TAN

TAN

Bayport

Bayport

Kikoa

Kikoa

Myway entertainment

Myway entertainment

FORE PLAN CLINIC

FORE PLAN CLINIC

MPINGA CUP 2016

MPINGA CUP 2016

Mashujaa Fm 89.3, Lindi

Saturday, March 15, 2014

BUNGE LA KATIBA KATIKA HARAKATI ZA KUAMUA HATIMA YA VIKAO VYA BUNGE MAALUM LA KATIBA MJINI DODOMA

Mwenyekiti mteule wa Bunge Maalumu la Katiba, Samuel Sitta akizungumza na mwandishi wa Mwananchi, Fidelis Butahe nyumbani kwake mjini Dodoma juzi. Na Mpiga Picha Wetu.


DODOMA.
MWENYEKITI Mteule wa Bunge Maalumu la Katiba, Samuel Sitta amezungumzia uwezekano wa kutumia kura ya siri katika kuamua ibara nyeti katika Rasimu ya Katiba.
Sitta aliyechaguliwa juzi kushika wadhifa huo, alisema atashirikiana na kamati ya uongozi itakayoundwa ya wenyeviti wa Kamati 15 za Bunge hilo na kamati ya ushauriano kupata jawabu la suala hilo.
Akizungumza katika mahojiano maalumu nyumbani kwake mjini Dodoma juzi, Sitta alisema: “Unajua kuna baadhi ya vifungu na ibara za Rasimu ya Katiba ni vizuri vipigiwe kura ya wazi na vingine ambavyo ni nyeti zaidi vipigiwe kura ya siri.”
Alisema si vizuri vifungu vyote vipigiwe kura sawa, yaani si lazima zote ziwe za siri au ziwe za wazi.
Alitoa mfano wa ibara inayosema kutakuwa na Mahakama Kuu ya Tanzania na kusema: “Hatuwezi kushindana katika suala la kuwapo kwa Mahakama na ni wazi kuwa jambo hilo mnaweza kupiga kura ya wazi. Nasema hivyo kwa sababu Katiba yoyote lazima ionyeshe mihimili yote ambayo ni Bunge, Serikali na Mahakama.”
Sitta ambaye pia ni Waziri wa Ushirikiano wa Afrika Mashariki alishinda kiti hicho katika uchaguzi uliofanyika juzi kwa kura 487 kati ya 563 (sawa na asilimia 85).
Mbunge huyo wa Urambo Mashariki ambaye kaulimbiu yake ni ‘kasi na viwango’, alisema vifungu na ibara za Rasimu ya Katiba vinavyoweka misingi ya Katiba, ni vizuri vikapigiwa kura ya siri.
“Unajua tuna viongozi wa dini na halitakuwa jambo la busara kama tukizijua hisia zao. Kama wewe uko karibu na imamu au askofu halafu anapiga kura ya wazi ya kutaka Serikali tatu wakati wewe muumini unataka Serikali mbili ni wazi kuwa jambo hilo linaweza kuleta hisia tofauti na kuwanyima watu haki na uhuru wa kuamua,” alisema Sitta.
Alitoa mfano wa Sura ya Sita ya Rasimu ya Katiba inayozungumzia Serikali na muundo wa madaraka katika Jamhuri ya Muungano na kufafanua kuwa katika sura hiyo atapendekeza ipigiwe kura ya siri.
Kuhusu suala hilo la muundo wa Serikali alisema: “Kikubwa ni wajumbe kujenga hoja, hatuwezi kwenda na misimamo isiyobadilika kwa sababu tunataka maridhiano. Nitatenda haki na nitatoa muda mrefu zaidi kwa wajumbe kujadili sura ya kwanza na ya sita ambazo zina uzito mkubwa kuliko sura nyingine ambazo ni za maelezo tu. Mfano suala la haki za binadamu ambazo wote tunakubaliana nazo.”
Alisema wakati wa kujadili muundo wa Serikali ndani ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ukifika, ataishauri kamati ya uongozi, kutenga muda wa ziada katika suala hilo na mengine yenye utata.
Mwenyekiti huyo alisema suala la upigaji kura linatakiwa kuamuliwa kwa busara na atatumia hekima zake na za wajumbe wa Bunge hilo, kutatua mgogoro wa kura ya siri au ya wazi. MWANANCHI 

TB JOSHUA" NDEGE YA MALAYSIA IPO CHINI YA MAJI BAHARINI WATAIPATA HIVI KARIBUNI"


“The plane concerned is deep inside the sea. Some of the particles will be seen on the surface of the sea any moment from now.May their souls rest in peace. We pray the Lord gives the family and loved ones the strength to bear the loss. Our prayer and love are always with them, the nation of Malaysia and other countries who had passengers on this flight.”However,US Counter-terrorism officials now suspect that the plane flew for a total of five hours based on data automatically downloaded and sent back to Rolls Royce - the manufacturers of the Boeing 777's engines.
They are now pursuing the astonishing possibility that the plane and its 239 passengers was diverted to an undisclosed location 'with the intention of using it later of another purpose.The pilot or somebody else turned the planes' transponders off to avoid detection and flew it to another location

Friday, March 14, 2014

WABUNGE WA BUNGE MAALUM LA KATIBA KUKIONA CHA MOTO ,


MWENYEKITI wa Bunge Maalumu la Katiba, Samuel Sitta ameanza kazi na kuwaonya wajumbe wa bunge hilo ambao wamekuwa na tabia ya kupayuka ovyo kwenye vipaza sauti, kuwa wasimlaumu kwa vile atawabana kwa kutumia kanuni walizozitunga wao wenyewe. Sitta ameanza kazi huku wajumbe wengi wakiwa na imani naye kuwa ataliendesha Bunge hilo lenye mchanganyiko wa watu kwa haki na kwa viwango na kasi; lakini mwisho wake ni kuwapatia watanzania katiba nzuri wanayoitarajia.

Akizungumza jana baada ya kupishwa kiti hicho na mwenyekiti wa muda Pandu Ameir Kificho, Sitta alimsifu mwenyekiti huyo wa muda kwa vile aliendesha bunge hilo bila kanuni, hivyo kulifanya kutawaliwa na vituko vya wabunge kupiga kelele.

“Sasa tuna kanuni mambo ya kupiga kelele na kuwasha kipaza sauti bila kuruhusiwa, mtanilaumu bure, tusilaumiane, nitakuwa ndio natimiza wajibu wangu,” alisema Sitta.

Mwenyekiti huyo alisema Kificho alitumia busara, hekima na ustahimilivu mkubwa kuliongoza Bunge hilo ambalo halikuwa na kanuni, “Nina kitu cha kujifunza kwa mzee huyu kwa namna alivyoliendesha bunge hili kwa wiki tatu bila kuwa na kanuni.”

Alisema kitu kikubwa ambacho Kificho atakumbukwa ni kuliongoza Bunge hilo; lakini kwa kuteua kamati nzuri ya kanuni ambayo ilifanya kazi yaKe kwa weledi mkubwa na akaahidi kuwatumia wajumbe hao katika kamati zingine zitakazoundwa.

Katika ahadi yake baada ya kuchaguliwa, Sitta aliahidi kuhakikisha wanamaliza vikao vya Bunge kwa muda uliowekwa na sheria ili wananchi wasiwaone kama wajumbe hao ni waroho wa posho.

Mara tu baada ya kuanza kazi, Sitta aliamuru siku tatu kuanzia jana jioni hadi kesho Jumapili zitumike kwa wajumbe kuapa ili Jumatatu kazi kubwa ianze kwa Mwenyekiti wa Tume ya Marekebisho ya Katiba, Jaji Joseph Warioba kuwasilisha rasimu bungeni hapo.

“Tunatarajia kuwa kati ya Jumanne na Jumatano, Rais atakuja kulizindua Bunge hili,” alisema Sitta na kuongeza kuwa ameamua kuwa siku tatu kabla ya wajumbe kwenda kwenye kamati wapate muda wa kuwa na mjadala mpana kwa wajumbe wote wa kujadili mambo ya jumla yaliyoko kwenye rasimu hiyo.

Kwa upande wake Kificho aliwataka wajumbe wa Bunge Maalumu la Katiba kuwa wavumilivu na kutumia hekima na busara kwa kutoa hoja zenye mashiko zisizowagawa watanzania katika kupata Katiba mpya.

Kificho alitoa nasaha hizo wakati akikabidhi uenyekiti kwa Mwenyekiti wa kudumu, Samuel Sitta ambapo aliwataka wajumbe hao kutotoa hoja za kuwagawa watanzania kikabila, kikanda, kidini na kijinsia.

“Kazi ya kutengeneza kanuni haikuwa rahisi kwa sababu kila mmoja alikuwa na maoni na msimamo wake na kazi ya sasa ya kupata katiba japo kutakuwa na muongozo wa kanuni itakuwa ngumu kama tulivyoona hapo nyuma,” alisema Kificho aliyeteuliwa kushika nafasi hiyo Februari 18 na kuongeza:

“Kinachotakiwa kwenye bunge hili ni uvumilivu na kuweka mbele maslahi ya taifa na si binafsi. Wajumbe tumieni hekima na busara tupate katiba ambayo wananchi wanaisubiri kwa muda mrefu na kutakapotokea vikwazo tumalize kwa busara”.

Awali Katibu wa Bunge, Yahya Khamis Hamad alimwapisha Sitta na makamu mwenyekiti, Samia Suluhu Hassan na baadaye wajumbe kuapishwa ambapo alianza Kificho na kufuatiwa na Waziri Mkuu Mizengo Pinda, Makamu wa Pili wa Rais wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, Balozi Seif Ali Idd, Waziri Mkuu wa zamani Edward Lowassa na kufuatiwa na wajumbe wenye mahitaji maalumu.

Baada ya wajumbe wenye ulemavu kuapa walifuata mawaziri wa serikali zote mbili ili kuwapa fursa ya kesho kuondoka kwenda ofisini kwa ajili ya kuendelea na vikao vya maandalizi ya bajeti. Baada ya hapo watafuatia wajumbe wengine ambao wataapa kwa kuafuta alfabeti zao kuanzia A hadi Z bila kujali nyadhifa zao

GODFREY MGIMWA AWAOMBA WANAKALENGA KUMKOPESHA IMANI, YEYE ATAWALIPA MAENDELEO KALENGA

1
Mgombea ubunge wa jimbo la Kalenga kupitia chama cha Mapinduzi CCM Bw. Godfrey Mgimwa akiwahutubia wananchi katika kijiji cha Ilandutwa kata ya Mgama Iringa vijijini akiendelea na mikutano mbalimbali ya kampeni ambapo amewaomba wananchi wa vijiji hivyo kumkopesha imani  yao na kumpa kura za ndiyo siku ya machi 16 jumapili ijayo ili aweze kuwalipa maendeleo katika jimbo hilo 2 
Mgombea ubunge wa jimbo la Kalenga kupitia chama cha Mapinduzi CCM Bw. Godfrey Mgimwa na Ndugu Jesca Msambatavangu Mwenyekiti wa CCM Iringa wakiimba wimbo mara baada ya kuwasili katika kijiji cha Itwaga. 3
Msanii Dokii akitumbuiza katika kijiji cha Itwaga kabla ya kuanza mkutano huo. 4 
Mgombea ubunge wa jimbo la Kalenga kupitia chama cha Mapinduzi CCM Bw. Godfrey Mgimwa akishiriki kucheza ngoma na msanii Dokii katika kijiji cha Itwaga kabla ya mkutano huo kuanza wa pili kutoka kulia ni Ndugu Jesca Msambatavangu Mwenyekiti wa CCM Iringa 5 
Mgombea ubunge wa jimbo la Kalenga kupitia chama cha Mapinduzi CCM Bw. Godfrey Mgimwa akishiriki kucheza ngoma na msanii Dokii katika kijiji cha Itwaga kabla ya mkutano huo kuanza wa pili kutoka kulia ni Ndugu Jesca Msambatavangu Mwenyekiti wa CCM Iringa 6
Diwani wa kata ya Mgama Bw. Denis LupCala akipiga magoti kumuombea kura mgombea wa CCM Bw. Godfrye Mgimwa. 7
Wananchi wakinyanyua mikono yao juu kumuunga mkono Bw. Godfrey Mgimwa, 8
Umati wa wananchi waliohudhuria katika mkutano wa kampeni katika kijiji cha Itwaga. 9
Wananchi wakirejea nyumbani mara baada ya kumalizika kwa mkutano huo. 10
Katibu wa CCM mkoa wa Iringa . Hassan Mtenga wa pili kutoka kushoto na  kutibu wa CCM mkoa wa Mtwara Bw. Akwilombe wakiteta jambo wakati wa mkutano wa kampeni katika kijiji cha Ilandutwa kulia ni Meja Mbuta meneja wa kampeni hizo na kushoto ni Mwampamba kada CCM kutoka UVCCM.  12
Wananchi wakifuatilia kwa makini hotuba ya mgombea ubunge huyo. 13
Wananchi wakinyanyua mikono yao juujuu kuashiria kumkubali mgombea huyo.
11
Wananchi wakifuatilia kwa makini hotuba ya mgombea ubunge huyo.

Bunge maalum la Katiba -Wajumbe waapishwa mjini Dodoma leo.

Mwenyekiti wa Bunge Maalum la Katiba Bw. Samwel Sitta akila kiapo mbele ya Katibu wa Bunge hilo Bw. Yahya Khamis Hamad, wakati wa hafla ya kuwaapisha wajumbe wa Bunge Maalum la Katiba leo Mjini Dodoma.Kulia ni Naibu Katibu wa Bunge Hilo Thomas Kashilila.
Makamu Mwenyekiti wa Bunge Maalum la Katiba Samia Suluhu Hassan akila kiapo mbele ya Naibu Katibu wa Bunge Hilo Thomas Kashilila, wakati wa hafla ya kuwaapisha wajumbe wa Bunge Maalum la Katiba leo Mjini Dodoma.Kulia ni Katibu wa Bunge Hilo Yahya Khamis Hamad.
Mjumbe wa Bunge Maalum la Katiba ambaye ni Mwanasheria Mkuu FrederickWerema akitoa hoja wakati wa hafla ya kuwaapisha wajumbe wa Bunge Maalum la Katiba leo Mjini Dodoma.
Mjumbe wa Bunge Maalum la Katiba na aliyekuwa Mwenyekiti wa Muda wa Bunge hilo Pandu Ameir Kificho akila kiapo cha kuwa Mjumbe wa Bunge Hilo Mbele ya Mwenyekiti wa Bunge Hilo Samwel Sitta
Mjumbe wa Bunge Maalum la Katiba na Waziri Mkuu Bw. Mizengo Pinda akila kiapo cha kuwa Mjumbe wa Bunge Hilo Mbele ya Mwenyekiti wa Bunge Hilo Samwel Sitta
Mjumbe wa Bunge Maalum la Katiba Bw. Edward Lowassa akila kiapo cha kuwa Mjumbe wa Bunge Hilo Mbele ya Mwenyekiti wa Bunge Hilo Samwel Sitta

Bunge la Katiba lapata Katibu na Naibu Katibu- Waapisha na Rais Dkt Jakaya Kikwete leo.

Katibu wa Bunge Maalum la Katiba Bw, Yahya Khamis Hamad akiapa mbele ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Jakaya Kikwete Leo Mjini Dodoma.
Katibu wa Bunge Maalum la Katiba Bw. Yahya Khamis Hamad akisaini Kiapo mbele ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Jakaya Kikwete Leo Mjini Dodoma.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Jakaya Kikwete akisaini kiapo baada ya kumuapisha Katibu bunge Bw. Yahya Khamis Hamad (mbele aliyesimama)
Katibu wa Bunge Maalum la Katiba Bw. Yahya Khamis Hamad akipokea vitabu vya muongozo kutoka kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Jakaya Kikwete Leo Mjini Dodoma.
Naibu Katibu wa Bunge Maalum la Katiba Thomas Kashilila akiapa mbele ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Jakaya Kikwete Leo Mjini Dodoma.
Naibu Katibu wa Bunge Maalum la Katiba Bw, Thomas Kashilila akisaini Kiapo mbele ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Jakaya Kikwete Leo Mjini Dodoma.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Jakaya Kikwete akisaini kiapo baada ya kumuapisha Naibu Katibu bunge Maalum la Katiba Bw. Thomas Kashilila (aliyesimama)
Naibu Katibu wa Bunge Maalum la Katiba Bw, Thomas Kashilila akipokea vitabu ya muongozo kutoka kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Jakaya Kikwete Leo Mjini Dodoma.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Jakaya Kikwete akiwaeleza jambo Waziri Mkuu Mizengo Pinda(kulia kwa Rais) akifuatiwa na  Mwenyekiti wa Bunge Maalum la Katiba Samwel Sitta, Prof. Mark Mwandosya na Mwisho Pindi Chana.
Mwenyekiti wa Bunge Maalum la Katiba Bw. Samwel Sitta (kushoto) akisalimiana na aliyekuwa Mwenyekiti wa Muda wa Bunge hilo Pandu Ameir Kificho wakati wa Hafla ya kuwaapisha Katibu na Makamu Katibu wa Bunge Maalum la Katiba.Katikati ni Mjumbe wa Bunge hilo na Waziri wa Katiba na Sheria Dkt. Asha Rose Migiro Mjini Dodoma.
Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Ombeni Sefue (Mwenye tai ya bluu) akifurahia jambo na Mwenyekiti wa Bunge Maalum la Katiba Samwel Sitta (kulia), Katibu wa Bunge Maalum la Katiba Bw. na Naibu wa Bunge Hilo Thomas Kashilila (Kushoto kwa  Katibu wa Bunge) Leo Mjini Dodoma.
Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Ombeni Sefue akimweleza jambo Naibu Waziri Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Bw. Juma Nkamia wakati wa Hafla ya Kuapishwa kwa Katibu na Naibu Katibu wa Bunge Maalum la Katiba Leo Mjini Dodoma.          
   (PICHA NA HASSAN SILAYO-MAELEZO)

TASWA F.C YAITAMBIA DACICO F.C -KIBWEGELE

 Mwenyekiti wa Taswa Fc. Majuto Omary, akifafanua ambo kuhusiana na mchezo wao dhidi ya Dacico muda mfupi baada ya kuwasili Makao Makuu ya Chuo cha Uandishi wa Habari na Utawala. DACICO. Kibamba CCM.
 Baadhi ya Wanafunzi w Dacico na Wachezaji wa Taswa wakisikiliza kwa makini
 Wachezaji wa Taswa F.c, Ally Mkongwe(wa pili kushoto),na mbozi(kulia), wakifuatilia kwa makini mazungumzo hayo.
 Kikosi cha Timu ya Wachezaji wa Dacico Qween.
 Kikosi cha Timu ya Wachezaji wa Timu ya Dacico F.c.
 Wachezaji wa Timu ya Taswa Qween.
 Vikosi vya Timu za Dacico na Taswa F.c. katika picha ya Pamoja.

Na:  JENNY CHARLES.
 
Chou cha uandishi wa habari  na utawala DAR ES SALAAM CITY COLLEGE, Jana zmechuana vikali katika mchezo wa kirafiki wa mpira wa pete(Netball) kati ya Timu ya Tanzania Sport's Write Association[Taswa]  pamoja na Timu ya wanafunzi wa Dar es salaam city college[Dacico] .
Mechi hiyo ilifanyika kwenye uwanja wa kibwegere uliopo katika kata ya kibamba wilaya ya kinondoni jijini dar es salaam.
Mechi ilianza saa kumi na moja jioni, kutokana na hali ya hewa iliyosababishwa na Mvua kubwa iliyonysha mapema kabla ya mchezo ambapo katika kipindi cha kwanza  mpira ulikuwa mgumu kwa upande wa timu ya Taswa kutokana na wachezaji wa DACICO kukianza kipindi hicho kwa kasi ambayo hata hivyo haikuwachukua muda mrefu wachezaji wa Dacico kuchoka kutokana na kukosa Pumzi ya muda mrefu.
Taswa baada ya kuona hivyo waliweza kuitumia nafasi hiyo na hivyo kufanikiwa kupata bao kipindi cha kwanza ambalo lilipachikwa wavuni na mchezaji wao Ally Mkongwe baada ya kuitumia Vizuri Pasi ya Majuto Omary.
Kipindi cha pili timu zote zilifanya mabadiliko ambapo kwa upande wa Taswa walifanya mabadiliko na Dacico nao walifanya mabadiliko ambapo Mchezaji nyota (Kocha Mchezaji wa Dacico)Shaaban Mpalule, aliingia kuchukua nafasi ya dulla ambaye aliumia mabadiliko ambayo yalionekana kuisaidia kwa kiasia kkubwa kikosi cha Dacico, lakini hata hivyo muda huo huo Taswa ilifanikiwa kupata bao la pili kwa shuti kali ambalo liliwekwa kimiani na Side Boy, baada ya kuitumia vyema nafasi ya mchezaji wao Salumu Jaba.
Dacico baada ya kuona hivyo walikuja juu na kucheza kwa kasi kwa kumtumia nyota wake Shaaban Mpalule, ambaye kabla ya kujiunga na Dacico, Pia aliwahi kuitumikia Timu ya Taswa kwa zaidi ya Miaka 10, akiwa na vyombo mbali bali vya Habari, Vikiwemo, Tanzania Daima, Mlimani Radio, Praise Power, Times Fm na vingine Vingi, walifanikiwa kupata bao la kufutia machozi baada ya Mpalule kufanya kazi ya ziada ya kuwaramba vyenga kwa kasi na kutoa krosi iliyomkuta Side wa Dacico na kufanikiwa kufunga bao hilo.
mchezo wa marudiano baina ya timu hizo umepangwa kufanyika baada ya miezi miwili kwenye uwanja wa Taswa kijitonyama jijini Dar es Salaam.
Mpaka mechi inamalizika [Taswa]Tanzania Sport's Write Assoc
Wakati huo huo kikosi cha Timu ya Taswa Qween kilifanikiwa pia kuibuka na ushindi wa Mabao kumi na tatu dhidi ya mabao matatu ya Dacico katika mchezo uliokuwa mkali na wa kusisimua kutokana na Wachezaji wa Timu ya Dacico kutaka kuwafunga Taswa Qween ambao walionekana kucheza kwa kutumia uzoefu mkubwa.

Wednesday, March 12, 2014

Wakufunzi vya vyuo mbalimbali wapigwa msasa

_DSC0076Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais, Eng. Angelina Madete (Katikati) na Mkurugenzi wa mazingira Dkt. Julius Ningu (Kulia) wakimsilikiza Bw. Julio Esterban Mshauri Mwelekezi kutoka UNIDO akitoa ufananuzi kwa wakufunzi kutoka Vyuo vya ufundi nchini._DSC0100Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais, Eng. Angelina Madete akitoa hotuba ya ufunguzi wa warsha ya Mafunzo ya wakufunzi kutoka Vyuo vya Ufundi Nchini, mafunzo hayo yanafanyika katika Hotel ya Blue Pearl jijini Dar es Salaam
_DSC0111Washiriki wa Mafunzo wakiwa katika picha ya Pamoja na Mgeni rasmi Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais Eng. Angelina Madete watatu kutoka kulia mara baada ya ufunguzi wa warsha.
_DSC0119Sehemu ya washiriki wa warsha wakifatilia hotuba ya ufunguzi kutoka kwa mgeni rasmi.
Na Lulu Mussa na Rashda Swedi,
 Ofisi ya Makamu wa Rais, Dar es Salaam
Serikali inaendelea na jitihada za kutoa elimu kwa umma juu ya njia bora za kuhudumia majokofu na viyoyozi ili kulinda tabaka la Ozoni.
Hayo yamesemwa jijini Dar es Salaam jana na Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais, Eng. Angelina Madete wakati wa ufunguzi wa Warsha ya Mafunzo kwa Wakufunzi kutoka Vyuo mbalimbali vya Ufundi Nchi.
Katika Hotuba yake Bi Madete amesema kuwa kemikali haribifu zinauwezo mkubwa kuharibu tabaka la Ozoni na kuongeza joto angani. Kutokana na sababu hizo, Serikali ya Tanzania kwa kushirikiana na jamii za kimataifa zimekubaliana kufanya jitihada za kuondoa kemikali  hizo hatarishi.
Bi Madete ameainisha baadhi ya kemikali hizo kuwa ni methyl bromide, halons na chloroflorocarborns ambazo hutumika kama vipozi katika majokofu, viyoyozi, vifaa vya  kuzima moto, usafishaji chuma, ufukizaji wa mazao katika maghala na utengenezaji wa magodoro ambazo huleta madhara kwa tabaka la ozoni na adhari zake hutokea kwa binadamu, mimea na viumbe hai.
Katika awamu ya kwanza, Tanzania imefanikiwa kuondoka tani  296 za kemikali hizo haribifu ikiwa ni utekelezaji wa Mkataba wa Montreal na Vienna ambayo Tanzania iliridhia mwaka 1993.
Aidha, Bi Madete ameyataja madhara yatokanayo na uharibifu wa Tabaka la Ozoni kuwa ni kuongezeka kwa magonjwa ya saratani ya ngozi,uharibifu wa macho maarufu mtoto wa jicho, na upungufu wa uwezo wa mwili kujikinga na maradhi.  Athari hizi kwa kiasi kikubwa zinatokana na shughuli za kibinadamu kama vile matumizi ya kemikali haribifu na zisizo rafiki kwa mazingira. 
Warsha hii ya siku mbili imeratibiwa na Ofisi ya Makamu wa Rais na inajumuisha wakufunzi kutoka Vyuo vya Ufundi vya Zanzibar na Mikoa ya Kilimanjaro, Arusha, Kigoma, Mbeya na Mwanza.

RATIBA LIGI KUU BARA YAREKEBISHWA, SASA KUMALIZIKA APRILI 19!!

VPL1
Na Boniface Wambura, TFF
Bodi ya Ligi Kuu Tanzania (TPLB) imeifanyia marekebisho ratiba ya Ligi Kuu ya Vodacom (VPL) ambapo sasa itamalizika Aprili 19 mwaka huu badala ya Aprili 27 mwaka huu.
Marekebisho hayo yamefanyika ili kutoa fursa kwa timu ya Taifa 9Taifa Stars) kujiandaa kwa mechi za mchujo la Kombe la Afrika 2015 ambapo itacheza raundi ya awali Mei mwaka huu.
Kutokana na marekebisho hayo, Yanga itacheza na Prisons (Uwanja wa Taifa) Machi 26 mwaka huu katika mechi ya raundi ya 17 wakati Machi 19 mwaka huu kwenye uwanja huo huo ni Yanga na Azam.
Machi 15 mwaka huu kutakuwa na mechi mbili; Azam na Coastal (Azam Complex), na Mtibwa Sugar itacheza na Yanga (Jamhuri). Mgambo na Azam zitacheza Machi 26 mwaka huu Mkwakwani, na Aprili 9 mwaka huu Yanga itaialika Kagera Sugar (Taifa).
Kusoma zaidi bofya hapa chini

DACICO KUWAVAA TASWA FC, TASWA QWEEN KESHO KATIKA SONA NA NETBALL.

TIMU ya soka na netiboli ya waandishi wa habari za michezo nchini, Taswa FC na Taswa Queens kesho zitacheza mechi maalum za kirafiki dhidi ya Chuo Cha Uandishi wa Habari, Mawasiliano ya Umma na Utawala kijulikanacho kwa jina la Dar es Salaam City College (Dacico).
Baadhi ya Wanafunzi wa Dacio wakiwa kwenyeb maandalizi ya Mchezo huo, hapa wanafahamishwa kuhusiana na mikakati ya ushindi dhidi ya Taswa.
Mechi hiyo imepangwa kufanyika Kibamba, nje kidogo ya jiji la Dar es Salaam na maandalizi yake yamekwisha kamilika kwa mujibu wa mwenyekiti wa Taswa SC, Majuto Omary.
Majuto alisema kuwa  mechi hizo zimepangwa kuanza saan 9.00 alasiri na zimeandaliwa ili kuendeleza uhusiano baina yao na chuo hicho maarufu na bora nchini.
Alisema kuwa wanatarajia kuondoka jijini saa 5.00 asubuhi na kabla ya kucheza mechi hizo, watapata fursa ya kutembelea mazingira ya chuo hicho na baadaye kuzungumza na wanafunzi na walimu.
“Tumepokea mwaliko na naamini watataka kujifunza kutoka kwetu, sisi ni waandishi wa habari ambao tupo tayari kazini na pale kuna wanafunzi ambao wanataka kuja kufanya kazi tunayofanya sisi, hivyo hii ni ziara muhimu sana mbali ya kucheza michezo,” alisema Majuto.
Alisema kuwa kocha mkuu wa timu ya soka, Ali Mkongwe na msimamizi wa timu ya netiboli, Sharifa Mustapha waliendesha mafunzo mazuri kwa wachezaji kwenye mazoezi na lengo kubwa ni kupata ushindi.
Mkurugenzi wa Dacico, Idrisa Mziray alisema kuwa wamejiandaa vyema kwa ajili ya mechi hizo na lengo kubwa ni kuongeza mtandao wa chuo chao ambacho kina matawi handi mikoani. Mziray alisema kuwa wanafunzi wao wa tawi la Mbeya nao wamefika kwa ajili ya ziara hiyo na kuonyesha uwezo wao katika michezo.
“Tupo tayari kwa ajili ya mechi hizo, tunajua Taswa FC na Taswa Queens ni timu nzuri nah ii imetokana na kufanya vyema katika mechi zao mbali mbali, tupo tayari kwa changamoto,” alisema Mziray.
Mwisho….

Mkurabita Kuwanufaisha wakulima wa Miwa Mkoani Morogoro

MIWA. MIWANa Lorietha Laurence-maelezo
Mpango wa Kurasimisha Rasilimali na Biashara za Wanyonge  Tanzania, mapema mwaka huu umeanzisha  mradi wa urasimishaji wa  mashamba ya wakulima wadogo wa zao la miwa wilaya za Kilombero na Kilosa mkoani Morogoro.
Aidha taarifa  ilieleza kuwa Mpango huo  utahusisha vijiji vinne vya Ruhembe, Kidogobasi,Kihelezo, Kitete-Msindazi na vingine  sita  kutoka  Wilaya ya Kilombero  Mkula ,msolwa ujamaa, Katurukila, Sonjo, Sole na Magombera.
Katika taarifa iliyotolewa kwa vyombo vya habari leo jijini Dar es Salaam Jumla ya hati miliki 8,902 za kimila zimeandaliwa   3,679 zimesajiliwa na nyingine 2142 zimetolewa kwa wamiliki wa wilaya za Njombe, Mufindi na Rungwe katika kutekeleza zoezi hilo la urasimishaji lilioanza Novemba  2011.
Utekelezaji  huo ni wa awamu ya nne unaofanywa na MKURUBITA  kwa lengo la  kukuza  mtaji  na utawala  bora  ili kuwawezesha  wananchi kuinua mapato yao  kwa  kupunguza umaskini   kwa manufaa yao.
Pia MKURABITA kwa kushirikiana na wadau wake imetoa wito kwa wakulima wa   miwa  Kilosa na Kilombero  kuonana na uongozi wa vyama vya wakulima wa miwa kutoka Ruhembe, Kidatu na Msolwa kwa ajili ya  kuthibitisha umiliki  wa mashamba.
 MKURABITA    imeandaa mafunzo  kwa ajili ya mipango  na michanganuo ya  biashara  kwa kuwaunganisha  wakulima na Taasisi za mitaji na mikopo , baada ya kukamiliksha zoezi la mchakato wa urasimishaji wilayani Kilosa  na Kilombero.