Rais Jakaya Kikwete, akipokea mfano wa helikopta kutoka kwa mtoto wa
bilionea wa pili duniani, Warren Buffett, Howard ambaye familia yake
kupitia Mfuko wa Warren Buffett Foundation watatoa helikopta moja
itakayotumika kupambana na ujangili katika Pori la Akiba la Selous.
Picha ya Wizara ya Maliasili na Utalii.
DAR ES SALAAM.
FAMILIA ya bilionea namba mbili nchini Marekani, Warren Buffett imeunga mkono juhudi za kupambana na ujangili nchini kwa kuchangia helikopta moja.
FAMILIA ya bilionea namba mbili nchini Marekani, Warren Buffett imeunga mkono juhudi za kupambana na ujangili nchini kwa kuchangia helikopta moja.
Familia ya Warren Buffett imeamua kutoa msaada huo
kupitia Mfuko wa Howard Buffett Foundation, baada ya kuridhishwa na
hatua mbalimbali zinazochukuliwa na Serikali.
Helikopta hiyo itatumika kwa ajili ya kusaidia mapambano dhidi ya ujangili katika hifadhi za taifa na mapori ya akiba nchini.
Msaada huo ulikabidhiwa juzi kwa Rais Jakaya
Kikwete na mtoto wa bilionea huyo, Howard Buffett, ambaye yuko nchini
kwa mapumziko ya kitalii.
Akikabidhi mfano wa helkopta kwa Rais Kikwete,
Buffett alisema amevutiwa na kazi nzuri inayofanywa na Serikali ya
Tanzania katika kukabiliana na ujangili hususan wa tembo na faru.
Waziri wa Maliasili na Utalii, Lazaro Nyalandu
alisema wamepokea kwa furaha ufadhili huo, ambapo utahusisha mafunzo kwa
marubani wawili nchini Marekani ama Afrika Kusini kutokana na matakwa
ya wizara.
“Wametuambia pesa ipo tayari ila ni jukumu letu
sisi kama Serikali kuchagua aina ya helikopta tunayoitaka. Itakuwa na
uwezo wa kubeba watu sita na kwa sasa tunaangalia kama tuchukue Bell ama
Ecopter, wataalamu wanashughulikia,” alisema.MWANANCHI
No comments:
Post a Comment