TAN

TAN

Bayport

Bayport

Kikoa

Kikoa

Myway entertainment

Myway entertainment

FORE PLAN CLINIC

FORE PLAN CLINIC

MPINGA CUP 2016

MPINGA CUP 2016

Mashujaa Fm 89.3, Lindi

Tuesday, March 29, 2016

KESI UCHAGUZI YA ALIYEKUWA MBUNGE WA KINONDONI IDD AZZAN YAPIGWA KALENDA.


 Mbunge wa jimbo la Kinondoni Maulid Mtulia akizungumza na wandishi wa habari juu ya  kesi ya kupinga matokeo ya uchaguzi ya mbunge wa jimbo la kinondoni   haina madai ya msingi na hivyo mahakama ilistahili kuitupilia mbali badala ya kuendelea kuipiga kalenda leo jijini Dar es Salaam.
Wakili mshitakiwa  Juma Nassoro akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam. juu ya kesi hiyo kusikilizwa na Jaji Lugano Mwandambo kwa njia ya maandishi ilipangwa kutolewa maamuzi leo, ila kwa bahati mbaya jaji huyo hakuweza kufika mahakamani kulingana na kupangiwa kushughulikia kesi zingine za uchaguzi mkoani Kilimanjaro. Kulia ni .Mbunge wa jimbo la Kinondoni Maulid Mtulia.
Mbunge wa jimbo la Kinondoni Maulid Mtulia akitoka Mahakani hapo mara baada ya kesi hiyo kuahilishwa.
(Picha na Emmanuel Massaka wa Globu ya Jamii)

KESI ya kupinga matokeo ya uchaguzi ya Mbunge wa jimbo la Kinondoni Maulid Mtulia(CHADEMA) iliyofunguliwa na aliyekuwa Mbunge wa jimbo hilo, Idd Azzan imeshindwa kutolewa maamuzi hii leo kama ilivyokuwa imepangwa na mahakama kuu ya Tanzania.

Juma Nassoro ambaye ni wakili wa mshitakiwa Maulid Mtulia ambaye ni Mbunge wa Kinondoni amesema kuwa baada ya kesi hiyo kusikilizwa na Jaji Lugano Mwandambo kwa njia ya maandishi ilipangwa kutolewa maamuzi leo, ila kwa bahati mbaya jaji huyo hakuweza kufika mahakamani kulingana na kupangiwa kushughulikia kesi zingine za uchaguzi mkoani Kilimanjaro, ambapo amemuaomba msajili kumpanga jaji mwingine atakaye andika hukumu ya kesi hiyo, na hivyo wameambiwa kurudi tena kesho mahakamani kwa ajili ya kupangiwa tarehe nyingine.

Kwa upande wa Mbunge Mtulia anayekabiliwa na kesi hiyo ameeleza  kusikitishwa na kilichotokea kwa kile alicho dai kuwa kesi hiyo  haina madai ya msingi na hivyo mahakama ilistahili kuitupilia mbali badala ya kuendelea kuipiga kalenda.

SHIRIKA LA NDEGE LA ETIHAD LAWEKA REKODI KATIKA USHIRIKI WA MATEMBEZI YA HISANI.














TANESCO MKOANI PWANI YAWANASA WEZI SABA KWA TUHUMA Z AKUIBA UMEME KINYEMELA











WANANCHI WA CHATO WAJITOKEZA KWA WINGI KUMLAKI RAIS DKT JOHN POMBE MAGUFULI

 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Dkt John Pombe Magufuli akihutubia maelfu ya wakazi wa wilaya ya Chato Mkoani Geita mapema leo.

 Wakazi kutoka vitongoji mbalimbali wilayani Chato mkoa wa Geita,wakiwa wamekusanyika kwa wingi wakisubiri kumsikiliza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Dkt John Pombe Magufuli ambaye amewasili leo mjini humo alikozaliwa.Rais Dkt Magufuli anawasili wilayani Chato kwa mara ya kwanza tangu awe Rais.

 Wanannchi wakiwa wamejitokeza kwa wingi kumpokea mtoto wa nyumbani kwao Chato,Mh Rais Dkt.John Pombe Magufuli viwanja vya Mjini Chato mkoani Geita muda huu. Hii ni mara ya kwanza kufika chato tangu awe Rais.

Afya Sports Bara, Zanzibar Nguvu Sawa.

TIMU ya Afya Sports Bara na Afya Sports Zanzibar zimetoka sare bao moja kwa moja katika mchezo uliofanyika jana katika Uwanja wa Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH) jijini Dar es salaam.
Timu ya Afya Sports Zanzibar ilikuwa ya kwanza kutikisa nyavu na bao la kwanza lilifungwa na Haji Abdalah kwenye dakika ya 22 kipindi cha kwanza.

Katika kipindi cha pili timu ya Afya Bara ilifurukuta na kurejesha bao lililofungwa na Mesa, hatua iliyopelekea timu hizo kutoka sare ya bao moja kwa moja.

Katika hatua nyingine, timu ya Netibili ya Afya Bara imeifunga mabao 30 -29 timu ya Netiboli ya Afya Zanzibar kwenye mchezo uliofanyia kwenye Uwanja wa Netiboli iliyopo ndani ya Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH).

Mchezo huo ni Tamasha la Pasaka ambalo hufanyika kila mwaka kati ya Watumishi wa Sekta ya Afya Zanzibar na Watumishi wa Sekta ya Afya Bara kwa lengo la kuendeleza undugu na ushirikiano.
Mchezaji wa timu ya Afya Bara, Drisa akimtoka mchezaji wa Afya Zanzibar, Hassan Abdallah “Kimti” katika mchezo wa tamasha la Sikukuu ya Pasaka. Katika mechi hiyo timu hizo zilitoshana nguvu sawa. Afya Zanzibar 1-1 Afya Bara. Mchezo huo ulifanyika jana kwenye viwanja vya Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH).
Wachezaji wa timu ya soka Afya Bara na Zanzibar wakiwa katika picha ya pamoja baada ya mchezo.
 Wachezaji wa Netiboli ya Afya Zanzibar wakiwa katika picha ya pamoja baada ya kumalizika kwa mchezo. Afya Bara imeifunga Afya Zanzibar mabao 30-29. Mchezo huo umefanyika jana kwenye viwanja vya Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH).

SUMATRA NA JESHI LA POLISI WAKAMATA MABASI 105 NA 36 YAFIKISHWA MAHAKAMANI.




TAMKO LA WIZARA YA AFYA KUFUATIA WANANCHI KUSHAMBULIA WATUMISHI WA AFYA


JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
WIZARA YA AFYA, MAENDELEO YA JAMII, JINSIA, WAZEE NA WATOTO

TAMKO LA MHE. UMMY MWALIMU (MB), WAZIRI WA AFYA, MAENDELEO YA JAMII, JINSIA, WAZEE NA WATOTO KUHUSU WANANCHI KUSHAMBULIA WATUMISHI WA AFYA HASA MADAKTARI NA WAUGUZI KATIKA UTOAJI WA HUDUMA ZA AFYA NCHINI, TAREHE 29 MACHI, 2016




Nachukua fursa hii nikiwa Waziri mwenye dhamana ya masuala ya afya nchini, kutoa tamko kuhusiana na matukio ya hivi karibuni yaliyoripotiwa kwenye vyombo vya habari na mitandao ya kijamii kuhusiana na vitendo vya kusikitisha wanavyofanyiwa watumishi wa sekta ya afya, wakiwemo Madaktari kama vile kushambuliwa kwa maneno na vipigo. Pasi na shaka, vitendo hivyo vitaathiri upatikanaji wa huduma bora za afya kwa wananchi wanaopewa huduma hizo hususan wa kipato cha chini. 

Matukio haya yanajumuisha tukio lililotokea tarehe 27.03.2016 katika Hospitali ya Mkoa wa Mtwara, Ligula, ambapo Dr Dickson Sahini alishambuliwa na ndugu wa mgonjwa aliyepelekwa hapo kuhudumiwa. 
Napenda kutamka kwamba nimesikitishwa sana na tukio hilo, na ninalaani vikali matukio ya watumishi wa afya kushambuliwa kwa maneno au kwa vitendo na wananchi wanaopatiwa huduma. Jambo hili likiendelea litawavunja moyo watumishi wa afya na hivyo kuathiri upatikanaji wa huduma bora kwa wananchi.
Ningependa kuwafahamisha kwamba kwa ujumla wake sekta ya afya inakabiliwa na changamoto nyingi sana katika maeneo ya miundombinu, dawa na vifaa tiba, watumishi wa kutosha, pamoja na kuwa na watumishi wasiozingatia nidhamu, weledi na maadili katika kutimiza majukumu yao.
Ninatambua kwamba changamoto hizi zipo siku nyingi, na zimekuwa zikitafutiwa majawabu na Serikali za awamu zilizopita ikiwemo ile ya awamu ya nne. Lakini sote ni mashahidi kwamba Serikali ya awamu ya tano, chini ya uongozi wa Mheshimiwa Dr John Joseph Pombe Magufuli, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, inachukua hatua za makusudi katika kutatua changamoto hizi, likiwemo pia suala zima la utendaji unaozingatia uwajibikaji. 
Kwa hiyo ninawasihi sana wanachi wanaopatiwa huduma katika vituo vyetu vya afya kote nchini kuacha mara moja tabia ya kujichukulia sheria mikononi na kufanya vitendo vinavyoweza kuwakwaza watumishi wa afya. Kwa vile nchi yetu inafuata misingi ya utawala unaozingatia sheria, ni vyema wananchi wakafuata taratibu zilizowekwa wanapohisi kwamba hawakupatiwa huduma za afya wanavyostahili. 
Aidha nachukua fursa hii kuvitaka vyombo na mamlaka husika kutosita kuwachukulia hatua wananchi wanaokwenda kinyume na matakwa ya sharia ili kuwahakikishia watoa huduma za afya usalama na amani wakati wa utoaji wa huduma hiyo.
Ninaagiza vile vile kwamba hospitali na vituo vyote vya kutolea huduma za afya nchini ziweke utaratibu mwepesi wa wananchi kufikisha malalamiko yao pindi wanapoona kwamba hawakupatiwa huduma za afya kwa kiwango stahiki. 
Ndugu Wananchi, 
Ninatambua kwamba sehemu kubwa ya watumishi katika sekta ya afya nchini wanafanya kazi zao kwa ufanisi, upendo, uadilifu na kwa kuzingatia matakwa ya weledi (professionalism) na miiko ya taaluma zao (ethics). Pia ninatambua kwamba wengi wanafanya kazi katika mazingira magumu na wanatumia muda wa ziada kuendelea kuwahudumia wagonjwa hadi wanapoona wapo salama. Ninawapongeza kwa dhati watumishi hawa na ninawashukuru na kuwatia moyo waendelee kuwa na tabia hiyo nzuri, kwa maslahi ya Taifa letu. 
Hata hivyo ninasikitishwa sana na tabia ya watumishi wa afya wachache ambao wanafanya kazi kinyume na maadili na matakwa ya weledi wa taaluma zao. Napenda kusisitiza kuwa Wizara yangu haitavumilia matukio ambayo watumishi wa Sekta ya Afya watakwenda kinyume na matakwa ya weledi na maadili ya taaluma zao katika vituo vya kutolea huduma za afya nchini. Hivyo hatutasita kuchukua hatua stahiki kwa mujibu wa Sheria, Kanuni na Taratibu zilizopo ili kudhibiti hali hii. 
Nimeshaelekeza vyombo vya kusimamia maadili ya watoa huduma za afya nchini, yaani Baraza la Madaktari Tanganyika (MCT) na Baraza la Wauguzi na Wakunga Tanzania (TNMC) kuchukua hatua mara moja, kwa mujibu wa Sheria na Taratibu zao, juu ya watoa huduma wote wanaotuhumiwa kukiuka misingi ya weledi na maadili ya taaluma zao. Endapo tuhuma zao zitathibitika, hatua stahiki zitachukuliwa dhidi yao ikiwemo kufutiwa usajili au leseni zao ikibidi. 
Hivyo kwa tamko hili ninawaasa na kuwaagiza watoa huduma wa afya wote nchini kufanya kazi zao kwa bidii, kwa nidhamu na kwa kuzingatia weledi na maadili ya kitaaluma kama inavyoelekezwa. 
Ndugu Wananchi, 
Napenda pia kukumbusha kwamba kazi hii ya usimamizi wa mahusiano mema kati ya watoa huduma za afya na wananchi, na usimamizi wa weledi na maadili katika vituo vya kazi, itafanikiwa kwa ushirikiano wa pamoja wa Wakuu wa Mikoa na Wilaya, Makatibu Tawala, Wakurugenzi, Kamati za Usimamiaji wa Huduma za Afya za Mikoa na Wilaya, Kamati za Usimamiaji wa Huduma za Afya za Hospitali, na Wananchi wote kwa ujumla katika kuwasimamia, kuwaelekeza na kutambua mapungufu ya kimfumo au yale yanayohusu watumishi wa afya yaliyopo na kuchukua hatua zinazostahili mara moja. Ni lazima tuzingatie Sheria, Kanuni na Taratibu katika kutimiza jukumu hili. Wizara ya Afya itaendelea kuvijengea uwezo Mabaraza ya kitaaluma ya wataalamu wa afya ili kutimiza wajibu wao kikamilifu. 
Tufanye kazi kwa pamoja ili kutekeleza kauli mbiu ya Mhe. Rais Dkt. John Pombe Magufuli, inayosema ‘HAPA KAZI TU’. 
Asanteni sana. 
Imetolewa na: 
Mhe. Ummy Mwalimu (Mb) 
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto 
Mtwara – Tanzania 
29 Machi 2016

UVUVI HARAMU VICTORIA TISHIO KWA UHIFADHI



Na Woinde Shizza alivyotembelea ,Mwanza .

Uvuvi haramu wa kutumia sumu kali,pamoja na neti umekua ukitishia uhifadhi katika hifadhi ya Taifa ya Saa Nane na Lubondo ambazo zimepewa jukumu la kulinda mazalia ya samaki ili samaki hao wasipotee kwenye uso wa dunia.

Akizungumza na Waandishi wa Habari Ofisini kwake waliofanya ziara ya kutembelea hifadhi hiyo ya Saa Nane iliyoko jijini Mwanza ,ziara iliyoratibiwa na Tanapa Mhifadhi Mkuu Donatus Bayona amesema kuwa changamoto inayowakabili ni uvuvi haramu na uvamizi wa maeneo ya hifadhi unaofanywa na wavuvi wanaojipatia kipato bila kujali kuwa wanaharibu mazalia ya samaki . 

Askari Wanyamapori katika hifadhi hiyo Aloyce Mong`ee amesema kuwa wamekua wakiimarisha doria katika mipaka ya hifadhi ili kuzuia shughuli hizo za uvuvi ambazo ni tishio kwa uhifadhi.“Kuna mipaka ambayo tumeweka hakuna mtu anayeruhusiwa kufanya uvuvi ndani ya eneo la hifadhi ili kuhifadhi mazalia ya samaki” Alisema Askari huyo.

Mhifadhi huyo amesema kuwa Hifadhi hiyo ambayo iko katikati ya jiji la Mwanza inaongoza kwa kuwa na watalii wengi wa ndani ambao ni asilimia 90% ya wageni wanaotembelea hifadhi hiyo.Alisema Hifadhi ya Saa Nane ni moja kati ya hifadhi zilizopo kati kati ya miji hivyo kuvutia watanzania wengi kutembelea eneo hilo ambali lina wanyama pori pundamilia,swala na sokwe weusi pamoja na madhari nzuri na maridhawa ambazo hutumika kama sehemu ya kujifunzia na kupumzikia.

UKOSEFU WA MADAWATI MKOANI MANYARA MWISHO APRIL 30,2016-DKT JOEL BENDERA

Na Woinde Shizza,Manyara.

COSATO CHUMI APONGEZWA NA WANANCHI WA JIMBO LA MAFINGA MJINI










TAMASHA LA PASAKA LAHITIMISHWA MJINI KAHAMA MKOA WA SHINYANGA

23
18
25

5
2

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI











Amina Juma
Amina Juma Asante sana kwa taarifa na mungu akubariki
Unlike · Reply · 1 · 2 mins
Mpalule Shaaban
Mpalule Shaaban Mungu akupe baraka zote, usisahau kutembelea katika kusoma pia taarifa mbalimbali pamoja na hii naiweka. www.shaabanmpalule.blogspot.com