Picha ya pamoja ya Katibu mkuu wizara ya ujenzi Mhandisi, Mussa Iyombe (wa nne mstari wa mbele waliokaa kutoka kushoto) akiwa na wajumbe wa baraza la wafanyakazi kutoka kwenye vituo vya temesa mikoa ya Tanzania bara mara baada ya Katibu huyo kufungua mkutano wa baraza la wafanyakazi la wakala wa ufundi na umeme (TEMESA) inayowashirikisha wawakilishi wafanyakazi wa wakala kwa mikoa yote ya Tanzania bara uliofanyika hoteli ya Glonency mkoani Morogoro.
Katibu mkuu wizara ya ujenzi Mhandisi, Mussa Iyombe kushoto akimsikiliza Mtendaji Mkuu wa wakala wa ufundi na umeme (Temesa) Mhandisi Marcellin Magesa bara baada ya Katibu huyo kufungua mkutano wa baraza la wafanyakazi la wakala wa ufundi na umeme (TEMESA) inayowashirikisha wawakilishi wafanyakazi wa wakala kwa mikoa yote ya Tanzania bara unaofanyika hoteli ya Glonency mkoani Morogoro.
Katibu mkuu wizara ya ujenzi Mhandisi, Mussa Iyombe akizungumza jambo wakati wa mkutano wa baraza la wafanyakazi la wakala wa ufundi na umeme (TEMESA) inayowashirikisha wawakilishi wafanyakazi wa wakala kwa mikoa yote ya Tanzania bara unaofanyika hoteli ya Glonency mkoani Morogoro. kulia ni Mtendaji Mkuu wa wakala wa ufundi na umeme (Temesa) Mhandisi Marcellin Magesa.
Hapa Katibu Mkuu Iyombe alifurahia jambo na Mwenyekiti wa bodi ya ushauri wa wakala.
Mtendaji Mkuu wa wakala wa ufundi na umeme (Temesa) Mhandisi Marcellin Magesa akisoma taarifa katika mkutano huo.
Sehemu ya wajumbe wakifuatilia matukio mbalimbali katika mkutano huo.
TAASISI ya serilai ya wakala wa ufundi na umeme (TEMESA) imetakiwa kujiendesha kibiashara ili kuepukana na changamoto zinazozikabili ikiwemo kutengewa bajeti ya kujiendesha kutoka ndani ya serikali.
Akizungumza na wajumbe wa baraza la wafanyakazi kutoka kwenye vituo vya temesa mikoa ya Tanzania bara, Katibu mkuu wa wizara ya ujenzi, Mussa Iyombe alisema kuwa ili Temesa iendelee kudumu ni lazima ijiendeshe kibiashara itayosaidia kuondoa baadhi ya changamoto katika taasisi hiyo.
Iyombe alisema kuwa kabla ya kuanza mikakati ya kujiendesha kibiashara, viongozi wa juu wanapaswa kutoa mafunzo ya kibiashara kwa wafanyakazi watendaji ili kuweza kupata mbinu stahiki za temesa kujiendesha itayosaidia kupata vyanzo vingi vya fedha na hiyo itasaidia kuwa tegemezi katika bajeti kutoka serikalini.
“Njia ya kuepukana na utegemezi katika bajeti zenu kutoka serikalini, dawa yake temesa kujiendesha kibiashara kwani itasaidia kupunguza baadhi ya changamoto”. Alisema Iyombe.
Aliongeza kuwa temesa ikijiendesha kibiashara itaongeza ufanisi wa kazi zake katika kutoa huduma ndani na nje serikali.
Naye Mtendaji mkuu wa wakala wa ufundi na umeme (TEMESA) Mhandisi Marcellin Magesa akizungumza wakati wa mkutano wa baraza la wafanyakazi wa mwaka 2013/2014 na wajumbe hao alieleza kuwa mkutano hufanyika baada ya kukamilika kwa kwa maandalizi ya mpango na bajeti ya wakala kwa mwaka 2014/2015 pamoja na mambo mengine.
Magesa alisema kuwa mkutano huo husaidia kupitisha bajeti ya ya wakala kwa mwaka wa fedha 2014/2015 ambapo wakala wa ufundi na umeme (TEMESA) ndiyo iliyopewa dhamana na serikali ya kusimamia shughuli mbalimbali ikiwemo pamoja na utengenezaji wa magari, pikipiki, mitambo ya serikali, usimikaji wa mifumo ya umeme, elektroniki, viyoyozi na majokofu katika nyumba za serikali.
“Licha ya kupewa ushauri na Katibu mkuu wa Temesa kujiendesha kibishara taasisi hii imekuwa na changamoto mbalimbali na moja ya changamoto hizo ni kuwepo kwa madeni makubwa kutoka ndani ya serikali”. Alisema Mhandisi Magesa.
Shughuli zinafanya na Temesa ni pamoja na ukodishaji wa magari ya viongozi (V.I.P), mitambo mbalimbali, usimamizi wa vivuko vya serikali nchini na usanifu wa mifumo ya umeme, tehama, viyoyozi katika majengo ya serikali.
No comments:
Post a Comment