Mkurugenzi
Mtendaji wa BOA bank Tanzania, Bw. Ammish Owusu-Amoah akizungumza na waandishi
wa habari baada ya kukabidhi zawadi ya gari kwa mshindi.
Waandishi wa
habari wakizungumza na mshindi wa promosheni ya gari, Bw. Said Mohamed Bakari
Mwakilishi
wa mshindi wa pili wa Promosheni ya ‘Weka na Ushinde’, Bi. Rhoda Manase
(aliyemwakilisha Bi. Thureiya Zabron) akipoke pikipiki hiyo kutoka kwa Mkurugenzi
Mtendaji wa BOA bank Tanzania, Bw. Ammish Owusu-Amoah Dar es Salaam leo.
“Tumemaliza
salama”, ndivyo wanavyosema Mkurugenzi Mtendaji wa BOA benk Tanzania, Bw. Ammish
Owusu-Amoah na Afisa wa Benki hiyo, Bw. Solomon Haule, baada ya kukabidhi
zawadi kwa washindi leo
Mshindi wa
Gari, Bw. Bw. Said Mohamed Bakari akiwapungia waandishi wa habari mkono wakati
akiondoka na gari hilo leo.
MSHINDI
PROMOSHENI YA ‘WEKA NA USHINDE’ AONDOKA NA GARI
Mshindi wa Promosheni
ya ‘Weka na Ushinde’ iliyoendeshwa na Benki ya Afrika Tanzania (BOA Bank), Bw.
Said Mohamed Bakari ambaye ni mteja wa benki hiyo mkoani Mtwara, ameondoka Dar
es Salaam leo na gari mpya aina ya Toyota Brevis.
Bw. Bakari ameondoka
kwenye viwanja vya benki hiyo, Kijitonyama baada ya kukabidhiwa gari hilo na Mkurugenzi
Mtendaji wa BOA bank Tanzania, Bw. Ammish Owusu-Amoah watika wa hafla fupi
iliyofanyika.
Akizungumza kwa furaha baada ya kupokea funguo za hari hilo, Bw. (34) ambaye ni
mfanyibiashara wa vifaa vya umeme mjini Mtwara, amesema pamoja na kupigiwa
simu akifahamishwa kuwa mshindi wa promosheni ya ‘Weka na Ushinde, hakuamini kuwa
amejishindia gari.
“Niliona kama ndoto za mchana, sikutegemea kama nitamiliki gari kama hii, bado
naona kama ndoto, nimefurahi sana kushinda na kupewa gari
leo hii” alisema Bw. Bakari alipoongeza na waandishi wa habari Dar es Salaam
leo huku akisisitiza kuwa amefurahi sana na kuishukuru benki hiyo kwa kuanzisha
promosheni hiyo.
Bw. Bakari amesema anaona fahari kubwa kuwa mteja wa BOA bank Tanzania na
kwamba kitendo cha yeye kushiriki kwenye promosheni hiyo hakijamsaidia tu kwa kushinda
gari, bali pia kimemsaidia kujenga utamaduni wa kujiwekea akiba. “Pamoja na
kushinda zawadi hii kubwa, pia promosheni hii pia imenisaidia sana kuongeza
bidii ya kujiwekea akiba katika benki, kitendo ambacho kimesaidia sana katika
shughuli zangu za kijamii na kiuchumi” alisema
Amewaasa wananchi hususan wafanyabiashara wa aina zote kujijengea utamaduni wa
kujiwekea akiba katia benki hiyo mara kwa mara ili waweze kushinda zawadi.
Akizungumza baada ya kukabidhi gari hilo kwa
mshindi, Mkurugenzi Mtendaji wa BOA bank Tanzania, Bw. Ammish Owusu-Amoah
amesema benki yake imefurahishwa sana na imani kubwa waliyonayo watanzania kwa
benki hiyo na kwamba hiyo imewafanya wahakikishe waongeze jitihada za kutoa
huduma bora za kibenki zinazoendana na mazingira halisi ya soko la Tanzania.
Bw. Ammish Owusu-Amoah amesema promosheni
ya ‘Weka na Ushinde’ ni moja ya hatua ya benki hiyo kujwashawishi watanzania
kujenga utamaduni wa kujiwekea akiba, kwani hilo ni suala la msingi sana kwa
mtu kupata maendeleo kwa kujiwekea akiba.
“Tumekuwa hapa Tanzania kwa Zaidi ya miaka 10 Sasa na tunafurahi kuona kuwa
tumechangia kwa kiasi kikubwa katika ukuaji wa huduma za kibenki hapa nchini.
Pia tumeanzisha huduma na bidhaa mbalimbali ambazo zinawalenga wateja wetu wa
kada mbalimbali za kimaisha na kiuchumi”, anasema Bw. Ammish na kuongeza kuwa ndani
ya kipindi hicho, benki hiyo imefanikiwa kukua kwa kila Nyanja ikiwemo mtaji,
idadi ya wateja pamoja na mtandao wa matawi yake.
Amesema kwa sasa BOA bank Tanzania ina mtandao wa matawi 21 ambapo 11 yapo
jijini Dar es Salaam kikiwemo kituo cha kibiashara na mengine 9 yapo
Arusha, Mwanza, Kilimanjaro (Moshi), Morogoro (Morogoro Mjini na Mtibwa),
Mbeya, Mtwara, Tunduma na Kahama.
Mkurugenzi huyo amesema benki yake ipo kwenye mchakato wa kufungua matawi mengine
maeneo mbalimbali ya nchi ndani ya miezi sita.
Promosheni ya ‘Weka na Ushinde’ ilianza Octoba mwaka jana na takriban wateja
2,000 walishiriki huku wakijishindia zawadi mbalimbali ikiwemo T- shirts,
kofia, simu za mkononi, Tablets, Shopping Vouchers, na zawadi za juu ambazo ni
Pikipiki na Gari aina ya Toyota Brevis.
|
No comments:
Post a Comment