TAN

TAN

Bayport

Bayport

Kikoa

Kikoa

Myway entertainment

Myway entertainment

FORE PLAN CLINIC

FORE PLAN CLINIC

MPINGA CUP 2016

MPINGA CUP 2016

Mashujaa Fm 89.3, Lindi

Thursday, January 3, 2013

WAOMBOLEZAJI WAKIWA NYUMBANI KWA MAREHEMU SAJUKI TABATA BIMA


POLISI ALIYEFIA KATIKA OPERESHENI DARFUR SUDAN AZIKWA

Maofisa wa Polisi wakiwa wamebeba jeneza la mwili wa Mrakibu Mwandamizi  wa Polisi EX SSP Hawa Luzy aliyefia Darfur Sudan alipokuwa amekwenda kwa ajili shughuli za ulinzi wa amani katika jimbo hilo.Ofisa huyo alizikwa jana katika makaburi ya Kisutu. (Picha na Frank Geofray-Jeshi la Polisi)

SHEREHE ZA MIAKA 49 YA MAPINDUZI KUANZA KESHO ZANZIBAR

 
Na Maelezo Zanzibar  
Sherehe za miaka 49 ya Mapinduzi ya Zanzibar zinaanza rasmi kesho kwa kazi za kufanya usafi wa mazingira katika Wilaya zote za Unguja na Pemba.
Kwa mujibu wa Ratiba iliyotolewa na Kamati ya Sherehe na maadhimisho ya kitaifa imeonesha kuwa Miradi ipatayo 62 inatarajiwa kuzinduliwa katika Visiwa vya Unguja na Pemba.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Jakaya Kikwete atafungua Skuli mpya ya Sekondari ya Mlimani, iliyopo Matemwe Mkoa wa Kaskazini Unguja ikiwa ni Shamra shamra za Sherehe hizo.
 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt.Ali Mohamed Shein naye atazindua miradi mbalimbali ikiwemo Ufunguzi wa Jengo la Chuo cha Utawala wa Umma huko Tunguu Wilaya ya Kati Unguja.
 Pia atafungua mradi wa E-Government katika Wilaya ya Magharibi Unguja na kufungua Skuli mpya ya Sekondari ya Umoja, iliyopo Uzini Wilaya ya Kati Unguja pamoja na kuzindua Barabara kutoka Mfenesini hadi Bumbwini Wilaya ya Kaskazini B Unguja.
 Hali kadhalika Dkt.Shein atafungua Mradi wa kuhama kutoka Teknolojia ya Analojia kwenda Dijitali na Ufunguzi wa Studio ya kurikodia Sanaa na Muziki ambapo kwa upande wa Pemba atafungua Skuli mpya ya Sekondari ya Shamiani iliyopo Chake Chake Mkoa wa Kusini Pemba.
  Mbali na Shughuli hizo siku ya kilele hapo January 12 kwenye Uwanja wa Amani Rais Shein atakagua Gwaride lililoandaliwa na Vikosi vya ulinzi na usalama na Vikosi vya SMZ pamoja na kulihutubia Taifa na Usiku kuhudhuria Taarab rasmi huko katika Ukumbi wa Salama Hoteli ya Bwawani
 Naye Makamo wa Kwanza wa Rais Maalim Seif Shariff Hamad atafanya uzinduzi mbali mbali kwa ufunguzi wa Skuli na Maabara wakati Makamo wa Pili wa Rais Balozi Seif Idd atafanya Shughuli kama hizo kwa ufunguzi wa Skuli na Majengo mapya ya nyumba za Wazee zilizopo Sebleni Wilaya ya Mjini Unguja.
 Mbali na shughuli hizo baadhi ya Marais wastaafu,Mawaziri mbali mbali wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar na Muungano watafanya shughuli za ufunguzi wa Miradi mingine ikiwemo ya Maji, Skuli na Mradi wa Mnara wa Radio wa Masafa ya Kati uliopo Bungi Wilaya ya Kati Unguja.

Achomwa Kisu akidai haki yake


 Mkazi wa Mji wa Moshi akiwa katika majeraha baada ya kuchomwa kisu na mfanyabiashara wa kuuza nyama ya (Bucha) eneo la Moshi Mjini. tukio hili limetokea siku ya Mwaka Mpya 2013.
 Hapa Ndugu zake wakiwa katika Hospitali ya Mawenzi kupata Huduma ambayo hata hivyo iliwachukua Zaidi ya Masaa Mawili bila kupata ama kuonana na wauguzi.
Ndugu akijaribu Kumfariji

Tuesday, January 1, 2013

Manispaa ya Kinondoni kuongeza kasi ya utatuzi wa migogoro ya ardhi


 
MANISPAA ya Kinondoni  imeahidi  kuongeza nguvu katika kushughulikia masula ya migogoro ya ardhi , huku pia ikiwataka wananchi kutoa ushirikiano wao katika mapambano dhidi ya watu wote wanaokwenda kinyume na utaratibu uliopo.Akizungumza na jiji Dar es Salaam jana, Mkurugenzi wa Manispaa hiyo, Fortunatus Fwema alisisitiza kuwa katika  kukabiliana na migogoro hiyo, uongozi wa manispaa umekuwa ukichukua hatua za haraka kuhakikisha  viongozi na watendaji wanaojihusisha na migogoro na kashfa za ardhi wanachukuliwa hatua mara moja.
Alisema katika kuishughulikia migogoro hiyo, manispaa imekuwa ikiendelea kuyafanyia kazi mapendekezo ya Kamati ya migogoro ya ardhi iliyoundwa kwa maelekezo ya Rais, hatua aliyosema kuwa kwa kiasi kikubwa imeweza kuleta mafanikio. 
“Hadi sasa migogoro iliyokuwepo imeshughulikiwa kwa asimilia 95 na kupatiwa ufumbuzi, kwa sasa migogoro iliyopo ni ile inayotokana na uvamizi wa ardhi unaofanywa na makundi ya watu kinyjme na sheria ambayo manispaa kwa kushirikiana na Serikali kuu imeendelea kuipatia ufumbuzi” alisema Fwema. 
Aidha alisema kumekuwa na mawazo potofu ya baadhi ya watu kwamba  manispaa hiyo imekuwa ikifanya upendeleo kwa wakubwa wakati wa uuzaji wa viwanja vyake, madai aliyosema kuwa si ya kweli na zaidi yamelenga kuichafua manispaa hiyo. 
“Madai haya si ya kweli ikizingatiwa kuwa katika kipindi kinachokaribia miaka 10 manispaa ya Kinondoni haijawahi kupima viwanja na kuviuza kwa wananchi kutokana na changamoto mbalimbali hasa zinazohusiana na utwaaji wa ardhi na ukosefu wa fedha kwa ajili ya kugharamia fidia na upimaji” alisema Fwema.
Alisema manispaa kwa muda mrefu imekuwa ikihangaika kutafuta fedha za kupimia viwanja kutoka sehemu mbalimbali zikiwemo taasisi za fedha na madhumuni ni kuvipima viwanja hivyo ili kukabiliana na ongezeko la ujenzi holela katika maeneo yasiyopangwa.
Kuhusu utoaji wa vibali vya ujenzi na kushughulikia maombi ya kubadili matumizi ya ardhi, Fwema alisema manispaa hiyo kwa kutumia wataalam wake, kabla ya kutoa vibali hivyo wameweka utaratibu wa kuhakikisha maombi yaliyotolewa, hayakinzani na matumizi yaliyopo na yaliyoidhinishwa katika mpango wa matumizi ya ardhi.

“NAFSI NI NYONGE” Tusameheane na maisha yaendelee. karibu 2013 kwa ufanisi zaidi.!

Wapendwa ndugu,jamaa na marafiki popote pale mlipo,yamebaki masaa kadhaa kuuaga mwaka 2012,ambao kwa hakika ulikuwa na changamoto nyingi za kimaisha,dhoruba za hapa na pale wengi zilitukumba,lakini kwa kudra za Mwenyezi Mungu akatushika mkono akatuinua na maisha yakaendelea.
Binafsi mpaka dakika hii namshukuru Mungu nikiwa mwenye afya njema kabisa.Maisha ya sasa Wanadamu wengi wamekuwa dhaifu kwa mambo mengi,lakini Mungu ndiyo njia sahihi wa kumtumia katika sala zako kuyashinda majaribu na madhaifu ya Dunia.Yako mengi ambayo naweza nikayaandika hapa lakini bado yasitoshe pia.Nasema asanteni kwa ushirikiano wenu mkubwa kwa namna moja ama nyingine,kama kuna mahali nilikosea,tukakwaruzana kidogo basi “NAFSI NI NYONGE” Tusameheane na maisha  yaendelee.
Tunahamia mwaka mwingine mpya kabisa 2013,basi na tuendelee na ushirikiano huu tuliokuwa nao kwa mambo mbalimbali yenye kujenga na kuleta tija katika maisha yetu,Mwaka 2013 uwe wa kuhakikisha kweli sote pia tumehamia kwenye mfumo wa kidijitali,tushauriane,tuelemishane tunyooshane njia iliyo sahihi ili kila mmoja kila wakati abaki nafsini mwake mwenye furaha daima,Pia tumtangulize Mungu kila wakati kwa kila jambo ili pia azidi kuzibariki kazi za mikono yetu daima.
Kwa Blogaz wenzangu,changamoto nyingi tumekumbana nazo 2012,ikiwemo tatizo kuu la KUKOPY NA KUPASTE.! Na nyinginezo nyingi tuzijuazo zinatusumbua kwa namna moja ama nyingine,basi ni nyema 2013 iwe ya kuzitafutia ufumbuzi,kama si kuzimaliza kabisa basi angalau tuendelee kuzipunguza ili kuzimaliza kabisa,huku suala la kujituma na ubunifu vikiwa ndio ngao kuu ya mabadiliko miongoni mwetu.Ushirikiano tuliokuwa nao umeonesha tuna uwezo mkubwa wa kuisadia jamii inayotuzunguka na hata serikali pia kwa namna moja ama nyingi,basi tusimame kidete kuhakikisha ushirikiano huu hauteteleki ama haupotei kirahisi,badala yake tuiimarishe zaidi kila kona .
Natoa shukurani za dhati kabisa kwa makampuni na wadau mbalimbali ambayo/ambao kiukweli yametoa mchango mkubwa kuhakikisha tunasonga mbele na libeneke hili ,si vibaya nikiyataja makampuni hayo kuwa ni Serengeti Breweries Ltd,Airtel,Bayport,Msama Promotions Ltd,kampuni ya R&R,Dada Teddy Mapunda,Hoyce Temu,Blogaz wote (bila kinyongo) na wengine waliotupa hatua ya kusogea kwa namna moja ama nyingine,Mungu awabariki sana.
Asanteni 
Nawatakia heri ya sikukuu ya Mwaka mpya.

MSTAHIKI MEYA JERRY SILAA AKABIDHI ZAWADI ZA MWAKA MPYA KWA KITUO CHA TUSHIKAMANE CHILDREN CARE TRUST FUND


Mstahiki Meya wa Manispaa ya Ilala Jerry Silaa akikabidhi Mbuzi kwa Mkurugenzi wa Taasisi ya Tushikamane Children Care Trust Fund Bw. Gratho Messy Mbele (wa kwanza kulia) na Mkuu wa Shule ya Tushikamane Bi. Euphrosine Mtundu, kama zawadi kwa watoto yatima wa kituo hicho ambapo panapo majaliwa hapo kesho atajumuika nao kupata chakula cha mchana. Anayeshuhudia tukio hilo ni Diwani wa Kata ya Tabata Hajati Mtumwa Mohamedi (wa pili kushoto)

Mstahiki Meya Jerry Silaa akikabidhi ndoo ya mafuta kwa kituo hicho chenye lengo la kuhudumia watoto yatima na watoto wanaoishi katika mazingira magumu na hatarishi kwa kuwapa mahitaji muhimu kama vile elimu, afya, chakula, malazi, mahitaji ya shule, pamoja na huduma za kisaikolojia na ulinzi dhidi ya manyanyaso.

Viongozi wa kituo hicho wakimshukuru Mstahiki Meya Jerry Silaa.

Meya wa Manispaa Mstahiki Jerry Silaa akibadilishana mawazo na baadhi ya viongozi wa kituo hicho mara baada ya kukabidhi zawadi za vyakula ikiwa ni mchango wake kwa vijana hao katika kusherehekea mwaka mpya 2012/2013.
Kila mwaka wakati wa sherehe za mwaka mpya Mstahiki Meya wa Manispaa ya Ilala yeye binafsi hutoa sadaka kwa wahitaji kwa kumshukuru Mungu kwa kumuwezesha kumaliza mwaka salama.
Leo Mstahiki Meya Jerry Silaa ametoa chakula kwa kituo cha Watoto Yatima na watoto Yatima na watoto Waishio Katika Mazingira Hatarishi cha Tushikamane Children’s Care Trust Fund ambapo pamanapo majaliwa hapo kesho atakula chakula pamoja nao.
Asasi hiyo ya Tushikamane Children’s Care Trust Fund ilianzishwa mwaka 2001 na kupata usajili wa kudumu mwaka huo huo ili iweze kujiendesha kwa mujibu wa sheria za nchi.

Rais Kikwete azindua matokeo ya sensa ya watu na makazi 2012.

 
Rais Jakaya Kikwete akibonyeza kitufe kwenye kompyuta kuzindua matokeo ya Sensa ya Watu na Makazi mwaka 2012  jana jijini Dar es salaam ambapo idadi ya watu Tanzania imefikia milioni 44 929 002.Picha na Aron Msigwa -MAELEZO
 
Rais Jakaya Kikwete katika picha ya pamoja na baadhi ya viongozi wa serikali na vyama vya siasa.
 
Rais Jakaya Kikwete akiwa katika picha ya pamoja  kwenye bango linaloonyesha idadi ya watu Tanzania na viongozi na watendaji wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu mara baada ya kutangazwa kwa matokeo ya sensa ya watu na makazi ya mwaka 2012.
Rais Jakaya Kikwete akiwa katika picha ya pamoja  kwenye bango linaloonyesha idadi ya watu Tanzania na viongozi na watendaji wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu mara baada ya kutangazwa kwa matokeo ya sensa ya watu na makazi ya mwaka 2012.

Rais Kikwete azindua matokeo ya sensa ya watu na makazi 2012.

 
Rais Jakaya Kikwete akibonyeza kitufe kwenye kompyuta kuzindua matokeo ya Sensa ya Watu na Makazi mwaka 2012  jana jijini Dar es salaam ambapo idadi ya watu Tanzania imefikia milioni 44 929 002.Picha na Aron Msigwa -MAELEZO

Mkurugenzi wa Rahabu Ulcers Clinic, Dk Rahabu Rubago atoa msaada kituo cha yatima Kurasini


OFISA mfawidhi kituo cha kulelea watoto yatima Kurasini, Ramadhani Yahaya ameiomba serikali kufanya jitihada za kuwaondoa vijana wanaoendelea kuishi katika kituo hicho, licha ya kupoteza sifa ya kuishi katika kituo hicho kwa kuwa wamevuka miaka 18.
Ofisa huyo aliyaeleza hayo jijini Dar es Salaam jana, wakati Mkurugenzi wa Rahabu Ulcers Clinic, Dk Rahabu Rubago alipokuwa akitoa zawadi mbalimbali kwa ajili ya kusherehekea mwaka mpya ikiwemo chakula, vinywaji na vifaa vya shule kwa watoto wa kituo hicho waliokuwa wamechanganyika na watoto wa kituo cha wasabato.
Ramadhani alisema kituo hicho kwa sasa kinakumbwa na changamoto kubwa ya kuwa na vijana wengi wenye umri zaidi ya miaka 18 hivyo wanashindwa kufuata masharti ya kituo hicho ikiwemo kuwa ndani ya uzio ifikapo saa 12 jioni. 
“Changamoto kubwa ni vijana wenye umri mkubwa kuendelea kuishi katika kituo hiki naiomba serikali iwatengenezee vijana hawa mazingira ya kuwaondoa katika maeneo haya ili nao wakawe na maisha yao na kuachana na utegemezi wa hapa” alisema Ramadhani
Naye Dk Rahabu aliwataka vijana na watoto hao kutokukata tamaa katika maisha yao huku akiwataka kusoma kwa bidii ili waweze kukamilisha ndoto zao na  malengo waliyojiwekea.
“Mimi niliishi hapa nimekuja kufurahi nanyi na kuwatia moyo msijione kama mpo peke yenu tupo pamoja na kutokana na kujibidiisha tumefanikiwa hivyo nanyi nawahasa mjibidiishe kwa bidii zote ili muweze kufanikiwa na kufikia malengo yenu,” alisema Dk Rahabu”alisema Rahabu
Naye mwanafunzi anayesoma chuo cha uhasibu, ambaye anaishi katika kituo hicho, Robert Bernard ameiomba serikali kutowaondoa vijana waliozidi miaka 18 bila kuwatengenezea mazingira mazuri ya kwenda kuishi. 
“Kuondoka hapa si tatizo tunachoomba kama serikali inataka kutuondoa hapa kwa kuwa umri wetu mkubwa hatukaidi bali tunachoomba watuwekee mazingira mazuri huko wanakotaka twende lakini bila hivyo watakuwa hawajatusaidia” alisema Bernard.

Wasanii Richard wa Big Brother na Mwanamuziki Dully, usiku wa Mkesha wamekuwa ni miongoni mwa watu waliofanya shangwe katika kusherehekea kuingia mwaka 2013.

Shangwe hizo zimefanyika mara tu baada ya kugonga sekunde ya 60 ya kuthibitisha kuingia mwaka mpya ambapo walisikika wakipiga kelele na shangwe huku wakiwaomba mashabiki wao kuingia jukwaa kusakata Ngoma huku wakizongwa na maelfu ya wanawake na Vijana wa mji wa Moshi kutaka kucheza na kufurahi nao.
aidha alikuwa ni Richard ambaye muda wote alionekana akigandwa na wanawake wengi wa kizungu huku yeye akionekana kuwakwepa na kuendelea kucheza hadi furaha yake ilipokwisha na kwenda kujipumzisha
"kiukweli nimefurahi sana mpalule, kwani kumbuka kumaliza mwaka wakati mwingine inabidi ufurahi na kumshukuru Mungu, mimi hapa leo pia nimefurahi baada ya kukutana na rafiki yangu Dully na ndiyo kama unavyotuona hatuna budi kusherehekea kufika mwaka 2013, wapo wengi walitamani sana kufika lakini aikuwa hivyo" alisema Richi
na nilipomuuliza kuhusu kufuatwa na kundi la kina dada wa kizungu richi alisema" nina msimamo na mke wangu swahiba wangu mpalule, ni kweli kama unavyoona wengi wanapenda kucheza na mimi, na hata mimi siwezi kukataa kucheza na wao, ila kiukweli ni kwamba siwezi kufanya chochote kwa sababu nampenda sana mke wangu" alisema  Richard
na kwa Upande wake Dully yeye alionekana kuwa na furaha nyingi paspi mawaa, kwani apia alionekana kuwa na kundi kubwa la ulinzi, lakini hata hivyo pamoja na ulinzi huo aikutosha kuwafanya Walimbwende wa Mji wa Moshi ambao kwa sasa unafumuka kwa idadi  kubwa ya Soko la Wanawake wanaojiuza usiku(CHANGUDOA) kutotimiza wajibu wao , kutokana na kwamba baada ya Shangwe hizo Dully aliangukia mikononi mwa kichunchede ambaco alionekana kugandana nacho kisha kutokomea zao usiku wa Manane.
" nafurahi sana kufika hapa nilipo, pia namshukuru Mungu kwa kunifikisha 2013, nipo hapa Moshi mji mdogo lakini wa Starehe, ila napenda kuwaomba mashabiki wangu kuwa nipo na hata hivyo nitahakikisha mwaka huu nawapa vitu vipya kama ulivyo mwaka mpya, nahisi huu ni mwaka wangu tena Mpalule, subiri hata wewe utaona" alisema Dully
na kuhusu kugandwa na kuwa na kundi kumbwa la ulinzi Dully " hawa ni jamaa zangu yaani Mashabiki wangu, ambao siku zote wananipa sapoti kubwa, hivyo mara baada ya kuingia katika mji wa Moshi wamenipokea vizuri na ndiyo maana unawaona, na kuhusu kina dada hawa hilo siwezi kusema kwani wewe mwenyewe unajua mimi mashabiki wangu ni kina nani, na hata siku moja siwezi kuacha kuwasifia na kutaka kuja kwangu vile wapendavyo"alisema Dully huku akitoweka na Mmoja wa Wasichana waliokuwa wakimganda Tangu alipoingia ndani ya CLUB LA-LIGGA.


























































PICHA ZOTE NI TUKIO AMBALO LIMEFANYIKA WAKATI WA KUUKARIBISHA MWAKA MPYA KWENYE UKUMBI WA KISASA WA -CLUB LA- LIGGA