Mwenyekiti wa Taswa Fc. Majuto Omary, akifafanua ambo kuhusiana na mchezo wao dhidi ya Dacico muda mfupi baada ya kuwasili Makao Makuu ya Chuo cha Uandishi wa Habari na Utawala. DACICO. Kibamba CCM.
Baadhi ya Wanafunzi w Dacico na Wachezaji wa Taswa wakisikiliza kwa makini
Wachezaji wa Taswa F.c, Ally Mkongwe(wa pili kushoto),na mbozi(kulia), wakifuatilia kwa makini mazungumzo hayo.
Kikosi cha Timu ya Wachezaji wa Dacico Qween.
Kikosi cha Timu ya Wachezaji wa Timu ya Dacico F.c.
Wachezaji wa Timu ya Taswa Qween.
Vikosi vya Timu za Dacico na Taswa F.c. katika picha ya Pamoja.
Na: JENNY CHARLES.
Chou cha uandishi wa habari na utawala DAR ES SALAAM CITY COLLEGE, Jana zmechuana vikali katika mchezo wa kirafiki wa mpira wa pete(Netball) kati ya Timu ya Tanzania Sport's Write Association[Taswa] pamoja na Timu ya wanafunzi wa Dar es salaam city college[Dacico] .
Mechi hiyo ilifanyika kwenye uwanja wa kibwegere uliopo katika kata ya kibamba wilaya ya kinondoni jijini dar es salaam.
Mechi ilianza saa kumi na moja jioni, kutokana na hali ya hewa iliyosababishwa na Mvua kubwa iliyonysha mapema kabla ya mchezo ambapo katika kipindi cha kwanza mpira ulikuwa mgumu kwa upande wa timu ya Taswa kutokana na wachezaji wa DACICO kukianza kipindi hicho kwa kasi ambayo hata hivyo haikuwachukua muda mrefu wachezaji wa Dacico kuchoka kutokana na kukosa Pumzi ya muda mrefu.
Mechi ilianza saa kumi na moja jioni, kutokana na hali ya hewa iliyosababishwa na Mvua kubwa iliyonysha mapema kabla ya mchezo ambapo katika kipindi cha kwanza mpira ulikuwa mgumu kwa upande wa timu ya Taswa kutokana na wachezaji wa DACICO kukianza kipindi hicho kwa kasi ambayo hata hivyo haikuwachukua muda mrefu wachezaji wa Dacico kuchoka kutokana na kukosa Pumzi ya muda mrefu.
Taswa baada ya kuona hivyo waliweza kuitumia nafasi hiyo na hivyo kufanikiwa kupata bao kipindi cha kwanza ambalo lilipachikwa wavuni na mchezaji wao Ally Mkongwe baada ya kuitumia Vizuri Pasi ya Majuto Omary.
Kipindi cha pili timu zote zilifanya mabadiliko ambapo kwa upande wa Taswa walifanya mabadiliko na Dacico nao walifanya mabadiliko ambapo Mchezaji nyota (Kocha Mchezaji wa Dacico)Shaaban Mpalule, aliingia kuchukua nafasi ya dulla ambaye aliumia mabadiliko ambayo yalionekana kuisaidia kwa kiasia kkubwa kikosi cha Dacico, lakini hata hivyo muda huo huo Taswa ilifanikiwa kupata bao la pili kwa shuti kali ambalo liliwekwa kimiani na Side Boy, baada ya kuitumia vyema nafasi ya mchezaji wao Salumu Jaba.
Dacico baada ya kuona hivyo walikuja juu na kucheza kwa kasi kwa kumtumia nyota wake Shaaban Mpalule, ambaye kabla ya kujiunga na Dacico, Pia aliwahi kuitumikia Timu ya Taswa kwa zaidi ya Miaka 10, akiwa na vyombo mbali bali vya Habari, Vikiwemo, Tanzania Daima, Mlimani Radio, Praise Power, Times Fm na vingine Vingi, walifanikiwa kupata bao la kufutia machozi baada ya Mpalule kufanya kazi ya ziada ya kuwaramba vyenga kwa kasi na kutoa krosi iliyomkuta Side wa Dacico na kufanikiwa kufunga bao hilo.
mchezo wa marudiano baina ya timu hizo umepangwa kufanyika baada ya miezi miwili kwenye uwanja wa Taswa kijitonyama jijini Dar es Salaam.
Mpaka mechi inamalizika [Taswa]Tanzania Sport's Write Assoc
Mpaka mechi inamalizika [Taswa]Tanzania Sport's Write Assoc
Wakati huo huo kikosi cha Timu ya Taswa Qween kilifanikiwa pia kuibuka na ushindi wa Mabao kumi na tatu dhidi ya mabao matatu ya Dacico katika mchezo uliokuwa mkali na wa kusisimua kutokana na Wachezaji wa Timu ya Dacico kutaka kuwafunga Taswa Qween ambao walionekana kucheza kwa kutumia uzoefu mkubwa.
No comments:
Post a Comment