TAN
Bayport
Kikoa
Myway entertainment
FORE PLAN CLINIC
MPINGA CUP 2016
Mashujaa Fm 89.3, Lindi
Sunday, December 14, 2014
KATIBU MTENDAJI BARAZA LA BIASHARA ZANZIBAR AZUNGUMZA NA WANAHABARI KUHUSU MKUTANO WA NANE WA BARAZA HILO
MAMA KIKWETE AWAPA TAHADHARI VIJANA KUTOKUBALI KUDANGANYWA NA KUTUMIWA KUFANYA VURUGU
Na Anna Nkinda –
Maelezo, Lindi
14/12/2014 Vijana wa wilaya ya Lindi mjini wametahadharishwa kutokubali kudanganywa na kutumiwa kufanya vurugu ambazo zinaharibu vitu vichache walivyonavyo na kwa kufanya hivyo wanarudisha nyuma maendeleo yao.
14/12/2014 Vijana wa wilaya ya Lindi mjini wametahadharishwa kutokubali kudanganywa na kutumiwa kufanya vurugu ambazo zinaharibu vitu vichache walivyonavyo na kwa kufanya hivyo wanarudisha nyuma maendeleo yao.
Tahadhari hiyo imetolewa jana na
Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) ya Chama Cha Mapinduzi (CCM)
kupitia wilaya hiyo Mama Salma Kikwete wakati akiwanadi wagombea wa
chama hicho kwenye mkutano wa kufunga kampeni za uchaguzi wa Wenyeviti
na Wajumbe wa Serikali za mitaa uliofanyika katika Kata ya Makonde.
Mama Kikwete ambaye ni Mke wa
Rais Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete alisema ni vyema vijana wakaelewa
historia ya nchi yao na kujua lipi jema na baya kwani kuna baadhi ya
wanasiasa wanawashawishi ili wafanye vurugu kwa madai kuwa hakuna
maendeleo yoyote yaliyopatikana jambo ambalo siyo kweli.
“Hao wanaowadanganya nyinyi
mfanye vurugu na kuharibu vile vichache mlivyonavyo eti kwa kuwa maisha
yenu hayajaimarika kwao hawafanyi hivyo, kwao kuna maendeleo na ninyi
mnazidi kujirudisha nyuma kimaendeleo. Msikubali mkoa wetu uwe sehemu
ya majaribio na kutumika kwa manufaa yao”.
Kama wangekuwa wanawapenda na
kutaka kuwasaidia ili muendelee wangewajengea hata shule ambazo
zingewafanya vijana na watoto wetu wasome, hapo hakuna kipingamizi kwani
Elimu ni mkombozi wa maisha na elimu inaleta maendeleo”, alisema Mama
Kikwete.
MNEC huyo alisema Serikali makini
ni lazima ijali maisha ya watu wake, kwa kutambua hilo Serikali ya CCM
imeimarisha miundo mbinu kwa kujenga barabara za lami, shule ili watoto
wasome na kuimarisha huduma za afya ikiwa ni pamoja na kujenga
Hospitali na vituo vya afya na kuhakikisha wahudumu wa afya
wanaongezeka.
Alisema, “Maisha bora kwa kila
mtanzania siyo Chama kinapita nyumba kwa nyumba kugawa pesa bali ni kwa
kuboresha miundombinu, kukiwa na shule watoto watasoma, kukiwa na
barabara nzuri wananchi wasafirisha mazao yao, kukiwa na huduma bora za
afya wananchi watatibiwa haya yakifanikiwa maisha ya mtu mmoja mmoja
yataimarika”.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa CCM
wilaya ya Lindi Mjini Muksini Rafii alisema katika uchaguzi huo ndani
ya wilaya hiyo wagombea za nafasi za wajumbe 147 na wenyeviti saba
wamepita bila kupingwa.
Kwenye mkutano huo mwanachama
mmoja aliyejulikana kwa jina la Raphael Mahuna kutoka Chama Cha
Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) ambaye alikuwa ni mgombea wa nafasi
ya Mwenyekiti wa mtaa wa National Housing kwa tiketi ya chama hicho na
mwanachama mmoja kutoka Chama cha Wananchi (CUF) walijiunga na Chama
Cha Mapinduzi.
Mahuna alisema ameamua kwa hiari
yake mwenyewe bila ya kulazimishwa kujiunga na CCM kwani alipokuwa
anagombea nafasi ya Mwenyekiti wa mtaa wa National Housing alishindwa
kufanya kampeni kwa kuwa alikosa wajumbe wa kumuunga mkono.
Katika uchaguzi wa Serikali za
mitaa, vijiji na vitongoji mkoani Lindi wagombea wa Chama Cha Mapinduzi
katika vitongoji 600, vijiji 87 na mitaa nane wamepita bila kupingwa.
SECURITYGROUP (T) LTD (SGA) WAFANYA USAFI KUADHIMISHA MIAKA 30 YA UTENDAJI KAZI NCHINI
Neno La Leo: Kwenda Kupiga Kura Ni Kwenda Kuchagua.
Leo ni siku ya kupiga kura kwenye
Serikali za Mitaa, Vijiji na Vitongoji. Huu ni Uchaguzi Muhimu sana
katika nchi. Uchaguzi huu ndio MSINGI wa siasa kubwa za Kitaifa.
Siasa ya nchi inaanzia kwenye
Mtaa, Kijiji na Kitongoji. Na hakika, siku ya leo ilipaswa uwe ni
uchaguzi pia kwa ngazi ya Manispaa na Halmshauri, kwa maana ya
kuwachagua Madiwani.
Inahusu Serikali za Mitaa ( Local
Goverment). Nimepata kuandika, kuwa Mahtama Ghandhi alipata kusema, kuwa
ukitaka kuujua moyo wa nchi, nenda vijijini.
Katika nchi zetu hizi, uchaguzi wa
leo ni kipimo cha Uchaguzi Mkuu ujao. Chama ama kambi itakayofaulu
kupata asilimia 80 ya viti vyote vinavyogombaniwa, basi, naweza kuandika
hapa, Kuwa ni ndio chama au kambi itakayounda Serikali baada ya matokeo
ya uchaguzi mkuu wa Oktoba mwakani.
Na kama kwenda kupiga kura ni
kwenda kuchagua swali ni je, wapiga kura wanajua wanachokwenda kuchagua?
Jibu, yumkini kuna wapiga kura wenye kwenda kuchagua sura na majina ya
watu, lakini, kwa wengi waliohamasika au kuhamasishwa kujiandikisha, leo
Jumapili wanakwenda kuchagua wanachokijua na kukiamini.
Na siasa ni itikadi, na kwenye
itikadi, kama nilivyoandika huko nyuma, kuwa kuna KULIA na KUSHOTO. Ni
imani. Hivyo, kuwa na msimamo kisiasa ina maana ya kusimama ama Kulia,
au Kushoto. Kushoto ni wenye mrengo wa Kijamaa na Kujitegemea na kujali
zaidi maslahi ya walio wengi. Kushoto ni Mrengo wenye kusimamia katika
Haki na Usawa kwenye jamii. Kulia ni upande wa Mabwanyenye ama Mabepari.
Ni wenye kuamini zaidi katika Mtaji na kukuza mtaji, bila kujali
maslahi ya wengi. Na walio kwenye upande huo, wanaamini, kuwa Kutokuwepo
kwa Usawa kwenye jamii ni jambo lisiloepukika.
Na kuna Katikati ya kiitikadi,
kwamba kuna waliosimama kati. Lakini, aliyesimama kati anapo
anapoegemea. Hivyo, kuna waliosimama kati wakiegemea Kushoto na wengine
wakiegemea Kulia. Nao waweza kuwa viongozi bora, kama mpiga kura
atafanya maamuzi yake.
Leo tunakwenda kuwachagua viongozi
wetu kwenye Mitaa yetu, Vijiji na Vitongoji. Na kuna kisa cha mume
aliyegombea nafasi ya uongozi. Alikwenda kituo cha kupigia kura na
mkewe. Kura zilipohesabiwa aliambulia kura moja, ya kwake mwenyewe.
Nyumbani akamuulizia mkewe; ” Hivi mke wangu hata wewe hukunipigia
kura?”
Mkewe akajibu: ” Mume wangu,
tulikwenda kupiga kura kumchagua Kiongozi Bora, na kama ingelikuwa
kumchagua Mume Bora, kura yangu ingeangukia kwako!”
Naam, e twendeni tukapige kura kuwachagua viongozi bora, nao watokane na itikadi bora wenye kuzisimamia.
Ni Neno La Leo.
6TH ANNIVERSARY GROOVEBACK PARTY 2014 YAFANA NA BIA YA WINDHOEK DRAUGHT NDANI YA THE ARCADE HOUSE.
Meneja
Biashara wa Bia ya Windhoek Joseph Boniface akielezea kuhusiana na
Grooveback Party ambayo wao wamekuwa wadhamini wakuu kwa mwaka 2014
katika kutimiza miaka sita ya Grooveback
Wa
pili kushoto ni Msimamizi wa Windhoek Salum Kabanda akielezea ni jinsi
gani wanavyotoa fursa kwa vijana na kuweza kuitumia hususani kwa
wanamuziki ambapo wanaandaa matamasha mbalimbali na kuweza kuwa
wadhamini wakuu hivyo kuwapa changamoto vijana kwa kuweza kuandaa
michanganuo mbalimbali ya kazi kuifikisha kwao na kuifanyia kazi kwa
kuwasaidia.
Wahudumu
wa The Arcade wakiwa katika Pouzi wakati wakiwahudumia wateja wao
waliofika katika Sherehe ya Miaka Sita ya Grooveback iliyofanyia jana
Dj JB akiendelea kumwaga Burudani ya nguvu ya ngoma za Zamani na kukuna nyoyo za watu wengi waliofika katika Sherehe hiyo.
Wapambe wa Windhoek wakiwa wanapata Picha ya pamoja wakati wa Sherehe ya kuadhimisha Miaka sita ya Grooveback
Dj Nijo ambaye aliingia kwa awamu ya pili na kubadirisha radha ya muziki wa Lingara zile za Kitambo na kukonga nyoyo za wengi
6th Anniversary Grooveback Party 2014 Cheers ! na Windhoek Draught
Party ikiwa inaendelea huku Windhoek Draught zikiwa zimezagaa kwa kila Meza!
Dj
Pierra Kutoka Nchini Kenya nae hakuwa nyuma kuendeleza Burudani ya
Muziki kwa ajili ya Kusherekea Grooveback Party iliyotimizia Miaka sita
Ni mwendo wa ku party…..
Mashabiki wa Grooveback na watumiaji wa Windhoek Draught wakiwa katika Tabasamu la Hatari …
Dj KT kutoka Tanzania akiwa anaangusha bonge la moja Burudani …..
Hakuna kulala full ku party …
DJ
Pinye Mkali kutoka nchini Kenya .. akiangusha Burudani … Hii ilikuwa
hatare sana Mashabiki walifurahia Burudani hii ya nguvu.
Twende Dj Pinye….
Dj Crusia Toni kutoka Nchini Kenya akiendelea na Burudani ya Nguvu … Party inaendela..
Sumaye kubariki Tamasha la Krismas Mbeya
WAZIRI Mkuu mstaafu, Frederick
Sumaye, anatarajiwa kuwa mgeni rasmi wakati wa Tamasha la Krismas
Desemba 25 mwaka huu Uwanja wa Sokoine, Mbeya.
Taarifa kwa vyombo vya habari
iliyotolewa na Mwenyekiti wa Kamati ya Maandalizi ya tamasha hilo, Alex
Msama ilieleza kuwa maandalizi kuhusiana na tamasha hilo yanaenda
vizuri.
“Tulikubaliana katika kamati
tumuombe Waziri Mkuu mstaafu Sumaye aje atupe baraka kwenye tamasha la
Krismasi, nafurahi kusema ni mtu wa watu, amekubali kujumuika na wadau
wengine siku hiyo. Hili ni jambo la furaha kubwa kwetu.
“Wasanii mbalimbali tunaendelea kuzungumza nao kuhakikisha wanashiriki katika tamasha hilo,” alisema Msama katika taarifa yake.
Sumaye alikuwa Waziri Mkuu
katika Serikali ya Awamu ya Tatu kuanzia mwaka 1995 hadi mwaka 2005,
akiwa ndiye Waziri Mkuu aliyekaa muda mrefu katika wadhifa huo kwa
historia ya Tanzania.
Alisema wamepanga kufanya
maboresho makubwa katika tamasha hilo na moja ya maboresho hayo ni
kuweka kiingilio rahisi zaidi ili kila mmoja aweze kuhudhuria na kupata
baraka kutoka kwa waimbaji hao wanaomsifu Mungu.
“Waimbaji wote maafuru wa muziki
wa Injili watakuwepo, kwani tumejipanga vizuri mno kuhakiksha kwamba
tamasha hili litakuwa gumzo kila mahali.
“Wapendwa wajiandae kushiriki
kwa wingi kwani watashiba kiroho kutokana na kuwa na waimbaji wengi
wenye hamasa ya kiroho,” anasema. Baada ya onesho la Desemba 25 mkoani
Mbeya, siku inayofuata itakuwa Uwanja wa Samora Iringa na Desemba 28
Uwanja wa Majimaji Songea.
Tigo yadhamini maonesho ya Tehema kwa vijana, Viwanja vya Posta Moja
PSPF YAPATA TUZO YA KIMATAIFA KWA KUTOA HUDUMA BORA KWA WATEJA WAKE
MIKUTANO YA KAMPENI KATIKA KATA ZA JAMHURI NA MAKONDE HUKO LINDI MJINI ZANOGESHWA NA HUTUBA ZA MAMA SALMA KIKWETE
TANGAZO LA KIFO CHA MAMA MZAZI WA AKINA MWAIBALE
Twitikege Mlagha Mafumu enzi za uhai wake
Familia ya Mwaibale inatangaza kifo cha mama yao mpendwa, Twitikege
Mlagha Mafumu kilichotekea leo saa 5 usiku wakati akipelekwa Hospitali
ya Hindu Mandal jijini Dar es Salaam kwa ajili ya matibabu.
Mipango ya mazishi inafanywa nyumbani kwa mtoto wake Mwalimu Mary Anyitike, eneo la Bucha Mbagala Kuu jijini Dar es Salaam.
Kwa
mawasiliano zaidi wasiliana na ndugu Kulwa Mwaibale kwa simu namba
0712-707630, O758-971351 na Dotto Mwaibale kwa namba ya simu
0712-727062, O786-858550, 0754-362990.
Bwana alitoa na Bwana ametwaa jina lake lihimidiwe.
Subscribe to:
Posts (Atom)