Naibu
Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais, Eng. Angelina Madete (Katikati) na
Mkurugenzi wa mazingira Dkt. Julius Ningu (Kulia) wakimsilikiza Bw.
Julio Esterban Mshauri Mwelekezi kutoka UNIDO akitoa ufananuzi kwa
wakufunzi kutoka Vyuo vya ufundi nchini.Naibu
Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais, Eng. Angelina Madete akitoa hotuba
ya ufunguzi wa warsha ya Mafunzo ya wakufunzi kutoka Vyuo vya Ufundi
Nchini, mafunzo hayo yanafanyika katika Hotel ya Blue Pearl jijini Dar
es Salaam
Washiriki
wa Mafunzo wakiwa katika picha ya Pamoja na Mgeni rasmi Naibu Katibu
Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais Eng. Angelina Madete watatu kutoka kulia
mara baada ya ufunguzi wa warsha.
Na Lulu Mussa na Rashda Swedi,
Ofisi ya Makamu wa Rais, Dar es Salaam
Serikali
inaendelea na jitihada za kutoa elimu kwa umma juu ya njia bora za
kuhudumia majokofu na viyoyozi ili kulinda tabaka la Ozoni.
Hayo
yamesemwa jijini Dar es Salaam jana na Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu
wa Rais, Eng. Angelina Madete wakati wa ufunguzi wa Warsha ya Mafunzo
kwa Wakufunzi kutoka Vyuo mbalimbali vya Ufundi Nchi.
Katika
Hotuba yake Bi Madete amesema kuwa kemikali haribifu zinauwezo mkubwa
kuharibu tabaka la Ozoni na kuongeza joto angani. Kutokana na sababu
hizo, Serikali ya Tanzania kwa kushirikiana na jamii za kimataifa
zimekubaliana kufanya jitihada za kuondoa kemikali hizo hatarishi.
Bi Madete ameainisha baadhi ya kemikali hizo kuwa ni methyl bromide, halons na chloroflorocarborns
ambazo hutumika kama vipozi katika majokofu, viyoyozi, vifaa vya
kuzima moto, usafishaji chuma, ufukizaji wa mazao katika maghala na
utengenezaji wa magodoro ambazo huleta madhara kwa tabaka la ozoni na
adhari zake hutokea kwa binadamu, mimea na viumbe hai.
Katika
awamu ya kwanza, Tanzania imefanikiwa kuondoka tani 296 za kemikali
hizo haribifu ikiwa ni utekelezaji wa Mkataba wa Montreal na Vienna
ambayo Tanzania iliridhia mwaka 1993.
Aidha,
Bi Madete ameyataja madhara yatokanayo na uharibifu wa Tabaka la Ozoni
kuwa ni kuongezeka kwa magonjwa ya saratani ya ngozi,uharibifu wa macho
maarufu mtoto wa jicho, na upungufu wa uwezo wa mwili kujikinga na
maradhi. Athari hizi kwa kiasi kikubwa zinatokana na shughuli za
kibinadamu kama vile matumizi ya kemikali haribifu na zisizo rafiki kwa
mazingira.
Warsha
hii ya siku mbili imeratibiwa na Ofisi ya Makamu wa Rais na inajumuisha
wakufunzi kutoka Vyuo vya Ufundi vya Zanzibar na Mikoa ya Kilimanjaro,
Arusha, Kigoma, Mbeya na Mwanza.
No comments:
Post a Comment