TAN

TAN

Bayport

Bayport

Kikoa

Kikoa

Myway entertainment

Myway entertainment

FORE PLAN CLINIC

FORE PLAN CLINIC

MPINGA CUP 2016

MPINGA CUP 2016

Mashujaa Fm 89.3, Lindi

Saturday, March 22, 2014

IKONDOLELO HOTELI YATAJWA KUWA HOTELI BORA KINONDONI-DAR ES SALAAM.

Na:zuhura Masoud.
Hoteli ya Kimataifa ya Ikondolelo ya Kibamba jijini Dar es Salaam, imeendelea kuwa gumzo kutokana na kuweka burudani mbali mbali ndani ya Kumbi zinazopatikana katika hoteli hiyo ambayo ni ya kisasa na yenye adhi ya kimataifa.

Wakizungumza kwa nyakati tofauti wakazi wa Maeneo  tofauti tofauti ya Jijini Dar es salaam , wamesema kuwa wanampongeza mkurugenzi wa IKONDOLELO HOTELI kwa kuweka miundombinu kabambe ya kuhakikisha wakazi wa maeneo mbalimbali  wanapata fursa ya kushiriki Kimichezo ya aina mbalimbali iliyopo katika hotel hiyo.

Aidha Hoteli hiyo ambayo imejengwa kwa ustadi mkubwa, imewekewa mandhari ya kuvutia kwa wageni wote wanaopata fursa ya kwenda kutembelea maeneo hayo ikiwamo wakazi wa jiji wanaokwenda kwa lengo la kujiburudisha kwa njia mbali mbali ikiwamo, Kuogelea, kucheza Poltable,Burudani ya Muziki na mengine mengi.

Hata hivyo wameogeza kusema kuwa, hapo awali kabla ya hoteli hiyo kujengwa maeneo hayo, kwao burudani zilikuwa zikionekana tu kama ni kwa baadhi ya watu kutokana na kuwa kimya kwa muda mrefu kitendo kilichokuwa kinawaweka katika Dunia ya giza na kuwaondoa katika utandawazi wa Dunia ya Sayansi na Teknolojia.

IKONDOLELO ambayo kwa ujumla imejengwa kwa Ustadi mkubwa, imefanikiwa kuwekewa Bwawa la kuogela la kisasa ambalo linakidhi mahitaji ya watu wa aina zote nje na ndani ya  jimbo la Ubungo kwa ujumla ikiwemo na maeneo ya Kibaha wilaya ya Pwani.

mbali na bwawa hilo pia IKONDOLELO ni moja ya Hoteli ambayo inamazingira ya kupendeza hususani kuna maeneo ya kupendeza kwa ajili ya mapumziko kwa watu walio na fungatena serehe mbalimbali kupata kumbi kuwa zenye uwezo wa kuingiza watu wengi pamoja na waleMikutano, na mengine mengi.

katika Hoteli ya IKONDOLELO kati ya vitu ambavyo pia vinaonekana kuwavutia wakazi wa maeneo hayo ni pamoja na Eneo la Maegesho ya Magari(Parking) ambayo ni ya kipekee kutokana na kila mgeni mwenye usafiri kuwa na uhakika na Ulinzi wa Mali ama vifaa wanapokuwa ndani ya Hoteli hiyo .
Meneja wa Hoteli hiyo Bwana, Samweli mnyika ambaye aliweka wazi kuwa kutokana na kutambua hali ya maisha na mahitaji ya watu, waliamua kuweka burudani kwa lengo la kuwaweka watoto  na vijana karibu na mazingira ya nyumba zao pasipokutoka kwenda mbali ususani wakati wa sikukuu ambazo burudani zinakuwa zimeandaliwa kwa ajili ya kuwafurahisha watu wote waoapata fulsa ya kuingia ndani ya IKONDOLELO.
Aidha amesema kuwa pamoja na hali hiyo pia wamezingatia ubora wa gharama kwa wahitaji, ambapo alisemakuwa garama zao ni nafuu kwa wale wanaokwenda kwa ajili ya kukodi Ukumbi kwa ajili ya Maharusi na sherehe alimbali.
naye Mkurugenzi wa Hoteli hiyo bwana Philip Selekwa Humbie alisema kuwa anawashukuru wote wanaoendelea kumpa ushirikiano katika kuijenga upya Hoteli hiyo ambayo kwa sasa inaonekana kuwa ndiyo Hoteli kubwa kuliko zingine inayopatikana maeneo ya Jimbo la Ubungo, ikiwa CCM Kibamba, njia ya Kibwegele.
"Binafsi ninawakaribisha sana wateja wangu ambao wanapata muda na kuweza kuja hapa, kwa hiyo niseme kuwa nawapenda kwa kuwa wanapata fulsa pia ya kuniunga mkono, na hata nyinyi wandishi pia nawakaribisha, hapa kwangu kuna kumbi nyingi, mnaweza hata kuja kubadilisha manzali kwa ajili ya sherehe zenu, au hata mje mpate kuogelea kama unavyoona jinsi watu walivyowengi yaani wanaendelea kufurahi kila mmoja kwa nafasi yake. KWA MAWASILIANO ZAIDI PIGA SIMU HIZI
 0713210839 au 0712884082 

KAULI YA WAPINZANI KUHUSU HOTUBA YA JK BUNGE LA KATIBA


Wenyeviti wa vyama vya Upinzani vya Chadema, Chama cha Wananchi (CUF) na Chama cha NCCR-Mageuzi, jana usiku walikutana ili kutoa kauli ya pamoja, kutokana na hotuba ya ufunguzi wa Bunge kwa maelezo kuwa tayari Rais amevuruga mchakato mzima wa kupata Katiba Mpya.
Wakati viongozi hao wakikutana, Mwenyekiti wa Chama cha DP Mchungaji, Christopher Mtikila alisema, Rais ameingilia mchakato na kutoa maelezo jinsi ya  kuandika Katiba.
Wakizungumza na gazeti hili jana mara baada ya hotuba hiyo, Freeman Mbowe, James Mbatia na Profesa Ibrahim Lipumba, walisema wameipokea kwa masikitiko makubwa hotuba hiyo.
“Tunakwenda kujadili hotuba ya Rais na tutatoa msimamo wetu,” alisema Mbowe.
Awali Katibu wa muda wa Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa), Julius Mtatiro alisema Rais Jakaya Kikwete amevuruga mchakato wa Katiba, kwani walitarajia angetumia mamlaka yake kama Rais kuwaunganisha.
“Rais tulitarajia angeongea kama mkuu wa nchi, lakini amezungumza kama Mwenyekiti wa CCM na kutoa msimamo juu ya muundo wa Muungano jambo ambalo hatukulitegemea,” alisema Mtatiro.
Alisema kwa Rais kutoa msimamo ni sawa na mwongozo jambo ambalo limevuruga mchakato mzima.
Hofu ya kuvunjika Bunge
Wakizungumza nje ya Bunge, baadhi ya wajumbe wameeleza kuwa hotuba ya Rais Kikwete kama ikitekelezwa uwezekano wa kupata Katiba Mpya utakuwa mgumu.
Mjumbe Luhaga Mpina alisema kwa jinsi rasimu ilivyoandikiwa na kama muundo wa serikali mbili ukipita basi rasimu ya Katiba itabidi iandikwe upya.
“Rasimu yote imetengenezwa kwa mfumo wa serikali tatu sasa hapa kuna hatari ya Bunge kukwama ,” alisema.
Mtatiro kwa upande wake alisema sasa kuna hofu ya kushindwa kupatikana Katiba Mpya kwani Rais amewachanganya wajumbe na kama watapitisha maoni yake itabidi rasimu kuandikwa upya.
Mjumbe Mustapha Akoonay, alisema upatikanaji wa katiba upo shakani kwani sasa upinzani utakuwa mkubwa juu ya muundo wa muungano.
“Kwa sasa nadhani itabidi turudi upya kwa wananchi kupata kura ya maoni juu ya muundo wa muungano,” alisema.
Lucy Owenya alisema  Rais amegeuza mkutano wa Bunge kuwa ni mkutano wa Chama Cha Mapinduzi, kwani ameshindwa kabisa kutoa mwelekeo wa nchi na badala yake ametoa msimamo wa CCM.
“Kutokana na hili, naamini kabisa Bunge halitakuwapo na ni bora iwe hivyo kwa kuwa amejibu hotuba ya Warioba na kwa maana hiyo amepingana na mawazo ya wananchi.”
Godbles Lema alisema kuwa Rais hakuja kuhutubia taifa bali alikuja kufanya semina na kujibu hotuba ya Warioba.
Mjumbe huyo ambaye ni mbunge wa Arusha Mjini alionyesha shaka kuwa baada ya muda wa wiki tatu hakutakuwa na Bunge la Katiba kwa kuwa wako baadhi ya watu ambao hawatakubali kilichofanywa na Rais Kikwete.
“Waliochukua fedha ni vyema wakaenda kumalizia nyumba zao kwa kuwa kiongozi wetu amefanikiwa kwa kiasi kikubwa kuwafurahisha wanaCCM lakini kwa Watanzania hatutakubali,” alisema Lema.
John Cheyo alisema, “Mimi ninachokiona ni maridhiano tu, suala la kufumua rasimu halinipi shida kwa kuwa vitu vyote vinavyoletwa bungeni huwa ni mali ya Bunge na hivyo tutafanya tunavyoona sisi inafaa.”
Mchungaji Peter Msigwa, alisema kuwa kosa kubwa ambalo lilifanywa na upinzani ni kukubali na kuruhusu Jaji Warioba atangulie kuwasilisha rasimu yake akasema hilo ndilo lililowagharimu.
Alitaka Bunge livunjwe mara moja ili warudi kwa wananchi wakaamue na kuwahukumu kutokana na kile ambacho walikifanya katika Bunge ambalo kwa maoni yake wamekula fedha za walipa kodi bure.
Naye Waziri Mkuu Mstaafu, Edward Lowassa aliipongeza hutuba ya Rais Jakaya Kikwete ya uzinduzi wa Bunge la Katiba.
Lowassa ambaye pia ni Mjumbe wa Bunge la Katiba, alisema kwa kifupi hotuba ya Rais Kikwete ni nzuri. Lowassa alitoa kauli hiyo, wakati akitoka nje ya Bunge, muda mfupi baada ya Rais Jakaya Kikwete kumaliza hotuba ya uzinduzi wa Bunge hilo.

Zitto Kabwe anena Baada ya Rais Kikwete Kuhutubia Bunge La Katiba

Serikali 2 zitaendeleza hisia za Utanganyika kwa kasi 

Mkuu wa Nchi kamaliza kuhutubia Bunge la Katiba. Kimsingi kaegemea upande wa msimamo wa Serikali 2 ambao ndio msimamo wa CCM chama anachoongoza. Hata hivyo kasisitiza kuwa iwapo tunataka Serikali 3 basi tuzingatie hofu zilizopo ikiwemo masuala ya Uraia, uwezo wa kifedha wa Serikali ya Muungano nk.

Ni dhahiri kero za Muungano zilizodumu kwa zaidi ya miaka 50 haziwezi kutatuliwa na muundo ule ule uliozitengeneza. 
Jawabu la muungano wa Tanzania ni muundo wa Serikali tatu wenye Serikali ya Muungano yenye nguvu na rasilimali. Tunaloweza kuongeza ni kuweka mfumo wa Tawala za Mikoa wenye kupanua demokrasia zaidi kwa kuchagua wakuu wa mikoa na kufuta wakuu wa wilaya. 
Ni dhahiri Uraia itakuwa ni 'deal breaker' kwenye suala la muundo wa Muungano. Hili litajibiwa kwa kuwa na Nchi moja, dola moja na Serikali tatu.


AJALI MOROGORO : TRAFIK AGONGWA NA GARI MOROGORO.

Askari wa  kikosi cha usalama barabarani mkoa wa Morogoro Analijulina Bw Crispan 'Mandela' amegongwa na gari eneo la Mtawala Barabara inayotoka Msavumu  kuingia katikati ya Mji wa Morogoro.Hii ni Mara ya Pili kwa Askari Huyo Kugongwa na Gari Mkoani Hapa.

Friday, March 21, 2014

MWIGULU ATAKA MAJESHI YA TANZANIA KUSHIRIKIANA NA MAJESHI YA NCHI NYINGINE

MWIGULUNCHEMBA 
NAIBU waziri wa fedha,Mwigulu Nchemba amesema, kukua kwa utandawazi kumeifanya dunia kuwa  kijiji , hivyo kuna kila hali ya kuimarisha majeshi ya ulinzi  ya ndani kwa kushirikiana na majeshi ya nchi za nje kwa kuyaongezea ujuzi zaidi wa kinadhalia katika kuimarisha usalama wa nchi.
Kauli hiyo ameitoa jana katika mahafari ya kwanza ya kuhitimu kozi ya mafunzo mkakati kwa maafisa wa jeshi la wananchi Tanzania(JWTZ)kutoka chuo cha mafunzo ya kijeshi Monduli(TMA) baada ya kumaliza kozi  ya mwaka mmoja katika chuo cha uhasibu Njiro(IAA),ambapo jumla ya maofisa  52 kutoka nchi 10 za Afrika  wahitimu kozi ya shahada ya udhamili na stashahada na kutunukiwa vyeti .
Nchemba alisema kuwa kwa sasa nchi nyingi za afrika haziitaji kupigana kwa ajili ya kupata uhuru ila zinahitaji ulinzi ili kupiga hatua katika masuala ya kiuchumi wakati nchi hizo zikiwa salama ,hivyo alitoa rai kwa mafunzo hayo kuendelezwa zaidi katika  program mbalimbali ambazo zitasaidia wahitimu kufanya vizuri zaidi katika kuimarisha utendaji wa kazi zao.
Alisisitiza kuwa lazima majeshi ya kiafrika yajiendeshe kisasa zaidi kwa kutumia elimu na ujuzi kutoka kwenye vyuo mbalimbali vya ndani na nje ili kwendana na hali ya utandawazi na teknolojia ya kisasa.
Naye mkuu wa chuo hicho Prof,Johannes Monyo alisema kuwa ushirikiano wa chuo cha uhasibu Arusha na chuo cha kijeshi Monduli ulikuja kwa kutiliana saini mapema mwaka jana,katika kutoa taaluma hiyo baada ya mitaala yake kupitishwa na taasisi ya elimu ya juu(Nacte).
Alisema mafunzo hayo yatawasaidia wanajeshi hao na raia  kuongeza ujuzi katika shughuli zao,na kwamba chuo hicho kinatarajia  kuanzisha program nyingine ya mafunzo inayotarajiwa kuanza mapema mwakani,baada ya mtaala yake kukamilisha na kupitishwa.
Monyo alisema makubalinao ya kuanzisha mafunzo hayo yanawezesha chuo hicho kupeana mafunzo juu ya kuboresha masuala mbalimbali ya kitaaluma ikiwemo katika sekta ya fedha,utawala na diplomasia.
Aliongeza kuwa mafunzo hayo yatawasaida pia kuwapa  ujuzi wa kimkakati  katika masuala ya Kiuongozi ,kutatua migogoro,usimamizi wa miradi,Diplomasia,Mawasiliano na sekta za kiraia, na matumizi ya teknolojia  .
Alisema chuo hicho kilianza kutoa kozi ya kwanza kwa maofisa wa jeshi zaidi ya 52 pamoja na wakufunzi kutoka TMA wanaotoka katika Nchi mbalimbali zikiwemo za Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) pamoja na Nchi za Kusini mwa Jangwa la Afrika (SADC) .

RATIBA YA ROBO FAINALI KLABU BINGWA ULAYA 2014

MSD, CSR WAJITOLEA KUMSAFIRISHA MTOTO ALIYEUNGUA MOTO KUTOKA MBEYA KWENDA HOSPITALI YA CCBRT DAR ES SALAAM KWA MATIBABU

1 
Mama wa mtoto Dorothea Njavike (1) ambaye aliunga moto mkoani akiwa mchanga na kuathirika kwa kupata ulemavu, Milka Kabelege (kulia), mama mkubwa wa mtoto huyo, Salome Kyegulo (kushoto), wakiwasili Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA), Dar es Salaam juzi ambapo wamefika jiji kupata matibabu katika Hospitali Maalumu ya CCBRT. Gharama za kusafiri kutoka mkoani Mbeya kwa ndege kuja Dar es Salaam zimefanywa na Bohari ya Dawa (MSD). (PICHA KWA HISANI YA MSD)
…………………………………………………….
Na Dotto Mwaibale
BOHARI ya Dawa (MSD), imejitolea kumsafirisha hadi Dar es Salaam kwa matibabu katika Hospitali ya CCBR mtoto Dorothea Njavike (1) aliyepatwa na janga la kuungua moto mkoani akiwa mchanga.
MSD na CSR wamejitolea kummsafirisha mtoto huyo juzi pamoja na mama yake mzazi Milka Kabelege, mama yake mkubwa Salome Kyegulo kwa ajili ya kumsaidia mtoto huyo wakati wa matibabu yake katika hospitali hiyo maalumu ya CCBRT ya jijini Dar es Salaam.
“Baada ya kupata taarifa ya kuungua mtoto huyo kupitia vyombo vya habari sisi MSD tuliguswa tukaona ni vizuri tumsaidie kumsafirisha mtoto huyo kwa ndege pamoja na wazazi wake kuja Dar es Salaam kwa kupata matibabu na kuwarudisha mkoani Mbeya baada ya matibabu” alisema Mkurugenzi wa Rasilimali Watu na Utawala wa MSD, Victoria Elangwa.
Dorothea, ambaye ameathiriwa kwa kiasi kikubwa na janga la moto amepata ulemavu sehemu za uso, ambapo pua, mdomo, kidevu na jicho moja viliungua pamoja na mikono yake yote miwili kuanzia sehemu za maungio ya viganja.
Kutokana na hali hiyo juhudi mbalimbali zimekuwa zikichukuliwa na vikundi mbalimbali hadi kufikia uamuzi wa kumpeleka jijini Dar es Salaam kwa matibabu.
Kwa mujibu wa mmoja wa wawezeshaji kutoka kundi la Motherhood la Dar es Salaam aliyefahamika kwa jina moja la Anitha alisema madaktari watakao mtibu mtoto huyo ni kutoka Tanzania ambao wataungana na wale wa mataifa mengine kwa ajili ya kuangalia namna ya kuweza kurekebisha uso na maeneo mengine yaliyoathiriwa na moto huo.
Mmoja wa madaktati aliyempokea mtoto huyo juzi baada ya kufika katika Hospitali ya CCBRT ambaye hakupenda jina lake liandikwe gazetini alisema mtoto huyo ataanza kupata matibabu kwa hatua za awali wakati zikisubiriwa taarifa zaidi zilizomo kwenye faili lake kutoka Hospitali ya Rufaa ya Mbeya akikokuwa akipatiwa matibabu.

HOSPITALI YA KALOLENI KUBORESHWA, WATEMBELEWA NA UJUMBE WA WANAWAKE WASICHANA

Dr Anna Kimaro mganga wa zamu wa kituo cha afya Kaloleni aliyebeba faili kwapani akiwa na wajumbe wa mkutano wa umoja wa wanawake vijana wa kikristo duniani YWCA walipo tembelea katika kituo hicho jijini arusha.
 Baadhi ya wajumbe wa mkutano wa umoja wa wanawake vijana wa kikristo duniani walipofanya ziara katika kituo cha afya cha Kaloleni jijini arusha kujionea hali ya huduma kwa akina mama wajawazito na wasichana wenye ujauzito.
Baadhi ya wajumbe wa mkutano wa umoja wa wanawake vijana wa kikristo duniani walipofanya ziara katika kituo cha afya cha Kaloleni jijini arusha wakipata maelezo ya kina kutoka kwa moja ya wafanyakazi wa kituo hicho.
 Baadhi ya wajumbe wa mkutano wa umoja wa wanawake vijana wa kikristo duniani walipofanya ziara katika kituo cha afya cha Kaloleni jijini arusha kujionea hali ya huduma kwa akina mama wajawazito na wasichana wenye ujauzito.
 Bi Severa joseph akitoa maelezo ya aina ya dawa zinazotumika kwa akina mama wajawazito katika kituo cha afya Kaloleni cha jijini arusha kwa baadhi ya washiriki wa mkutano wa umoja wa wanawake vijana wa kikristo duniani.

RAIS KIKWETE KUONGOZA KIKAO CHA BARAZA LA MAWAZIRI MJINI DODOMA.

D92A4920Waziri Mkuu Mizengo Pinda akimlaki Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete muda mfupi baada ya kuwasili katika uwanja wa ndege mjini Dodoma leo mchana ambapo kesho anatarajiwa kulihutubia na kuzindua rasmi Bunge maalum la Katiba.

Mkoa wa Mtwara kuboresha Uwanja wa Ndege

????????  
Timu ya Ukaguzi wa Miradi ya Maendeleo kutoka Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango ilipowasili katika Uwanja wa Ndege wa Mtwara kwa ajili ya kujionea maendeleo ya uwanja huo.???????? 
Mmoja wa viongozi wa Timu Ukaguzi wa Miradi ya Maendeleo kutoka Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango, Bibi Florence Mwanri (aliyevaa fulana nyeusi) akihoji uimara wa sehemu ya kutulia ndege wakati walipofanya ziara ya kujionea maendeleo ya Uwanja wa Ndege wa Mtwara.
 
 
Na Saidi Mkabakuli

Katika kukabiliana na kasi ya maendeleo ya ukuaji wa uwekezaji katika maeneo ya viwanda vikubwa na biashara za huduma mkoani Mtwara, Serikali imesema kuwa kuna haja ya kuuimarisha Uwanja wa Ndege wa Mtwara ili kuongeza ufanisi katika utoaji wa huduma kwa watumiaji wa uwanja huo, hasa kufuatia kugundulika kwa gesi mkoani humo,
Hayo yamebainishwa mmoja wa viongozi wa timu ya ukaguzi wa miradi ya maendeleo kutoka Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango, Bibi Florence Mwanri  wakati ilipofanya ziara kwa ajili ya kujionea maendeleo ya uwanja wa huo.
Bibi Mwanri alisema kuwa Serikali inaendelea kufanya tathmini na mikakati mbalimbali itakayopelekea kuuimarisha uwanja wa ndege wa Mtwara ili kuweza kuhudumia uwekezaji mkubwa unaofanywa na makampuni mbali mbali ya ndani na nje ya nchi mkoani humo. Aliongeza:
“Tathmini ya awali inaonesha kuwa miradi mingi ipo mkoani Mtwara kufuatia kugundulika kwa gesi hivyo kuna haja ya dhati ya kuuimarisha uwanja wa ndege wa Mtwara kwa lengo la kutoa huduma za uhakika wakati huu wa mfumuko wa kiuchumi mkoani Mtwara,” alisema Bibi Mwanri.
Akizungumza wakati wa ukaguzi huo, Naibu Katibu Mtendaji (Uchumi Jumla), Prof. Longinus Rutasitara ambaye alikuwa kiongozi mwenza wa ukaguzi, alisema kuwa kuna haja ya dhati ya kuwekeza katika uwanja huo ili kukabiliana na kasi ya maendeleo ya mkoa wa Mtwara kufuatia wawekezaji wengi kuendelea kumiminika na kuwekeza mkoani humo.
“Uwanja wa ndege wa Mtwara una fursa za nyingi za kuhudumia wafanyabiashara wa ndani na nje ya nchi, hakika ni lango la biashara hasa kipindi hiki cha uchumi wa gesi mkoani Mtwara, hivyo uendelezaji wa uwanja huu ni jambo lisilo epukika,” alisema Prof. Rutasitara.
Kwa mujibu wa Mpango wa Maendeleo wa Taifa wa Miaka Mitano (2011/12 – 2015/16),  Miundombinu ni kipaumbele cha kwanza, hasa uwekezaji mkubwa katika miundombinu ya nishati, usafirishaji (bandari, reli, barabara na usafiri wa anga), maji (safi, taka na ya uzalishaji) na TEHAMA.
Serikali imeandaa Mpango wa Maendeleo wa Miaka Mitano (2011/12 -2015/16) wa kutekeleza Dira ya Taifa ya Maendeleo 2025. Lengo kuu la Mpango huu ni kufungulia fursa za ukuaji uchumi wa nchi ili kuweka misingi ya ukuaji mpana wa uchumi na unaolenga watu walio masikini zaidi. Mpango wa Kwanza wa Maendeleo wa Miaka Mitano unawianisha katika mfumo mmoja wa mipango mbalimbali ya maendeleo ya kitaifa ili kutoa mwongozo wa utekelezaji na kuipa Serikali fursa na mfumo rasmi wa ufuatiliaji na tathmini wa miradi ya maendeleo kitaifa.
Lengo la Dira ni  kuibadili Tanzania kuwa nchi ya uchumi wa kati ifikapo mwaka 2025.

Mabaki ya NDEGE YA MALAYSIA yameonekana Nchini Australia


Kama week sasa imepita Muhubiri na Mtabiri mkubwa wa Nchini Nigeria alitabiri kuwa Ndege ya Malaysia iliyopotea muda si mrefu wataipata ikiwa chini ya maji na wataanza kuona mabaki ya ndege yakielea juu ya maji ..Sasa leo habari mpya kuhusu ndege hiyo ni kuwa Huku Nchini Australia yameonekana mabaki ya ndege kwa njia ya Setelite ambayo bado yanafanyiwa uchunguzi kama ni ya ndege hiyo ..Habari kamali soma hapa chini:

"The Malaysian prime minister has confirmed that there is a new lead in the investigation into the missing Malaysia Airlines flight MH370.
Australian search aircraft are investigating two objects spotted by satellite floating in the southern Indian Ocean that could be debris from a Malaysian jetliner missing with 239 people on board, Prime Minister Tony Abbott said on Thursday.
"I can confirm we have a new lead," Malaysian Transport Minister Hishammuddin Hussein told reporters in Kuala Lumpur, where the investigation into the missing airliner is based.
"I am meeting the Australian delegation now," he added. we are waiting for some information."
Another official in Malaysia said investigators were "hopeful but cautious" about the Australian discovery. The satellite images were being reviewed and they were awaiting visual confirmation, the source said.
No confirmed wreckage from Malaysia Airlines Flight MH370 has been found since it vanished from air traffic control screens off Malaysia's east coast early on March 8, less than an hour after taking off from Kuala Lumpur for Beijing.
"New and credible information has come to light in relation to the search for Malaysia Airlines Flight MH370 in the southern Indian Ocean," Abbott told the Australian parliament.
"The Australian Maritime Safety Authority (AMSA) has received information based on satellite imagery of objects possibly related to the search."
"Following specialist analysis of this satellite imagery, two possible objects related to the search have been identified," he said.
Abbott said he had already spoken with his Malaysian counterpart Najib Razak and cautioned that the objects had yet to be identified.
"The task of locating these objects will be extremely difficult and it may turn out they are not related to the search for MH370," Abbott said"

WAKAZI WA SINZA WAENDELEA KUNUFAIKA NA HUDUMA ZA NMB

  • Wateja zaidi ya 300 kupata huduma kila siku katika tawi hilo
NMB ikiwa ni benki  chaguo la watanzania wengi. Jana Machi 19, 2014 ilifungua rasmi tawi lake jipya maeneo ya Sinza Mori mkabala na kituo cha kuwekea mafuta cha ‘Big Born’ ikiwa na lengo la kuwafikia wateja wake, ambapo takribani zaidi ya wateja 300 wamekuwa wakihudumiwa kila siku katika tawi hilo.
Tawi hili limeanza kufanya kazi hivi karibuni, ambapo limeonekana kuwa ni msaada mkubwa kwa wakazi wa Sinza ikiwa ni moja kati ya maeneo yenye wakazi wengi jijini Dar es salaam.
Hii itakua pamoja na mitaa jirani kama, Kijitonyama, Mabatini, Afrikasana,Tandale, Sayansi na maeneo mengine kwa kupata huduma za kibeki kwa uharaka zaidi.
_DSC4688 
Afisa Utumishi Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Bw. Godfrey Mugomi akikata utepe kuashiria uzinduzi rasmi wa tawi la NMB Sinza.
Wa Kwanza kulia ni ni Meneja wa Tawi la NMB Sinza Bi.Kidawa Masood na Meneja wa NMB Kanda ya Dar es salaam Bw. Salie Mlay wakishuhudia ufunguzi huu uliofanyika jana jijini Dar es salaam.
Akizungumza katika ufunguzi huo, Meneja wa NMB Kanda ya Dar es salaam Bw. Salie Mlay alisema lengo kubwa la kupeleka tawi hilo ni kuwapa huduma kwa ukaribu wateja wao waliopo katika eneo hilo.
Alifafanua kwamba, tangu kuanzishwa kwake tawi hilo limekuwa ni mkombozi kwa wateja wengi wakiwemo wafanyabiashara wakubwa na wadogo pamoja na watu mbalimbali.
“Tawi letu linatoa huduma zote za kibenki, na tunazidi kuwakaribisha wateja wetu ili wajionee huduma bora zitolewazo na benki yetu na pia tunatoa huduma mbalimbali zikiwemo za Mashine za kutolea fedha(ATM) ambayo hufanya muamala kwa masaa 24”
sinzainside 
Meneja wa NMB Kanda ya Dar es salaam, Bw. Salie Mlay (kati) akimwelezea Afisa Utumishi Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Bw. Godfrey Mugomi (pili kushoto) huduma mbalimbali zitolewazo na tawi jipya la NMB Sinza.
Ufunguzi wa tawi hili la Sinza unafanya idadi ya matawi yaliyopo Kanda ya Dar es Salaam kufikia ishirini na tatu.
Hivyo basi, kuifanya NMB kuendela kuwa benki yenye matawi mengi zaidi Tanzania.
Tawi hili linatoa huduma mbalimbali kwa wateja wa NMB kama mikopo ya pikipiki za miguu miwili na mitatu, kufungua akaunti, kuweka na kutoa fedha nk.
Pia litakua linafunguliwa Jumatatu hadi Ijumaa kuanzia  saa mbili  na nusu asubuhi hadi saa kumi na nusu jioni ( 2:30 asubuhi – 10:30 jioni) na Jumamosi kuanzia saa mbili na nusu asubuhi hadi saa sita na nusu mchana (2:30 asubuhi- 6:30 mchana), Jumapili na siku za Sikukuu hakutakuwa na huduma ndani ya tawi hili.
_DSC4609
Sehemu wa wageni waalikwa waliohudhuria uzinduzi huo
Akizungumza kwa upande wake wakati wa ufunguzi huo kwa niaba ya Mkuu wa wilaya ya Kinondoni, Afisa Utumishi Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Bw. Godfrey Mugomi aliipongeza benki ya NMB kwa kutambua umuhimu wa huduma za kifedha na kusogeza karibu na jamii ili iweze kufaidika na kuwataka wananchi na wateja wapya kutumia tawi hili pekee katika eneo hilo ili kupata huduma za kibenki badala ya kutembea umbali mrefu kufuata huduma hizo kwenye matawi yaliyo mbali.

Wakala wa Usafirishaji Mizigo ya DHL kuhusishwa na tuhuma za kusafirisha madawa ya kulevya kwenda nchini Liberia

RAIA watatu wa Nigeria na mwanamke wa Kitanzania wamekamatwa na polisi jijini Dar es Salaam, wakituhumiwa kujaribu kusafirisha madawa ya kulevya kwenda nchini Liberia. Watuhumiwa hao wanadaiwa kuwa walikuwa mbioni kutuma mihadarahi hiyo, ikiwa kwenye vitabu, kwa kutumia Wakala wa Usafirishaji Mizigo ya DHL.
clip_image002

Kamanda wa Polisi, Kanda Maalumu Dar es Salam, Suleiman Kova alitaja majina ya Wanaijeria hao kuwa ni Sunday Chaidikaobi (42), Chukwuma Favour (31), na Franklin Indubuisi (41). Mtanzania aliyebambwa pamoja na Wanaijeria hao ametajwa kuwa ni bi Hadija Ngoma (43), mkazi wa Kimara Temboni, Dar es Salaam.

Kwa mujibu wa Kamanda Kova, polisi walipata taarifa juzi, Machi 18, kuwa kuna watu wanne wanajihusisha na usafirishaji wa dawa za kulevya waliokuwa katika ofisi za DHL zilizopo Barabara ya Sam Nujoma.
Kufuatia taarifa hizo, Kamanda Kova amesema “makachero walifuatilia suala hilo na hatimaye siku hiyo saa 8:30 mchana watu hao walikamatwa wakiwa na kifurushi wakijiandaa kukisafirisha kwenda nchini Liberia.”
Alisema polisi walipopekua kifurushi hicho, walikuta vitabu vitatu vya Kiingereza. Walipopekua vitabu hivyo, walikuta madawa aina ya heroin katika kurasa za mwanzo.
“Katika vile vitabu kurasa ya kwanza inayofunika lile jalada gumu kwa ndani, walikuwa wamefunua na kuweka unga huo na katika ukurasa wa nyuma vivyo hivyo kwa vitabu vyote,”aliongeza.
Unga huo unaokadiriwa kuwa na uzito wa nusu kilo, umepelekwa kwa mkemia mkuu wa serikali kwa uchunguzi zaidi kubaini thamani na uthibitisho wa madawa hayo. H/T HabariLeo
Inaonekana Wanigeria wanakuja kwa kasi kwenye biashara hii ndani ya Afrika Mashariki. Miezi kadhaa iliyopita, Wanigeria wawili walikamatwa katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Jomo Kenyatta nchini Kenya, wakijaribu kusafirisha dawa za kulevya aina ya cocaine zenye thamani ya takriban shilingi milioni 120; kama inavyoonesha video hii hapa chini

Thursday, March 20, 2014

A White House official said the latest wave of US sanctions targeted 20 Russian individuals with interests in the Crimea.

The Russian bank being targeted - for supporting government officials - is Bank Rossiya, the US Treasury said.
Among the 20 individuals facing sanctions are members of Russian President Vladimir Putin's inner circle.
They include his chief of staff Sergei Ivanov and wealthy businessmen Arkady Rotenberg and Gennady Timchenko.
Those targeted will be unable to make transactions in dollars, will have any assets in the US frozen and will be barred from doing business in the US.
Pro-Russian forces hang up a Russian flag after seizing the Ukrainian corvette Khmelnitsky in Sevastopol, Crimea (March 20, 2014) 
  The Ukrainian corvette Khmelnitsky was among those seized by pro-Russian forces on Thursday
A pro-Russia forces man holds a gun during seizure of the Ukrainian corvette Khmelnitsky in Sevastopol, Crimea (March 20, 2014) 
  The Khmelnitsky is anchored in the Crimean port of Sevastopol
European Union leaders meeting in Brussels also said they would expand the number of Russians facing sanctions, and said a summit with Russia planned for June would not go ahead.
German Chancellor Angela Merkel told the German parliament that the EU would be ready to impose economic sanctions against Russia if there were a further escalation in Russia's involvement in Ukraine.
Slovenia's Prime Minister Alenka Bratusek, Germany's Chancellor Angela Merkel and Lithuania's President Dalia Grybauskaite attend a European Union leaders summit in Brussels (March 20, 2014) EU leaders including Angela Merkel (centre) are in Brussels for talks on the Ukraine crisis

Mrs Merkel told reporters in Brussels that she was optimistic that EU nations would be able to present a unified voice on the Crimea crisis.
http://ambassadorofdemocracytanzania.blogspot.com/

Ethiopia's clothes firms aim to fashion global sales

 

Fikirte Addis (centre) attending an Ethiopian cultural festivalFikirte Addis (centre) is looking at increasing her overseas sales
She adds that Ethiopians take great pride in the country's ethnic diversity - about 84 languages and 200 dialects are spoken - and in displaying allegiances through clothing at special events such as weddings and festivals.
Her clothing line, Mafi, specialises in ready-to-wear garments offering a notably funky take on the country's ethnic melting pot, and one that has proved successful.
In 2012 Ms Mahlet won the Origin Africa Design Award, and showcased her work at African Fashion Week New York.
Home-spun skills
Ethiopia's successful fashion designers are predominantly women who grew up surrounded by traditionally woven cotton fabrics, and did not need to be taught the tailoring and embroidering skills required to make beautiful and delicate clothing.
At the same time, a lack of formal fashion design education is preventing many Ethiopian designers from breaking out internationally, says Ms Mahlet, who is self-taught, and credits Google Search as her primary tutor.
more story vist here:
http://ambassadorofdemocracytanzania.blogspot.com/

Crimea crisis: Merkel warns Russia faces escalating sanctions

Armed Crimean defence forces stand outside naval training centre in Sevastopol. 19 March 2014 Crimean pro-Russian forces seized two naval bases on Wednesday

Ukraine crisis

European Union leaders are gathering in Brussels to discuss their response to the crisis over Crimea.
The British Prime Minister David Cameron said more names would be added to the list of those facing travel bans and asset freezes.
German Chancellor Angela Merkel said the EU would be ready to impose economic sanctions against Russia if there were an escalation.
Crimea remains tense after its leaders signed a treaty to join it to Russia.
French President Francois Hollande said a summit planned for June between the EU and Russia would be cancelled. He described the events of the past weeks as "unacceptable".
Mr Cameron said the countries of the European Union needed to speak with a clear and united voice.
Over dinner Europe's leaders will discuss their next moves. A few more Russian names may be added to the sanctions hat. That is the easy part. The names are already drawn up.
The question is whether, this time, they will go after people closer to President Putin. That is less certain.
The treaty signed by Crimean leaders with Moscow on Tuesday absorbs the peninsula - an autonomous republic in southern Ukraine - into Russia, following a referendum which the West and Kiev say was illegal.
The treaty has now been approved by Russia's lower house of parliament - the Duma - and is expected to be ratified by the upper house on Friday.
Speaking ahead of the vote in the Duma, Russia's Foreign Minister Sergei Lavrov described possible sanctions as "illegitimate" and "not based on international law".
Mr Lavrov said the treaty with Crimea would "be a turning point in the fate of the multi-ethnic peoples of Crimea and Russia, who are linked by the close ties of historical solidarity".
He reiterated Moscow's position that the annexation is necessary to protect ethnic Russians from "nationalists, anti-Semites and other extremists on whom the new [Ukrainian] authorities depend".
In a resolution on Thursday, Ukraine's parliament said the country would "never and under no circumstances end the fight to free Crimea of occupants, no matter how difficult and long it is".
continue@. 
http://ambassadorofdemocracytanzania.blogspot.com/