TIMU ya soka na netiboli ya waandishi wa habari za michezo
nchini, Taswa FC na Taswa Queens kesho zitacheza mechi maalum za kirafiki dhidi
ya Chuo Cha Uandishi wa Habari, Mawasiliano ya Umma na Utawala kijulikanacho
kwa jina la Dar es Salaam City College (Dacico).
Baadhi ya Wanafunzi wa Dacio wakiwa kwenyeb maandalizi ya Mchezo huo, hapa wanafahamishwa kuhusiana na mikakati ya ushindi dhidi ya Taswa. |
Mechi hiyo imepangwa kufanyika Kibamba, nje kidogo ya jiji
la Dar es Salaam na maandalizi yake yamekwisha kamilika kwa mujibu wa
mwenyekiti wa Taswa SC, Majuto Omary.
Majuto alisema kuwa
mechi hizo zimepangwa kuanza saan 9.00 alasiri na zimeandaliwa ili kuendeleza
uhusiano baina yao na chuo hicho maarufu na bora nchini.
Alisema kuwa wanatarajia kuondoka jijini saa 5.00 asubuhi na
kabla ya kucheza mechi hizo, watapata fursa ya kutembelea mazingira ya chuo
hicho na baadaye kuzungumza na wanafunzi na walimu.
“Tumepokea mwaliko na naamini watataka kujifunza kutoka
kwetu, sisi ni waandishi wa habari ambao tupo tayari kazini na pale kuna
wanafunzi ambao wanataka kuja kufanya kazi tunayofanya sisi, hivyo hii ni ziara
muhimu sana mbali ya kucheza michezo,” alisema Majuto.
Alisema kuwa kocha mkuu wa timu ya soka, Ali Mkongwe na
msimamizi wa timu ya netiboli, Sharifa Mustapha waliendesha mafunzo mazuri kwa
wachezaji kwenye mazoezi na lengo kubwa ni kupata ushindi.
Mkurugenzi wa Dacico, Idrisa Mziray alisema kuwa wamejiandaa
vyema kwa ajili ya mechi hizo na lengo kubwa ni kuongeza mtandao wa chuo chao
ambacho kina matawi handi mikoani. Mziray alisema kuwa wanafunzi wao wa tawi la
Mbeya nao wamefika kwa ajili ya ziara hiyo na kuonyesha uwezo wao katika
michezo.
“Tupo tayari kwa ajili ya mechi hizo, tunajua Taswa FC na
Taswa Queens ni timu nzuri nah ii imetokana na kufanya vyema katika mechi zao
mbali mbali, tupo tayari kwa changamoto,” alisema Mziray.
Mwisho….
No comments:
Post a Comment