Mkuu
wa Mkoa wa Katavi Dkt Rajabu Rutengwe amewataka wakazi wa mkoa huo
kuwasomesha watoto wa kike bila ubaguzi kwa kuwa ukimuelimisha mototo wa
kike umeielimisha jamii kubwa.
Dkt
Rutengwe alitoa kauli hiyo mwishoni mwa wiki katika kilele cha
maadhimisho ya siku ya mwanamke yaliyofanyika kimkoa katika Tarafa ya
Karema Wilaya ya Mpanda na kuhudhuliwa na mamia kwa maelfu ya wanawake
na kupambwa na burudani za ngoma na michezo mbalimbali.
Katika
hotuba yake hiyo Mkuu wa Mkoa ametoa wito kwa wananchi mkoani humo
kuhakikisha wanawasomesha watoto wa kike hadi mwisho wa upeo wa kielimu
sawa na wanavyowasomesha watoto wa kiume.
Pia
amewataka wanawake kushiriki katika shughuli za uzalishaji mali ili
ziweze kuwasaidia katika maisha na kuepukana na hali ya utegemezi.
Akatolea
mfano kuwa eneo la mwambao wa ziwa Tanganyika hasa Tarafa ya Karema
wamepewa mradi wa Mwalo unaojengwa na serikali ambapo utakapokamilika
utatumike vizuri kwa manufaa ya kuwaletea maendeleo.
Amehimiza
wananwake wachangamkie mradi huo. Pia akawasisitiza kujitokeza katika
kugombea na kushika nafasi mbalimbali za uongozi katika jamii kwa kuwa
akina mama wanaweza hata bila kuwezeshwa maadamu tu kujiamini na
kujitokeza .
Katika
hatua nyingine amewasisitiza kujitokeza kutumia madawati ya jinsia
yaliyoanzishwa kwa ajili ya kutoa malalamiko na unyanyaswaji wanao
fanyiwa wanawake na watoto majumbani.
Awali
katika risala yao wanawake walieleza changamoto wanazokabiliwa nazo
ikiwa ni pamoja na ukosefu wa mitaji kwa ajili kuendeleza miradi yao
katika vikundi vya uzalishaji mali.
Waliiomba serikali kuendelea kuwasaidia kwa kuwapa mikopo ya riba nafuu,.
Pia walishauri vyombo vya mikopo kupunguza riba katika mikopo yao ili waweza kukopo.
Naye
Mratibu wa Dawati la jinsia kutoka jeshi la polisi Inspekta Vijinia
Sodoka amewahamasisha akina mama kujitokeza kutumia dawati hilo kutoa
matatizo na unyanyasaji wanaofanyiwa na waume zao majumbani kwani kwa
kutoa taarifa wataweza kusaidia kupunguza nap engine kukomesha kabisa
hali hiyo.
Hata
hivyo alisema pamoja na unyanyasaji kwa akina mama na watoto, nao
wanaume wameshauriwa wanapofanyiwa vitendo vya ukatili na wake zao
wajitokeze kutoa taarifa polisi ambapo kupitia kitengo cha dawati la
jinsia watasaidiwa kuliko kukaa kimya majumbani bila kutolea taarifa
vitendo hivyo.
Alieleza
kuwa wapo akina baba wananyanyaswa na wake zao kutokana na mfumo uliopo
wanaogopa kutoa taarifa, lakini ukweli ni kuwa wanaume nao
wananyanyasika kwenye ndoa zao ila wanaogopa kusema na kutolea taarifa
vitendo hivyo.
No comments:
Post a Comment