WAZIRI Mkuu mstaafu, Frederick
Sumaye, anatarajiwa kuwa mgeni rasmi wakati wa Tamasha la Krismas
Desemba 25 mwaka huu Uwanja wa Sokoine, Mbeya.
Taarifa kwa vyombo vya habari
iliyotolewa na Mwenyekiti wa Kamati ya Maandalizi ya tamasha hilo, Alex
Msama ilieleza kuwa maandalizi kuhusiana na tamasha hilo yanaenda
vizuri.
“Tulikubaliana katika kamati
tumuombe Waziri Mkuu mstaafu Sumaye aje atupe baraka kwenye tamasha la
Krismasi, nafurahi kusema ni mtu wa watu, amekubali kujumuika na wadau
wengine siku hiyo. Hili ni jambo la furaha kubwa kwetu.
“Wasanii mbalimbali tunaendelea kuzungumza nao kuhakikisha wanashiriki katika tamasha hilo,” alisema Msama katika taarifa yake.
Sumaye alikuwa Waziri Mkuu
katika Serikali ya Awamu ya Tatu kuanzia mwaka 1995 hadi mwaka 2005,
akiwa ndiye Waziri Mkuu aliyekaa muda mrefu katika wadhifa huo kwa
historia ya Tanzania.
Alisema wamepanga kufanya
maboresho makubwa katika tamasha hilo na moja ya maboresho hayo ni
kuweka kiingilio rahisi zaidi ili kila mmoja aweze kuhudhuria na kupata
baraka kutoka kwa waimbaji hao wanaomsifu Mungu.
“Waimbaji wote maafuru wa muziki
wa Injili watakuwepo, kwani tumejipanga vizuri mno kuhakiksha kwamba
tamasha hili litakuwa gumzo kila mahali.
“Wapendwa wajiandae kushiriki
kwa wingi kwani watashiba kiroho kutokana na kuwa na waimbaji wengi
wenye hamasa ya kiroho,” anasema. Baada ya onesho la Desemba 25 mkoani
Mbeya, siku inayofuata itakuwa Uwanja wa Samora Iringa na Desemba 28
Uwanja wa Majimaji Songea.
No comments:
Post a Comment