Kikosi cha Taifa Stars Maboresho
kinarejea leo Dar es Salaam kutoka Bulyanhulu mkoani Shinyanga ambapo
kiliweka kambi kwa ajili ya mechi ya kimataifa dhidi ya Burundi
itakayochezwa Desemba 9 mwaka huu.
Timu hiyo ambayo leo asubuhi
imefanya mazoezi kwenye Uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza, itatua
Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA) kwa ndege ya
Fastjet saa 12.30 jioni na kwenda moja kwa moja kambini hoteli ya
Tansoma.
Stars inayodhaminiwa na
Kilimanjaro Premium Lager kesho (Desemba 7 mwaka huu) itafanya mazoezi
asubuhi na jioni kwenye viwanja vya Gymkhana wakati keshokutwa (Desemba 8
mwaka huu) itafanya mazoezi jioni kwenye Uwanja wa Taifa
Nayo timu ya Taifa ya Burundi
inatua nchini keshokutwa (Desemba 8 mwaka huu) saa 10 jioni kwa ndege ya
RwandAir. Kikosi hicho kitafikia hoteli ya Tiffany Diamond kitakwenda
moja kwa moja Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam ambapo kitafanya mazoezi
kuanzia saa 11 jioni.
Kiingilio cha mechi kati ya
Tanzania na Burundi itakayochezwa Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam kuanzia
saa 10 jioni kitakuwa sh. 3,000 kwa viti vya raungi ya chungwa, bluu na
kijani wakati VIP B na C ni sh. 5,000 tu.
No comments:
Post a Comment