Ndege ya Fastjet FJA FN141
inayofanya safari kati ya Dar es Salaam na Mwanza, ikiwa imebeba abiria
142 iliruka kutoka airport ya kimataifa ya Julius Nyerere mida
ya takribani saa 12:49 asubuhi siku ya Alhamisi ya tarehe 4 Disemba
2014.Muda mfupi baada ya ndege kuruka chombo hicho kilikumbana na ndege
aliyekuwa akiruka. Kama sehemu ya maangalizi rubani wa ndege hiyo
aliamua kugeuza safari na kurudi katika uwanja wa Julius Nyerere, Dar
es Salaam.
Ndege ilitua salama bila
kashikashi zozote zile. Abiria wote na wahudumu wa ndege walikuwa salama
bila majeruhi ya aina yeyote ile.Abiria waliwekwa kwenye ndege za
baadae na mida ya safari za Fastjet za siku hiyo zilibadilika kimasaa
kutokana na msukosuko huo. Injini ya ndege husika ilirekebishwa ndani ya
siku moja na kuendelea na shughuli zake kesho yake siku ya tarehe 5
Ijumaa Disemba 2014.
Uongozi wa Fastjet unasisitiza kuwa usalama ni kitu muhimu
zaidi kwa kampuni ya Fastjet na inashukuru kwa uelewa wa wateja wote na
kuomba radhi kwa usumbufu wowote uliojitokeza.
No comments:
Post a Comment