Mpango
wa Kurasimisha Rasilimali na Biashara za Wanyonge Tanzania, mapema
mwaka huu umeanzisha mradi wa urasimishaji wa mashamba ya wakulima
wadogo wa zao la miwa wilaya za Kilombero na Kilosa mkoani Morogoro.
Aidha
taarifa ilieleza kuwa Mpango huo utahusisha vijiji vinne vya Ruhembe,
Kidogobasi,Kihelezo, Kitete-Msindazi na vingine sita kutoka Wilaya
ya Kilombero Mkula ,msolwa ujamaa, Katurukila, Sonjo, Sole na
Magombera.
Katika
taarifa iliyotolewa kwa vyombo vya habari leo jijini Dar es Salaam
Jumla ya hati miliki 8,902 za kimila zimeandaliwa 3,679 zimesajiliwa
na nyingine 2142 zimetolewa kwa wamiliki wa wilaya za Njombe, Mufindi na
Rungwe katika kutekeleza zoezi hilo la urasimishaji lilioanza
Novemba 2011.
Utekelezaji huo
ni wa awamu ya nne unaofanywa na MKURUBITA kwa lengo
la kukuza mtaji na utawala bora ili kuwawezesha wananchi kuinua
mapato yao kwa kupunguza umaskini kwa manufaa yao.
Pia
MKURABITA kwa kushirikiana na wadau wake imetoa wito kwa wakulima
wa miwa Kilosa na Kilombero kuonana na uongozi wa vyama vya wakulima
wa miwa kutoka Ruhembe, Kidatu na Msolwa kwa ajili ya kuthibitisha
umiliki wa mashamba.
MKURABITA imeandaa
mafunzo kwa ajili ya mipango na michanganuo ya biashara kwa
kuwaunganisha wakulima na Taasisi za mitaji na mikopo , baada ya
kukamiliksha zoezi la mchakato wa urasimishaji wilayani Kilosa na
Kilombero.
No comments:
Post a Comment