NMB
yazindua rasmi tawi la Buzuruga mkoani Mwanza .Tawi hili likiwa ni tawi
la tisa kuzinduliwa katika mkoa huo, huku NMB ikiendelea kuwa ndio
benki yenye matawi mengi zaidi Tanzania.
Mheshimiwa Mkuu wa Wilaya ya Nyamagana, Bw. Baraka Konisaga akikata utepe kuashiria uzinduzi rasmi wa tawi la NMB Buzuruga. Wanaoshuhudia
uzinduzi huo kutoka kushoto ni Naibu Meya Jiji la Mwanza mhe. John
Minja, Mkurugenzi wa jiji la Mwanza Bw. Halifa H. Hidana kutoka kulia ni
Meneja wa NMB Kanda ya Ziwa, Bw. Straton Chilongola, Meneja Tawi la NMB
Buzuruga, Gadiel Sawe na Meneja Mawasilianowa NMB, Josephine Kulwa.
Akizungumza katika sherehe ya ufunguzi huo, Mkuu wa Wilaya ya Nyamagana, Mh. Baraka Konisaga ameipongeza
benki ya NMB kwa hatua nyingine iliyopiga kwa kusogeza zaidi huduma kwa
wateja na kuitaka iendelee kuwa kinara wa huduma za kibenki nchini.
Aliwahamasisha
wafanyabiashara, wakulima na wafanyakazi waitumie fursa ya kuwepo kwa
tawi la NMB Buzuruga kukidhi mahitaji yao ya kibenki. Vilevile,
aliwasihi wananchi waache kuweka fedha kwenye chaga za vitanda na badala
yake watumie njia salama ya kuweka fedhabenki.
“Ni
matumaini yangu kuwa uwepo wa tawi hili la Buzuruga ni neema kubwa kwa
wakazi wa Mabatini, Buzuruga, Nyakato, Igoma, Kishili, Buswelu na hadi
Kisesa hasa wafanyabiashara katika hizi mashine za mpunga kwani
kesi za watu kuporwa fedha majumbani au maofisini zitapungua badala ya
kuongezeko kwasababu wateja wanaofungua akaunti ndio itakua habari ya
eneo hili” alisema Konisaga.
Kwa upande wake, Bw.Straton Chilongola, ambaye ni Meneja wa NMB Kanda ya Ziwa, alisema “Tangu
kuanzishwa kwa tawi hili tumeshuhudia wakazi wengi wakija kufungua
akaunti na kutumia huduma za benki hii. Hii ni uthibitisho kuwa wakazi
hawa walikuwa na kiu ya kupata huduma za kibenki karibu na milangoni
kwao. Lakini pia tutaendelea kubuni mbinu mbalimbali
zitakozotuwezesha kuwafikia wateja wetu karibu zaidi ili kuondoa
msongamano kwenye matawi na pia kuokoa muda wa wateja ili waweze kutumia
muda wao kwa shughuli endelevu.”
Tawi
hili la Buzuruga, linatoa huduma zote za kibenki, ikiwa ni pamoja na
huduma ya mikopo ya aina mbalimbali bila kusahau mikopo ya Kilimo.
Tawi
hili litakuwa wazi kila Jumatatu hadi Ijumaa kuanzia saa mbili na nusu
asubuhi hadi saa kumi jioni ( 2:30 asubuhi – 10:00jioni) na Jumamosi
kuanzi saa mbili na nusu asubuhi hadi saa sita na nusu mchana (2:30
asubuhi – 6:30 mchana), Jumapili na siku za Sikukuu hakutakuwa na huduma
ndaniyatawihili.
NMB daima benki yako!
No comments:
Post a Comment