Rais
Jakaya Kikwete akiongoza Kikao cha Ujumbe wa Mawaziri na Wakuu wa
Taasisi za Uhifadhi nchini kabla ya kuanza rasmi kwa Mkutano wa
Kimataifa wa Kuzuia Biashara Haramu ya Wanyamapori jijini London,
Uingereza. (Picha na Pascal Shelutete, TANAPA)
Na Pascal Shelutete, TANAPA
Mkutano
wa Kimataifa kuhusu Biashara Haramu ya Wanyamapori (Conference on
Illegal Wildlife Trade) unaanza rasmi leo katika ukumbi wa Lancaster
House.
Mkutano
huu utakaohudhuriwa na jumla ya mataifa 47 na Mashirika 13 ya Kimataifa
umeitishwa na Serikali ya Uingereza kwa lengo la kujadiliwa na masuala
maalum matatu kuhusiana na biashara haramu ya wanyamapori. Masuala
maalum uyanayotarajiwa kujadiliwa ni Jinsi ya Kuimarisha Usimamizi wa
Sheria (Law Enforcement) na mchango wa mfumo mzima wa sheria za jinai
(criminal justice system) katika kukabiliana na biashara hiyo.
Aidha,
utajadili Jinsi ya kupunguza hitaji la bidhaa zinazotokana na
wanyamapori (demand for wildlife products) na Jinsi ya kusaidia
Maendeleo Endelevu kwa Jamii zilizoathiriwa na biashara hiyo haramu.
Mkutano
huu utazungumzia wanyama aina ya tembo, faru na tiger. Wanyama hawa
wamechaguliwa kwa kuzingatia jinsi wanavyoshambuliwa zaidi na makundi ya
wawindaji haramu kwa lengo la kuu pembe na ngozi zao.
Rais
Jakaya Mrisho Kikwete tayari ameshawasili Uingereza akiongoza ujumbe wa
maafisa kutoka Serikali ya Tanzania kwa ajili ya kushiriki Mkutano huu
No comments:
Post a Comment