TAN

TAN

Bayport

Bayport

Kikoa

Kikoa

Myway entertainment

Myway entertainment

FORE PLAN CLINIC

FORE PLAN CLINIC

MPINGA CUP 2016

MPINGA CUP 2016

Mashujaa Fm 89.3, Lindi

Thursday, March 12, 2015

Magereza Watinga Kilele cha Mlima Kilimanjaro

1

BARAKA SHELUKINDO ATOA TAHADHARI JUU YA MATAPELI WA MITANDAONI

unnamed (4)

WADAU wameuomba Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya NHIF kuendeleza upimaji wa afya bure KWA wanachama wake na wananchi

Wednesday, March 11, 2015

MSHINDI PROMOSHENI YA ‘WEKA NA USHINDE’ AONDOKA NA GARI

Mkurugenzi Mtendaji wa BOA bank Tanzania, Bw. Ammish Owusu-Amoah, akiangalia funguo za gari hilo kabla ya kumkabidhi, Bw. Said Mohamed Bakari, mshindi wa gari aina ya Toyota Berevis, baada ya kushinda promosheni ya ‘Weka na Ushinde’ iliyoendeshwa na benki hiyo, Dar es Salaam leo. Kulia ni Afisa wa Benki hiyo, Bw. Solomon Haule.
Mshindi wa Gari Bw. Bw. Said Mohamed Bakari akingia ndani ya gari hilo leo baada ya kukabidhiwa
Mkurugenzi Mtendaji wa BOA bank Tanzania, Bw. Ammish Owusu-Amoah akizungumza na waandishi wa habari baada ya kukabidhi zawadi ya gari kwa mshindi.
Waandishi wa habari wakizungumza na mshindi wa promosheni ya gari, Bw. Said Mohamed Bakari

Mwakilishi wa mshindi wa pili wa Promosheni ya ‘Weka na Ushinde’, Bi. Rhoda Manase (aliyemwakilisha Bi. Thureiya Zabron) akipoke pikipiki hiyo kutoka kwa Mkurugenzi Mtendaji wa BOA bank Tanzania, Bw. Ammish Owusu-Amoah Dar es Salaam leo.
“Tumemaliza salama”, ndivyo wanavyosema Mkurugenzi Mtendaji wa BOA benk Tanzania, Bw. Ammish Owusu-Amoah na Afisa wa Benki hiyo, Bw. Solomon Haule, baada ya kukabidhi zawadi kwa washindi leo

PINDA AKUTANA NA RAIS WA KAMPUNI YA CONTRACTUS YA POLAND

pol1 Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akizungumza na  Makamu wa Rais wa  Kampuni ya Contractus ya Poland, Bw. Witold Kartzewski (wapili kulia) na watendaji wa kampuni hiyo, Daniel Junusz (kulia) na Honorata Musloviska Ofisini kwake jijini Dar es salaam Machi9, 2015. Kampuni hiyo pamoja na mambo mengine bingwa katika  ujenzi wa vihenge vya kisasa vyenye uwezo wa kuhifadhi tani nyingi za nafaka. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

PINDA AKUTANA NA BALOZI WA KUWAIT NCHINI

pin1 Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akisalimiana na balozi wa Kuwait nchini, Mhe Jaseem Al Najem kabla ya mazungumzo yao, ofisini kwa Waziri Mkuu jijini Dar es salaam Machi 9, 2015. (Picha na ofisi ya Waziri Mkuu) 
pin2 Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akizungumza na balozi wa Kuwait nchini, Mhe. Jaseem Al Najem, Ofisini kwake jijini Dar es salaam Machi 9, 2015. Katikati ni Ofisa wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Batholomeo Jungu. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

Mrembo Miss Tanzania aongoza wakazi wa dar katika zoezi la uchangiaji damu

Mshindi
wa tatu wa Miss Tanzania 2014,Doris Mollel akishiriki zoezi la
uchangiaji damu katika ikiwa ni sehemu ya kusherehekea Siku ya wanawake
Duniani,iliyofanyika Buguruni Chama jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki. Kushoto
Ofisa Muuguzi kutoka Benki ya Damu Salama,Selina Joseph. Zoezi hilo la
uchangiaji damu liliandaliwa na Mrembo huyo. Katika kuadhimisha siku ya wanawake duniani,mrembo Doris Mollel
ambaye ni Miss Tanzania namba tatu kwa mwaka 2014 ameongoza mamia ya
watanzania katika zoezi la kizalendo la kuhamasisha kuchangia damu kwa
watanzania kwa ajili ya wagonjwa mbalimbali,zoezi ambalo limefanyika
jijini Dar es salaam mwishoni mwa wiki. 
Zoezi hilo ambalo lilikuwa
linaongozwa na mpango wa taifa wa damu salama kwa udhamini wa kampuni ya
METL lilikuwa na lengo la kupata damu kwa ajili ya kuokoa maisha ya Mama na Mtoto kwani matatizo ya damu katika hospitali za Tanzania
yamekuwa yakiongezeka siku hadi siku,jambo lililompelekea mrembo huyo
kuamua kujitoa kuhamasisha watanzania kujitokeza kwa wingi katika zoezi
hilo. 

43 WAAPISHWA KUWA MANAIBU WASAJILI WA MAHAKAMA YA TANZANIA LEO JIJINI DAR ES SALAAM.

 Jaji Kiongozi wa Mahakama Kuu ya Tanzania Mhe. Shaaban Ali Lila akimwapisha Mhe. Lenatus Ishengoma (kulia) kuwa Naibu Msajili wa Mahakama ya Tanzania leo jijini Dar es salaam. Wanaoshuhudia kiapo hicho ni Jaji Mkuu wa Tanzania Mhe. Mohamed Othman Chande (kushoto) na Mhe. John Kahyoza, Msajili Mahakama Kuu ya Tanzania.
 Jaji Kiongozi wa Mahakama Kuu ya Tanzania Mhe. Shaaban Ali Lila akimkabidhi Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Mwongozo wa utendaji kazi wa Mahakama Mhe. Zahara Abdallah Mlacha mara baada ya kumwapisha kuwa Naibu Msajili wa Mahakama ya Tanzania leo jijini Dar es salaam.
Mhe. Elizabeth Mkwizu  akisaini hati ya kiapo cha kuwa Naibu Msajili wa Mahakama mbele ya Jaji Kiongozi Mhe. Shaaban Ali Lila baada ya kuapishwa leo leo jijini Dar es salaam.
 Naibu Msajili wa Mahakama ya Tanzania Mhe. Hussein Shaaban Mushi akipokea Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Mwongozo wa utendaji kazi wa Mahakama  kutoka kwa Jaji Kiongozi  Mhe. Shaaban Ali Lila mara baada ya kuapishwa kuwa Naibu Msajili wa Mahakama ya Tanzania leo jijini Dar es salaam.
 Mhe. Isaya Khalfan (kulia) akila kiapo cha kuwa Naibu Msajili wa Mahakama ya Tanzania mbele ya Jaji Kiongozi wa Mahakama Kuu ya Tanzania Mhe. Shaaban Ali Lila (kulia) leo jijini Dar es salaam.
Jaji Kiongozi wa Mahakama Kuu ya Tanzania Mhe. Shaaban Ali Lila (aliyekaa) akisaini kiapo cha Mhe. Angela Maria Thei (kulia) aliyeapishwa kuwa  Msajili wa Mahakama ya Tanzania katika hafla fupi iliyofanyika viwanja vya Mahakama ya Rufani leo jijini Dar es salaam. Anayetazama kiapo hicho ni Msajili wa Mahakama kuu ya Tanzania Mh. John Kahyoza (katikati).Picha na Aron Msigwa –MAELEZO.

Tuesday, March 10, 2015

Jumuiya ya Bango Sangho watoa huduma za afya bure Kibugumu

Dk Hamza Mzige kutoka Hospitali ya Wilaya ya Kisarawe akimpima moja ya mtoto aliyeletwa kupata huduma katika zoezi hilo lililoendeshwa eneo la Kibugumu Kigamboni jijini Dar es Salaam.
Dk Hamza Mzige kutoka Hospitali ya Wilaya ya Kisarawe akimpima moja ya mtoto aliyeletwa kupata huduma katika zoezi hilo lililoendeshwa eneo la Kibugumu Kigamboni jijini Dar es Salaam.
Mratibu wa huduma hizo, Dk. Ali Mzige (wa kwanza kulia) akitoa huduma kwa wagonjwa katika zoezi hilo.
Mratibu wa huduma hizo, Dk. Ali Mzige (wa kwanza kulia) akitoa huduma kwa wagonjwa katika zoezi hilo.
Mmoja wa wahudumu wa afya akitoa huduma kwa baadhi ya watoto waliofikishwa katika zoezi hilo lililoendeshwa eneo la Kibugumu Kigamboni jijini Dar es Salaam.
Mmoja wa wahudumu wa afya akitoa huduma kwa baadhi ya watoto waliofikishwa katika zoezi hilo lililoendeshwa eneo la Kibugumu Kigamboni jijini Dar es Salaam.
Dk Hamza Mzige kutoka Hospitali ya Wilaya ya Kisarawe akitoa huduma kwa mmoja wa wateja wake katika zoezi hilo.
Dk Hamza Mzige kutoka Hospitali ya Wilaya ya Kisarawe akitoa huduma kwa mmoja wa wateja wake katika zoezi hilo.

BALOZI WA HARAKATI ZA “IMETOSHA!” HENRY MDIMU APELEKA UJUMBE WAKE UWANJA WA TAIFA

Na Henry Mdimu
Tangu asubuhi leo nilikuwa busy na awareness za uwanja wa Taifa katika mechi ya watani wa Jadi Yanga na Simba (picha ya pili). Ila jioni hii nilipoangalia simu yangu nikakuta watu wakinilaumu kutokana na tukio la mtoto Baraka Cosmas (picha ya kwanza) ambaye usiku wa kuamkia leo amekatwa mikono yake. 
Wanasema nilikuwa nakula Bata Uwanja wa Taifa huku watu wanateketea.
Hasa alikuwa akiongea mtu anaitwa @hmgeleka. 
Kwanza nalaani kitendo hicho cha kikatili  na kuzidi kumuomba Rais wangu Mhe Jakaya Mrisho Kikwete aongee na vyombo vyake vya usalama, wasiliache hili lipite hivi hivi. 
Lakini jingine jamani suala hili sio la mmoja. Kwa sababu nimejitwika ubalozi ndio nilaumiwe kwa hata lililo mbali na mimi?
Vita hii ni ya wote, mimi nina wiki mbili tu tangu nianze kazi hii na bado natafuta mtaji wa kuendesha zoezi langu.
Tafadhali tutende wote tusinyoosheane vidole, huku tukiwa vijiweni, mmenielewa?
#IMETOSHA
 Bango la harakati za “Imetosha!” likiingizwa uwanjani sambamba na ya FIFA ma FIFA Fair Play wakati wa mchezo wa ligi kuu wa watani wa jadi Simba na Yanga Uwanja wa Taifa leo. Chini ni Balozi wa Harakati za Imetosha Henry Mdimu akiongea machache kuhusu harakati hizo zenye lengo la kuhamasisha wadau wote kukomesha vitendo vya mauaji na vya kikatili dhidi ya ndugu zete Albino.

NHIF MOROGORO YAADHIMISHA WIKI YA WANAWAKE KWA KUTEMBELEA KITUO CHA WATOTO YATIMA MKOANI MOROGORO

ha1 
Katika kuadhimisha wiki hiyo Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya ulitembelea kituo cha watoto yatima cha Aldee Musleem Chidren Centre cha Morogoro , na kugawa vitu mbalimbali ili kukidhi mahitaji ya kituo hicho vikiwemo vyandarua, vyakula na vifaa vya shule kama anavyoonekana Kiongozi wa msafara wa wafanyakazi wa NHIF Bi. Rose Ongara akikabidhi zawadi hizo kwa mmoja wa viongozi wa kituo hicho Bwana Rajabu Shomari. ha2Baadhi ya watoto wa kituo hicho wakikabidhiwa zawadi hizo na kiongozi wa msafara kutoka NHIF Bi Rose Ongara pamoja na wafanyakazi wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya mkoani Morogoro. ha3Bi.Rose Ongara akifurahi na watoto wa kituo hicho wakati akikabidhi zawadi hizo.

KATIBU MKUU WA CCM NDUGU ABDULRAHMAN KINANA AMALIZA ZIARA YAKE CHILONWA, KESHO KUENDELEA JIMBO LA MTERA

2 Katibu Mkuu Ndugu Abdulrahman Kinana akipuliza dawa ya kuua wadudu wanaoshambulia zabibu kwenye shamba la mradi wa kilimo cha zabibu katika kijiji cha Chinangali II wilayani Chamwino Kinana yuko katika ziara ya mikoa mitatu ya Dodoma, Arusha na Kilimanjaro akihimiza na kukagua utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya CCM ya mwaka 2010 akiongozana na Nape Nnauye Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi ambapo kesho atakuwa katika jimbo la Mtera linalowakilishwa na mbunge kijana machachali Mh. Livingstone Lusinde.(PICHA NA KIKOSIKAZI CHA FULLSHANGWE- CHAMWINO -DODOMA) 3Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Dodoma Mh. Adam Kimbisa naye akishiriki katika kazi ya kupuliza dawa ya kuuwa wadudu katika shamba la Zabibu katika kijiji cha Chinangali II.

WEMA SEPETU NDANI YA STUDIO ZA RADIO 5 JIJINI ARUSHA

SAM_1388
Wema Sepetu akiwa ndani ya studio za Radio 5 jana mara baada yan kufanya ziara fupi mjengoni hapo akielezea pia kuhusu show yake ya black and white party iliyofanyika jana usiku tarehe 7/3/2015 jijini Arusha kushoto ni mtangazaji mahiri wa kituo hicho Wilfredy akiwa anafanya kipindi na mwanadada huyo, Wanaonekana pichani ni team Wema.(Habari Picha na Pamela Mlollel wa jamiiblog)
SAM_1387
Wema Sepetu akiwa anaeleza furaha yake yakuwepo jiji Arusha ambapo amesema jiji la Arusha ni miongoni mwa majiji anayoyapenda, Mwanza ikiwa ya kwanza na Arusha ya pili, Kulia ni msanii Petiman a.k.a Wakuache.
SAM_1372
Msafara wa Wema Sepetu ukiingia kwa mbwembwe katika studio za Radio5 zilizopo njiro jijini Arusha.

WANAWAKE WA MSD WASHEREHEKEA SIKU YA WANAWAKE DUNIANI KWA AINA YAKE.

 Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa (MSD), Bw. Cosmas Mwaifani akifungua sherehe za Siku ya Akina Mama Duniani zilizofanyika.
Bw. Mwaifani akimkaribisha mgeni rasmi wa sherehe hizo, Bi.Helen Mwakipunda ambaye ni Mhasibu Mkuu wa Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii.
Bi. Mwakipunda akizungumza na wafanyakazi wa (MSD) wakati wa sherehe hizo

CMEA ni suluhilisho kwa wanamuziki- January Makamba

jan1
Naibu Waziri Sayansi na Teknolojia January Makamba akizungumza wakati wa uzinduzi wa kampuni ya na kampuni ya Copyrights Management East Africa Limited (CMEA).
jan2
Afisa Mtendaji Mkuu wa CMEA, Paul Matthysse akisisitiza jambo wakati wa uzinduzi wa kampuni hiyo yenye lengo la kuwakwamua wanamuziki katika umaskini. CMEA pia  itawawezesha pia watayarishaji wa muziki na wasanii wengine pamoja na vyombo vya habari kupata kufahami takwimu sahihi za nymbo zilizochezwa kwa siku, wiki, mwezi na kwa mwaka.
…………………………………………………………………………………………..

MAMA SALMA KIKWETE MGENI RASMI KILELE CHA SIKU YA WANAWAKE DUNIANI MKOANI DAR

RAY1Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akipokewa na Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Ndugu Raymond Mushi wakati akiwasili kwenye viwanja vya Mnazi Mmoja katika kilele cha maadhimisho ya siku ya wanawake duniani mkoani Dar esb Salaam terehe 8.3.2015. RAY3 Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akipunga mkono ikiwa ni ishara ya kuyapokea  maandamano ya akina mama wa Mkoa wa Dar es Salaam kwenye viwanja vya Mnazi Mmoja wakati wa kilele cha maadhimisho ya siku ya wanawake duniani tarehe 8.3.2015.

RAIS DR. SHEIN AFUNGUA WA HOTELI YA PARK HYATT ZANZIBAR

sh1Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (kushoto) akifungua pazia kuashiria ufunguzi wa Hotel ya Park Hyatt Zanzibar iliyopo Mambo Msiige Mji Mkongwe wa Zanzibar (kulia) Kaimu Waziri wa Fedha na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Ikulu na Utawala Bora Dkt.Mwinyihaji Makame Mwadini (katikati) Mmiliki wa Hoteli hiyo Sheikh Ali Sayeed  Albawardy [Picha na Ikulu.] sh2Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (katikati) akikata utepe kama ishara ya ufunguzi wa Hotel ya Park Hyatt Zanzibar iliyopo Mambo Msiige Mji Mkongwe wa Zanzibar (kulia) Kaimu Waziri wa Fedha na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Ikulu na Utawala Bora Dkt.Mwinyihaji Makame Mwadini (kushoto) Mmiliki wa Hoteli hiyo Sheikh Ali Sayeed  Albawardy [Picha na Ikulu.]

Moruwasa kufanya upanuzi wa bwawa la Mindu

bw1
Hussein Makame-MAELEZO MAMLAKA ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Manispaa ya Morogoro (MORUWASA) imepanga kuongeza uwezo wa bwala la Mindu mara mbili zaidi ili liweze kukusanya maji mengi zaidi kukidhi mahitaji ya maji ya wakazi wa manispaa ya Morogoro.
Akizungumza na waandishi wa habari waliomtembelea ofisi kwake mjini Morogoro mwisho mwa wiki hii, Mkurugenzi Mtendaji wa Mamlaka hiyo Mhandisi Nicholaus Angumbwike, alisema pia wamepanga kujenga mtambo mwengine wa kutibu maji ili kuongeza kiasi cha maji kutoka chanzo hicho. Alisema tayari mkandarasi ameshaandaa pendekezo la mradi (proposal) kupitia awamu ya kwanza ya Programu ya Maendeleo ya Sekta ya Maji (WSDP) na kwamba imeshakamilika na ameiwasilisha Wizara ya Maji kwa ajili ya utekelezaji. Mhandisi Angumbwike aliongeza kuwa wanatarajia kwamba utekelezaji wa mradi huo utafanyka katika awamu ya pili ya WSDP iliyoanza Juni mwaka jana iwapo Wizara itawapatia fedha kwa ajili ya kazi hiyo. “Kuna utafiti imeshafanyika kuhusu bwawa la Mindu, kuna uwezekano kwamba uwezo wa bwala la Mindi ukaongezeka mara mbili zaidi yaani uwezo wa kukusanya maji mengi zaidi kuliko ilivyo sasa na tukajenga mtambo mwengine wa kutibu maji ili kuongeza kiasi cha maji yanayotoka chanzo cha bwawa la Mindu” alisema Mhandisi Angumbwike na kuongeza: “Hii kazi imeshafanyika katika mradi wa WSDP awamu ya kwanza, mkandarasi amefanya akaandaa proposal yake na tuna matumaini kwamba ameshakamilisha na amewasilisha Wizara ya Maji, tunatarajia katika hii awamu ya pili kama Wizara ikitufikiria tuweze kutekeleza mradi huo”

Alisema kinachotakiwa kufanyika ni kuongeza tena urefu wa tuta la bwawa hilo kwa urefu wa mita 2 na kujenga mtambo mwingine wa kutibu maji kwani mtambo ulipo una uwezo wa kutibu maji kwa siku lita milioni 27 tu. Aliongeza kuwa gharama za mradi huo wa kuongeza uwezo wa chanzo hicho cha maji cha bwawa la Mindu na mtambo wa kutibu maji, kwa mwaka 2008 ilikuwa ni shilingi Bilioni 35. Alisema mbali na juhudi hizo MORUWASA imekuwa ikitafakari vyanzo vingine vya maji kukidhi mahitaji ya wakazi 315,000 wa manispaa ya Morogoro ikiwemo kufikiria kwenda juu zaidi ya milima ya Uluguru kutafuta vyanzo hivyo. Alisema wanaangalia uwezekano wa kuchimba visima virefu lakini changamoto iliyopo ni kwamba ni shida kupata maeneo ambayo watapata maji baridi kwa sababu maeneo mengi ya Morogoro ukichimba unapata maji ya chumvi. Kwa upande wa uboreshaji wa miundombinu chakavu, Mhandisi Angumbwike alisema wamepokea fedha kiasi cha shilingi Milioni 240 kutoka Wizara ya Maji ambayo itatusaidia kubadilisha kilomita kadhaa ya miundombinu ya maji iliyochakaa ili kuboresha upatikanaji wa maji. Katika kuhakikisha wanatunza vyanzo vya maji vilivyopo, Mhandisi Angumbwike alisema wanashirikia na wadau wengine kama Ofisi ya Bonde la Maji, Ofisi ya Mkuu wa Wilaya na Ofisi ya Mkurugenzi wa Halmashauri ya Manispaa ya Morogoro, katika kulinda vyanzo hivyo. “Tumekuwa tukifanya kazi pamoja, tunakutana pamoja tunakwenda kwenye miradi (sites) tumeainisha maeneo ambayo yanataka kuyatunza, tumetoa elimu kwa wananchi watambue kwamba jukumu la kutunza vyanzo vya maji ni la kila Mtanzania na wao wakiwemo”alisema na kuongeza: “Wananchi wanatakiwa watambue kwamba jukumu la kutunza vyanzo vya maji ni muhimu kwa manufaa ya Watanzania wote” Kuhusu wizi wa maji, Mkurugenzi huyo alisema wana Operesheni za kukamata watu wanaojiunganishia maji kwa kupita nyumba kwa nyumba ili kuwabaini na kuwakamata watu ambao wanatumia maji bila kuyalipia. “Wapo watu ambao wanataka wapate maji bila kuyalipia, tunafanya operesheni nyumba kwa nyumba na tunapowakamata tunawatoza faini na kuwachukulia hatua lakini shida kubwa ni uunganishaji mwingine ni ngumu kuubaini” alisema Mkurugenzi huyo na kuongeza: “Wapo tuliowakamata kwa ushirikiano na wananchi na tunatoa motisha wa fedha kwa wananchi wanaotupa taarifa hizo. Pia tunacho kikosi maalum kinachopita mitaani na katika hoteli mbalimbali kuchunguza mifumo ya maji ili kubaini watu wanaoiba maji. Tumeshakamata baadhi ya hoteli zimejiunganishia maji, tukawauliza wanasema wamechimba kisima lakini baada ya kupima sampuli ya maji tunakuta kwamba ni maji ya Morowasa” Hivyo aliwataka wananchi kuendelea kutoa ushirikiano kwa kuwafichua wezi wa waji au watu wanaojiunganishia maji kiholela ili kudhibiti asimilia 40 ya maji ambayo hayaipatii mapato MORUWASA.
Programu ya Maendeleo ya Sekta ya Maji (WSDP) ya mwaka 2006 hadi 2025, inatekelezwa kwa awamu ya miaka mitano mitano ambapo awamu ya Kwanza ilianza mwaka 2007 na kukamilika 2014 na awamu ya Pili ilizunduliwa na Waziri wa Maji Juni mwaka jana tayari kwa utekeleaji.