote uliojitokeza.

Rais Kikwete aendelea na mazoezi Ikulu

unnamedRais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akifanya mazoezi leo katika viwanja vya Ikulu kufuatia ushauri wa madaktari waliomtaka afanye hivyo mara tatu kwa siku ili kuendelea kuimarisha afya yake baada ya kufanyiwa upasuaji mwezi uliopita katika hospitali ya Johns Hopkins nchini Marekani.(Picha na Freddy Maro)

TAIFA STARS MABORESHO YAREJEA DAR

Taifa Stars
Kikosi cha Taifa Stars Maboresho kinarejea leo Dar es Salaam kutoka Bulyanhulu mkoani Shinyanga ambapo kiliweka kambi kwa ajili ya mechi ya kimataifa dhidi ya Burundi itakayochezwa Desemba 9 mwaka huu.
Timu hiyo ambayo leo asubuhi imefanya mazoezi kwenye Uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza, itatua Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA) kwa ndege ya Fastjet saa 12.30 jioni na kwenda moja kwa moja kambini hoteli ya Tansoma.
Stars inayodhaminiwa na Kilimanjaro Premium Lager kesho (Desemba 7 mwaka huu) itafanya mazoezi asubuhi na jioni kwenye viwanja vya Gymkhana wakati keshokutwa (Desemba 8 mwaka huu) itafanya mazoezi jioni kwenye Uwanja wa Taifa
Nayo timu ya Taifa ya Burundi inatua nchini keshokutwa (Desemba 8 mwaka huu) saa 10 jioni kwa ndege ya RwandAir. Kikosi hicho kitafikia hoteli ya Tiffany Diamond kitakwenda moja kwa moja Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam ambapo kitafanya mazoezi kuanzia saa 11 jioni.
Kiingilio cha mechi kati ya Tanzania na Burundi itakayochezwa Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam kuanzia saa 10 jioni kitakuwa sh. 3,000 kwa viti vya raungi ya chungwa, bluu na kijani wakati VIP B na C ni sh. 5,000 tu.

NHIF Yanyakuwa Tuzo tatu za Ubunifu Hifadhi ya Jamii Barani Afrika

Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Bima ya Taifa ya Afya Bw. Khamis Mdee akipokea tuzo  tuzo tatu za ubunifu katika sekta ya hifadhi ya Jamii Barani Afrika zinazosimamiwa na
Shirikisho la Mifuko ya Hifadhi ya Jamii Duniani (ISSA) unnamed1 
Mandhari ya jiji la Cassablanca Morocco
……………………………………………………………………………………………….
Mwandishi Maalum Casablanca, Morocco Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya, NHIF umenyakua tuzo tatu za ubunifu katika sekta ya hifadhi ya Jamii Barani Afrika zinazosimamiwa na Shirikisho la Mifuko ya Hifadhi ya Jamii Duniani (ISSA).
Halfa ya kukabidhi tuzo hizo ilifanyika Jijini Casablanca nchini Morocco usiku wa tarehe 3 Desemba, 2014 katika hoteli ya Serana jijini Casablanca ambapo washiriki zaidi ya 360 kutoka taasisi 75 katika mataifa 45 ya Afrika zilihudhuria.
Ujumbe wa Tanzania katika mkutano huo wa Kanda ya Afrika ambacho pia kilijadili mambo muhimu kuhusu sekta ya hifahi ya jamii na kutambua kazi za ubunifu uliongozwa na Waziri wa kazi Mheshimiwa Gaudensia Kabaka pamoja na Viongozi waandamizi wa Mamlaka ya Usimamizi na Udhibiti wa Sekta ya Hifadhi ya Jamii nchini (SSRA) na baadhi ya Watendaji wakuu wa Mifuko ya Hifadhi ya Jamii nchini.
Tangu kuanza kutolewa kwa ambazo hushindaniwa kila baada ya miaka mitatu, NHIF imeng’ara mara zote.Mwaka 2008 ilipata tuzo ya cheti cha heshima cha ubunifu mjini Kigali kwa kuwashirikisha wadau wake katika utoaji wa elimu kwa makundi mbalimbali ngazi ya mkoa. Mwaka 2011 ulikuwa mshindi wa kwanza wa jumla barani Afrika na mwaka huu umeibuka tena na ushindi huo muhimu unaoitangaza Tanzania kimataifa kupitia
Bima ya Afya.
Mbali ya NHIF, Tanzania pia imengara kwa kuzoa jumla ya tuzo 6 mbapo
Mamlaka ya Udhibiti ya SSRA, Mfuko wa Pensheni wa PPF na Mfuko wa PSPS
pia ilijizolea tuzo moja moja kwa kila mmoja hivyo kufanya Tanzania
kuwa na jumla ya tuzo 6 na kuifanya kuwa kinara katika ukanda wa nchi
za Afrika mashariki na ya Kati.
Mifuko ya Hifadhi ya Jamii katika nchi nne ilipata heshima ya pekee kwa kazi zao za ubunifu. Mifuko hiyo ni kutoka Cameroon yenyewe iliyonyakua tuzo 8, Gabon, Maurtania, wenyeji Morocco.
Washindi wa jumla wa kwa mwaka 2014 ni wenyeji Morocco na Jirani zao wa Mauritania ambao kwa pamoja wamepata tuzo ya jumla kwa kutoa huduma bora, kuongeza uwigo wa wanaonufaika na huduma za mifuko hiyo hasa wasio na uwezo, matumizi ya TEHAMA na huduma kwa wateja na ufanisi kwa
ujumla.

MAONYESHO YA KIMATAIFA YA ELIMU KUANZA DISEMBA 17-21, 2014 JIJINI DAR

Mkurugenzi Mtendaji wa Global Education Link, Abdulimalik Mollel, akisisitiza jambo kwa wanahabari (hawapo pichani)
 
Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam.

Kampuni ya Global Education Link (GEL) kwa kushirikiana na Ofisi ya Waziri Mkuu (TAMISEMI), Wizara ya Elimu na Ufundi pamoja na Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania (Tantrade) wameandaa maonyesho ya kwanza ya kimataifa ya elimu (TIEE) yanayotarajiwa kufanyika Disemba 17 hadi  21 mwaka huu katika viwanja vya Mwalimu Nyerere jijini Dar es Salaam.
Akizungumza jijini Dar es Salaam, Mkurugenzi Mkuu wa Global link Education, Abdulmalik Mollel, alisema lengo la maonyesho hayo ni kutambulisha wadau wa elimu kwa pamoja ili kuweza kutoa huduma ya pamoja kwa wananchi na kuwaelimisha juu ya mambo muhimu yaliyopo katika kila sekta.
Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania (Tan Tred), Jacqueline Mneney, akizungumza jambo.
Alisema ushiriki wa asasi mbalimbali kwa kushirikiana na sekta binafsi utakuwa na chachu ya mabadiliko ya elimu kwa kupitia mpango wa matokeo makubwa sasa.
Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania (TanTrade), Jacqueline Mneney, alisema wakati umefika kwa Watanzania kujua umuhimu wa maonyesho ya Elimu maana yamekuja kutatua matatizo mbali mbali waliyokuwa wakiyapata wazazi pindi wanapokuwa wanawatafutia shule na vyuo watoto wao.
Aidha alisema maonyesho hayo yataleta manufaa makubwa na changamoto chanya hasa katika kuongeza ushindani katika sekta ya elimu ambayo itasaidia mpango wa matokeo makubwa sasa.
Maonesho hayo yanatarajiwa kupata washiriki zaidi ya 500 na wananchi mbalimbali zaidi ya 350,000 kutoka ndani na nje ya nchi.
 
Kauli mbiu ya maonesho hayo ni ‘KUWEKA JITIHADA ZA PAMOJA KATIKA KUBORESHA MFUMO WA ELIMU TANZANIA NI NJIA THABITI YA KULETA MAENDELEO ENDELEVU KATIKA TAIFA.’

MAMA SALMA KIKWETE AFANYA KAMPENI KATIKA KATA ZA MTANDI NA MWENGE HUKO LINDI MJINI


Mke wa Rais na Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Chama Cha Mapinduzi, CCM, anayewakilisha Lindi Mjini, Mama Salma Kikwete akisalimiana na viongozi wa Kata ya Mtandi iliyoko Lindi Mjini wakati alipotembelea Kata hiyo kwa ajili ya kufanya mkutano wa kampeni katika uchaguzi wa viongozi wa serikali za mitaa unaotarajiwa kufanyika nchini kote tarehe 14.12.2014. unnamed1 
Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM anayewakilisha Lindi mjini na Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akionyesha ishara ya vidole viwili kuashiria kuunga mkono pendekezo la muundo wa serikali mbili nchini wakati alipozungumza na viongozi wa Chama Cha Mapinduzi wa Kata ya Mtandi tarehe 5.12.2014. unnamed2 
Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM anayewakilisha wilaya ya Lindi Mjini na Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akiwahutubia viongozi wa Chama Cha Mapinduzi wa Kata ya Mtandi katika mkutano uliofanyika katika Mtaa wa Maisara kwa ajili ya uchaguzi wa viongozi wa serikali za mitaa nchini unaotarajiwa kufanyika tarehe 14.12.2014. unnamed5 
Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM anayewakilisha wilaya ya Lindi Mjini na Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akiwahutubia viongozi wa Chama Cha Mapinduzi wa Kata ya Mtandi katika mkutano uliofanyika katika Mtaa wa Maisara kwa ajili ya uchaguzi wa viongozi wa serikali za mitaa nchini unaotarajiwa kufanyika tarehe 14.12.2014. unnamed6 
 Mama Salma Kikwete, Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Chama Cha Mapinduzi anayewakilisha Lindi Mjini akishiriki kucheza na baadaye kuwahutubia wananchi wa Kata ya Mwenge huko Lindi Mjini wakati akishiriki kuwapigia kampeni za uchaguzi wa viongozi wa serikali za mitaa unaotarajiwa kufanyika nchini kote tarehe 14.12.2014. unnamed7 unnamed8 
Baada ya kuhutubia mkutano wa kampeni kwenye Kata ya Mwenge huko Lindi Mjini Mama Salma Kikwete anaonekana akimbeba mtoto Juma Selemani ambaye naye alikuwa miongoni mwa watu waliohudhuria mkutano wa kampeni.
…………………………………………………..
Na Anna Nkinda – Lindi
Wanachama wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) wilaya ya Lindi mjini wametakiwa kutokubali kurubuniwa kwa kitu chochote kile ili wawapigie kura wagombea wa vyama vya upinzani  bali  waungane kwa pamoja katika kampeni na kuhakikisha chama hicho kinapata ushindi wa kishindo.
Mwito huo umetolewa jana na  Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) ya CCM kupitia wilaya ya Lindi mjini Mama Salma Kikwete wakati akiwanadi kwa wananchi wagombea wa chama hicho wanaowania nafasi za uongozi kwenye uchaguzi wa Wenyeviti na Wajumbe wa Serikali za Mitaa katika Kata ya Mwenge.
Mama Kikwete ambaye ni Mke wa Rais Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete alisema lengo la chama chochote cha Siasa ni kushika Dola kuanzia ngazi ya mtaa  hadi Taifa hivyo  basi wanachama hao wasikubali kurubuniwa bali waendelee kukitetea na kukipigania Chama chao ili kipate  ushindi katika mitaa yote 117 ya Kata hiyo.
“Viongozi wanaogombea tena wamechaguliwa kutokana na kazi yao nzuri. Nanyi ambao kura zeu hazikutosha wakati wa mchakato wa kuchagua msilaumu, bali muwapiganie  wagombea wote na kuhakikisha wanashinda angalieni maslahi ya chama kwanza  mambo binafsi baadaye”, alisema Mama Kikwete.
Aidha Mama Kikwete aliwaomba wananchi wa wilaya hiyo kutumia maarifa na ujuzi waliopewa na Mwenyezi Mungu wa kutambua mema na mabaya na kutokubali kudanganywa na kundi la watu wachache ili waipoteze amani yao.
Mama Kikwete alisema, “Wenzenu wamepiga hatua kubwa za maendeleo  katika mikoa yao huku Lindi Mwenyezi Mungu katupa neema maendeleo yanakuja sasa. Wanakuja huku kuwadanganya ili mfanye vurugu na kurudisha maendeleo yenu nyumba, msifuate mkumbo na kuchezea  amani kwani vurugu zinarudisha nyuma maendeleo”.
Aliwasihi wananchi waliohudhuria mkutano huo kuhakikisha watoto wao wanaenda shule ili wapate viongozi wazuri wa baadaye ambao watawaletea maendeleo kwani bila ya kuwa na elimu ni vigumu kupata maendeleo.
MNEC huyo pia aliwashukuru wanaume waliowaruhusu wake zao kugombea nafasi mbalimbali za uongozi na kuwapongeza wanawake kwa kutokukubali kubaki nyuma na kuomba kugombea nafasi hizo.
Mama Kikwete yupo wilayani humo kwa ajili ya shughuli za kichama ikiwa ni pamoja na kushiriki  kwenye kampeni na kuwanadi wagombea wa chama hicho wanaowania nafasi mbalimbali za uongozi katika uchaguzi wa viongozi wa Serikali za Mitaa, Vijiji na Vitongoji  utakaofanyika tarehe 14 mwezi huu.

MICHUANO YA WANAWAKE TAIFA CUP KUANZA DESEMBA 28

Twiga+Stars
Michuano ya Taifa ya mpira wa miguu kwa wanawake ya Proin Women Taifa Cup inaanza rasmi Desemba 28 mwaka huu kwa mechi ya ufunguzi kati ya timu za mikoa ya Mara na Mwanza itakayochezwa Uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza.
Kombaini za mpira wa miguu za mikoa yote ya Tanzania Bara zitashiriki mashindano hayo yatakayochezwa kwa raundi mbili mwanzoni, na baadaye hatua ya robo fainali hadi fainali.
Mashindano hayo yanayodhaminiwa na kampuni ya Proin Promotions Limited, kuanzia hatua ya robo fainali, mechi zote zitafanyika jijini Dar es Salaam.
Meneja Biashara wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania, Peter Simon Shankunkuli aliishukuru kampuni ya Proin ambao ni watengenezaji, wazalishaji na wasambazaji wa filamu za kitanzania kwa kuwezesha mashindano hayo kufanyika kwa mara ya kwanza
Proin Promotions imekua ikivumbua vipaji mbalimbali vya uigizaji na sasa imeamua kujikita katika mpira wa miguu ili kuweza kuvumbua vipaji kwa wachezaji wa kike.
Shankunkuli alisema nafasi bado zipo kwa wadhamini watakaoguswa na mashindano hayo, kwa kuwasiliana na TFF au Proin Promotions Limited kwa maelezo zaidi.

Waziri Mwakyembe awapongeza fastJet Kwa Huduma Nzuri kwa Wateja.

vvvvv3 
Ofisa wa Mahusiano na Masoko wa kampuni ya ndege ya FastJet Lucy Mbogoro akitoa maelezo kwa ujumbe kwa Waziri wa Uchukuzi Harrison Mwakyembe na ujumbe wake wakati wa maadhimisho ya siku ya anga duniani kushoto kwake ni Mwenyekiti wa Bunge ya Miundombinu, Peter Serukamba.
vvvvv6
Wafanyakazi wa kampuni ya ndege ya Fast Jet wakiwa kwenye picha ya pamoja
vvvvvv2
Wafanyakazi wa kampuni ya FastJet wakipita mbele ya mgeni rasmi ambae ni Waziri wa Uchukuzi Mh.Harrison Mwakyembe wakati wa maadhimisho ya siku ya anga duniani
vvvvvv4
Waziri wa Uchukuzi Harrison Mwakyembe akizungumza na wafanyakzi wa kampuni ya ndege ya FastJet wakati wa maadhimisho ya siku ya anga duniani ambapo aliipongeza kampuni hiyo kwa kutoa huduma kwa bei rahisi kwa wasafiri pembeni yake ni Mwenyekiti wa Bunge ya Miundombinu, Peter Serukamba.
vvvvvv5
Meneja Biashara wa FastJet, Jean Uku akitoa maelekezo kwa Waziri wa Uchukuzi HarrisonMwakyembe kuhusiana na utendaji kazi wa kampuni hiyo wakati wa maadhimisho ya siku ya anga duniani pembeni ya Mwakyembe ni Mwenyekiti wa Bunge ya Miundombinu, Peter Serukamba.
vvvvvvvvvvv
Waziri wa Uchukuzi HarrisonMwakyembe akizungumza na wafanyakzi wa kampuni ya ndege ya FastJet wakati wa maadhimisho ya siku ya anga duniani ambapo aliipongeza kampuni hiyo kwa kutoa huduma kwa bei rahisi kwa wasafiri.

KITUO CHA RADIO 5 WAANDA “KAMPENI YA RADIO 5 VIWANJANI”MSIMU HUU WA SIKUKUU YA XMASS NA MWAKA MPYA

SAM_0369
Radio 5 FM 105.7 imeandaa “kampeni ya RADIO 5 viwanjani” katika mkoa wa Arusha ambapo itawakutanisha watangazaji  na madjs na wasikilizaji wao katika kumbi za starehe kwa takribani wiki tano ikiwa ni sehemu ya kuwashukuru mashabiki wa Redio hiyo kwa kuwa pamoja kwa mwaka mzima huku mashabiki wakijipatia zawadi mbalimbali katika kampeni hiyo(katika picha ni Mtangazaji wa kituo cha Redio 5 Julius Kamafa aliyejizolea umaarufu mkubwa jijini Arusha kupitia kipindi chake cha funiko base kinachosikilizwa zaidi na vijana akishow love na msikilizaji wake katika kampeni  ya “Redio 5 viwanjani”ndani ya ACTIVE CLUB – Mbauda jijini Arusha
SAM_0349
Timu kazi ya Redio 5 wakifatilia show 
SAM_0350
Mtangazaji maarufu aliyejizolea umaarufu mkubwa  kupitia kipindi chake cha love cuts Semio Sonyo akiwa anauliza maswali kwa vijana wa Arusha waliofika katika kampeni ya Redio 5 viwanjani ndani ya ACTIVE CLUB – Mbauda jijini Arusha
SAM_0358
Meneja  ubunifu wa Redio 5 Vicky Mwakoyo akifurahia jambo katika kampeni ya Redio 5 viwanjani iliyofanyika jijini Arusha
SAM_0353
Mtangazaji maarufu aliyejizolea umaarufu mkubwa  kupitia kipindi chake cha love cuts Semio Sonyo akimuuliza maswali shabiki wa redio 5 katika kampeni ya Redio 5 viwanjani yenye nia ya kuwashukuru wasikilizaji wa kituo hicho kwa kuwa pamoja kwa mwaka mzima
SAM_0383
Meneja  ubunifu wa Redio 5 Vicky Mwakoyo kushoto akieleza nia ya kampeni hiyo itakayofanyika katika bar mbalimbali jijini hapa ambapo pia wasikilizaji wa kituo hicho watajizolea zawadi mbalimbali zikiwemo T-shart,vikombe,vinywaji kutoka TBL

Njuweni Institute Hoteli, Eden Hill College zatesa bonanza la vyuo mkoa wa Pwani(NACTE INTER COLLEGE DAR ES SALAAM).

Na: Mwandishi Wetu

Chuo cha njuweni Institute na Eden Hill College vyote vya mkoa wa Pwani mwishoni mwa wiki viliweza kutama kwenye Bonanza la Wanavyuo lililofanyika kwenye viwanja vya Shirika la elimu Kibaha ikiwa ni sehemu ya tatu kwa kanda ya kaskazini chini ya Kampuni ya Miss Demokrasia Tanzania  &  Entertainment C.o Ltd .
Timu ya Chuo cha Njuweni kwa upande wa mchezo wa mpira wa miguu ndiyo iliyong’ara zaidi huku ikifuatia na timu ya chuo cha Eden hill waliokuwa washindi wa ili na kujihakikishia kuingia kwenye hatua ya timu 32 bora za NACTE zitakazoshiriki kwenye fainali kubwa ya Kanda ya Kaskazini itakayofuata baada ya awamu hii ya mchujo wa awali kumalizika katika mfuno wa Bonanza.
Akizngumzia Bonanza hilo ambalo ni kwa ajili ya kupata timu zitakazoshiriki michuano ya NACTE,  Mkurugenzi wa chuo cha Njuweni Institute Hoteli, Bwana Saidi Mfinanga aliema kuwa ni jambo la kupendeza kutokana na kukutanisha vyuo mbalimbali kwa ajili ya kushiriki kwa pamoja michezo inayojenga ubora wa afya zao lakini pia ikiwa ni njia ya kuwaunganisha wanavyuo, Makampuni pamoja na wadau mbalimbali.
“mfumo huu unapendeza sana, na hata niwapongeze walioanziasha utaratibu huu wa vyuo vya elimu ya kati kukutanishwa na michezo, mimi binafsi hata chuo changu kisingetwaa nafasi ya kwanza lakini ningebaki na amani tu kwani huu ni mwanzo, lakini tuwapongeze hawa walioweza kubuni njia hii sahihi na uliokuwa tukiitamani wakati mwingi, mimi vijana wangu unisumbua sana inapofika wakati fulani wakidai niwatafutie timu wakacheze nao, huwa inasumbua sana lakini sasa ufumbuzi umekuja na si kwangu tu nadhani hata kwa wenzangu, tuwape ushirikiano hawa waliobuni hili jambo, na pia sisi wenyewe tujitunzie heshima zetu wakati tunashiriki siku zote katika michezo hii, michezo ni furaha, amani na upendo hivyo tushiriki kwa Upendo” alisema Mfinanga

Jumla ya Vyuo nane vilishiriki katika bonanza hilo linaloendelea katika siku za jumamosi kwa kushirikisha michezo ya Soka, Netball, Basketball na Voleyball, ambapo kwa upande wa mchezo wa Netball ni timu ya chuo cha Njuweni na Dacico waliofanikiwa kufuzu hatua ya pili huku Heden hili pia ikiibuka kidedea katika mchezo wa Basketball.
Aidha kwa upande wa mchezo wa Voleyball ni chuo cha Njuweni waliofanikiwa kuingiza timu huku vyuo vingine vikishindwa kuwasilisha wachezaji na hivyo kuwafanya njuweni kuingia hatua ya pili bila jasho katika mchezo huo.
Mratibu wa Michezo hiyo Vyuoni, Mpalule Shaaban alisema kuwa Michezo hiyo imeanza kwa kusuasua kutokana na washiriki wengi (Wanafunzi) kutokuwa na vifaa vya michezo jambo linalowapa tabu wakati wawapo michezoni.

“Jambo ni jema na hata mwitikio kwa wanavyuo pia ni mkubwa, lakini tatizo ninalolitazama hapa ni ukosefu wa vifaa vya michezo kwa vyuo pamoja na wachezaji wao, wengi hata viatu vya mchezo husika hawana wanacheza na viatu visivyokuwa vya mchezo husika, jezi wakati mwingine wanatumia hazina namba, hivyo bado ni tatizo kwa upande mwingine, ila kuhusu mwitikio wao kama wanafunzi wamependa sana michezo hii, kubwa tu mimi niombe kwa serikali na wadhamini wajitokee wasaidie michezo hii ya vyuo, Wanavyuo ndiyo wafanyakazi wa kesho hapo Ofisini kwako, sasa ni nani anapenda kuwa na mfanyakazi goigoi? Na hata watu binafsi kama wewe ni mdau jitokeze kusaidia vifaa vya michezo” alisema Mpalule.
Na kuongeza kwamba, heshima hii ni ya pekee ambayo Serikali imetoa kwa Vijana wa vyuo vya elimu ya kati kushiriki michezo, haijawahi kuwepo tangu NACTE imeanzishwa hivyo hii ni fulsa ya pekee tuliyonayo katika kuhakikisha kwamba tunahamasisha michezo hii wakati wote ili vijana wanaojiunga na Vyuo vya Elimu ya Ufundi, Veta, na wale wa ngazi ya Diploma kushiriki michezo vyuoni.

 Sehemu ya kwanza mpaka sehemu ya tatu zimefanyika mwezi uliopita kwenye viwanja vya D.I.T, Ustawi wa jamii kijitonyama na Viwanja vya Shirika la Elimu Kibaha ambako Vyuo mbalimbali vya NACTE mkoa wa pwani na dar es salaam vilicheza katika michezo ya soka, Basketball, Voleyball na netball katika kutafuta timu zitakazoshiriki ligi ya NACTE Tanzania katika msimu wa 2014/2015.


Ukiachilia mbali michezo hiyo, michezo mingine itakayokuwa ikifanyika kati ya wanafunzi na wanafunzi ni DEBATE, Marathon, Modoling, Mashindano ya Vipaji  kwa viongozi wanaosimamia serikali za wanafunzi kwa nafasi za Rais na Makamu, Waziri Mkuu, Mawaziri wa Michezo, Fedha,  na Spika , watakaokuwa wakichuana katika kujielezea, kujibu maswali, na kuelezea Mada katika nafasi zao na changamoto wanazokabiliana nazo na washindi watakuwa wakipata tuzo mbali mbali kulingana na ushindi wa kila mmoja.
Mwisho.