TAN
Bayport
Kikoa
Myway entertainment
FORE PLAN CLINIC
MPINGA CUP 2016
Mashujaa Fm 89.3, Lindi
Thursday, March 12, 2015
UWT MERU WACHANGA MILIONI 17 KWA AJILI YA UNUNUZI GARI
Na Gladness Mushi, Arusha
…………………………………………
UMOJA wa wanawake wa chama cha mapinduzi Meru(UWT) umefanikiwa kuchanga kiasi cha Milioni kumi na saba kwa ajili ya kuweza kuendesha miradi mbalimbali ambayo itaweza kuwanufaisha wanananchi zaidi na hivyo kuinua uchumi wa Meru
Hataivyo fedha hizo zitatumikia kununulia gari aina ya Noah ambalo litatumika kama mradi wa wananwake hao hasa pale ambapo wanahitaji usafiri kwa ajili ya kuendeleza shuguli zao za uchumi
=Akiongea katika harambee hiyo mgeni rasmi ambaye ni mjumbe wa kamati ya siasa ya mkoa wa Arusha John Palangyo alisema kuwa ili umaskini uweze kutoweka ni lazima miradi iwepo tena ya kila siku
Palangyo alisema kuwa kwa sasa msaada wa fedha wa mara kwa mara unawweza usikidhi haja za muombaji ila kama muombaji akiwa na mradi ni raisi sana kwake kuweza kupambana na hali duni ya maisha
Kutokama na hilo john aliwataka kina mama hao kuweza kuwa wabunifu na kisha kubuni miradi ambayo itaweza kuwasaidia hata kina mama wengine kwani uwezo huo upo kabisa kwani Meru ina fursa nyingi sana.
“mlichokifanya leo ni kumeza kidonge kichungu sana cha kujifunga na kisha kuchanga mpaka hapa mlipofika ila bado mnachangamoto ya kuendelea kuwa wabunifu hata zaidi ya hapa na kisha mtushirikishe ili tuweze kupambana na umaskini wote kwa pamoja”aliongeza John
Katika hatua nyingine John aliwataka wanawake hao kuhakikisha kuwa wanakuwa kitu kimoja na kulijenga taifa la Tanzania kwani nafasi ambayo wanayo kwenye jamii ni kubwa sana hasa kama watashirikiana na kuwa kitu kimoja.
“nipende kuwaaambia UWT Meru kuwa ninyi ni jeshi kubwa na mna uwezo mkubwa sana wa kufanya hii jamii yetu ikawa kitu kimoja na tunatakiwa turuke kama ndege wanaofanana kwa kila kitu embu sasa kila mama asimame kwenye nafasi yake kaunzia sasa tuweze kujikomboa “aliongeza John
Awali mwenyekiti wa Umoja huo Bibi Anna nanyaro alitumia nafasi hiyo kuwaambia wanawake kuwa wana haki ya kujiandikisha kwenye daftari la wapiga kura na kamwe wasipotoshwe na baadhi ya watu ambao hawana mapenzi mema na nchi
Anna alisema kuwa tayari wana mikakati mbalimbali ya kuweza kutoa elimu kwa wananachi juu ya umuhimu wa kujiandikisha, na hata kupiga kura kwani kwa sasa wapo baadhi ya wanasiasa ambao wanatumia nafasi zao kupotosha maana halisi ya katiba lakini hata zoezi la upigaji wa kura.
No comments:
Post a Comment
Newer Post
Older Post
Home
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment