Naibu Waziri Sayansi na Teknolojia January Makamba akizungumza wakati wa
uzinduzi wa kampuni ya na kampuni ya Copyrights Management East Africa
Limited (CMEA).
Afisa Mtendaji Mkuu wa CMEA,
Paul Matthysse akisisitiza jambo wakati wa uzinduzi wa kampuni hiyo
yenye lengo la kuwakwamua wanamuziki katika umaskini. CMEA pia
itawawezesha pia watayarishaji wa muziki na wasanii wengine pamoja na
vyombo vya habari kupata kufahami takwimu sahihi za nymbo zilizochezwa
kwa siku, wiki, mwezi na kwa mwaka.
Na Mwandishi Wetu
Naibu Waziri wa Sayansi na
Teknolojia, January Makamba amewataka wanamuziki nchini kuachana na
kutegemea kupata shoo za majukwaani na kupata umaarufu usiokuwa na tija
kwa kujiunga na kampuni ya Copyrights Management East Africa Limited
(CMEA) ambayo inasimamia haki miliki za kazi za wasanii wa ukanda wa
nchi ya Afrika Mashariki.
Naibu Waziri Makamba alisema
hayo wakati wa uzinduzi rasmi wa kampuni ya CMEA ambayo ipo chini ya
mtayarishaji wa muziki maarufu, Paul Matthysse (P-Funk) ambaye ni Afisa
Mtendaji Mkuu wa kamuni hiyo.
Makamba alisema kuwa wanamuziki
wengi nchini wanapata umaarufu mkubwa wa bila kipato kutokana na kazi
zao bora kwani hawafaidiki na utunzi wa nyimbo zao zinazopigwa kwenye
televisheni na vituo vya redio mbalimbali.
Alisema kuwa matokeo yake
wanapotea katika fani hiyo na kuwa maskini maarufu na faida kubwa kwao
ni kupata sifa kwa warembo mbalimbali ambao huwakimbia pale wanaposhuka
katika fani.
“Mimi najua muziki na
wanamuziki, hakuna mtu anayeweza kunidanganya, wanamuziki wanapata tabu
katika utunzi na baadaye kutafuta fedha za kurekodi kwa kukopa au kwa
kuombaomba, baadaye watafute fedha za kuwapa madj wa redio na wa vipindi
vya televisheni ili wimbo wake uchezwe na kupata shoo mbalimali kwa
kipato kidogo,” alisema Makamba.
Alisema kutokana na hali
ilivyo, mwanamuziki anaishia kukuapata shoo kwa ujira mdogo na akipotea
katika fani, anakuwa maskini maarufu.
“CMEA ni sululisho kwenu,
kampuni hi itafanyakazi pamoja na Chama Cha Hakimiliki Tanzania (Cosota)
kuweza kujua wimbo wako au video yako imechezwa mara ngapi redioni au
kwenye televisheni na unastahili kulipwa shilingi ngapi,” alisema.
Alisema kuwa hata baada ya
kuacha muziki, utaendelea kupata fedha ‘pensheni’ kutokana na wimbo au
video yako kuchezwa redioni na kwenye televisheni.
Afisa Mtendaji Mkuu wa CMEA,
Paul Matthysse alisema kuwa mbali ya wanamuziki, kampuni yao itawawezeha
pia watayarishaji wa muziki na wasanii wengine pamoja na vyombo vya
habari kupata kufahami takwimu sahihi za nymbo zilizochezwa kwa siku,
wiki, mwezi na kwa mwaka.
Matthysse alisema kuwa kampuni
yao imewekeza mitambo ya kisasa inayowezesha kuchapisha na kuhakiki
nyimbo pindi zinapochezwa hewani na televisheni na redio na kutoa ripoti
za aina mbalimbali zinazohitajika kutumika kwa malengo maalum.
“Pia tunapokea na kuhifadhi
nyimbo kwenye mitambo maalum kwa matumizi ya uhakiki, na kudhibiti kiasi
cha mirabaha ambacho Cosota kupitia vyombo vya habari inatakiwa
kuwalipa wasanii kulingana na idadi kamili ya urushwaji wa kazi zao,”
alisema Matthysse.
No comments:
Post a Comment