Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa (MSD), Bw. Cosmas Mwaifani akifungua sherehe za Siku ya Akina Mama Duniani zilizofanyika.
Bw.
Mwaifani akimkaribisha mgeni rasmi wa sherehe hizo, Bi.Helen Mwakipunda
ambaye ni Mhasibu Mkuu wa Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii.
Daktari
Bingwa wa Magonjwa ya Akina mama kutoka Hospitali ya Taifa
Muhimbili,.Matrida Ngarina aliyealikwa kwa ajili ya kutoa mada kuhusiana
na magonjwa ya akina mama, akizungumza na wafanyakazi wa (MSD)
Mjasiriamali
maarufu wa saluni jijini Dar es Salaam, Maza Sinare akitoa mada kuhusu
ujasiriamali wakati wa sherehe hizo. Sinare alialikwa mahususi kwa ajili
ya kuwafundisha akina mama wa MSD namana wanavyoweza kuanzisha biashara
zao huku wakiendelea kufanya kazi.
maarufu wa saluni jijini Dar es Salaam, Maza Sinare akitoa mada kuhusu
ujasiriamali wakati wa sherehe hizo. Sinare alialikwa mahususi kwa ajili
ya kuwafundisha akina mama wa MSD namana wanavyoweza kuanzisha biashara
zao huku wakiendelea kufanya kazi.
Dr. Chris Mauki, akiwazungumza na akina mama wa MSD namna wanavyoweza kukabiliana na msongo wa mawazo sehemu ya kazi
Afisa Habari wa (MSD),Eti Kusiluka ambaye siku hiyo alikuwa mshereheshaji wa sherehe hizo akizungumza jambo
Mmoja wa wafanyakzi wa (MSD) akimuuliza swali, Dk. Ngarina kuhusiana na uvimbe wa titi kwa wanawake.
Mfanyakazi wa (MSD), Gendi Machumani akimuuliza swali Dk, Ngarina kuhusiana na magonjwa ya njia ya uzazi kwa mwanamke.
Baadhi ya wafanyakazi wa (MSD), wakimsikiliza kwa makini Bi, Mwakipunda aliyekuwa mgeni rasmi.
Mgeni rasmi katika sherehe hizo, Bi. Mwakipunda akicheza muziki wa Nani Kama Mama wakati wa sherehe hizo.
Kaimu
Mkurugenzi Mkuu wa (MSD), Bw. Mwaifani akiwa katika picha ya pamoja na
wafanyakazi wa (MSD) pamoja na mgeni rasmi kulia kwake, Bi. Mwakipunda.
Wafanyakazi wa (MSD) ambao wapo kwenye Club ya mazoezi ya MSD, wakifanya mazoezi katika sherehe hizo.
Wafanyakazi wa hao wakiwapigia makofi wenzao waliokuwa wakifanya mazoezi ya viungo.
Ikiwa
leo ndiyo Siku ya Wanawake Duniani, wanawake wa Ghala la Kuhifadhi
Madawa la Taifa (MSD) jana walisherehekea siku hiyo kwa aina yake baada
ya kuifanya katika eneo lao la kazi.
Akizungumza
na akina mama hao, Victoria Elangwa ambaye ni Mkurugenzi wa Rasirimali
Watu na Utawala, alisema wameamua kufanyia sherehe hizo eneo la kazi ili
akina mama hao wapewe elimu kuhusu afya ya uzazi, ujasirimali pamoja na
kukabiliana na msongo unaowakabili wafanyakazi katika maisha yao ikiwa
ni pamoja na sehemu ya kazi.
Kaimu
Mkurugenzi Mkuu wa (MSD), Bw. Cosmas Mwaifwani akifungua sherehe hiyo
kabla ya kumkaribisha mgeni rasmi, Bi. Helen Mwakipunda ambaye ni
Mhasibu Mkuu wa Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii, aliwapongeza akina
mama hao kwa kuadhimisha sherehe hiyo kwa aina ya tofauti.
“Nawapongeza
kwa kuamua kuadhimisha siku yenu kwa kuwaalika watoa mada ya afya,
ujasiriamali na msongo unaoweza kumkabili mtu akiwa kazini na nyumbani,”
alisema mkurugenzi huyo.
Naye
mgeni rasmi, Bi. Mwakipunda aliwapongeza akina mama hao na kuwaambia
wazidi kujitokeza katika nafasi mbalimbali za uongozi kwa sababu
wanaweza.
“Hivi
sasa wanawake tumeweza kupigania haki zetu mbalimbali na kuondokana na
ukandamizwaji uliokuwepo huko nyuma wa kutoshirikishwa kwenye masuala ya
mirathi na mambo mengine,” alisema Mwakipunda.
Daktari
Bingwa wa Magonjwa ya Akina wa Hospitali ya Taifa Muhimbili, Matrida
Ngarina akitoa mada juu ya magonjwa ya wanawake aliwata akina mama kuwa
na utamaduni wa kujichunguza matiti yao mara kwa mara ili kubaini kama
kuna uvimbe wowote.
Daktari
huyo aliongeza kuwa, kufanya hivyo kutawasaidia kujiepusha na kansa ya
ziwa ambayo imekuwa ikiua wanawake wengi hivi sasa.
Aliwaeleza
wanawake hao maradhi mbalimbali ya via vya uzazi na kuwashauri wawape
somo mabinti zao wasijihusishe na mapenzi wakiwa na umri mdogo kwani
baadaye wanaweza kupatwa na saratani ya kizazi.
No comments:
Post a Comment